Binafsi ntamtibu gaidi kwanza ili niokoe roho za watoto walio wengi....maana matokeo ya kumtibu mume na kumwacha jambazi unaweza kupoteza kazi yako kwani utaonekana unafanya kazi kwa kuongozwa na hisia hata jamii haiwezi kukuelewa hata kidogo....wacha mmoja aende wengi wapone
Kwanini ulizizungumzia kwenye post yako?
We unafahamu maana ya dakika 45? Kama ndio kwa nini umezizungumzia kwenye post yako?
Back to topic, Dk 30 zinatosha kabisa ku evacuate hao watoto kwa kuwa ameshataja kuwa katega kwenye shule, angekuwa hajataja kabisa, hapo angepata matibabu
Umenikumbusha mkuu
Kwanini roho inakusuta mkuu?
kuwatoa watoto katika shule zote kwa wakati inawezekana tu kwa nchi zilizoendelea ambazo zina mifumo bora ya mawasiliano. kuna shule ngapi za chekechea hapa mjini? je shule zote zitapata taarifa kwa muda muafaka? sikatai kwamba kuwaondoa shuleni ni muhimu lakini pia kwa nafasi yako kama daktari unapaswa kufanya jambo. utafanya maamuzi yapi?
kwenye hii mizani waweke na watoto zaidi ya 50!
nafikiria... Nipo ndani ya chumba cha upasuaji nina vifaa vyote. Nipo bize kumtibu gaidi (soma kwa msisitizo gaidi) kitanda cha kando amelazwa mke wangu kipenzi (soma kwa msisitizo kipenzi) anahangaika roho yake ipo rehani. Nje ya chumba kuna maaskari, viongozi wakubwa na waandishi wa habari wote wanasubiri taarifa kutoka kwangu juu ya hali ya gaidi na sio mke wangu!... Inahitaji moyo wa ujasiri nitaendelea kumtibu gaidi kwa kuwa endapo sitomtibu basi nitaangamiza maisha ya watoto zaid ya 300 na kamwe sitokuja kuisamehe nafsi yangu. Endapo watoto wataokolewa na mke wangu kufariki basi naamini mke wangu ataenda moja kwa moja peponi na hakika atakaa huko kwa amani akinisubiri niende nikaungane nae.
Usiende nje ya box
Unatakiwa ubaki kwenye maamuzi ya utakachochagua hapo na sio kitu kingine
Ungechagua kumtibu yupi?
sawa, ngoja niwe na subira
Mkuu,hakuna muda wa kushauriana hapo
Tangu atoe hiyo taarifa hadi anafikishwa hospital kwako muda ushapita na kitendo cha kuendelea kuzungumza ni kupoteza muda!
Nafikiria... Nipo ndani ya chumba cha upasuaji nina vifaa vyote. Nipo bize kumtibu gaidi (soma kwa msisitizo GAIDI) kitanda cha kando amelazwa mke wangu kipenzi (soma kwa msisitizo KIPENZI) anahangaika roho yake ipo rehani. Nje ya chumba kuna maaskari, viongozi wakubwa na waandishi wa habari wote wanasubiri taarifa kutoka kwangu juu ya hali ya gaidi na sio mke wangu!... inahitaji moyo wa ujasiri nitaendelea kumtibu gaidi kwa kuwa endapo sitomtibu basi nitaangamiza maisha ya watoto zaid ya 300 na kamwe sitokuja kuisamehe nafsi yangu. Endapo watoto wataokolewa na mke wangu kufariki basi naamini mke wangu ataenda moja kwa moja peponi na hakika atakaa huko kwa amani akinisubiri niende nikaungane nae.
umeongeaje kwa hisia ila ndo unafiki ndani yake