Uchumi wa China watarajiwa kukua kwa asilimia 5 mwaka huu

Yoyo Zhou

Member
Jun 16, 2020
72
111
VCG111425670136.jpeg
Mkutano wa Bunge la Umma la China na Mkutano wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China inafanyika, na suala la kiuchumi linafuatiliwa sana na jumuiya ya kimataifa. Katika ripoti ya kazi ya serikali iliyowasilishwa tarehe 5 kwenye mkutano wa Bunge la Umma, China iliweka lengo la ukuaji wa uchumi kwa mwaka huu kuwa asilimia 5.

Katika mwaka uliopita, uchumi wa China ulikua kwa asilimia 5.2. Kiwango hiki ni cha kasi zaidi kuliko kiwango cha wastani wa ukuaji wa asilimia 4.5 katika miaka mitatu wakati dunia ilipokabiliwa na janga la COVID-19, na pia ni cha kasi zaidi kuliko kiwango cha ukuaji wa uchumi cha asilimia 2.5 nchini Marekani, asilimia 0.5 cha Umoja wa Ulaya, na asilimia 1.9 nchini Japan. Mchango wa China katika ukuaji wa uchumi wa dunia unatarajiwa kuendelea kuwa zaidi ya asilimia 30. Tangu mwanzoni mwa mwaka huu, uchumi wa China umeendelea kuwa na mwelekezo mzuri wa ukuaji. Hata hivyo, baadhi ya watu wa nchi za Magharibi wanapuuza ukweli na kusema “uchumi wa China ni dhaifu”, na “maendeleo ya China yanakaribia mwisho”. Baadhi ya vyombo vya habari vya Magharibi pia vinapiga kelele kwamba ukuaji wa uchumi wa China “umefikia kilele” na utaanza kuteremka.

Kusema kweli, maendeleo ya uchumi wa China yamekabiliwa na changamoto mbalimbali katika miongo miwili iliyopita, likiwemo janga la SARS mnamo mwaka 2003, msukosuko wa fedha duniani pamoja na tetemeko kubwa la ardhi la Wenchuan mwaka 2008, na janga la COVID-19 kuanzia mwaka 2020 hadi 2023. Wakati China ilipokabiliwa na hali ngumu, baadhi ya vyombo vya habari vya Magharibi husema “uchumi wa China utaporomoka”, lakini kila mara mwishowe walifyata mdomo wao. Kwani China haiwezi kushinda changamoto zote na kudumisha maendeleo ya kasi ya uchumi?

Hivi sasa, uchumi wa China unakabiliwa na changamoto kadhaa, ikiwa ni pamoja na ukuaji wa polepole wa uchumi wa dunia, mazingira ya kutatanisha ya kiuchumi na kibiashara duniani, na uwezo mkubwa wa uzalishaji kupita kiasi katika baadhi ya sekta. Wakati huohuo, uchumi wa China una mategemeo makubwa zaidi ya kukua.

Kwanza, msingi wa uchumi wa China ni imara, na mwelekeo wake mzuri wa ukuaji haujabadilika. China ni nchi pekee duniani ambayo ina sekta zote ya viwanda zilizoorodheshwa na Umoja wa Mataifa, na thamani yake ya uzalishaji wa viwanda inachukua karibu asilimia 30 duniani. China ina soko kubwa la pili la wateja, na soko kubwa zaidi la biashara ya mtandaoni. Zaidi ya hayo, China ina rasilimali kubwa zaidi ya watu wenye kipaji.

Pili, mfumo maalumu wa ujamaa wa Kichina una uwezo wa kipekee katika kukabiliana na changamoto za kiuchumi. Mfumo huo una nguvu zaidi katika uhamasishaji, uratibu na utekelezaji, ambavyo vimesaidia China kushinda matatizo mbalimbali yaliyokabili maendeleo ya uchumi katika miaka mingi iliyopita.
 
Hongera china kwa kasi ya maendeleo. Hakika xi jingpin ni Nuru ya taifa la Mao the Dong mtawala mkuu
 
Back
Top Bottom