Kafulila na Zitto wanaivuruga NCCR - Moses Machali

Kafulila na Zitto wanaivuruga NCCR - Moses Machali

Status
Not open for further replies.
OmarIlyas,
Wow! nimekusoma na hakika unatisha lakini pale tu ulipoandika haya sasa ndio naipata picha halisi..Umeandika:-

"Kwa ujumla na kwa jinsi nijuavyo mimi Zitto bado hajawahi kuwa na nia ya kuondoka CHADEMA ingawa kuna mengi yanayomvunja moyo kila kukicha. Lakini kama atakuja kuhama CHADEMA na kujiunga na NCCR naamini itakuwa ni suala la kiitikadi zaidi kuliko nafasi yake kisiasa.

NCCR tofauti na ilivyo CHADEMA, ni chama pekee cha upinzani chenye mizizi ya itikadi za KIJAMAA zilizojikita katika nia ya kujenga Tanzania yenye kujali na kuthamini utu. Na naamini mpaka sasa Zitto, Mnyika, Baregu, Kitila Mkumbo bado wanaamini katika itikadi ya UJAMAA ingawa wanalazimika kunyamazia sera, nyendo na matamanio ya kibepari ambao ndio mzizi wa CHADEMA na unaolindwa na kuendelezwa na mahafidhina wa chama hicho ambao hawaishi kufanya kila wawezalo kutumia frustrations za watanzania waliowengi kwa ajili ya maslahi yao binafsi na chama chao nay a watanzania wote kama wanavyolaghai.

Na ni wazi kuwa ili NCCR ifufuke na kuteka hisia za watanzania kuwa wanaweza kuwa chama mbadala wanachotamani kukiona na kukiunga mkono kwa dhati, kuna ulazima wa kubadili uongozi uliokuwepo na kusimika uongozi mpya utakaoweza kukipa uhai. Vilevile ni mabadiliko ya uongozi sasa ndiyo yatakayoweza kutoa nafasi kwa WAJAMAA MASALIA wanaolazimika ama kulazimishwa kubaki CHADEMA na CCM kupata uwanda wa kisiasa kujaribu kujenga Tanzania waitakayo na kurudisha siasa za kiitikadi badala kuendelea kutumika kuendeleza siasa za tuhuma, chuki, uzandiki, personalities na ujanjaujanja mwengine."

Kumbuka hapa ni uwanja wa great thinkers.. tunaweza kujumlisha mawazo ya mtu na tukapata jibu..
Ndugu Mkandara,
Nashawishika kuamini kwamba Ndg. OmariIlyas amesoma na kuelewa nyaraka za NCCR-Mageuzi zinazoeleza falsafa na itikadi za chama hiki. Hivyo haya si mawazo yake tu.
 
Wanabodi,

Kwanza kabisa napenda kuwaonya wale wote wanaojaribu kwa nguvu zote kukiua chama cha Chadema kwamba hawatafanikiwa na kama watafanikiwa ni kwa sababu viongozi wa Chadema wenyewe wamepuuzia haya nitakayo andika.

Kutoka reliable sources ambayo ziwezi kuzietaja hapa ni kwamba Chadema kaa chama kinapigwa vita kubwa sana na CCM na vyombo vya usalama vinatumika sana ktk kuendesha zoezi kali na kubwa la kukiua chama. Kuna watu wawili ambao ni tishio kubwa la uongozi wa CCM nao ni Mbowe na Zitto ambao kwa imani yao ndio nguzo ya chama na wanatakiwa kushughulikiwa haraka na mapema..

Kazi hii haikuanza jana imeanza toka mwaka 2003 au 2004 kwa kutengenezwa nyaraka za siri ambazo aidha zinamhusisha Zitto au Mbowe ktk kuleta Upinzani baina yao wenyewe. Hawa wote wawili kama wapo hapa nawaomba wanisome vizuri na kama nasema uongo wanirudi na kupinga maelezo yangu. Kwa nyuakati Tofauti Mbowe au Zitto wamekuwa wakiletewa habari zingine zenye uthibitisho wa kimaandishi jinsi mmoja wao anavyompiga vita mwenzake na kwa bahati mbaya kila mmoja wao amefikia kuamini yale aloyaona na kufikia kweli kuamini na kujenga uhasama baina yao...

