Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Kuna hili suala la watu kusema hata ukioa mwanamke ambaye kwao wana uwezo kukuzidi sio tatizo. Huko ni kujidanganya. Inakuwa sio tatizo labda mwaka wa kwanza wa ndoa yenu, wakati wa honeymoon period.
Ndani ya moyo wake, mkeo ambae ataishi na wewe katika mazingira duni kuliko ya nyumbani kwao ataanza tu kuya-miss mazingira ya nyumbani kwao.
Utakuta kila mwaka anataka aende likizo kwao, na wewe siku zote utakuwa unasita kwenda nae kwao, kwa sababu kila wanachofanya utaona ni kama wanakuonyesha maisha bora ya mke wako akiwa kwao kuliko unayompa. Ukiwa na shemeji zako wakati huo ndio kabisa.
Na utambue kuwa kila mkeo akienda kwao baba yake au mama yake huwa atamwita chemba na kumuuliza vipi mwanangu, mnamudu maisha? Unahitaji msaada wowote?
Kaka zake watakuwa wanatoa ofa za ada za shule, au kumkatia pochi, au namna tu fulani ya kumsaidia, mara nyingine kwa makusudi tu kukuonyesha humtunzi vema dada yao. Mkizaa watoto ndio kabisa, kila wakifunga shule utasikia baba tunataka kwenda kuwasalimia babu na bibi!
Changamoto ni kubwa zaidi kama mazingira ya kwenu wewe ni duni, maana itakuumiza kwamba watoto wako na mkeo wanasita kwenda kwenu kwa wazazi wako wakati wa likizo, hata kama mkeo anaonyesha angependa kwenda. Ujue huwa anawaita watoto chemba anawakemea kusema hawataki kwenda kwenu! Kwa hiyo pia, unapofanikiwa kimaisha, tengeneza mazingira mazuri kwenu pia.
Kwa hiyo bwana, ukioa, kwa udi na uvumba jitahidi kwamba mazingira ya nyumbani kwako yawe ni bora kuliko yale ya nyumbani kwa mkeo. Ukishindwa basi omba mkweo akusaidia ili kumtengenezea mwanae mazingira kama ya kwao alikotoka!