Kama unasumbuliwa na panya pitia hapa

Kama unasumbuliwa na panya pitia hapa

Usidanganywe indocide ni salama ikiwa kwenye capsule zake tu nje ya hapo ni sumu kama sumu zingine na hasa ikiingia mfano kwenye kidonda au sehemu ulipojikata hata uuzaji wake mpaka uwe na cheti cha dactari ndio unauziwa.

Ila ni sumu nzuri sana kwa panya na wakifa hawanuki

Mkuu kwenye ununuaji sio kweli mkuumbona tunazinunua tu fresh kabisa
 
Ila kama unasumbuliwa na panya vitu vya kufanya:
1. Dhibiti njia/nyufa zote
2. Mabaki ya vyakula
3. Uhifadhi mzuri wa vyakula
4. Tunza sehemu thabiti nyaraka zote
5. Tunza vizuri nguo

Hapo ndio ufanye maarifa ya kuweka mitego yako, bila ya hivyo unajisumbua.
Indocid ni nzuri sana kwenye kuulia panya, anakauka bila kuyoa harufu kali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Je umekuwa ukisumbuliwa na panya sana?

Je umetumia pesa sana kununua sumu za panya bila mafanikio?

Kama jibu ni ndiyo basi soma na ufanye hivi;

Nenda duka la dawa nunua dawa inaitwa INDOCID (indomethacin 25 mg capsules) halafu katege kama unavyotegaga sumu nyingine za unga za panya. Baada ya siku 4-5 matokeo utakayoyapata naamini mwenyewe utaleta mrejesho

Dawa hii hutumiwa na binadamu kama dawa zingine tu ila kwa panya ni sumu kwani wakishakula utaona siku ya nne panya wanakufa na wengine wanashindwa kutembea kwa kusagika sagika mifupa

Kama una jirani yako mshauri naye atumie maana muda mwingine waweza kuta unahangaika kumbe wanahamia kutoka nyumba ya pili

Dawa hii inaepusha gharama kwani pakiti ya buku (tembe 10) unaweza tega mara kadhaa bila kuimaliza pia ni salama kabisa wakati wa kutega kwani siyo sumu kwa binadamu

mkuu mimi kwangu kuna shida ya panya mmoja tu!
ubaya panya huyu anakula nyaya za umeme tu na soksi, nishatega nyanya, samaki nazikuta vile vile ila nikinunua soksi tu, yeye aichukua moja inabaki moja tu!

nifanyaje!
 
Hahahqhq
Ahhh aseeh kwenye sabufa yangu pale kweny lile tobo aliingia nikiwa namuona kabisa ilikuwa mchana basi ilikuwa on nikaweka bluetooth nikatafuta nyimbo yenye mdundo wa maana alafu nikaongezaaaa sauti volume hadi mwisho nikapita kinyuma nyuma nikaziba kwa haraka lile tundu na nguo kisha nika play [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] nilimchangamsha niliplay nyimbo tano zenye mdungo mkubwa kisha nikatoa tambara alitoka anatembea kama mlevi nikamalizia kuua saafi
 
Tahadhari iliwekwa. Nikafungia mbwa na kuku ndani. Huyu mtoto kaamka sijui kajisahau au ni wenge. Kafungulia kuku. Kuna mambo yanatokea unaweza piga mtu ila unaishia kusonya tu.
Pole sana mkuu. Hawa wanaoitwa wasichana wa kazi mimi mara nyingi huwa siwaamini sana. Hawako makini kabisa. Kuna mifano mingi sana ya uzembe wanaofanya.
 
Mimi alikaa kwenye sofa, anatoka usiku mchana anakausha unamsikia anavyohangaika.

Muda ukaenda akatanuka nakuongezeka size..... Kunasiku anatembea kwenye sofa namsikia anavyojipenyeza..... Aiseee nilipiga ngumi, vipepsi na mateke lile eneo alipo hadi akaanza kupiga ukunga....

Aisee nilitandika ngumi za maana hadi akatulia baada ya siku mbili nikaanza kusikia harufu ya mzoga nikajua tayari....
Nimecheka sana AKAANZA KUPIGA UKUNGA
 
Panya hujificha juu darini na kushuka chini kupata misosi au kuzaa/kulea.

Ukiiziba dari vizuri kwa singibodi au jipsam unakuwa umekata mzizi wa fitna.

Hapo akibaki juu lazma afe kwa njaa au ahame na akishuka chini unamkamata kilaini.

**penye panya wengi ni salama zaidi, hamna nyoka hapo mahali.
Nyoka wanafuata panya.

Usishangae ukawa unaishi na mzee sneki shadow miaka yote mnapishana kwa timing tu
 
Back
Top Bottom