Navyoandika hapa Zitto ana ushahidi dhidi ya Mbowe vile vile Mbowe ana ushahidi dhidi ya Zitto na wote hawajawahi kukaa na kuzungumzia maswala haya isipokuwa kila mmoja anamtazama mwenzake kama mchawi bila kufahamu ya kwamba uchawi huu umetengenezwa kisayansi na utakubalika kwa kila hali na kuponza mahusiano ya viongozi hawa. Binafsi naamini kabisa Zitto na washabiki wake waligombea Uenyekiti wa chama kwa sababu walitaka tu kugombea kiti hicho kidemokrasia isipokuwa kwa dhana ya kwamba Chadema inatakiwa kuokolewa toka mikononi mwa Mbowe vile vile Mbowe na washabiki wake walikataa Upinzani wa Zitto kwa imani kwamba Zitto alikuwa analengo la kukiua chama..

Hivi zote ni habari walizolishwa pande zote mbili, namwona OmarIlyas akizungumza kwa machungu na jazba kubwa dhidi ya Mbowe lakini sintomlaumu kwa sababu kawa feeded information ambazo anaamini sawa na kina Mnyika ambao wanayajua mengi ya Zitto kulingana na walicholishwa toka zamani na sasa hivi wanafanya wao wenyewe. Makundi yote haya mawili hawaaminiani kwa sababu Usalama wa Taifa wameisha ifanya kazi yao na kinachosubiriwa tu ni kifo cha Chadema kupitia hawa watu wawili..

Dr.Slaa alikuwa tishio lakini sii tena kwa sababu naye walimjengea Udini na kundi la watu kumpa nafasi kubwa ya kuwa katikati ya mzozo huu mkubwa wa viongozi. Kama mnakumbuka nilipotoa pendekezo la Dr.Slaa kugombea kiti cha Urais ilikuwa na sababu na kusema kweli CCM walikuwa hawakujiandaa kwa hilo..Nilitegemea kabisa Dr.Slaa atashinda uchaguzi huo lakini wakatafuta mbinu ya Udini na ikaweza kufanya kazi japokuwa lengo kubwa la CCM lilikuwa kuleta mgogoro ndani ya Chadema kwa kupitia Mbowe na Zitto..

Kwa hiyo tuwe makini sana na jitihada za CCM ktk kukibomoa chama. Zitto kayafanya makosa aloyafanya ni kutokana na jinsi alivyolishwa na Mbowe pia amekuwa akilishwa habari mbaya dhidi ya Zitto lakini nawahakikishia hakuna lolote kubwa la ukweli isipokuwa chuki imeundwa. Zipo Nyaraka za Udini na zina mihuri ya Chadema, zipo nyaraka, sms, e-mails za Chadema, Zitto na Mbowe ambazo zimetengenezwa kwa utaalam mkubwa kuonyesha aidha chuki baina yao au agenda za chama na Udini ili mradi CCM na wana IT wake wanaifanya kazi kubwa ya kukibomoa chama kutoka ndani... kazi hii haikuanza jana na sasa hivi tunaona matunda ya kazi kubwa ilitangulia. Mbowe ataendelea kuwa kiongozi bora wa chama kisiasa na Zitto ataendelea kuwa kiongozi bora wa kisera na utekelezaji.

Jihadharini sana na nguvu ya kiza!.. Masalaam.

Mkuu huwajuii vyema hawa jamaa wawili (Mbowe na Zitto) ndio maana ndio maana unawaongea hivyo, au la upo kazini na mara zote kila kosa linarushiwa UWT na hata pale ambao ipo wazi kuwa wajanja wajanja, wasani, wabinafsi, na waroho wa madaraka wachache wanapobainika kwa kuweka uzembe wao mbale ya maslahi ya Umma na hata wanapo uwa vyama kwa ubinafsi wao bado UWT inarushiwa lawama zote.

Ukweli ni kuwa UWT haina muda, nia wala sababu ya kuuwa chama chochote hapa nchni na mara zote wamekuwa mstari wa mbele kuvijenga hivyo vyama ndio maana hata JF imepata kuwepo hapa nchni yote hii ni bayana ya kuwa UWT na vyombo vyetu vya Usalama vyote havina nia hiyo unayoihubiri hapa, vyama vyote vinakufa na vitakufa kutokana na wanasiasa uchwara tulionao, tokea kuanza kwa siasa ya vyama vingi hii imekuwa bahati mbaya ya Tanzania kuwa vyama vya upinzani vimekuwa bila watu makini na wa kweli bali mmoja mmoja katika vyama. Hawa unaowasema wewe huwajui na hakika watu waongo na wanaotumiwa kama wewe ndio mliotuletea Kikwete 2005, mkome na mjuwe tumewachoka na hakuna nafasi tena ya watu wahuni na wenye ukoma wa ubongo kupewa nafasi katika nchni hii tena maana hatutaki kurudi nyuma na hata kuingia vitani kama. Hao ni wezi na Mafisadi kuliko kama RA, EL na Wengineo wote unawajuwa.
 
mimi nina hakika asilimia mia moja.anachosema machali ni ukweli na huyu jamaa na mpaka vizuri na kafulila pia nimeishia naye.hivyo huo ndy ukweli h6nhesa macia

mmh! kwa hili kaka/dada unaniangusha, huwezi kutumia vigezo vya kuishi naye ukampa 100% hata kama angekuwa mwanao!!!!
Huwezi kushawishi umma kwa hili as far as human psychology is concerning, you seem to know very little this concept au ni ushabiki tu au huelewi unaposema unauhakika wa 100% una maanisha nini!!!!!!!
 
Zittophobia na siasa za kichokoraa za wakombozi wetu…
Kuna wakati unaposoma akili za watu katika jukwaa la Jamiiforums na hasa wale wanaojitambulisha kama makada wa Chadema unaweza ama kukata tamaa na mabadiliko ya kweli katika nchi yetu ama hata kuamua kujilipua na kujiunga na CCM.

Inashangaza kuona kuna watu wanaojifaragua kama “great minds” wanakuwa rahisi kuamini sumu za kisiasa ambazo ukweli zinalenga kulinda maslahi ya watu kwa kuwaharibia sifa wengine na hata kubomoa misingi mikuu ya utanzania ambayo ni utu, umoja na amani.

Inakuwaje mtu mwenye akili zake timamu akaamini habari za kutengenezwa za udaku wa kisiasa unaomilikiwa na kufadhiliwa na mahasimu wa kisiasa na kibinafsi wa Zitto wakiwemo Kubenea na Mweka Hazina wa Kudumu wa Chadema Anthony Komu ambaye kwake yeye Zitto ni tishio kwa maslahi yake na maslahi ya "wenzake" wanaoamini kuwa Chadema ni chama chao?

Inakuwaje wanaojiita “great minds” kuwa tayari kuamini kuwa Zitto ana mpango wa kugombea urais mwaka 2015 wakati wote tunajuwa kuwa wakati huo atakuwa hajatimiza umri wa miaka 45.

Inasikitisha zaidi kuona kuwa kuna baadhi ya wapenzi wa Chadema wanamshutumu Zitto kwa madai ya kuonyesha dalili za kutaka kugombea Urais eti huku akijua kuwa chama chake tayari kina mgombea. Yaani Chama cha DEMOKRASIA na maendeleo tayari kina mgombea wa Urasi wa mwaka 2015 wakati ndio kwanza tupo mwaka 2011? Halafu wana jeuri ya kuwalaumu wengine kwa ukandamizaji wa haki za kidemokrasia.

Na hili suala la Zitto kuwa na nia ya kuivuruga CHADEMA eti kwa mipango yake ya kuhamia ama kugombea Urais kupitia NCCR linaonyesha dalili kubwa za kutokujiamini ndani ya kundi la wahafidhina wa Chadema. Iweje Zitto huyu mnayemtukana, kumpiga vita na hata kudai kuwa hana nguvu kisiasa ama hisia za yeye kuondoka Chadema kuhusishwa na nia ya kuvuruga chama hicho? Kama kweli yeye ni kama wanavyotaka watu waamini na kuwa hana umaarufu tena kama hapo awali kuondoka kwake si ndio kulitakiwa kuonekana kama baraka kwa Chadema?

Lakini kama wanaDEMOKRASIA inakuwaje mnakuwa na mitazamo hasi ya nia ya mtu (kama ipo) ya kuhama chama kimoja kujiunga na chama kingine atakachoamini kuwa kinaendana na fikira, ndoto ama hata tamaa zake ziwe za kisiasa ama za hatima ya nchi yetu. Hizi si fikira za wanademokrasia, ni fikira za mafashisti wanye nia ya kutumia kauli mbiu za demokrasia kuhalalisha matamanio yao ya kifashisti.

Ninachosoma kutoka katika siasa hizi za kichokoraa zinazoendeshwa na makada na hata viongozi wa Chadema humu ndani ya jukwaa letu na kwengineko dhidi ya Zitto ni ishara za kutojiamini miongoni mwa establishment ya CHADEMA wenye mitazamo na malengo ya kihafidhina. Badala ya kufanya jitihada za kujisafisha na kujipanga upya kuondokana na tuhuma mbalimbali zinazowakabili zinazopelekea chama chao kuvikwa ama kujivika magamba mbalimbali kama ya udini, ukabila, ufisadi nk, wako busy kumsulubu mtu ambaye anaonekana kuwa kama kioo cha Chadema tofauti ambayo watanzania wangependa kuiona inakuwa na sio Chadema waliyoikumbatia wao. Chadema yenye kufikiri na kutenda kidemokrasia. Chadema yenye kuongoza katika kuleta suluhu ya matatizo ya watanzania na nchi kwa ujumla na sio kuongeza, kupalilia na hata kufurahia kuongezeka kwa matatizo hayo.

Kwa ujumla na kwa jinsi nijuavyo mimi Zitto bado hajawahi kuwa na nia ya kuondoka CHADEMA ingawa kuna mengi yanayomvunja moyo kila kukicha. Lakini kama atakuja kuhama CHADEMA na kujiunga na NCCR naamini itakuwa ni suala la kiitikadi zaidi kuliko nafasi yake kisiasa.

NCCR tofauti na ilivyo CHADEMA, ni chama pekee cha upinzani chenye mizizi ya itikadi za KIJAMAA zilizojikita katika nia ya kujenga Tanzania yenye kujali na kuthamini utu. Na naamini mpaka sasa Zitto, Mnyika, Baregu, Kitila Mkumbo bado wanaamini katika itikadi ya UJAMAA ingawa wanalazimika kunyamazia sera, nyendo na matamanio ya kibepari ambao ndio mzizi wa CHADEMA na unaolindwa na kuendelezwa na mahafidhina wa chama hicho ambao hawaishi kufanya kila wawezalo kutumia frustrations za watanzania waliowengi kwa ajili ya maslahi yao binafsi na chama chao nay a watanzania wote kama wanavyolaghai.

Na ni wazi kuwa ili NCCR ifufuke na kuteka hisia za watanzania kuwa wanaweza kuwa chama mbadala wanachotamani kukiona na kukiunga mkono kwa dhati, kuna ulazima wa kubadili uongozi uliokuwepo na kusimika uongozi mpya utakaoweza kukipa uhai. Vilevile ni mabadiliko ya uongozi sasa ndiyo yatakayoweza kutoa nafasi kwa WAJAMAA MASALIA wanaolazimika ama kulazimishwa kubaki CHADEMA na CCM kupata uwanda wa kisiasa kujaribu kujenga Tanzania waitakayo na kurudisha siasa za kiitikadi badala kuendelea kutumika kuendeleza siasa za tuhuma, chuki, uzandiki, personalities na ujanjaujanja mwengine.

Napenda kuwaasa wale waliodedicate maisha na akili zao katika kummaliza Zitto iwe kisiasa ama kimaisha watambue kuwa adui wao sio Zitto bali yale anayoamini kuwa yanaopaswa kubadilishwa na kuepukwa na chama chake. Nguvu mnazotumia hapa kujaribu kumbomoa Zitto ni vizuri mkazitumia kujenga chama chenu kiweze kuaminika na watanzania na sio kuendelea kutegemea mtaji wa sumu ya chuki dhidi ya CCM na serikali yake tu.

Naamini historia ipo wazi kuwaamsha kuwa kwa siasa hizi za chuki na uzandiki, kamwe hamtaweza kupambana na nguvu na akili za Zitto kisiasa. Lakini pia wakati mwengine mjaribu kuonyesha ubinadamu kidogo hata kama uungwana kwenu mwiko.

Mnachokifanya sasa hakina tofauti na aliyokuwa akiyafanya Mchungaji Mtikila wakati Mwalimu alipokuwa amelazwa hospitalini na hata baada ya kufairiki. Huu sio Utanzania!

Kuna wale wanaojidanganya kuwa udikteta wa Mbowe ni sawa kwani una nia ya kuzuia Chadema isitekwe na CCM.

Hivi Mbowe huyu aliyefanya makubaliano na wanamtandao mwaka 2005 ili kuitumia Chadema kuwatishia CCM wabadili taratibu na kumbeba mgombea wao.

Mbowe huyuhuyu ambaye kwa makubaliano maalum alikubali gazeti lake la TanzaniaDaima kutumika na kina Lowassa na Rostam kufanyia kampeni za kumjenga mgombea wao na kuwabomoa na kuwatukana wagombea wengine.

Mbowe huyuhuyu aliyefikia kuruhusu waajiriwa wake wa TanzaniaDaima kulipwa mishahara na marupurupu mengine ikiwemo kwenda kusomeshwa nje na kina Roastam wa CCM.

