Kama wewe ndio huyu doctor ungefanyaje ...!?

Eiyer

JF-Expert Member
Apr 17, 2011
28,268
2,000
Tuchukulie kuwa wewe ni daktari mkuu wa eneo fulani na upo kwenye ndoa

Siku moja ukiwa kazini unasikia habari za kigaidi eneo husika kuwa kutokana na habari za kiintelijensia kuna mahali limetegewa bomu na inasemekena ni eneo na mkutanyiko wa watu wengi ila hawajui ni wapi,lakini baada ya muda mfupi unapokea simu kutoka kwa kiongozi mkuu wa eneo husika kuwa wanausalama wamefanikiwa kumkamata mtu mmoja ambae anahusika na njama hizo za kigaidi na katika harakati za wanausalama kumkamata walimjeruhi sehemu za kifuani na amevuja damu sana na alikuwa amekubali kuwatajia eneo bomu lilipotegwa na alikuwa amesema kuwa ni shule moja ya chekechea

Lakini kabla ya kuitamka ni shule gani akawa amepoteza fahamu na alisema kuwa bomu hilo litalipuka baada ya dakika 45 hivyo wanakimbizana na muda na yupo njiani na mkuu alitaka wewe uendeshe zoezi la kumtibu na kumrudishia fahamu ili aitaje shule husika lilipotegwa bomu ili likateguliwe na kusalimisha maisha ya watoto hao

Lakini wakati unakata simu unapokea simu nyingine ikikujulisha kuwa mwenzi wako wa ndoa [mke/mume] amepata ajali mbaya sana na yupo njiani kuletwa hapo kazini kwako [hospital] kwaajili ya matibabu na unajulishwa kuwa hali yake sio nzuri kabisa

Kwa bahati sijui mbaya au nzuri wagonjwa wote hawa wawili wanafika hospital kwa pamoja na kwa kuwatazama unaona wote wako mahututi na kwa namna ambayo wameumia ni lazima wapelekwe "thieta" kwa upasuaji na kibaya zaidi daktari bingwa wakufanya hiyo kazi uko peke yako hakuna mwingine

Lakini kikubwa zaidi huwezi kuwafanyia wote kwa pamoja,yaani ni lazima uanze na mmoja na maamuzi yoyote yale utakayofanya utakuwa unahatarisha maisha au uhai wa mmoja kwa namna wote walivyojeruhiwa na matukio yao

Sasa hebu niambie,kama wewe ndio daktari huyu utachagua kumhudumia mgonjwa gani hapa?

Nijibu halafu nitakuja kuwapa sababu ya kuleta hiki kisa hapa ..........
Mtambuzi nakusalimu popote ulipo ......!!
 

Suprise

JF-Expert Member
Nov 2, 2012
2,697
2,000
mmmh ngumu kumtoa kafara mkeo kisa bomu la shule ila hata ingekua si bomu mkeo kumtibu ngumu akiwa na hali hiyo mwisho wa siku watakufa wote
 

Eiyer

JF-Expert Member
Apr 17, 2011
28,268
2,000
mmmh ngumu kumtoa kafara mkeo kisa bomu la shule ila hata ingekua si bomu mkeo kumtibu ngumu akiwa na hali hiyo mwisho wa siku watakufa wote

Nimeshindwa kuelewa hiki ulichokiandika hapa!
 

Suprise

JF-Expert Member
Nov 2, 2012
2,697
2,000
Ingekuwa na kauzito kama shule hiyo ndo kanasoma katoto kako afu kamoja then mkeo alishathibitishwa kuwa hawezi kuzaa tena! Mmmmh! Majanga!!

kama nakuona vile, mke afe ntazaa kwengine if nid arise
 

Eiyer

JF-Expert Member
Apr 17, 2011
28,268
2,000
Ingekuwa na kauzito kama shule hiyo ndo kanasoma katoto kako afu kamoja then mkeo alishathibitishwa kuwa hawezi kuzaa tena! Mmmmh! Majanga!!

Either way bado ina uzito

Watoto zaidi ya 50 vs Mumeo!
 

Kaunga

JF-Expert Member
Nov 28, 2010
12,564
2,000
Kwanza hauruhusiwi kumfanyia upasuaji mke/mume/mtoto wako maana unakuwa emotional kiasi cha kuweza kuhatarisha maisha yake kwa kushindwa kuwa objective.

Lakini siku zote families come first. Na pia technically kumrudisha fahamu mtu aliyepoteza fahamu ndani ya nusu saa inaweza isiwezekane. So watu wa usalama wanatakiwa wawe na more than one plan. Shule za chekechea haziwezi kuwa 300. So wanaweza wakajigawa na kucover maeneo yote au baadhi baada ya kuangalia facts zingine.
 

NJALI

JF-Expert Member
Jan 9, 2014
1,536
2,000
Okoa maisha ya wengi poteza ya mmoja, namtibu mtuhumiwa kisha mke anafuata. Maana nitakuwa nimeokoa maisha ya watu wengi kwa kumtoa sadaka mmoja. Wakongwe wa kuendesha mabasi wanajua hili, bora ukanyage mtu moja au wawili kuliko kuliangusha basi likau wengi zaidi.
 

lumanyisa

JF-Expert Member
Oct 2, 2012
887
500
bomu linalipuka baada ya dk 45 na mgonjwa kapoteza fahamu,afanyiwe upasuaji ili aseme bomu lilipo.ataamka muda upi? upasuaji dakika ngapi? hawi sedated?.....mgonjwa wa bomu acha tu afe kwani muda hauruhusu.ukimsaidia wa bomu dk 45 zitaishia kwenye upasuaji na mkeo atakufa na bomu litalipuka.
 

Eiyer

JF-Expert Member
Apr 17, 2011
28,268
2,000
Kwanza hauruhusiwi kumfanyia upasuaji mke/mume/mtoto wako maana unakuwa emotional kiasi cha kuweza kuhatarisha maisha yake kwa kushindwa kuwa objective.
Hili hapa sio mahala pake bana
Lakini siku zote families come first.
Siku zote zipi dear?
Hebu acha hadithi bana
Na pia technically kumrudisha fahamu mtu aliyepoteza fahamu ndani ya nusu saa inaweza isiwezekane.
Sio kweli

Lakini pia uchaguzi wa jambo ambalo ni sahihi ndio cha msingi hapa [kumbuka sijasema kipi cha msingi]
So watu wa usalama wanatakiwa wawe na more than one plan.
More than the plan kwenye situation hii kweli?
Yaani unatoa hii option kwenye mazingira haya ya dakika 45 kweli Kaunga?

I thought your better than that!!
Shule za chekechea haziwezi kuwa 300. So wanaweza wakajigawa na kucover maeneo yote au baadhi baada ya kuangalia facts zingine.
Unazungumzia wapi wewe?

Wafanye hayo kwa muda huo kweli?

Halafu hii ni kutafuta excuse kwenye mambo ambayo yanatakiwa maamuzi ya msingi
Hapo ni kufanya uchaguzi tu baasi hizi sababu zako hazitakiwi na zinakuongezea maswali tu!

Hebu acha zako bana!
 

Eiyer

JF-Expert Member
Apr 17, 2011
28,268
2,000
Okoa maisha ya wengi poteza ya mmoja, namtibu mtuhumiwa kisha mke anafuata. Maana nitakuwa nimeokoa maisha ya watu wengi kwa kumtoa sadaka mmoja. Wakongwe wa kuendesha mabasi wanajua hili, bora ukanyage mtu moja au wawili kuliko kuliangusha basi likau wengi zaidi.

Nimejifunza kitu kwenye maelezo yako haya!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom