Elungata
JF-Expert Member
- Jan 28, 2011
- 40,205
- 33,224
Kama mungu yupo, kila utawala hutoka kwake, ,SIYO KILA UTAWALA HUTOKA KWA MUNGU.
Kwa nini Mungu aliwaepusha wana wa Israel na mateso ya Farao nchini Misri kama Falme zote zinatoka kwa Mungu? (Mwanzo 12:10-20, Mwanzo: 37-50. na Kutoka: 1-40)
Je nao utawala wa Nebucadnezar wa Babeli ulitoka kwa Mungu? Mbona aliwatumia manabii kuwatoa mikononi mwao na kuwarudisha Jerusalem ? (Ezra: 1-10)
Kwenye agano jipya Yesu mwenyewe amejaribiwa mara tatu na Shetani lakini amekaidi akiwa kwenye mfungo wa siku 40. (Luka 4:1-13). Yesu amekataa kumtii Herode alipomtaka ageuze maji ili iwe mvinyo ili amuachie baada ya Wayahudi kumkamata kabla ya kuhukumiwa na Ponsio Pilato.(Luka 23:7-15)
Hii ina maana kuna tawala dhalimu ambazo zinatoka kwa shetani lazima tuzikatae kwa nguvu zote kama Wakristu. Kinyume cha hapo ni kudhalilisha Ukristu wetu.
Utawala wa Magufuri ulitoka kwa shetani, siyo kwa Mungu wetu aliye hai, na tuliukataa kwa nguvu zote. Magufuri hakuwa na Mungu kabisa katika matendo na fikra zake. Mtawala anayetoka kwa Mungu hawezi kuwa na roho kama ya Magufuri inayotuma kuua Tundu Lissu, kuua Ben Saanane, Azory Gwanda.
Utawala unaotoka kwa Mungu hauwezi kubomoa nyumba za watu wa Kimara- Mbezi bila kuwafidia halafu ukaacha nyumba za Wasukuma wa Mwanza bila kuzibomoa.
Utawala unaotoka kwa Mungu hauwezi kukawafukuza wafanyakazi waliofoji vyeti vya Form IV ili wawe madreva na kumuacha Makonda aliyefoji cheti cha form IV na kuwa Mkuu wa Mkoa. Ndiyo maana ameondolewa pamoja na kuiba uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa 2019 na uchaguzi Mkuu wa 2020. Mungu hazihakiwi
Mfalme Daud alikua mzinifu, basha na muuaji mkubwa, , lakini ndo akaonekana mfalme shujaa na hata bwana wetu, yesu kristo alipewa jina la nick name akaitwa MWANA WA DAUDI..
Kila mamlaka iliyopo, ipo kwasababu maalumu, na zote zina ok kutoka kwa alietuumba