Kama wewe ndio huyu doctor ungefanyaje ...!?

jibu nimekupa... itadepend na faida za huyo husband... huwez ukaamua kufanya kitu bila kukitafakari na kujipa reasons za kufanya hivyo... the problem with you hutaki plan B wala kutafakari kwanza.... it will depend.... mume akiwa kama Nicas Mtei inabidi tu nimrestishe in peace...

Hahahahahaahahaah jinga wee.
 
Last edited by a moderator:
Kwa hiyo wewe Eiyer unataka sote tuseme kile ambacho unakitaka wewe? Ambao hatusemi ndio hatujakuelewa? Au unataka kubisha tu? Ubishi wako hauna kichwa wala miguu. Umekaa kitoto tu.

Inawezekana ukawa kweli lakini kitakachokufanya uwe mkweli sio kile ambacho unakisema bali sababu unazotoa

Umeshindwa kuielewa mada ndio mana unaandika vitu ambavyo havihusiani na mada

Hapa sijataka maoni ya njia gani ichukuliwe kuhusiana na suala la ugaidi

Hapa nimeuliza na nilichouliza ni situation iliyomkumba daktari

Hapo wewe ulitakiwa kujibu maamuzi utakayochukua na si vinginevyo

Siwezi kumlazimisha yoyote chochote bali nawaambia wale wanaotoka nje ya mada warudi kwenye mada

Angalia wote waliojibu nilichouliza kama nimewapinga

Kwa mfano tazama post ya ICHANA ndio utajua ninachomaanisha hapa

Masuala ya utoto ni wewe unataka kuyaleta kwasababu watoto ndio wanafanya mambo bila kujali msingi wa wanachokifanya na hapa wewe ndio umetoka nje ya msingi wa tunachokifanya hivyo wewe ndie mwenye mambo ya kitoto!
 
Last edited by a moderator:
Tuchukulie kuwa wewe ni daktari mkuu wa eneo fulani na upo kwenye ndoa

Siku moja ukiwa kazini unasikia habari za kigaidi eneo husika kuwa kutokana na habari za kiintelijensia kuna mahali limetegewa bomu na inasemekena ni eneo na mkutanyiko wa watu wengi ila hawajui ni wapi,lakini baada ya muda mfupi unapokea simu kutoka kwa kiongozi mkuu wa eneo husika kuwa wanausalama wamefanikiwa kumkamata mtu mmoja ambae anahusika na njama hizo za kigaidi na katika harakati za wanausalama kumkamata walimjeruhi sehemu za kifuani na amevuja damu sana na alikuwa amekubali kuwatajia eneo bomu lilipotegwa na alikuwa amesema kuwa ni shule moja ya chekechea

Lakini kabla ya kuitamka ni shule gani akawa amepoteza fahamu na alisema kuwa bomu hilo litalipuka baada ya dakika 45 hivyo wanakimbizana na muda na yupo njiani na mkuu alitaka wewe uendeshe zoezi la kumtibu na kumrudishia fahamu ili aitaje shule husika lilipotegwa bomu ili likateguliwe na kusalimisha maisha ya watoto hao

Lakini wakati unakata simu unapokea simu nyingine ikikujulisha kuwa mwenzi wako wa ndoa [mke/mume] amepata ajali mbaya sana na yupo njiani kuletwa hapo kazini kwako [hospital] kwaajili ya matibabu na unajulishwa kuwa hali yake sio nzuri kabisa

Kwa bahati sijui mbaya au nzuri wagonjwa wote hawa wawili wanafika hospital kwa pamoja na kwa kuwatazama unaona wote wako mahututi na kwa namna ambayo wameumia ni lazima wapelekwe "thieta" kwa upasuaji na kibaya zaidi daktari bingwa wakufanya hiyo kazi uko peke yako hakuna mwingine

Lakini kikubwa zaidi huwezi kuwafanyia wote kwa pamoja,yaani ni lazima uanze na mmoja na maamuzi yoyote yale utakayofanya utakuwa unahatarisha maisha au uhai wa mmoja kwa namna wote walivyojeruhiwa na matukio yao

Sasa hebu niambie,kama wewe ndio daktari huyu utachagua kumhudumia mgonjwa gani hapa?

