Afrika inanufaika na ujenzi wa China yenye nguvu katika mtandao wa internet

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,035
cvbcxbxcb.png
Tarehe 27, Februari, mwaka 2014, rais Xi Jinping wa China alitoa dira ya "kujenga nchi kuwa na nguvu katika sekta ya mtandao wa internet". Katika muongo mmoja uliopita, China imejizatiti katika utekelezaji wa dira hiyo na kupata mafanikio makubwa, iwe katika upatikanaji wa huduma za internet au maendeleo ya sekta za ubunifu kama vile akili bandia.

Kadiri sauti na ushawishi wa China kimataifa unavyoongezeka, dhana, mapendekezo na mipango iliyopendekezwa na China katika sekta hiyo pia imetambuliwa na nchi nyingi zaidi, hasa "dunia ya kusini" ikiwa ni pamoja na Afrika.

Katika miaka ya hivi karibuni, China imetoa wito wa kupunguza pengo la kidijitali duniani mara nyingi baada ya kuona kwamba sekta ya mtandao wa internet inashuhudia maendeleo thabiti lakini yasiyo na usawa. Ikilinganishwa na nchi za Magharibi, "dunia ya kusini", hasa Afrika inakabiliwa na pengo kubwa zaidi la kidijitali kuliko miaka iliyopita.

Wakati teknolojia ya kidijitali na uchumi inapohusiana kwa karibu, pengo hilo la kidijitali litazidisha tofauti za utajiri kati ya Afrika na maeneo mengine. Ikiwa nchi kubwa zaidi inayoendelea na mwenza muhimu wa maendeleo ya Afrika, China imetumia ipasavyo nguvu zake kuimarisha ushirikiano na Afrika katika nyanja zifuatazo.

Kwanza, ujenzi wa miundombinu ya internet ni msingi wa ushirikiano wa China na Afrika na msingi wa kutimiza ujenzi wa "Afrika ya Kidijitali". Takwimu zinaonyesha kuwa China inashiriki katika asilimia 70 ya ujenzi wa miundombinu ya internet na inazalisha takriban 50% ya simu za mkononi barani Afrika. Nchi zaidi na zaidi za Afrika zimetambua kwamba teknolojia na bidhaa zinazotolewa na makampuni ya China leo zina nguvu zaidi na za bei nafuu zaidi kuliko zile za Magharibi.

Pia kushirikiana na China na kuboresha miundombinu ya mtandao bila kujali tabia ya kujichukulia kama mzazi na mizigo ya kihistoria ambayo nchi za Magharibi "huibeba" wakati wanapofanya biashara barani Afrika imekuwa maoni ya pamoja barani Afrika

Pili, China na Afrika zimeimarisha ushirikiano katika kuboresha uwezo wa matumizi ya kidijitali ili kukuza maendeleo endelevu barani Afrika. Katika miaka ya hivi karibuni, hali ya hewa ya ajabu, kama vile joto kali, ukame na mafuriko imetokea mara kwa mara, na mabadiliko ya hali ya hewa yameleta changamoto katika uzalishaji wa chakula duniani.

Jinsi ya kukabiliana kikamilifu na mabadiliko ya hali ya hewa, na kuboresha uzalishaji wa kilimo na kupunguza utoaji wa gesi chafuzi kwa njia endelevu ni suala la pamoja linalozikabili China na Afrika. Hivi sasa, China inaharakisha uvumbuzi wa sayansi na teknolojia ya kilimo na mabadiliko ya mbinu za uzalishaji, na kuendeleza suluhu za "kilimo cha busara" ili kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya hali ya hewa.

Wakati huo huo, China pia imepata maendeleo katika matumizi ya digitali kwa huduma za umma kama vile kupunguza umaskini unaolengwa, biashara ya mtandaoni na malipo ya simu, ambazo ni rasilimali muhimu kwa China na Afrika kubadilishana uzoefu.

Tatu, uwezo wa teknolojia ya kidijitali wa watu wa Afrika, hasa vijana, ni mustakabali wa maendeleo ya Afrika. Kwa kutegemea miradi midogo lakini mizuri ya China katika nchi za Afrika kama vile “Karakana ya ufundi ya Luban”, China imetoa ujuzi wa digitali kwa waafrika wengi. Aidha, kama mwelekeo muhimu katika enzi ya dijitali, biashara ya mtandaoni pia ni kazi muhimu kwa uandaaji wa vipaji vya teknolojia ya dijitali kati ya China na Afrika.

“Maendeleo ya pamoja” ndio kauli mbiu ya zama za leo. Inaaminika kuwa kadiri dira ya “ujenzi wa China yenye nguvu ya mtandao wa internet” inavyoimarishwa, ndivyo Afrika itanufaika zaidi na maendeleo ya China.
 
Wakati nchi nyingine zinatumia internet kwa ajili ya maendeleo viongozi wa Afrika wanatumia nguvu nyingi kudhibiti mawasiliano kwa sababu za kisiasa
 
Back
Top Bottom