Siasa Michezoni (Simba vs Al Ahly): Azam TV wanapaswa kuonywa, kuadhibiwa au kufungiwa!

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
10,129
35,153
Kilichotokea jana kwenye ufunguzi wa mashindano ya African Football League kwenye mechi kati ya Simba na Al Ahly kupitia Azam TV ambapo kwa sekunde kadhaa kimakusudi walionyesha bango la mashabiki lenye maandishi yenye mlengo wa kushabikia siasa za mashariki ya kati (kifupi bango lile lilikuwa na maandishi ya kiingereza likipeleka ujumbe wa kuunga mkono harakati za taifa la Palestina), kitendo kile kilikuwa ni kitendo cha aibu na fedheha kubwa kuonekana michezoni kupitia matangazo ya moja kwa moja kwenye TV. Wadau kadhaa duniani waliofuatilia matangazo yale wameonyesha kusononeshwa na namna Tanzania kupitia Azam Media nk walivyoamua kimakusudi kushafua taswira nzima ya matangazo ya mpira wa Afrika.

Kwa kifupi sana kwa sheria za soka za FIFA na CAF lile lilikuwa ni kosa, na kama litashikiwa bango huenda Azam TV na mamlaka za soka hapa Tanzania zikajikuta matatani.

Kimantiki tukio lile lilipangwa (kwa waliokuwepo uwanjani hususani jukwaa lile wanaelewa vizuri) na kuratibiwa kikamilifu huku Azam media ikihusika kwa 100%. Na hapa nitachambua kwa kina;

1. Bango lile lilikuwa kubwa, pana, refu na maridadi. Hivyo waandaji walikuwa ni watu waliojipanga vizuri.

2. Bango lile liliingizwa uwanjani bila usumbufu wowote na liliendelea kuwepo uwanjani kwa uhuru karibu muda wote wa mchezo. Hii inaashiria mamlaka za soka na usalama hapa Tanzania zilibariki tukio lile kwa 100%.

4. Bango lile liliandikwa kwa kiingereza, lengo likiwa kufikisha ujumbe kimataifa (wahusika wakijua 100% Azam Tv watarusha lile tukio!)

5. Bango lile lilikuwa limeshikiliwa kwa ujasiri na mashabiki wengi wa Al ahly (wamisri) na wachache wa simba (watanzania). Hii inaashiria ushirikishi wa pamoja.

6. Video zinaonyesha walioshirikia lile bango wakiwa standby kuchukuliwa video na Azam Tv, na wengine wakikimbilia kulifikia bango ili video inayochukuliwa iwaonyeshe. Hii inaashiria wapiga picha wa Azam walikuwa 100% attention&concious kuhakikisha ujumbe unafika.

7. Live coverage ya tukio ilikaa kwa sekunde kadhaa hewani ili kila mtazamaji aone, lakini pia kuna namna coverage ilihamia kwenye kitu kingine na haraka ikarejea kwenye tukio lile lile. Hii inaashiria umakusudi wa 100% tukio lile liende hewani.

8. Watangazaji wa Azam Tv hawakusema chochote (walikaa kimya) kama vile hawaelewi chochote wakati tukio lile likiwa hewani, huenda kwa kuwa walihisi ukakasi, hawakuandaliwa au kuogopa kitu.

9. Azam media wamekuwa na mtindo wa kurudia kuonyesha video za mechi iliyochezwa hapo kabla, hivyo wangeweza kuhariri kwa kuondoa vipande vya video vyenye utata, lakini kwa tukio la jana wameliacha vile vile mpaka sasa. Nadhani lengo ni ujumbe ufike vilivyo.

10. Mpaka sasa hivi Azam media hawajaomba radhi wala kutaka kutolea ufafanuzi tukio lile kuruka kwenye matangazo yao. Hii kuashiria Azam media wanaamini walikuwa sahihi na walijiandaa kurusha tukio lile kikamilifu.
 
