Biera
JF-Expert Member
- Dec 7, 2010
- 464
- 78
ZITTO ni PANDIKIZI la CCM lituachie chama chetu.
chama chenu wachaga na wakristo.
ZITTO ni PANDIKIZI la CCM lituachie chama chetu.
chama chenu wachaga na wakristo.
kwa mtanzania yoyote anayejua vizuri katiba ya nchi inasemaje kuhusu mgombea urais asingejiingiza kwenye propaganda za kumhusisha zitto na urais 2015!tumekuwa na watu ambao wamekuwa wepesi sana kuchangia mada na kupost thread za uchonganishi bila kufikiri impact zake!nadhani tuwe waelewa na tusiwe mstari wa mbele kuposha uma kwa maslahi yako au watu binafsi!cdm lazima kitasemwa sena, hujuma nyingi zitakiandama sana kwani ni chama chenye hoja, chama cha watu wenye akili na maono!chama kilichojawa watu makini walio tayari kubeba matumaini ya watanzania wengi!so sishangai kuona magazeti, blogs na nk wakikiandama pamoja na kuwaandama viongozi wake waandamizi!
,
tufike sehemu tusiwe mazuzu, tuangalie na kupima mstakabali wa nchi ukoje!maisha ya mtanzania wa sasa yako, afya ya mtanzania ikoje, elimu ya sasa ya mtanzania ikoje, miradi ya maendeleo ya nchi ikoje, tuende mbali zaidi tujadili hata siasa kandamizi zinazotokea nchini, uelewa wa viongozi wetu na uzalendo wao ukoje!hatima ya nchi ninini!HIVI UKIAMBIWA TANZANIA NI AUTOPILOT COUNTRY UTAKATAA???nadhani vyombo vya habari vingetumia nguvu yake kutusaidia kuendesha mijadara ya kujenga nchi na si kuandika maisha ya mtu kila siku, tyunaissue nyingi zinazolenga kila mtanzania mojakwamoja!tushachoka na habari za kujadili watu!hivi kuna gazeti lilishajaribu kujadili hatima ya vijana ikiwa ni pamoja na kutuunganisha vijana wote nchi kuwa na comon agenda??kuna gazeti lililotayari kutusisitizia umuhim wa kushikamana na kuwa kitu kimoja tunapotamka maslahi ya taifa?au kila siku fulani fulani fulani!we have a very hot and sensitive issues to discuss na sio upuuzi mnaoundekeza!
Omary mimi sijawahi kukupenda na huwa nakuchukia kabisa, lakini kwa hili nakubaliana na wewe.Salaam
Kuna wakati unaposoma akili za watu humu ndani na hasa wale wanaojitambulisha kama makada wa Chadema unaweza ama kukata tamaa na mabadiliko ya kweli katika nchi yetu ama hata kuamua kujilipua na kujiunga na CCM.
Inashangaza kuona kuna watu wanaojifaragua kama great minds wanakuwa rahisi kuamini sumu za kisiasa ambazo ukweli zinalenga kulinda maslahi ya watu kwa kuwaharibia sifa wengine.
Inakuwaje mtu mwenye akili zake timamu akaamini habari za kutengenezwa za udaku wa kisiasa unaomilikiwa na kufadhiliwa na mahasimu wa Zitto wakiwemo Kubenea na Mweka Hazina wa Kudumu wa Chadema Anthony Komu ambaye kwake yeye Zitto ni tishio kwa maslahi yake na maslahi ya "wenzake" wanaoamini kuwa Chadema ni chama chao?
Inakuwaje wanaojiita great minds kuwa tayari kuamini kuwa Zitto ana mpango wa kugombea urais mwaka 2015 wakati wote tunajuwa kuwa wakati huo atakuwa hajatimiza umri wa miaka 45.
Inasikitisha zaidi kuona kuwa kuna baadhi ya wapenzi wa Chadema wanamshutumu Zitto kwa madai ya kuonyesha dalili za kutaka kugombea Urais eti huku akijua kuwa chama chake tayari kina mgombea. Yaani Chama cha DEMOKRASIA na maendeleo tayari kina mgombea wa Urasi wa mwaka 2015 wakati ndio kwanza tupo mwaka 2011? Halafu mna jeuri ya kuwalaumu wengine kwa ukandamizaji wa haki za kidemokrasia...
