Mikutano miwili ya China yaendeleza desturi za uwakilishi na utulivu

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,036
VCG111371048772.jpg


Kipindi cha mikutano miwili ya China, yaani mkutano wa Bunge la Umma la China na mkutano wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China iliyomalizika hivi karibuni, ni kipindi muhimu zaidi kisiasa kwa China, kwani katika kipindi hili, kwanza demokrasia ya China huwa inapimwa na kukaguliwa, na pili matakwa na mahitaji ya wananchi yanafikishwa mbele ya watunga sera na wafanya maamuzi. Mwaka huu hayo pia yamefanyika kama ilivyotayarajiwa.

Nchini China mashauriano, ushirikiano na maslahi ya umma, ndio nguzo kuu za mfumo wa kisiasa, lakini kwenye nchi za magharibi na kwenye nchi nyingine zinazofuata mfumo wa kisiasa wa nchi za magharibi, ushindani, upinzani na maslahi ya watu au maslahi ya makundi ndio nguzo kuu za mfumo wa kisiasa.

Wajumbe wa mikutano miwili ya China wanapokutana mara zote wanakaa kutoa mapendekezo ya kushauriana kuhusu mambo yanayohusu nchi na wananchi, na wanajadili mambo hayo na kuyafikisha kwa wanaofanya maamuzi. Licha ya kuwa China ni nchi kubwa yenye watu zaidi ya bilioni 1.4, mfumo wake unahakikisha kuwa maoni ya wananchi kutoka ngazi ya chini kabisa ya njia za kukusanywa kujadiliwa na kufikishwa kwenye ngazi za juu kabisa za maamuzi. Kwenye mikutano hii miwili desturi hiyo iliendelea kudumishwa, kwanza kutokana na mambo yaliyojadiliwa na hata waliowakilisha maoni na mapendekezo kwenye mikutano hiyo.

Jambo lingine ambalo limekuwa ni msingi wa siasa za China, ni kuhakikisha kuwa siasa zinaendeleza utulivu wa jamii. Ni wazi kuwa hali ya kisiasa na kiuchumi duniani kwa sasa ina changamoto za kila namna, kubwa zaidi inayotatiza watu ni sintofahamu za kiuchumi. Kwenye mikutano miwili ya safari hii, kubwa lililoleta matumaini kwa watu ni kuwa lengo la ongezeko la uchumi lililopangwa katika mwaka uliopita ya 5.2% limetimizwa, na lengo la ongezeko la 5% na nafasi za ajira zaidi ya milioni 12 bila shaka litatimizwa. Hali hii inawapa matumaini wanafunzi wanaohitimu masomo, watu wenye hofu ya kupoteza ajira zao kutokana na mazingira ya uchumi na siasa za dunia, wajasiriamali wenyeji na hata wawekezaji kutoka nje. Kimsingi mambo haya yamefanya watu wasiwe na wasiwasi kuhusu mwelekeo wa uchumi.

Pamoja na kuwa sehemu kubwa ya mambo yanayojadiliwa kwenye mikutano miwili ni mambo ya ndani ya China, kutokana na jinsi uchumi wa China ulivyofungamana na uchumi wa nchi nyingine duniani, mambo yanayojadiliwa yanahusiana moja kwa moja na uchumi katika sehemu nyingine duniani. Uendelevu wa sera za uchumi za China, utulivu wa kijamii wa China na hata maamuzi mengi yanayofanywa na vyombo vya maamuzi vya China kwa namna moja au nyingine vina uhusiano wa karibu na nchi nyingine duniani. Mashauriano, ushirikiano na maslahi ya pamoja, sio kama ni mambo yanayoishia kwenye siasa za ndani za China.

Akizungumza na waandishi wa habari kando ya mikutano miwili ya safari hii, waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi alitaja mara kadhaa dhana ya majadiliano na ushirikiano kwa ajili ya kuleta maendeleo ya kunufaisha pande zote. Waziri Wang pia alizungumzia mambo ya ushirikiano kati ya China na Afrika, na kusema China itaendelea kushirikiana na nchi za Afrika, na hata nchi nyingine ambazo hapo awali zilizoliweka pembeni bara la Afrika kuleta maendeleo ya kunufaisha.
 
Back
Top Bottom