Kama tunataka kukimbia na kutoka hapa tulipo katika kundi moja na waafrika wenzetu tunahitaji mfumo wa China

Mto Songwe

JF-Expert Member
Jul 17, 2023
6,028
12,352
Kama tupo serious tunataka kutoka hapa tulipo katika umasikini huu tunahitaji zaidi mfumo wa China.

Kama kweli tunataka kukimbia kwa kasi tunahitaji zaidi mfumo wa China kuliko wakati wowote ule.

Ubaya wa huu mfumo

hauhitaji watu wazembe,

hauhitaji wanasiasa wenye maneno mengi na wapiga kelele,

Hauhitaji bunge la wapiga kelele na kupotezana muda mrefu kujadiliana mambo yasiyo ya msingi au ya msingi,

Hauhitaji wanasiasa waongeaji sana kuliko watendaji,

Hauhitaji watu wasio na akili sawa kuongoza watu unahitaji wale walio bora zaidi.

Mpaka sasa hakuna taifa duniani lililo tumia muda mfupi zaidi duniani kupata ukuaji mkubwa wa kiuchumi kushinda China.

Jambo lililo wahitaji mataifa mbalimbali duniani miaka zaidi ya 100 kufanikisha China wamelifanikisha ndani ya miaka 40.

Tuchague moja kunyoa au kusuka ila kumbuka Tanzania ni masikini wa kutupwa na njia pekee ya kujitoa kwa kasi huku tulipo ni kukanyaga walipo kanyanga wachina.
 
Back
Top Bottom