Mbowe huyu ambaye tangia miaka hiyo hadi leo ameingia makubaliano maalum ya kuhakikisha kuwa Magazeti yake yanatumika ama kwa kusifia, kutetea ama kukandamiza habari zinazohusu uchafu wa wanaoitwa MAFISADI wa CCM na pia kukubaliana kutoshambuliana nao kupitia majukwaa na vyombo vyao vya habari.

Mbowe huyuhuyu ambaye mwaka 2015 alilazimisha kuchelewesha uteuzi wa mgombea wa Chadema ili kusubiria kuokoteza mabaki ya CCM endapo Samwel Sitta atatimuliwa ama kujitoa CCm ili agombee Chadema.

Mbowe huyuhuyu ambaye amekuwa akipokea misaada ya kuchangia Chadema kutoka kwa vinara wa sura ya UFISADI CCM na kudai kuwa ni fedha zake hivyo akiwakopesha Chadema.

Mbowe huyuhuyu ambaye siku hizi amekuwa akimtumia Kada wa CCM Mzee Sabodo kupokea michango ya haohao mnaowaita MAFISADI wa CCM na hasa watanzania wenye asili ya Uhindi.

Leo hii ndio mnataka kudanganya watu kuwa Mbowe huyu amekuwa kikwazo kikubwa sana kwa mamluki kuimaliza CDM? Kweli omba Mungu akunyime mali lakini sio akili.

CLARIFICATION: Nakubali kuwa uongozi wa Mbowe uliweza kusaidia sana kukuwa kwa Chadema hadi pale wale aliokuwa akiwaamini kuwa wanasaidia ukuaji huo walipoanza kuhoji uadilifu wake na kutishia nafasi yake katika chama na ndoto ya kugombea Urasi ambayo ukweli hadi mwaka 2005 hakuwa nayo lakini makundi yaliyovutiwa na Helikopta yakamdanganya kuwa anaweza.

Naamini kuwa hadi hivi sasa Mbowe amekuwa nguzo ya busara za kisiasa (zenye malengo ya kujijenga kama Kiongozi Mkomavu anayeweza kuwa Rais we nchi kuliko uhalisia wake) ndani ya Chadema ambayo inaelekea kutekwa na wanasiasa waliokosa busara za kiuongozi na kupenda kuamini katika siasa za kichokoraa ambazo ukweli zimeonyesha mafanikio kwa maslahi yao binafsi na chama hasa ukizingatia na hali ya kukosa matumaini ndani ya CCM miongoni mwa watanzania wengi. Ni wazi hata kule Arusha Mbowe alikuwa akijaribu kuinspire busara za kumtoa Lema ili kupre-empty nia halisi ya Lema ambayo ni kuzusha Popular Protest ambaye ingemjenga yeye (LEMA) binafsi zaidi kuliko chama na kuendeleza jitihada zake na wanasiasa wa aina yake ndani na nje ya Chadema katika kuigawanya na hata kuvunja msingi wa Umoja na Amani wa Taifa.

Lakini kamwe siwezi kumuamini Mbowe kama ana uwezo, uaminifu na uadilifu wa kuwa Rais wa nchi kwa maslahi ya Watanzania walio wengi...Na wala siamini kuwa yeye ndiyo mzalendo zaidi wa Chadema kuliko Zitto na wengine...Na zaidi yeye ni mabaki ya waumini wa siasa za kidikteta ambao wanapenda kutrumia kauli mbiu za demokrasia pale tu ambapo kuna maslahi yao ya kuyalinda ama kuyatekeleza lakini sio kama muumini wa kweli wa UANADEMOKRASIA.

Why namshambulia Mbowe? Kwa sababu naamini kuwa yeye ndiyo sura na kinara wa siasa za chuki na ujanjaujanja ndani ya Chadema ambayo huelekezwa dhidi ya wote anaowaona kuwa wanatishia nafasi yake kama ilivyokuwa kwa Walid Kaborou na Marehemu Chacha wangwe na sasa wakiwemo Dr Slaa na Zitto kwa pamoja.....kama ambavyo Lowassa alivyo sura ama kinara wa maslahi ya wanasiasa MAFISADI na hovyohovyo pamoja na mabaki ya fikira za kidikteta CCM.

