Kamanda Kamuhanda: 4 Songea, 1 Iringa

Damu ya mtu asiye na hatia inalia,haki inabanwa na wachache. Polisi wa Tanzania sawa na wale askari wa Afrika kusini waliowafyatulia risasi wachimbaji wa mgodi wa Marikana....utu wa Mtanzania uko wapi??maadili ya Jeshi la Polisi yako wapi?? Uwajibikaji wa RPC na Waziri uko wapi??...ama kweli ni heri mkoloni mweupe kuliko mweusi....RIP Mwangosi
 
Angalia lilivyo nenepa kama nini sijui, hata aibu halina, muuuaji mkubwa wewe

IMG_1875.JPG

Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda akizungumza na wanahabari leo
kuhusu sababu za kuzuia mkutano wa Chadema leo Mufindi

IMG_1878.JPG

Tumejipanga kwa lolote asema kamanda wa polisi kuwa si Chadema pekee hata CCM na vyama vyote marufuku mikutano wanaruhusiwa kufanya vikao vya ndani ili kupisha zoezi la sensa hadi jumamosi litakapomalizika

Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda Baada ya kuua raia waliokuwa katika maandamano ya amani huko songea - Ruvuma hivi karibuni, amehamishiwa Iringa ambako ameua Mwenyekiti wa mwandishi wa habari akiwa kazini na vifaa vyake.
 
Haya matatizo si ya kamanda mmoja mmoja.Huyu awajibishwe,lakini haina maana eti hao wengine ndo better,no way MKJJ,inaelekea hujawahi kutana na kashkash za hawa watu,ni wanyama balaa!Halafu hata kama hakupandishwa cheo,kuna namna amekuwa rewarded baada ya hayo mauwaji ya Ruvuma.Ndo utaratibu wao.We unaona huu ni unyama,ndani ya jeshi la polisi,huo ndo uchapaji kazi unaotakiwa.Respect and more status inatokana na mauwaji etc,na kufanya matakwa ya wanasiasa.Isipokuwa wanasiasa,wanafanya matakwa ya majambazi wakubwa.
MKJJ,HAO WATU NI WABAYA NDUGU YANGU.Hili jeshi ni la kuvunjilia mbali ati.

Mkuu, umeeleza vizuri isipokuwa hapo kwenye nyekundu. Kama unavyofahamu, jeshi linafanya kazi katika mazingira ya uongozi yaliyopo. Kwa miaka kadhaa sasa nchi yetu inaongozwa kimafia; kuanzia juu kwenda chini mwendo ni wa kifisadi. Mfumo mzima wa kiuchumi, kijamii na kisisasa umegubikwa na rushwa na wizi katika ngazi zote. Viongozi wa juu wanataka watu wanaoulinda na kuudumisha mfumo huo - hao ndio wanaozawadiwa! Kumbuka uteuzi wa IGP awamu ya tatu ulisukumwa na nini.

Ni wazi kuwa askari Polisi na wakuu wao wamekwishadokezwa na kuaminishwa kuwa mafanikio yao kikazi yatapatikana na kuimarika kwa kadri watakavyoonyesha umahiri wa kudhibiti wapinzani wa "establishment" iliyopo - haijalishi chama. Na kigezo hicho, hakuna ubishi, sasa kimetanuliwa kuruhusu cold blooded murders! Hapo, kwa kuvunjilia mbali jeshi hilo bila kuibomoa establishment iliyopo hujafanya kitu.
 
Jamani polisi mkiambiwa tumieni na akili zenu, hivi siku wananchi wakichachamaa tukaanza kuwindana mtasalimika? wengi mnaishi uraiani kama si nyie basi familia zenu ebu haya mauaji si suala la afya kabisa tutakuja kujuta mbele ya safari
 
Kweli mkuu hata mimi nikichangia sredi ya awali jioni,nimekumbuka kwamba huyu Kamanda aliongoza mauaji mengine Songea. Kwasababu hakuchukuliwa hatua zozote za kinidhamu,matokeo yake tumeyaona tena leo. Ni jukumu la Waziri na IGP kujiuzulu angalau kuonyesha huzuni yao kwa kitendo hiki cha aibu kwa Taifa letu.

Wote hawa wanatakiwa wanyongwe hadharani coz ni janga la kitaifa kuendelea kuwa na watu kama hawa
 
Mwananchi nao kwa uchonganishi itabid wajieleze kwanini wasifungiwe
 
Simshangai kamhanda,hayo yamepangwa,walianza na mwahalisi wakalfungia,sasa kwa waandishi wa habari walioko kwenye matukio.Alitekwa ulimboka,alitokea mtu kama Kamhanda,akasema kilichompata ULIMBOKA ni halali yake(Mganga wa jadi,MAJIMAREFU)na hisi wataendelea
 
