Kalonzo Musyoka ambaye ni kiongozi wa chama cha upinzani cha Wiper Democratic Movement na aliyewahi kuwa Makamu wa Rais wakati wa uongozi wa Mwai Kibaki, amesema wanafanya uchunguzi juu ya mauzo ya hisa yaliyofanyika hivi karibuni kwenye taasisi ya Nation Media Group kwa bwana Rostam Aziz, akisisitiza kuwa taasisi hiyo iliyoanzishwa na Aga Khan ilikuwa ni sehemu ya harakati na kupigania uhuru na kwamba uhuru wa vyombo vya habari haupaswi kuingiliwa
Pia soma
"Tunachunguza kwa umakini uuzaji wa hivi karibuni wa hisa nyingi za shirika la Nation Media Group. Hii ni kwa sababu ni moja ya taasisi zilizoanzishwa na marehemu Aga Khan, na Nation Media Group ilikuwa sehemu ya harakati za kupigania uhuru wa nchi hii.
Kwa hivyo, uhuru wa vyombo vya habari hauwezi kuingiliwa kamwe. Tutachunguza mambo haya ili kuona nini hasa kimetokea, kwani nimeambiwa kuwa kwa siri, shilingi milioni 866 zimewekwa kwenye bajeti ya ziada kupitia Idara ya Serikali ya Utangazaji ili pesa hizo zilipwe haraka sana.
Jiulizeni, ni nani anayepokea pesa hizi? Tunataka kumuuliza mmiliki huyo mpya, au mwanahisa mkuu, jinsi atakavyohakikisha uhuru wa shirika la Nation Media. Hiki ni chombo muhimu sana cha mawasiliano katika nchi hii na ni lazima ahakikishe uhuru huo unakuwepo.
La sivyo, kumbukeni rafiki yangu Raila Odinga aliwahi kusema kuwa punda amechoka. Punda alilia hapa kwa sababu ya taarifa zilizotolewa na Rigathi Gachagua. Wakenya wamechoka!" - alisema Kalonzo
Pia soma
- Rostam Aziz anunua kampuni ya Nation Media Group ya Kenya
- Rostam amesema uwekezaji wake katika Kampuni ya Nation Media Group (NMG) unalenga kupanua shughuli za kampuni hiyo na si kupunguza wafanyakazi
- Rostam Aziz: Wakenya lazima mbadilike, someni alama za nyakati, Kenya sio mkubwa kuliko wenzake wote