Nijibu halafu nitakuja kuwapa sababu ya kuleta hiki kisa hapa ..........
Mtambuzi nakusalimu popote ulipo ......!!

[h=3]BREAKING NEWS:"WANAFUNZI CHUO KIKUU CHA SOKOINE-MOROGORO WAGOMA TENA"[/h]
 
Hahahaha hebu fikiria siku ya pili yake magazeti, redio, Tv na mitandao yote inatoa habari yangu. Ninapambwa kwa kila namna, nyimbo za kunisifu huko uso wangu ukionyesha matumaini makubwa ila moyoni nateketea kwa kumkosa mke wangu, moyoni sina amani, dunia inakuwa chungu, donge limenikaa moyoni...... sina maisha tena!

hahaha , nakupendaje
 
Hii kitu hapa chini mbaya sana .......

smoking-pot.jpg
 
hahaa...kuna somo moja nilijifunza miaka ya nyuma kidogo juu ya namna ya kuua kwa kukusudia bila kujutia, kwa manufaa ya jambo flan....kwa case kama hii ambayo ni ndogo sana unaweza kuangalia tu uzito wa jambo uko wapi na hivyo ukatenda kulingana na uzito wa jambo lililo mbele yako...kwa hiyo kwa ajili ya ''amani ya yerusalem'' mkeo itabidi awekwe kwanza pembeni kwa manufaa ya wengi....

ngoja nikuulize swali mleta mada japo naweza kutoka nje ya mada yako: ikitokea kuna watu wanamtafuta rafiki yako wa karibu ili wamuue na rafiki yako akaja kwako kujificha na akakwambia kama hao jamaaa(wauwaji) watakuja kwako kumtafuta basi waambie hayupo hujamuona..baada ya mda wauwaji wakafika kwako na kuuliza kama mtu flani yuko hapo kwako na wewe ukawaambia hayupo..hivi unadhani kwa jibu lako hilo nafsi yako inaweza kujuta kuwa umefanya dhambi kwa kusema uongo?....(ukijifunza juu ya misleading truth, outright lie, etc utajua kwa undani juu ya mada hizi)

au jambo lingine nikuulize mnasafiri ndani ya chombo ndani ya bahari mara ghafla mkapigwana dhoruba kali sana kiasi cha kutupa baadhi ya mizigo baharini ili kujinusuru yakiwemo maji ya kunywa...baada ya mda dhoruba ikaisha lakini mkawa mmepoteza uelekeo na hmna maji wala chakula...maji ya baharini hayafai kunywa binadam maana yana chumvi ..mmoja wenu ndani ya chombo kiu kikamzidi sana na akaamua kunywa maji ya bahari akidhani atamaliza kiu lakini kumbe anaongeza tatizo...baada ya kunywa maji hayo hali yake ikazidi kuwa mbaya sana na akadhoofika kweli...ikafika mahali akasema kwa kinywa chake yeye mwenyewe kuwa anatamani kufa na kisha akachukua kisu akajichoma...
ile damu yake mkainywa ninyi mliobaki na nyama ya mwili wake mkala kwa siku tatu hadi pale mlipookolewa na chombo kingine kilichokuwa kinapita...hivi nafsi yako inaweza kujuta kwa kula nyma ya yule bwana na kunywa damu yake?..

kwa hiyo kuna mambo hufanyika japo kwa wengi yataonekana ni mabaya lakini manufa ayake ni makubwa na mazuri kwa faida ya wengi...

kwa mada yako somo letu la philosophy ndani yake kulikuw ana topic inayosema ''the moral side of murder''.....ndani yake kulikuwa na mifano mingi sana na mmoja wa mifano hiyo ni kama huo uliotuoa hapo kwenye thread yako...
 