Poleni watanzania wenzangu. Huku USA hali ya Democrasia imekuwa kwa kiasi kikubwa na hivi hayo ni yakawaida pindi yanapotokea. Lakini huko nyumbani ni matatizo matupu. Ila ndio tupo katika kipindi cha mpito. Yote hayo yatapita na tutakomaaa tu. Ila kwa hili Kamhanga yupo sahihi katika kutekeleza majukumu yao. Kumbuka Dola wana kwenda kwa amri tena amri ya mwisho ndio mara zote hufuatwa. Tatizo la baadhi ya Watanzania hawataki kukubali ukweli kwamba kuna wakati ukifika yapasa kutii dola. Mimi sijaona sana sababu ya M4C KUSHINDANA NA DOLA. Serikali ikisema yatupasa kusikiliza. Tukileta ubishi madhara yake ndo kama haya. Wenyewe wanasema "UTII WA SHERIA BILA KUSHURUTISHWA" Kwa kuwa hatutii sheria na sasa tunashurutishwa na kwenye kusurutishwa kunakuwa na matokeo mabaya ndo hayo sasa. Tujifunze kutii dola na si kulazimisha mambo. Poleni!
Poles kwa kuwa mtumwa wa fikra ooooh no Upo USA ya wapi? Maana ulivyoropoka kama huna kichwa vile
 
RPC Michale Kamanda brutal and serial killer still goes unnoticed,but one day in this country justice will prevail
 
THIS IS DISGUSTING!! A TOTAL OUTRAGE!!! This police officer's took an oath to protect this country and his citizen not KILLING people!.
That's why we will deal with cops our own way, they protect each others a$$es and Mabwana zao waliopo Ikulu. I h@te cops with passion​
.
These CCM or Police men know nothing about policy law, they are also in both sides law side and fully political which makes it impossible for them to do their job appropriately.

Its suppose to be Tanzania Police Services and not Tanzania Police Force. our society is being badly terrorized each day,

Poleni watanzania wenzangu. Huku USA hali ya Democrasia imekuwa kwa kiasi kikubwa na hivi hayo ni yakawaida pindi yanapotokea. Lakini huko nyumbani ni matatizo matupu. Ila ndio tupo katika kipindi cha mpito. Yote hayo yatapita na tutakomaaa tu. Ila kwa hili Kamhanga yupo sahihi katika kutekeleza majukumu yao. Kumbuka Dola wana kwenda kwa amri tena amri ya mwisho ndio mara zote hufuatwa. Tatizo la baadhi ya Watanzania hawataki kukubali ukweli kwamba kuna wakati ukifika yapasa kutii dola. Mimi sijaona sana sababu ya M4C KUSHINDANA NA DOLA. Serikali ikisema yatupasa kusikiliza. Tukileta ubishi madhara yake ndo kama haya. Wenyewe wanasema "UTII WA SHERIA BILA KUSHURUTISHWA" Kwa kuwa hatutii sheria na sasa tunashurutishwa na kwenye kusurutishwa kunakuwa na matokeo mabaya ndo hayo sasa. Tujifunze kutii dola na si kulazimisha mambo. Poleni!

Ni heri kwangu leo nimetembea na MSAMAHA mwingi sana!! Nimeshakusamehe... Nakushauri ukipata muda kidogo ujisomee historia ujue hiyo "Democrasia" ya "huku USA" ilifikaje hapo ilipo.
 
inauma sana lakini Mungu ndie ajuaye jinsi gani tunauwawa bila makosa kisa wanatimiza matakwa ya wakubwa zao
 
He is probably hunting the top post (IGP) Nilimskiliza alipokuwa anahojiwa na waandishi wa Ch. 10, hata kuongea kwake ni mtu mmoja bure buresh kbs..

CV yake ipo? Na waliosoma naye wananena yapi? Kwa kumwangalia machoni anaonekana mtu wa bangi na unga kabisa. Macho mekundu kama ya faru!!! Muuaji huyo. Hivi ana familia? Watoto wako wapi? Wanasoma au kuajiriwa? Wako Tanzania hii au wapi? tuwafahamu tu!!
 
IMG_1875.JPG

Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda akizungumza na wanahabari leo
kuhusu sababu za kuzuia mkutano wa Chadema leo Mufindi

IMG_1878.JPG

Tumejipanga kwa lolote asema kamanda wa polisi kuwa si Chadema pekee hata CCM na vyama vyote marufuku mikutano wanaruhusiwa kufanya vikao vya ndani ili kupisha zoezi la sensa hadi jumamosi litakapomalizika

Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda Baada ya kuua raia waliokuwa katika maandamano ya amani huko songea - Ruvuma hivi karibuni, amehamishiwa Iringa ambako ameua Mwenyekiti wa mwandishi wa habari akiwa kazini na vifaa vyake.

ila fiesta ruksa mkuu si ndio maake na ulinzi unakuwepo ati ahahaha...au??
 
ila fiesta ruksa mkuu si ndio maake na ulinzi unakuwepo ati ahahaha...au??

03.jpg

Pamoja na hayo, CCM walikuwa na mkutano mkubwa kwenye ufunguzi wa Kampeni za uchaguzi huko Unguja kama inavyoonyeshwa katika picha hiyo jana.
 
Back
Top Bottom