Weka hilo Bango tulione acha maneno meeeeengi kama chiriku
Kilichotokea jana kwenye ufunguzi wa mashindano ya African Football League kwenye mechi kati ya Simba na Al Ahly kupitia Azam Tv ambapo kwa sekunde kadhaa kimakusudi walionyesha bango la mashabiki lenye maandishi yenye mlengo wa kushabikia siasa za mashariki ya kati (kifupi bango lile lilikuwa na maandishi ya kiingereza likipeleka ujumbe wa kuunga mkono harakati za taifa la Palestina), kitendo kile kilikuwa ni kitendo cha aibu na fedheha kubwa kuonekana michezoni kupitia matangazo ya moja kwa moja kwenye TV.
Jamaaa una deal na mabango tuu hata ID yako ime prove hivo..
😂😂😂😂😂😂😂
 
AZAM ni wadini sana, nshasema AZAM hawana ETHICS za habari. Matangazo yao yapo kidini zaidi na sijajua kwanini Wasirivoke leseni yao ya matangazo kutoka kuwa chombo cha habari cha kijamii SECULAR na kuwa cha kidini non SECULAR.
 
IMG_0164.png
 
Kilichotokea jana kwenye ufunguzi wa mashindano ya African Football League kwenye mechi kati ya Simba na Al Ahly kupitia Azam Tv ambapo kwa sekunde kadhaa kimakusudi walionyesha bango la mashabiki lenye maandishi yenye mlengo wa kushabikia siasa za mashariki ya kati (kifupi bango lile lilikuwa na maandishi ya kiingereza likipeleka ujumbe wa kuunga mkono harakati za taifa la Palestina), kitendo kile kilikuwa ni kitendo cha aibu na fedheha kubwa kuonekana michezoni kupitia matangazo ya moja kwa moja kwenye TV. Wadau kadhaa duniani waliofuatilia matangazo yale wameonyesha kusononeshwa na namna Tanzania kupitia Azam Media nk walivyoamua kimakusudi kushafua taswira nzima ya matangazo ya mpira wa Afrika.

Kwa kifupi sana kwa sheria za soka za FIFA na CAF lile lilikuwa ni kosa, na kama litashikiwa bango huenda Azam TV na mamlaka za soka hapa Tanzania zikajikuta matatani.

Kimantiki tukio lile lilipangwa (kwa waliokuwepo uwanjani hususani jukwaa lile wanaelewa vizuri) na kuratibiwa kikamilifu huku Azam media ikihusika kwa 100%. Na hapa nitachambua kwa kina;

1. Bango lile lilikuwa kubwa, pana, refu na maridadi. Hivyo waandaji walikuwa ni watu waliojipanga vizuri.

2. Bango lile liliingizwa uwanjani bila usumbufu wowote na liliendelea kuwepo uwanjani kwa uhuru karibu muda wote wa mchezo. Hii inaashiria mamlaka za soka na usalama hapa Tanzania zilibariki tukio lile kwa 100%.

4. Bango lile liliandikwa kwa kiingereza, lengo likiwa kufikisha ujumbe kimataifa (wahusika wakijua 100% Azam Tv watarusha lile tukio!)

5. Bango lile lilikuwa limeshikiliwa kwa ujasiri na mashabiki wengi wa Al ahly (wamisri) na wachache wa simba (watanzania). Hii inaashiria ushirikishi wa pamoja.

6. Video zinaonyesha walioshirikia lile bango wakiwa standby kuchukuliwa video na Azam Tv, na wengine wakikimbilia kulifikia bango ili video inayochukuliwa iwaonyeshe. Hii inaashiria wapiga picha wa Azam walikuwa 100% attention&concious kuhakikisha ujumbe unafika.

7. Live coverage ya tukio ilikaa kwa sekunde kadhaa hewani ili kila mtazamaji aone, lakini pia kuna namna coverage ilihamia kwenye kitu kingine na haraka ikarejea kwenye tukio lile lile. Hii inaashiria umakusudi wa 100% tukio lile liende hewani.

8. Watangazaji wa Azam Tv hawakusema chochote (walikaa kimya) kama vile hawaelewi chochote wakati tukio lile likiwa hewani, huenda kwa kuwa walihisi ukakasi, hawakuandaliwa au kuogopa kitu.

9. Azam media wamekuwa na mtindo wa kurudia kuonyesha video za mechi iliyochezwa hapo kabla, hivyo wangeweza kuhariri kwa kuondoa vipande vya video vyenye utata, lakini kwa tukio la jana wameliacha vile vile mpaka sasa. Nadhani lengo ni ujumbe ufike vilivyo.

10. Mpaka sasa hivi Azam media hawajaomba radhi wala kutaka kutolea ufafanuzi tukio lile kuruka kwenye matangazo yao. Hii kuashiria Azam media wanaamini walikuwa sahihi na walijiandaa kurusha tukio lile kikamilifu.
Ache inyeshe vuli ndio wakati
 
Back
Top Bottom