Wengine wangekuwa wanaelewa kama wewe ingekuwa rahisi sana kuelewa maamuzi ya watu

Watu wanatafuta justification kwa kuhofia kuboronga kwenye maamuzi yao

Sasa ICHANA ,ungemuacha honey "adedi" hivi hivi?

who told u anaded??

kwanini uangalie jamii kwenye maamuzi yko?
kwa upande wangu ninemwacha MUNGU ndiye angenilindia
 
Mada inakutaka ukumbuke ya zamani au ufanye nini?

Enzi hizo tulikuwa tunapewa assignment ya kusoma aya katika kitabu cha mtunzi wa kiafrika (African Writers) halafu munaandaa onyesho. Basi mambo yalikuwa ni kujipanga vizuri tu na kutekeleza.
 
Tuchukulie kuwa wewe ni daktari mkuu wa eneo fulani na upo kwenye ndoa

Siku moja ukiwa kazini unasikia habari za kigaidi eneo husika kuwa kutokana na habari za kiintelijensia kuna mahali limetegewa bomu na inasemekena ni eneo na mkutanyiko wa watu wengi ila hawajui ni wapi,lakini baada ya muda mfupi unapokea simu kutoka kwa kiongozi mkuu wa eneo husika kuwa wanausalama wamefanikiwa kumkamata mtu mmoja ambae anahusika na njama hizo za kigaidi na katika harakati za wanausalama kumkamata walimjeruhi sehemu za kifuani na amevuja damu sana na alikuwa amekubali kuwatajia eneo bomu lilipotegwa na alikuwa amesema kuwa ni shule moja ya chekechea

Lakini kabla ya kuitamka ni shule gani akawa amepoteza fahamu na alisema kuwa bomu hilo litalipuka baada ya dakika 45 hivyo wanakimbizana na muda na yupo njiani na mkuu alitaka wewe uendeshe zoezi la kumtibu na kumrudishia fahamu ili aitaje shule husika lilipotegwa bomu ili likateguliwe na kusalimisha maisha ya watoto hao

Lakini wakati unakata simu unapokea simu nyingine ikikujulisha kuwa mwenzi wako wa ndoa [mke/mume] amepata ajali mbaya sana na yupo njiani kuletwa hapo kazini kwako [hospital] kwaajili ya matibabu na unajulishwa kuwa hali yake sio nzuri kabisa

Kwa bahati sijui mbaya au nzuri wagonjwa wote hawa wawili wanafika hospital kwa pamoja na kwa kuwatazama unaona wote wako mahututi na kwa namna ambayo wameumia ni lazima wapelekwe "thieta" kwa upasuaji na kibaya zaidi daktari bingwa wakufanya hiyo kazi uko peke yako hakuna mwingine

Lakini kikubwa zaidi huwezi kuwafanyia wote kwa pamoja,yaani ni lazima uanze na mmoja na maamuzi yoyote yale utakayofanya utakuwa unahatarisha maisha au uhai wa mmoja kwa namna wote walivyojeruhiwa na matukio yao

Sasa hebu niambie,kama wewe ndio daktari huyu utachagua kumhudumia mgonjwa gani hapa?

Nijibu halafu nitakuja kuwapa sababu ya kuleta hiki kisa hapa ..........
Mtambuzi nakusalimu popote ulipo ......!!

Kama huyo daktari ni UKAWA atamtibu kwanza huyo jamaa aliyejeruhiwa na bomu ili ataje shule, si unajua UKAWA umma kwanza mimi baadaye. lakini kama ni INTERAHAMWE atamtibu kwanza mkewe, si unajua, sisi kwanza wao baadaye!
 
Umewaza mbali sana

Lakini,vipi kama hautafukuzwa kazi?

OOOhhh u are wrong nakubaliana na Khantwe hawezi kufukuzwa kazi kwanni uangalie hisia??unafanya kazi kutokana na sheria zake.lazima gaid atibiwe ili tuokoe maisha ya walio wengi mke/mume atafuata mkuu

mkuu Eiyer kumbuka simu ya kwanza uliopokea ilikuwa ya watu wa usalama kwa ajili ya gaid

je kwann uanze kumtibu mkeo???
 
