Kamanda Kamuhanda: 4 Songea, 1 Iringa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kamanda Kamuhanda: 4 Songea, 1 Iringa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Sep 3, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Sep 3, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Jina la Michael Kamuhanda nilipolisikia tu nilihisi kama nimewahi kulisikia tena siku si nyingi. Nina uhakika na wengine wamelikumbuka pia kuwa ndiye aliyekuwa Kamanda wa Polisi wa Ruvuma ambapo mapema mwaka huu (Februari) wananchi 4 waliuawa napolisi walipokuwa wakijaribu kuandamana kwenda ofisi ya Mkuu wa Mkoa. Natamani wamlete Dar-es-Salaam pia ili watu waelewe tatizo tulilonalo. Nikimuita ni mhalifu sijui kama nitakuwa nimetia chumvi sana... haiwezekani ndani ya mwaka mmoja kamanda unasimamia mauaji ya raia kisa wanataka kuandamana tu! Hivi hana mbinu nyingine zozote kichwani mwake zaidi ya kuwa trigger happy!
   
 2. Facilitator

  Facilitator JF-Expert Member

  #2
  Sep 3, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,288
  Likes Received: 802
  Trophy Points: 280
  He is probably hunting the top post (IGP) Nilimskiliza alipokuwa anahojiwa na waandishi wa Ch. 10, hata kuongea kwake ni mtu mmoja bure buresh kbs..
   
 3. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #3
  Sep 3, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,779
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Kweli mkuu hata mimi nikichangia sredi ya awali jioni,nimekumbuka kwamba huyu Kamanda aliongoza mauaji mengine Songea. Kwasababu hakuchukuliwa hatua zozote za kinidhamu,matokeo yake tumeyaona tena leo. Ni jukumu la Waziri na IGP kujiuzulu angalau kuonyesha huzuni yao kwa kitendo hiki cha aibu kwa Taifa letu.
   
 4. hovyohovyo

  hovyohovyo JF-Expert Member

  #4
  Sep 3, 2012
  Joined: Jul 8, 2012
  Messages: 540
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Wote tunatumikia matumbo yetu. Lakini ninapata shida kuelewa watu wengine wanvyoamua kuyatumikia matumbo yao. Watu wanalewa madaraka, wanasahau kuwa madaraka yao yana mwisho. Pili wanasababisha shida pia kwa wanafamilia wao na ndg na marafiki. Baba akilewa akajisaidia hadharani, ni aibu mpaka kwa mwanae. Tutaona mwisho wake.
   
 5. Companero

  Companero Platinum Member

  #5
  Sep 3, 2012
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,474
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Ana uhusiano wowote na Seth Kamuhanda?
   
 6. cjilo

  cjilo JF-Expert Member

  #6
  Sep 3, 2012
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 883
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 60
  Tena tukio hili limefanyika mbele yake, ila hapo kesho sitashangaa kusikia kuwa mwandishi huyo alijiandaa kufanya fujo katika mkutano huo kwani alikuja na vitu vinavyodhaniwa kuwa ni vya mlipuko(mabomu) ili kushindana na polisi na katika harakati za kumdhibiti ndipo mabomu yake hayo yalilipuka, mwandishi huyo anadaiwa kufanya uhalifu huo akishirikiana bega kwa bega na chadema ili kulichafua jeshi la polisi
  r i p mwandishi
   
 7. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #7
  Sep 3, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  To me all police are killers regardless their ranks and connection. Jeshi letu halina tofauti na wale Kamanyola wa Mboutu kule DRC wakati ule Zaire au jamaa wa Amin waliokuwa chini ya Isaack Maliamungu wakitesa na kuua waganda kama wadudu. Kikwete ni rais anayeingia kwenye vitabu vya historia kama goigoi aliyeruhusu kila mhalifu kujifanyia atakavyo. Kwanini wananchi wasimtegee huyu Kamuhanda siku moja na kumchoma moto? Watanzania tuamke na kupambana kwa ajili ya haki na uhai wetu.
   
 8. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #8
  Sep 3, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,552
  Likes Received: 1,898
  Trophy Points: 280
  Haya matatizo si ya kamanda mmoja mmoja.Huyu awajibishwe,lakini haina maana eti hao wengine ndo better,no way MKJJ,inaelekea hujawahi kutana na kashkash za hawa watu,ni wanyama balaa!Halafu hata kama hakupandishwa cheo,kuna namna amekuwa rewarded baada ya hayo mauwaji ya Ruvuma.Ndo utaratibu wao.We unaona huu ni unyama,ndani ya jeshi la polisi,huo ndo uchapaji kazi unaotakiwa.Respect and more status inatokana na mauwaji etc,na kufanya matakwa ya wanasiasa.Isipokuwa wanasiasa,wanafanya matakwa ya majambazi wakubwa.
  MKJJ,HAO WATU NI WABAYA NDUGU YANGU.Hili jeshi ni la kuvunjilia mbali ati.
   
