Kama naanza kuichoka Azam TV vile

Kama naanza kuichoka Azam TV vile

ndg. Rweye asante kwa ushauri.
ila utaitwisha azam TV jukumu kubwa mno kama itaamua kufanya hayo mambo uliojadili ktk post yako.

content kama hizo zinapaswa kutengenezwa na idara inayo husika na elimu kwa wakulima pale wizara ya kilimo.

azam inacho weza kufanya ni kuingia mkataba na serikali kupitia wizara ya kilimo ili content hizo zirushwe hewani.

siyo kila jambo lifanywe na azam TV,ile siyo TV ya umma.jukumu hilo ni la TBC1.
 
Last edited by a moderator:
Ukweli nimetumia aina tofauti ya ving'amuzi Ila Azam pay tv wamejitahidi sana hawajafikia lengo la kunaliza haja za watazamaji wote Ila wameonyesha njia huwezi kulinganisha na watoa huduma wengine tz pia kuhusu vipindi vya chaneli zao ni kweli wanatakiwa kuvutia watazamaji kwa kuandaa vipindi vinavyoendana na mazingira ya watanzania bado hawajawa na vipindi shindani kulinganisha na local channels nyingine
 
ndg. Rweye asante kwa ushauri.
ila utaitwisha azam TV jukumu kubwa mno kama itaamua kufanya hayo mambo uliojadili ktk post yako.

content kama hizo zinapaswa kutengenezwa na idara inayo husika na elimu kwa wakulima pale wizara ya kilimo.

azam inacho weza kufanya ni kuingia mkataba na serikali kupitia wizara ya kilimo ili content hizo zirushwe hewani.

siyo kila jambo lifanywe na azam TV,ile siyo TV ya umma.jukumu hilo ni la TBC1.

Ok mkuu, adante sana.
 
Last edited by a moderator:
Kingne kinachoniuzi mm mvua ikianza tu kunyesha kinakata mawasiliano hata kama ni mvua ndogo,iwe na upepo au haina upepo hata kama ni ndogo aje lazima kizime,nauzika bas tu. Na wenzangu ni hivyo jamani? Au mm tu.

Hii ndio kero kubwa kupita zote. Vimanyunyu tu kwisha kazi. Sijui haya madude yao yana allergy na maji?
 
Nilikuwa na kimuhemuhe na kiroho papo kuwa na kisimbuzi cha Azam Tv ndio, ni kutokana na jinsi walivyokuwa wanajimwambafy (kujisifia kwa ubora wa miatambo na modern technology na watangazaji manguli), tuna studio bora kama za Al-Jazeera na BBC...l

Lakini pamoja na hayo yoote naona swala la uchangamfu wa channel zao na uchanganyaji picha, bado sanaaa.. Na hata ule ubunifu wa watangazaji kupresent taarifa ili kumvutia mtazamaji haupo..

Nilitegemea utumizi wa technology kama tunavyoona BBC na Al-Jazeera wanavyofanya bt kinyume chake naona hakuna utofauti na channel zingine ambazo si Pay Tv kama Clouds Tv n.k..

Utangazaji na uwasilishaji wa habari hauko designed, uondoshaji wa habari moja kwenda nyingine bado uko local sana... Bora hata kuangalia EATV wamechangamka na wanacheza na technology vizuri.. Sijui ni kwanini hawajilinganishi na international Tv, wanabaki kuwaza kushindana na local tv za kibongo..

Jueni kuwa tunatoa hela kupata huduma zenu..

Tangu uchaguzi uishe mi siangalii taarifa ya habari ya azam,zaidi zaidi naangaliaga mechi za vpl mara moja moja.
 
Ubaguzi wa rangi ni mkubwa sana hapa

Kila mtu anaponda chanell za kihindi

Racism
 
Ubaguzi wa rangi ni mkubwa sana hapa

Kila mtu anaponda chanell za kihindi

Racism

Yaaani kero zooote watu tumeweka tena kwa kuzirudia na msisitizo wewe umeona la wahindi kwako ndo focal? haya bwana make aliwazalo mtu ....
 
Sijui kwanini sijawahi na sina mpango wa kuitumia Azam, sijawahi kushawishika nao. Mi ni startimes na Dstv inatosha.

Duh, kesho nilitaka kwenda kununua kumbe ni majanga??

Sasa mnishauri kisembuzi kizuri nikipi?? Maana m nilitaka kwa ajir mpira, na ubora wa pc ninacho cha startimes yaan ni majanga,

Wadau plz ushaur

DSTV ila kina gharama kubwa premium 219,000 kwa mwezi
 
Kwa sisi masikini kwa kweli Azam bado inabamba... Unless una hela za kulipia dstv! Kwa umaskini wangu azam yatosha kwa sana namiss EPL na dora explorer tu
 
Azam hawaeleweki na wamefeli kwenye Marketing maana kila mwezi wanapandisha bei channel wanaziminya wakati nyingi ya hizi channel wao wanazipata bure kwenye Free to air satelite, Hotbird,Arab sat,Nile sat,Astra satelites. MBC ukiwa kenya tuu na dish la bure ukizitafuta unazipata sudan,misri,ethiopia,egypt mbc channels ni za bure isipokuwa labda dubai one. Muache ubabaishaji wezi wa makontena nyinyi. Mi nimelipa mnaniwekea channel zisizoeleweka nitawashitaki TCRA Kwenye Consumer consultative council.
 
Tatizo huku kwetu tanzania Tv channels hata Huduma za internet zinaonekana kama anasa na big deals wakati tech inavyopanda vitu hivyo vinashuka thamani asia na europe na vyatumika kama nyanja za maendeleo hususan internet
 
Tukifika level ya kuona internet sio anasa na utajiri hapo tutamshukuru sana waziri wa Science na Technology. Otherwise na yeye atakuwa mwajiriwa asiyetimiza majukumu yake. Hii fiber optic nilidhani itashusha gharama lakini hawa wasanii wa kampuni za simu ndio wanazidi kupandisha bei za bundle kiujanja na.kuja na majina vodacom red etc
 
Azam mmejitahidi sana kuboresha huduma zenu ijapo changamoto nazo huwa haziishi.

Leo langu moja tu, tunaomba chaneli walau moja tu ya movie ( actions ) za kichina i.e boxing, kung fu, judo, karate n.k. Sie wengine hayo ndo maujanja yetu na mkiwekea hii chaneli hakika tutafurahi sana
 
Back
Top Bottom