Umeandika mengi lakini mtu makini akisoma ataona wazi kuwa ni mengi yasiyo na kitu tangible. Yote aliyoandika ni ya kufikirika zaidi kuliko kuwa yaliyo na uhakika. Hayo makubaliano mengi uliyoyaandika unaweza kutuletea ushahidi? Maana kuandika kama ulivyoandika, yeyote anaweza kuandika hata pasipokuwa na ukweli. Umelishambulia sana gazeti la Tanzania Daima, lakini gazeti hilo halimilikiwi na Mbowe pekee yake, japo inawezekana yeye akawa na hisa kubwa kuliko wenzake - hilo sina uhakika. Lakini mmiliki wa gazeti ndiye anakuwa mwandishi wa gazeti analomiliki? Gazeti hili, licha ya wamiliki wake kuwa ni wa CHADEMA, wakati wa uchaguzi wa mwakajana lilitajwa kuwa ndilo gazeti lililoongoza kwa kuandika habari za vyama vyote bila upendeleo. Uliyoyaandika mpaka sasa yanaonekana kuwa ni majungu zaidi kuliko kuwa habari.
 
Zitto ni mnafiki tu kama wanafiki wengine kina omarIlyas wanaandika topic ndefu upupu mtupu, group lenu ben, pasco, waberoya makandara hamtafanikiwa hata mkihamia wote NCCR na zitto awe mwenyekiti wenu you will always be losers. Mmeulizwa maswali ya msingi hamtaki kujibu badala yake mnarukia masuala ya Mbowe, mmeulizwa kwanini mgombea wa Musoma vijijini alijitoa, kwanini Zitto aliandika barua kuachia jimbo la Pinda, kwanini Zitto hakukisaidia chama kupata wabunge Kigoma? badala yake akaisaidia NCCR kwa kujifanya yeye ni mbunge wa kitaifa? kwanini alikuwa anachagua wabunge wa kupigia kampeni kama Kibaha mjini na Lindi? (alikwenda musoma kuficha unafiki), kwa nini katikati ya kampeni alikwenda nje kwa muda mrefu na kukiacha chama? haya ni yale yanayoonekana kwa macho achilia mbali yasiyoonekana kama ya kuwasiliana na mtu wa usalama na ufadhili wa king makers na ya kupingana mara kwa mara na uongozi wa chama hadi kupelekea wabunge wenzake kumtenga(bagamoyo). Kabla ya kukimbilia kujadili ya Mbowe jibuni kwanza hoja iliyopo ya yeye kutaka kumpindua Mbatia.
 
Wewe ndo mnafiki mkubwa! aliyejitoa mwingine unalaumu mwingine. Unahitaji elimu gani kujua kua wakati akizunguka kwenye majimbo ya wengine wananchi wa Kigoma Kaskazini walikua wanamuhitaji. Acha unafiki tutajie Mbunge(Mgombea) aliyezunguka majimbo mengi kuliko Zitto. Alijiatahidi kutumia vizuri muda wake kwa kufanya kampeni jimboni kwake na kuzungukia majimbo ya wenzake hilo halipingiki hata kama hutaki kulikubali.
 
Kauli tata za Zitto
Imechapwa na MwanaHALISI - 13 Januari 2010

MBUNGE wa Chadema katika jimbo la Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe ameibua mjadala mwingine. Anasema siasa halikuwa "chaguo la kwanza" katika maisha yake.