Na hili suala la Zitto kuwa na nia ya kuivuruga CHADEMA eti kwa mipango yake ya kuhamia ama kugombea Urais kupitia NCCR linaonyesha dalili kubwa za kutokujiamini ndani ya kundi la wahafidhina wa Chadema. Iweje Zitto huyu mnayemtukana, kumpiga vita na hata kudai kuwa hana nguvu kisiasa suala ama hisia za yeye kuondoka Chadema kuhusishwa na nia ya kuvuruga chama chenu?
Lakini kama wanaDEMOKRASIA inakuwaje mnakuwa na mitazamo hasi ya nia ya mtu (kama ipo) ya kuhama chama kimoja kujiunga na chama kingine atakachoamini kuwa kinaendana na fikira, ndoto ama hata tamaa zake ziwe za kisiasa ama za hatima ya nchi yetu. Hizi si fikira za wanademokrasia, ni fikira za mafashisti wanye nia ya kutumia kauli mbiu za demokrasia kuhalalisha matamanio yao ya kifashisti.
Ninachosoma kutoka katika siasa hizi za kichokoraa zinazoendeshwa na makada na hata viongozi wa Chadema humu ndani ya jukwaa letu na kwengineko dhidi ya Zitto ni ishara za kutojiamini miongoni mwa establishment ya CHADEMA wenye mitazamo na malengo ya kihafidhina. Badala ya kufanya jitihada za kujisafisha na kujipanga upya kuondokana na tuhuma mbalimbali zinazowakabili zinazopelekea chama chao kuvikwa ama kujivika magamba mbalimbali kama ya udini, ukabila, ufisadi nk, wako busy kumsulubu mtu ambaye anaonekana kuwa kama kioo cha Chadema tofauti ambayo watanzania wangependa kuiona inakuwa na sio Chadema waliyoikumbatia wao.
Kwa ujumla na kwa jinsi nijuavyo mimi Zitto bado hajawahi kuwa na nia ya kuondoka CHADEMA ingawa kuna mengi yanayomvunja moyo kila kukicha. Lakini kama atakuja kuhama CHADEMA na kujiunga na NCCR naamini itakuwa ni suala la kiitikadi zaidi kuliko nafasi yake kisiasa.
NCCR tofauti na ilivyo CHADEMA, ni chama pekee cha upinzani chenye mizizi ya itikadi za KIJAMAA zilizojikita katika nia ya kujenga Tanzania yenye kujali na kuthamini utu. Na naamini mpaka sasa Zitto, Mnyika, Baregu, Kitila Mkumbo bado wanaamini katika itikadi ya UJAMAA ingawa wanalazimika kunyamazia sera, nyendo na matamanio ya kibepari ambao ndio mzizi wa CHADEMA.
Na ni wazi kuwa ili NCCR ifufuke na kuteka hisia za watanzania kuwa wanaweza kuwa chama mbadala wanachotamani kukiona na kukiunga mkono kwa dhati, kuna ulazima wa kubadili uongozi uliokuwepo na kusimika uongozi mpya utakaoweza kukipa uhai. Vilevile ni mabadiliko ya uongozi sasa ndiyo yatakayoweza kutoa nafasi kwa WAJAMAA MASALIA wanaolazimika ama kulazimishwa kubaki CHADEMA na CCM kupata uwanda wa kisiasa kujaribu kujenga Tanzania waitakayo na kurudisha siasa za kiitikadi badala kuendelea kutumika kuendeleza siasa za tuhuma, chuki, uzandiki, personalities na ujanjaujanja mwengine.
Napenda kuwaasa wale waliodedicate maisha na akili zao katika kummaliza Zitto iwe kisiasa ama kimaisha watambue kuwa adui wao sio Zitto bali yale anayoamini kuwa yanaopaswa kubadilishwa na kuepukwa na chama chake. Nguvu mnazotumia hapa kujaribu kumbomoa Zitto ni vizuri mkazitumia kujenga chama chenu kiweze kuaminika na watanzania na sio kuendelea kutegemea mtaji wa sumu ya chuki dhidi ya CCM na serikali yake tu.