 9. s

  sanga malua JF-Expert Member

  #9
  Sep 3, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 228
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  INGEKUWA zamani Nyerere angekemea uovu huu wa polisi na kuamru watafute njia mbadala za kukabiliana na waandamanaji wasio na silaha yoyote.unajua wakati wanakabilianana waandamanaji hawachukui tahadhari ya kulinda mabomu yao yasifyatuke.
   
 10. m

  mambomengi JF-Expert Member

  #10
  Sep 3, 2012
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 829
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Na hapo ndio mwisho wa story....mpaka mwi(we)engine watapouawa tena
   
 11. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #11
  Sep 3, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
  Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda akizungumza na wanahabari leo
  kuhusu sababu za kuzuia mkutano wa Chadema leo Mufindi


  [​IMG]
  Tumejipanga kwa lolote asema kamanda wa polisi kuwa si Chadema pekee hata CCM na vyama vyote marufuku mikutano wanaruhusiwa kufanya vikao vya ndani ili kupisha zoezi la sensa hadi jumamosi litakapomalizika

  Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda Baada ya kuua raia waliokuwa katika maandamano ya amani huko songea - Ruvuma hivi karibuni, amehamishiwa Iringa ambako ameua Mwenyekiti wa mwandishi wa habari akiwa kazini na vifaa vyake.
   
 12. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #12
  Sep 3, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  Hayati Daud Mwangosi siku ya tukio akiwa kazini mwenye suruari nyeupe na ameshika camera mkono, hakujua kama mauti yatamfika tena kwa unyama kama ule.
   
 13. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #13
  Sep 3, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Mkuu Mwanakijiji Polisi ya sasa,hii ya kutenda kazi kwa kutotumia weledi bali kwa lengo la kujipendekeza kwa chama tawala haitashangaza kuona Kamuhanda safari hii akapandishwa cheo c kuhamishwa mkoa tena
   
 14. i

  iseesa JF-Expert Member

  #14
  Sep 3, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 944
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Tukubali kuwa sisi wabongo ni waoga. Former IGP Mahita aliua wangapi Mwembechai na Zenj, na bado anadunda mitaani Moro?
   
 15. only83

  only83 JF-Expert Member

  #15
  Sep 3, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Tukubalianae jambo moja la msingi, kuna tatizo la msingi kwenye uongozi wa polisi na usalama wa Taifa. Ni kweli wamedhamiria kuvunja nguvu za upinzania hasa CHADEMA.
   
 16. PJ

  PJ JF-Expert Member

  #16
  Sep 3, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 297
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Tatizo ni kwamba tunao mapolisi ambao ni mbumbumbu. kwanza hawajaenda shule, pili wanafikiri kwa makalio yao na tatu hisia zao kuhusu thamani ya maisha haipo.

  Just imagine wale askari wa Misri ambao walikwa na vifaru kama wangelikuwa na akili kama za askari wa tanzania ambao hawajui thamani ya maisha wangeua watu wangapi?

  lakini kutokana na weledi wao walitumia silaha zile kulinda maisha ya wamisri ha hatimae Mubarak akanyosha mikono,

  Na walaaniwe wale wanaoua raia wa tanzania wasio na hatia na kuwaacha wajane na mayatima wakiteseka.

  Na yawakute kama yayo hayo ili wake zao nao wawe wajane na watoto wao mayatima.
   
 17. Mbaha

  Mbaha JF-Expert Member

  #17
  Sep 3, 2012
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 697
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  "Kamuhanda the Executioner" ... Nafikiri jina hilo litamfaa mkuu...
   
 18. REMSA

  REMSA JF-Expert Member

  #18
  Sep 3, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 2,569
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Ukubwa wa tumbo lake unaonyesha kuwa yupo kwa maslahi ya tumbo lake tu,maisha
  na uhalali wa watu wengine kuishi si muhimu kwake ni kama nzi tu"
   
 19. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #19
  Sep 3, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,314
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Polisi wa aina yake wanalitia doa jeshi la polisi. Ukimuangalia tu unagundua ni mtu mchovu wa akili, mwili na roho yake pia. Anafurahia nini kuua watu wasio na hatia maana kama mtu hajapelekwa mahakamani na kuhukumiwa huwezi kumuita ana hatia? Au yeye yuko juu ya sheria? JK hawa makamanda wako wanakutia doa...tunaanza kujiuliza wana uwezo kiasi gani kuwa makamanda wanaoweza kutoa amri kwa maaskari wadogo chini yao?
   
 20. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #20
  Sep 3, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,317
  Likes Received: 2,604
  Trophy Points: 280
  Polisi wanafanya wanachokijua kwa kuwa hakuna mahali wanapowajibika...
  Hiyo ndiyo kazi waliyoelekezwa kuifanya na wanaifanya kwa juhudi zote...
  Hakika wamesahau jukumu namba moja la Jeshi la Polisi...
  Nalo ni kulinda na kutetea haki za raia dhidi ya waovu na maovu...
   
Loading...