Bali Zitto anasema, “nimeingia katika siasa kwa bahati mbaya,” na kwamba kazi anayoipenda zaidi ni ualimu. Anajiandaa kwa kazi hiyo.
Alitoa kauli hiyo katika mahojiano aliyofanya na kituo cha televisheni cha TBC1 na kunukuliwa na vyombo vingine vya habari tarehe 4 Januari 2010.
Kauli ya Zitto, imekuja takribani miezi mitano tangu kumalizika kwa kinyang’anyiro cha uchaguzi mkuu ndani ya chama chake. Yeye aligombea nafasi ya uenyekiti.
Hii si mara ya kwanza kwa Zitto kutoa kauli zenye utata. Wakati mwingine kauli zake zinatofautiana hata na msimamo wa chama chake.
Ni kweli kuwa Zitto ni mtu huru. Aweza kuamua na kutenda atakacho. Lakini huyu ni kiongozi. Ni kioo ndani ya chama na jamii. Kauli yake yoyote inachukuliwa kwa uzito unaostahili ndani na nje ya chama chake.
Wiki iliyopita, mshiriki wa kongamano la wanachuo wa Chadema, Owawa Steven alisema wengi wa vijana waliohudhuria kongamano walivutika na mwelekeo wa Zitto.
Sasa swali muhimu la kujiuliza ni hili: Kwa nini Zitto anapenda kuzungumza vitu ambavyo vinazua mjadala unaoweza kuangamiza kisiasa hata yeye mwenyewe?
Kwa mfano, kama Zitto anasema “siasa halikuwa chaguo lake la kwanza,” kwa nini aligombea uenyekiti wa Chadema kumpinga Freeman Mbowe?
Alitaka kugombea ili iweje? Kwa faida ya nani? Nani alishinikiza Zitto kugombea nafasi hiyo?
Je, alitaka akishinda afanye nini? Angelipa nini wale waliomsukuma kugombea – kama hakuwa amegombea kwa utashi wake?
Maswali yaweza kuwa mengi. Kwa mfano, wengine wangeuliza: Aligombea kwa lengo lipi? Kuvuruga Chadema au kuimarisha?
Mapema mwaka jana Zitto alishinikiza serikali kununua mitambo ya kampuni ya kitapeli ya Richmond/Dowans hadi kuibua mjadala mpana ndani na nje ya Bunge.
Alitenda hivyo huku akijua kuwa msimamo wa chama chake, ni kutaifishwa kwa mitambo hiyo.
Hata pale Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Dk. Idris Rashid walipotangazia ulimwengu kuwa wamesitisha mpango wa kununua mitambo hiyo, bado Zitto aliendelea kung’ang’ania mitambo inunuliwe, kana kwamba taifa zima linamulikwa na Dowans.
Zitto alitenda yote hayo huku akijua kwamba Sheria ya Manunuzi ya Umma (PPRA) ya mwaka 2004 katika kifungu cha 58 (3) inakataza kabisa ununuzi wa mitambo chakavu.
Majuzi, Zitto amenukuliwa akimtetea David Kafulila, aliyekuwa “karani” katika kurugenzi ya habari ya Chadema.
Kafulila alienguliwa katika nafasi yake kutokana na kile Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa alichoita, “utovu wa nidhamu.”
Tayari Kafulila ametimkia chama cha NCCR- Mageuzi. Lakini Zitto anasema atakufa na Kafulila na atatumia kila uwezo wake kuhakikisha anatingia bungeni kabla ya John Mnyika, mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa Chadema.
Hii ina maana kwamba Zitto yuko tayari kusaliti hata chama chake, iwapo kitaamua kusimamisha mgombea katika jimbo la Kigoma Kusini ambako Kafulila anatajwa kugombea.
Kama hivi ndivyo Zitto anavyotenda na kuamini, inawezekana kuwa hakustahili kuwa mwanasiasa, na kwamba aliingia katika kapu hilo kwa bahati mbaya. Tusubiri mwisho wake tuone!
 
Username: *
Password: *

[h=2]MAONI YA WASOMAJI[/h]

endelea

[h=2]KURA YA MAONI[/h] Je CHADEMA wako sahihi kukataa kuyatambua matokeo ya uchaguzi Igunga?
Ndiyo

85%
Hapana

11%
Sijui

[h=1]Zitto Kabwe: Kumbikumbi huruka na kuliwa na kunguru[/h]

