Azam TV wao wanajua faida ya media wanaipata kwenye VPL. Na ndiyo huko waliko invest. Mleta mada kama Azam hawako vizuri kwenye live coverage naomba uniambie.
Pili, taarifa ya habari. Muundo wa taarifa yao ya habari bado haujazoeleka lakini wapo vizuri.
Kuhusu qaality hill nadhani labda uwe na lingine. Quality ya matangazo yao ni nzuri ukitoa kasoro mbili ambazo kwangu ipo moja ya mvua ikinyesha matangazo yanasumbua. Wengine wameongeza na jua Kali.
Tatu, ukilinganisha gharama za Azam na DSTV ni umbali wa magharibi na mashariki. Gharama za Azam zipo fair kuliko DSTV kwa mtanzania wa kawaida. Azam wakianza kuonyesha EPL nadhani ndiyo utakuwa mwisho wa DSTV EA. Sijaona cha ziada DSTV zaidi ya vipindi ambavyo wananunua kutoka channel nyingine.
Kuhusu uchanganyaji inawezekana standard ndiyo hiyo inayotakiwa kimataifa ila we we inapenda mbwembwe za local Tvs ambazo Hazina viwango.
Mbona haulaumu ITV saizi wamebadili tangazo lao la taarifa ya habari limekaa kishamba zaidi ya lile la awali?