Kama naanza kuichoka Azam TV vile

Kama naanza kuichoka Azam TV vile

Azam TV wao wanajua faida ya media wanaipata kwenye VPL. Na ndiyo huko waliko invest. Mleta mada kama Azam hawako vizuri kwenye live coverage naomba uniambie.

Pili, taarifa ya habari. Muundo wa taarifa yao ya habari bado haujazoeleka lakini wapo vizuri.

Kuhusu qaality hill nadhani labda uwe na lingine. Quality ya matangazo yao ni nzuri ukitoa kasoro mbili ambazo kwangu ipo moja ya mvua ikinyesha matangazo yanasumbua. Wengine wameongeza na jua Kali.

Tatu, ukilinganisha gharama za Azam na DSTV ni umbali wa magharibi na mashariki. Gharama za Azam zipo fair kuliko DSTV kwa mtanzania wa kawaida. Azam wakianza kuonyesha EPL nadhani ndiyo utakuwa mwisho wa DSTV EA. Sijaona cha ziada DSTV zaidi ya vipindi ambavyo wananunua kutoka channel nyingine.

Kuhusu uchanganyaji inawezekana standard ndiyo hiyo inayotakiwa kimataifa ila we we inapenda mbwembwe za local Tvs ambazo Hazina viwango.

Mbona haulaumu ITV saizi wamebadili tangazo lao la taarifa ya habari limekaa kishamba zaidi ya lile la awali?

Mzee Wa Rula naomba unisome kuna mambo nimeyaandika kwa mamba lakini naomba zaidi unijibu katika 3 - 5. Yale maelezo yangu ni ya mkakati na si ya kitaalamu kwahiyo usijibu kama unavojibu za rangi, picha n.k .Ya kwangu yanataka kusikia mnaanza lini kuingiza na kupunguza baadhi ya vingine
 
Azam TV wao wanajua faida ya media wanaipata kwenye VPL. Na ndiyo huko waliko invest. Mleta mada kama Azam hawako vizuri kwenye live coverage naomba uniambie.

Pili, taarifa ya habari. Muundo wa taarifa yao ya habari bado haujazoeleka lakini wapo vizuri.

Kuhusu qaality hill nadhani labda uwe na lingine. Quality ya matangazo yao ni nzuri ukitoa kasoro mbili ambazo kwangu ipo moja ya mvua ikinyesha matangazo yanasumbua. Wengine wameongeza na jua Kali.

Tatu, ukilinganisha gharama za Azam na DSTV ni umbali wa magharibi na mashariki. Gharama za Azam zipo fair kuliko DSTV kwa mtanzania wa kawaida. Azam wakianza kuonyesha EPL nadhani ndiyo utakuwa mwisho wa DSTV EA. Sijaona cha ziada DSTV zaidi ya vipindi ambavyo wananunua kutoka channel nyingine.

Kuhusu uchanganyaji inawezekana standard ndiyo hiyo inayotakiwa kimataifa ila we we inapenda mbwembwe za local Tvs ambazo Hazina viwango.

Mbona haulaumu ITV saizi wamebadili tangazo lao la taarifa ya habari limekaa kishamba zaidi ya lile la awali?
Binafsi, nilitegemea makubwa toka Azam. Ukitoa chanel za nje, Azam1 na Azam2 materials ni very ordinary.
 
Rweye kumbe tatizo channel za kiarabu na kihindi tu. Ninavyojua

Mkuu usijitoe uFAHAMU kama hujamuelewa mkuu Rweye rudia tena kusoma alichoandika ila sio huu ujinga ulioleta hapa
 
Last edited by a moderator:
kuendelea kuijadili azam tv kwa namna hii,ni ishara kwamba mnaitazama sana.

kama kukatokea mtu akafanya audience measurement kwa upande TV station za Tanzania,nina hakika azam TV itaibuka kinara wa kuwa na viewership kubwa.
 
Ni kweli unayosema ila wajirekebishe..kama hawana rasilimali watu husika wakope wataalam watatu au wanne waje wawape training staff wao ili waweze kuendana na yechnology iliyowekezwa hapo...
 
and for all you haters out there.....something big from azam tv is coming this December.it's called azam gold.stay tuned.hutaki unaacha.hahahaha
 
mkuu kuna kitu kinaitwa TING,kama vp kaa humo....achana na king'amuzi cha azam.

Mkuu jazba ya nini hii sinibiashara mmeleta sokoni? Sasa wateja wenu kama wanaona mapungufu wasiwaambie? kwanini naww hukuweka nyumbani kwako ungalie mwenyewe Kubalini changamoto zitawasaidia kwenye biashara yenu
 