Naamini historia ipo wazi kuwaamsha kuwa kwa siasa hizi za chuki na uzandiki, kamwe hamtaweza kupambana na nguvu na akili za Zitto kisiasa ..Lakini pia wakati mwengine mjaribu kuonyesha ubinadamu kidogo hata kama uungwana kwenu mwiko!
Mnachokifanya sasa hakina tofauti na aliyokuwa akiyafanya Mchungaji Mtikila wakati Mwalimu alipokuwa amelazwa hospitalini na hata baada ya kufairiki. Huu sio Utanzania!
Waweza kusema hili tena na tena, hakika UTU ndio falsafa ya NCCR-Mageuzi. Hakika ndio chama bora kabisa Tanzania kiitikadi kwa sasa. Hawa 'wengine', mara ubepari, mara katikati ..aagh!Salaam
NCCR tofauti na ilivyo CHADEMA, ni chama pekee cha upinzani chenye mizizi ya itikadi za KIJAMAA zilizojikita katika nia ya kujenga Tanzania yenye kujali na kuthamini utu. Na naamini mpaka sasa Zitto, Mnyika, Baregu, Kitila Mkumbo bado wanaamini katika itikadi ya UJAMAA ingawa wanalazimika kunyamazia sera, nyendo na matamanio ya kibepari ambao ndio mzizi wa CHADEMA.
Hii ameitoa wakati akijibu hoja/tuhuma za kuhusu yeye na Kafulila na kuivuruga NCCR kwa malengo yao binafsi..
"Gazeti la Mwanahalisi limekuwa ni gazeti linalonisakama sana kila kukicha lina ajenda yake. Gazeti ambalo limepoteza mvuto wake kwa jamii halinishughulishi. Hata juzi Mzee Samweli Sitta amelishutumu kwa kununuliwa na mafisadi na kutumiwa. Niseme nini zaidi kuhusu gazeti hili linaloongozwa na mtu ambaye hata hajamaliza darasa la saba. Mwanahalisi wanajua kwamba wakiandika habari yenye jina langu mauzo yao yanakua makubwa. Hili ni gazeti mufilisi ambalo kazi yake ni kutumiwa tu."
SOURCE;
JF
Sina uhakika na hiyo source, nafikiri hayo ni ya kutunga. Hata kama ingekuwa ni kweli, je ukweli unaosemwa na mtu aliyeishia darasa la nne hauwezi kukubaliwa katika jamii? Keyword ni UKWELI.
Ujasoma maelezo yake vizuri, amesema katiba haimruhusu kugombea urais na hata ikibadilishwa atagombea kwenye chama chake baada ya muafaka na wakuu wake hata ikiwa kweli zitto ni mwanachama na ana haki za kimsingi kugombea cheo chochote iwe ndani ya chama au nchiniNiliwahi kucoment kuhusu suala hili katika moja ya posts kwa facebook wall ya Zitto kipindi cha October - January wakati sakata lake likifukuta ndani ya CDM..alifuta comments zangu zote ambazo zilikuwa liked na watu kadhaa na kuni-block from friendship..!
I can bet..90% of this news is TRUE.
Unafikiri kwa nini alisema kwenye kampeni zake za ubunge mwaka jana huko Kigoma Kaskazini kwamba 2015 atarudi kama mgombea urais wakati huo huo chama chake kina mgombea wa urais na yeye bado hajajihakikishia kugombea kupitia CDM 2015!!!???
Wait and see.
hawamtaki Mbowe na Slaa kwa sababu ya misimamo yao makini.mbowe amekuwa kikwazo kikubwa sana kwa mamluki kuimaliza CDMNimeisoma hii thread yote nikataka nisichangie kabisa lakini nimeona niwaambie vijana wenzangu tunafanya makosa yale yale! Hii thread imeibua wapinzani wa Mbowe na wengine wazi wazi na wengine kwa kipropaganda wamemnanga Mbowe humu utafikiri wengine hatuelewi mlengo wao! Mbowe ana mapungufu kama binadamu lakini kama mwenyekiti ktk siasa za Tz anafanya kazi kubwa sana! Chama hakiwezi kuendelea kama kina mwenyekiti dhaifu,hali ya sasa ya CDM tunaiona na haijatokea kwa bahati mbaya bali uongozi bora chini ya Mbowe!
