Kama Rais Samia anashaurika na msikivu awafute kazi ya uwaziri January Makamba na Nape, ni mawaziri mzigo kwa taifa

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Oct 2, 2020
4,086
6,568
Wananchi wa kila kada wamepiga kelele na kushauri mkuu wa nchi amfute kazi January Makamba maana tangu aingie Wizara ya Nishati kila kitu kimeenda mrama. Bwawa la Nyerere ambalo kama lingekamilika Juni 2022 lingekuwa msaada mkubwa kwa Watanzania na kuleta ahueni ya maisha maana gharama za maisha zingepungua.

Upo ushahidi wa wazi na kimazingira January Makamba amezembea na kuhujumu mradi wa JNHP maana alileta zengwe la krane mpaka kuchepusha maji kukakwama.

Sasa hivi amegeuza Tanesco kama mradi wake wa kupiga madili yeye na Maharage Chande kila kukicha ni matengenezo yasiyoisha na kuingia mikataba ya ajabuajabu na Mahindra Tech.

Huyu mwingine anaitwa Nape anatumia madaraka vibaya na kusababisha upotevu wa pesa za umma ambazo zingetumika kwa manufaa ya umma. Anazunguka nchi nzima na helikopta kwenda kupaka rangi vibao vya mitaani. Huu ni uhujumu uchumi wa wazi kabisa.

Mama sababu unapaswa kushaurika. Sikia kilio cha Watanzania na wafute kazi hawa mawaziri wawili ukiwa huko huko USA.
 
Wananchi wa kila kada wamepiga kelele na kushauri mkuu wa nchi amfute kazi January Makamba maana toka aingie wizara ya Nishati ma madini kila kitu kimeenda mrama. Bwawa la Nyerere ambalo kama lingekamilika June 2022 lingekuwa msaada mkubwa kwa watanzania na kuleta ahueni ya maisha maana gharama za maisha zingepungua.

Upo ushahidi wa wazi na kimazingira January Makamba amezembea na kuhujumu mradi wa JNHP maana alileta zengwe la krane mpaka kuchepusha maji kukakwama.

Sasa hivi amegeuza shirika la Tanesco kama mradi wake wa kupig madili yeye na Maharage Chande kula kukicha ni matengenezo yasiyoisha na kuingia mikataba ya ajabu ajabu na Mahindra tech.

Huyu mwingine anaitwa Nape anatumia madaraka vibaya na kusababisha upotevu wa pesa za umma ambazo zingetumika kwa manufaa ya umma. Anazunguka nchi nzima na helikopta kwenda kupaka rangi vibao vya mitaani. Huu ni uhujumu uchumi wa wazi kabisa.

Mama sababu unapaswa kushaurika. Sikia kilio cha watanzania na wafute kazi hawa mawaziri wawili ukiwa huko huko Usa.

Nani hataki Mama Chamira
 
Attachments

  • VID-20220413-WA0012.mp4
    7.4 MB
... kupitia helcopta "yake", Nnape kwa sasa "anaamsha waliolala" wakafanye kazi. Msimuonee wivu.
 
Kuna kikao cha CCM elites kilikaa siku waliyoiita Nauye Day. Mzee Makamba alisema Brigedia Nauye ndiye alikua mwalimu wake wa uhamasishaji jeshini kwa kutumia burudani ya kwaya.

Ukiisikiza hiyo clip utaelewa kuwa CCM ina wenyewe na wenyewe ndiyo hao.
 
Kuna kikao cha CCM elites kilikaa siku waliyoiita Nauye Day. Mzee Makamba alisema Brigedia Nauye ndiye alikua mwalimu wake wa uhamasishaji jeshini kwa kutumiaburudani ya kwaya.

Ukiisikiza hiyo clip utaelewa kuwa CCM ina wenyewe na wenyewe ndiyo hao.
👍
 
Kuna kikao cha CCM elites kilikaa siku waliyoiita Nauye Day. Mzee Makamba alisema Brigedia Nauye ndiye alikua mwalimu wake wa uhamasishaji jeshini kwa kutumia burudani ya kwaya.

Ukiisikiza hiyo clip utaelewa kuwa CCM ina wenyewe na wenyewe ndiyo hao.
Kwa hiyo hata wakizingua waachwe tu?
 
Huyu January anategemea Sana msaada wa baba yake.😂😂😂😂😂
 
Wapeni muda reforms huchukua muda.Ukizingatia taifa limetoka kipindi kigumu maelekezo na maagizo ya MTU mmoja.
 
Hata kama ningalikua mimi ni Samia ningemwacha makamba afanye kazi,
Unaona kabisa Kalemani anahangaika sana kuona makamba kawa mrithi wake.

Hivi ni kweli kwamba Makamba ndio mzigo kuliko mawaziri wote?Iweje kila siku ni Makamba tu?Vipi wizara nyingine zinafanya vizuri?

Siasa ni strategy,kuna waajiriwa wa Kalemani wachache mtandaoni ambao wameanzisha upepo ambao unasomba na watu wengine wanahangaika na Makamba ilihali hawajui nini kinaendelea Nyuma ya pazia.
 
We huathiriki na utendaji mbovu wa Makamba na Tanesco yake? Mbona huko nyuma haikuwa hivi?
 
Wananchi wa kila kada wamepiga kelele na kushauri mkuu wa nchi amfute kazi January Makamba maana tangu aingie Wizara ya Nishati na Madini kila kitu kimeenda mrama. Bwawa la Nyerere ambalo kama lingekamilika Juni 2022 lingekuwa msaada mkubwa kwa Watanzania na kuleta ahueni ya maisha maana gharama za maisha zingepungua.

Upo ushahidi wa wazi na kimazingira January Makamba amezembea na kuhujumu mradi wa JNHP maana alileta zengwe la krane mpaka kuchepusha maji kukakwama.

Sasa hivi amegeuza Tanesco kama mradi wake wa kupiga madili yeye na Maharage Chande kila kukicha ni matengenezo yasiyoisha na kuingia mikataba ya ajabuajabu na Mahindra Tech.

Huyu mwingine anaitwa Nape anatumia madaraka vibaya na kusababisha upotevu wa pesa za umma ambazo zingetumika kwa manufaa ya umma. Anazunguka nchi nzima na helikopta kwenda kupaka rangi vibao vya mitaani. Huu ni uhujumu uchumi wa wazi kabisa.

Mama sababu unapaswa kushaurika. Sikia kilio cha Watanzania na wafute kazi hawa mawaziri wawili ukiwa huko huko USA.
Umerogwa?
 
We huathiriki na utendaji mbovu wa Makamba na Tanesco yake? Mbona huko nyuma haikuwa hivi?
Mwendazake alikuwa anawaachia warithi wake matatizo,wakati watu wanaunganishiwa umeme kwa 27000 huku anashindwa kuajiri walimu na watu wa kada nyingine kwakukosa pesa,shule inawalimu wawili,anatafuta sifa zakijinga kwa watu wajinga.
 
Wakati wa Magufuli kulikuwa na viongozi majambazi na walionekana hadi kwenye kamera za kiusalama lakini pamoja na wananchi kutaka waondolewe madarakani bado Magufuli aliwalinda lakini haukuliona hilo ndio unaliona hili la Makamba.
Hii yote ni kwa sababu ya chuki ulizonazo kuanzia kwa Rais mwenyewe hadi hao wasaidizi wake.
 
Back
Top Bottom