Last edited by a moderator:
"Simu kutoka kwa kiongozi mkuu wa eneo husika.....

Sasa kumbe eneo husika linajulikana basi,wanausalama wakadili nalo hilo eneo kuakikisha waliopo wanatoka salama

Mimi naangalia afya ya MKE wangu ati...
 
Tuchukulie kuwa wewe ni daktari mkuu wa eneo fulani na upo kwenye ndoa

Siku moja ukiwa kazini unasikia habari za kigaidi eneo husika kuwa kutokana na habari za kiintelijensia kuna mahali limetegewa bomu na inasemekena ni eneo na mkutanyiko wa watu wengi ila hawajui ni wapi,lakini baada ya muda mfupi unapokea simu kutoka kwa kiongozi mkuu wa eneo husika kuwa wanausalama wamefanikiwa kumkamata mtu mmoja ambae anahusika na njama hizo za kigaidi na katika harakati za wanausalama kumkamata walimjeruhi sehemu za kifuani na amevuja damu sana na alikuwa amekubali kuwatajia eneo bomu lilipotegwa na alikuwa amesema kuwa ni shule moja ya chekechea

Lakini kabla ya kuitamka ni shule gani akawa amepoteza fahamu na alisema kuwa bomu hilo litalipuka baada ya dakika 45 hivyo wanakimbizana na muda na yupo njiani na mkuu alitaka wewe uendeshe zoezi la kumtibu na kumrudishia fahamu ili aitaje shule husika lilipotegwa bomu ili likateguliwe na kusalimisha maisha ya watoto hao

Lakini wakati unakata simu unapokea simu nyingine ikikujulisha kuwa mwenzi wako wa ndoa [mke/mume] amepata ajali mbaya sana na yupo njiani kuletwa hapo kazini kwako [hospital] kwaajili ya matibabu na unajulishwa kuwa hali yake sio nzuri kabisa

Kwa bahati sijui mbaya au nzuri wagonjwa wote hawa wawili wanafika hospital kwa pamoja na kwa kuwatazama unaona wote wako mahututi na kwa namna ambayo wameumia ni lazima wapelekwe "thieta" kwa upasuaji na kibaya zaidi daktari bingwa wakufanya hiyo kazi uko peke yako hakuna mwingine

Lakini kikubwa zaidi huwezi kuwafanyia wote kwa pamoja,yaani ni lazima uanze na mmoja na maamuzi yoyote yale utakayofanya utakuwa unahatarisha maisha au uhai wa mmoja kwa namna wote walivyojeruhiwa na matukio yao

Sasa hebu niambie,kama wewe ndio daktari huyu utachagua kumhudumia mgonjwa gani hapa?

Nijibu halafu nitakuja kuwapa sababu ya kuleta hiki kisa hapa ..........
Mtambuzi nakusalimu popote ulipo ......!!

Ingekua mm ndo doctor ningemshauri mkuu wa polisi watoe alert kwa shule zote za chekechea ziwe evacuated effective immediately while i am busy trying to revive the thug atleast azinduke na kutoa informations ambazo ni nyeti katika usalama wa taifa. Mke wangu (in this case mume wangu) ningekubali tu afe coz i know i'ld be saving a lot more lives by letting her die and save the thugs life. Na pia nikifanikiwa kumtibu huyo jambazi na akapona atakua ni asset kubwa kwa usalama wa taifa coz watamtumia kupata njamaa zinginezo za kuiteketeza nchi. That is what we call making sacrifices.
 
Namtibu mke wangu... shule zifungwe ghafla watoto wakimbie home...
 
maswali mengine ni kutiana majaribuni!ni sawa na mkeo kukuuliza kama unampenda!!
 
Namtibu mke wangu... shule zifungwe ghafla watoto wakimbie home...

under consequential reasoning, categorical moral of principals and also under the theory of utilitarianism which is the balance of pleasure over pain,happiness over suffering: by treating your wife you will be totally wrong bro!
 
Aa wapi... hizo principles huko huko... mke wangu kwanza
 
Back
Top Bottom