Mie naitumia toka 2014 mwanzoni lakini kuna mda najiuliza kwanini hawa jamaa wamekwama. Ukweli unauma saaana lakini unabaki haupingiki. Kwanza wana vituo vyao 3 i.e Xtra, 1 & 2.
Mapungufu yao sasa.
1. Wana staff kali isiyolingana na delivery inayotolewa.
2. Wana vifaa vya kisasa vikali lakini naona haviwi full utilized.
3. Wanatumia mda mchache saaana kuonesha yanayotokea ndani ya Tz, ikiwemo taharifa za habari tu.
4. Wameshindwa kuishi maneno yao. Walisema wanataka kuwa BBC ya Afrika. BBC ninayoijua wana habari live kila saa inayoanza yaani saa 2,3,4,5... wakati hawa wenzetu wana Habari usiku saa 2 mara moja tu kwa siku nzima. Unajiuliza staff iko na vifaa mnavyo sasa tatizo nini miezi 7 imepita sasa toka wajinasibu.
5. Hawako seriazi na ratiba ya maana. Stations zao zote 3 hazioneshi kitu cha maana toka asubuhi hadi jioni. Ni vikatuni tu, documentari za DW, na Africa time. Hakuna vipindi vinavyooneshwa mahususi toka Tz. Alasiri lounge ina maongezi mengi, utani na matangazo. mengi mpaka inaondoa maana yote ya kipindi. Nakumbuka Mme wa Ivyona alipotambulishwa walisema yeye atakuwa maalum kwa ajiri ya habari za mchana saa 7 lakini hadi leo si yeye wala hicho kipindi kuruka.
6. Kujazwa kwa chaneli zisizo na tija na zingine wala hazioneshi milele. Wamejaza wahindi na waarabu sana wakati chnl. kama bukedde 1, Ntv Uganda, na nyingine kibao hizi wala huwa haziko active. Azam wanakoelekea wanapoteza dira kwa kweli mwenye kupinga na apinge lakini nejitahidi kuongea kwa viashiria harisi.

Cc: Adrian Stepp.
 
Last edited by a moderator:
wateja wenu kama wanaona mapungufu wasiwaambie? kwanini naww hukuweka nyumbani kwako ungalie mwenyewe Kubalini changamoto zitawasaidia kwenye biashara yenu

mkuu kukushauri uhamie TING ni kosa?.this is a free market zone,usinga'ng'anie bidhaa ambayo mwisho wa siku haikidhi viwango vyako ulivyo vitegemea.lets be realistic (in jerry muro voice), kwanini mnang'ang'ana na azam TV?.
 
Mwisho Wa Siku Hata Iweje Huwezi Kufanya Jambo Litakalo Wapendeza Watu Wote Duniani. Binafsi Naikubali AZAM Tv Kwa Pale Walipo Fikia Ukilinganisha Na Muda Toka Waingie Sokoni. Naamini Kadri Siku Zinavyo Songa Ipo Siku Wanaweza Kuleta Kitu Kizuri Zaidi Ya Hiki Tunacho Kipata Leo.

:TUWAPE MUDA"
 
Unajua kuwa na watangazaji wengi na wazuri haitoshi kabisa kama huna vipindi vya kuvutia watazamaji!

Azam wamejikita sana kuongeza watangazaji kuliko kutengeneza vipindi vya kugusa jamii na kuvutia watazamaji....!

Bila shaka kwa sasa bado wanapaswa kujifunza kwa wengine....
 
kuendelea kuijadili azam tv kwa namna hii,ni ishara kwamba mnaitazama sana.

kama kukatokea mtu akafanya audience measurement kwa upande TV station za Tanzania,nina hakika azam TV itaibuka kinara wa kuwa na viewership kubwa.

Mkuu sio kwamba vituo vya Azam tv vinatazamwa sana, bali king'amuzi cha Azam ndio kinatumiwa sana na watu na hii ni kwasababu ya mpira. Ukiondoa mpira Azam One na Two huenda zikakosa watazamaji. Tuleteeni vipindi vyenye mvuto na kukugusa maisha ya mtanzania moja kwa moja!
 
mtoa mada bado anaakili za kizamani alitaka azamtv iisifie chadema itukane serikali kwanza hajui hata habari zinapangwaje kwenye tv
 
hapa tanzania kwa sasa hakuna mbadala wa azam TV,be it in all angles of TV broadcasting like picture quality, advanced equipment,news anchors,man power etc.

hivyo basi wale wenye chuki binafsi na bidhaa za mzee bakhresa,mtanunua tu king'amuzi cha azam ili mtizame TV zake maana hakuna namna.

TBC ndio kwanza wanarusha harusi live.kwanini watu msitokwe povu hapa kuhusu azam.chezeya azam nyinyi....
 
mtoa mada bado anaakili za kizamani alitaka azamtv iisifie chadema itukane serikali kwanza hajui hata habari zinapangwaje kwenye tv

Hapa tunaongea vitu dhahiri shairi ambavyo tunaviishi kupitia Azam tv kila siku. Hivi unajiona wa aina gani mtu anakushauri utengeneze vipindi vinavyoongelea jamii yetu sana watanzania alafu wewe unasema huyo mtu anaongea uchadema? kivipi?. Andaeni vipindi vya ufugaji wa kisasa/ kienyeji kule vijijini muoneshe kama makala. Kuna kuku, ng'ombe, nguruwe n.k. Andaeni vipindi vya kilimo mfano miwa, mahindi, mchele, alizeti n.k. Andaeni makala kuhusu masoko toka vijijini kwenda mijini kama vile kuvuna, kupakia, kuuza na jinsi masoko yalivyo n.k. Huduma za jamii katika marneo ya vijijini n.k. Shughuri ndogondogo za wazalishaji wadogo na hata viwanda n.k. Hizi ndo habari haswa zetu watanzania na muitumie Azam one ioneshe hizi makala ili muonekane munaleta ubunifu. Katuni na vipindi vya nje havitusaidii sisi watz na msisahau hata siku ya uzinduzi wa studio Kikwete aliwaambia onesheni habari za kitanzania na muwe wazalendo, badala yake nyie mko na DW na makala zao za In Good Shape, hazisaidii sana.
 
Back
Top Bottom