Tulinje twayene
Senior Member
- Aug 7, 2020
- 141
- 183
Azam TV kulikoni mmeamua kwa kuiondoa channel ya Russia today siku mbili tu baada ya umoja wa ulaya kuifungia channel hiyo huko Ulaya?
Hii channel ilikuwa inatusaidia sana kubalance propaganda na habari zenye tija hasa kuhusu yanayoendelea huko Ukraine. Badala yake mmeziacha channel za magaribi na Ulayan kama sauti ya America, France 24, BBC na Aljazeera pekee zitamalaki kwenye kingamuzi chenu.
Mimi binafsi sijapenda kwani msimamo wa mataifa mengi ya Afrika ungekuwa mzuri zaidi kwenu kwa kutofungamana na upande wowote, na nyie kama shirika mbakie kuleta habari za pande zote ili wasikilizaji na watazamaji wenu tuchambue wenyewe pumba na mchele.
Au na nyie mmeamua kuingia uwanjani na kuilaani Urusi kwa namna hii? Sisi wafuatiliaji wa siasa mmetunyima haki yetu kwani tuliamua kulipia kifurushi kikubwa ili tuweze kufuatilia habari zote za ndani na nje ya nchi kwa ufasaha, channel hiyo mliyoitoa ni muhimu sana kwetu kwa sasa ili tuweze kubalance habari kuliko kutulisha habari za upande mmoja.