Hawa vijana wanaojifanya wanafamya siasa za hoja kwanini wasiendelee kumpinga Mbowe ndani ya chama kwa hizo hoja na kama kweli hoja ni za msingi zitashinda tu kwani CDM imesheheni wanachama makini tu. Hawa vijana wanaojiona "vichwa" kuliko wengine mbona dhamira zenu zina walakini? Hamumtaki Mbowe au mnataka demokrasia?
Kama kweli MwanaHalisi linaongozwa na darasa la saba basi angepata fooo ya fomu fooo mngemkoma! Hapo tu anawachachafya mpaka mnamuota mkiwa India......Poleni jamani.sie darasa la saba tunashida, mazereu yote kwetu
Mimi nikiona mtu anaanza kuattack personality ya mtu badala ya hoja naanza kupata mashaka. Ingekuwa vema akatuambia ni vipi hoja/habari iliyoandikwa na gazeti analolituhumu haina mashiko/ukweli badala ya kutuambia aliyeiandika hana elimu ya kutosha (hakumaliza hata darasa la saba!). Kimantiki kutomaliza darasa la saba, pekee, hakufanyi habari/hoja iliyoandikwa na muhusika kuwa ya uwongo.
Na kwa maoni yangu kama ni kweli huyo mmiliki/mwandishi hajamaliza darasa la saba basi ni wa kusifiwa zaidi kuliko kubezwa....nikijaribu kumlinganisha na hayo magazeti yaliyojaa wasomi kwa hakika sioni tofauti....sana sana amewazidi!. Lakini again, hili halifanyi kila anachoandika kuwa cha kweli pia....anaweza kununuliwa kama 'wengine' wanavyonunuliwa!
Ndo kagundua sasa kuwa katiba haimruhusu? Mbona alikwisha litamka hili hapo kabla? Zitto unaanza kuniangusha sana hivi sasa.....sipendi.Ujasoma maelezo yake vizuri, amesema katiba haimruhusu kugombea urais na hata ikibadilishwa atagombea kwenye chama chake baada ya muafaka na wakuu wake hata ikiwa kweli zitto ni mwanachama na ana haki za kimsingi kugombea cheo chochote iwe ndani ya chama au nchini
Na sisi watanzania tusipende kusema bila kufanya uchunguzi,tujiulize ni kwa nini asemee mwanahalisi.Na yeye anatumiwa na nani.ni mbatia au ni nani hasa.
Tangu lini Mbatia akawa mpinzani hadi ionekane anayetaka kumpindua ni mhaini asiye na nia nzuri. Ni nani ndani ya hicho chama chao alishawahi kuhoji dhamira ya mbatia hasa pale anaposimamia mstari tata wenye mwelekeo wa mahaba na CCM.
Tatizo wenyeviti wa vyama vya siasa Tanzanzania hawataki challenge wanandhani uenyekiti ni haki ya kuzaliwa.hizi hulka za do or die political mentality zinadumaza demokrasia. Baadhi ya Wenyeviti wa vyama vya siasa na hasa upinzani wana mawazo ya kijima katika kufanya siasa na imefikia hatua wanaogopa watu wanaowapa changamoto za kweli na hasa vijana.Hili ni pigo kwa demokrasia.
Sitaki kuingilia mambo ya ndani ya NCCR lakini tujiulize ina maana huko NCCR hakuna mwenye haki ya kupinga mwenyekiti au kugombea nafasi ya juu ya uongozi ndani ya chama hicho...na je ina maana Mbatia ndiye mwenye kauli ya mwisho katika kupitisha nani awe mgombea urais kupitia NCCR....
WanaJF, ukiona Mbunge anajadili watu bila kuwa na uhakika wa anachosema ujue ni dalili za watu kuwa na ombwe la fikra. Sisi tunaingia mkenge kisa kasema mtu ambaye unamkubali SANA ! ! ! Tunaacha kufikiri kwa sababu mtu unayemkubali sana kasema, tuwe makini yasije yakatukuta yale ya Kibwetere kule Uganda