Magari hayo anayatoa kama msaada kwa Kafulila ili aweze kushinda kampeni za ubunge katika jimbo la Kigoma Kusini. Hizi ni habari zinazozua maswali mengi, ikiwamo utajiri na uwezo wa Zitto kiuchumi.
Je, inakuwaje Zitto aweze kumiliki magari matatu wakati kipato chake kinajulikana? Lakini la pili, Kafulila na Zitto wanawezaje kuanza kampeni za ubunge wakati Tume ya Taifa ya Uchaguzi haijatangaza?
Tayari Zitto amekaririwa akisema, "Ni jambo la msingi kupunguza idadi ya wabunge wa CCM…ndiyo maana nimeamua kumsaidia Kafulila katika chama alichopo (NCCR-Mageuzi). Nipo tayari kujitolea kwa kijana mwingine anayegombea, hata kwa chama kingine, isipokuwa CCM."
Kwa maneno ya Zitto ni kwamba anamuunga mkono Kafulila, ingawa bado anadai yuko CHADEMA. Ni ajabu kidogo. Je, kama CHADEMA wataamua kusimamisha mgombea Kigoma Kusini wakati Zitto ana mtu wake, atamuunga mkono nani kati ya mgombea wa chama anachodai kimemlea na kumkuza na kumfikisha hapo alipo na rafiki yake kipenzi?
Si vizuri kumsemea Zitto wala Kafulila. Kuna haja ya CHADEMA kuuliza swali hili kabla mambo hayajafika huko. Kwa sasa, Zitto ama kwa kujua au vinginevo, anaanza kujiona maarufu kuliko chama, kama Jakaya Kikwete-kwa mujibu wa maneno ya katibu mkuu wa CCM, Yusufu Makamba.
Ifahamike. Kumbikumbi akaribiapo mauti huotesha mbawa na kuruka na kuishia kuliwa na kunguru.
Inapofikia mtu akafikia kujiona bora kuliko chama, huyu bila shaka hakifai chama wala chama hakimfai. Na lazima kuna tatizo, tena kubwa tu. Hivyo, uwezekano wa kukitosa chama wakati mbaya, hasa ule wa uchaguzi, ni mkubwa. CHADEMA wasingoje kufika huko.
Siasa za Tanzania zina bahati mbaya. Chama kinamlea mtu hadi kufikia umaarufu kama alivyo Zitto Kabwe sasa. Halafu mtu huyu aliyefinyangwa na kulelewa na chama, analewa sifa kiasi cha kujiona bora kuliko chama.
Mwisho wake huwa mbaya kwa mhusika na chama. Daniel arap Moi wa Kenya alifikia hatua ya kulewa sifa hizi pale alipoitwa profesa wa siasa. Alifanya ubabe hadi akakikosesha dola chama chake cha KANU.
Kuna haya ya wanasiasa kuchagua kati ya chama na urafiki. Tumekuwa tukimshutumu Kikwete na CCM kwa kuendekeza urafiki na kujuana. Hata wapinzani wanamlaumu kwa hili, hasa kwa kusema anaendesha nchi "kishikaji." Hili sina mjadala nao wala sitaki kuingia undani wake. Lakini CHADEMA waangalie wasitoe kibanzi kwenye jicho la mwenzao wakaacha boriti kwao.
Zitto kwa watu wa nje ya chama chake anaonekana kuwa mguu mmoja ndani na mwingine nje. Ushahidi ni shaka juu ya msimamo wake. Kwenye mkutano wa Opesheni Sangara kule Tanga watu wanataka kujua kama Zitto bado yumo chamani au la.
Ni rahisi mtu kukanusha, lakini ushahidi wa mazingira unaweza kupaaza sauti kuliko mwenye kukanusha. Ingawa Zitto anasisitiza kuwa yuko CHADEMA, matendo husema zaidi ya maneno matupu.
Inakuwaje Kafulila awe mali kuliko chama? Zitto anapaswa kubanwa ajibu swali hili kwa usahihi na majibu yanayoingia akilini siyo kupiga siasa. Je, kwa kumuunga mkono Kafulila, hata dhidi ya uamuzi wa CHADEMA, Zitto hadhihirishi asivyokubaliana na hukumu aliyopewa Kafulila?
Kama chama kilimuona Kafulila ana makosa na kikafuata taratibu zote za kumtimua, naye akaamua kujitoa na kutoa kashfa nyingi, maana yake ni kwamba kuna mgongano hata kama wahusika hawataki kulikubali hili.
Litakuwa jambo la ajabu kwa mtu wa cheo na elimu ya Zitto kutoliona hili. Wenzake wamekaa chini wakamtimua Kafulila na kutaja makosa yake-kuvujisha siri za CHADEMA.
Yeye bado anamtetea. Je, huku si kutetea madhambi yake au kuonyesha kuwa kipenzi chake kimeonewa? Kwanini asimtetee kwa namna inayoeleweka badala ya kuendelea kukidhoofisha chama?
Ifahamike. Tunaelekea kwenye uchaguzi mwakani. Kwa uzoefu wangu, wanasiasa nyemelezi watavitelekeza vyama vyao, hasa baada ya kuahidiwa vinono na CCM. Nani mara hii amesahau akina Masumbuko Lamwai, Tambwe Hiza, Walid Aman Kabourou, Shaib Akwilombe, Salum Msabaha na wengine wengi? Kwanini uone ubaya wa chama baada ya kutimuliwa?
Ingawa kuhama vyama ni haki ya wahusika, wengi wa wanasiasa, hasa waliojirejesha CCM baada ya kukosa ukuu kwenye vyama vyao, wameonyesha kuwa nyemelezi na "changudoa."
Ukiwaondoa watu kama Wifred Rwakatare na wengine wachache, wengi wamedhihirisha wanavyosaka madaraka badala ya kutumikia umma. Wamejivua nguo hata kama baadhi yao wanapewa madaraka ya kufinyangwa kama ilivyo sasa ofisi ya propaganda ya CCM, ambayo imegeuka dampo la wanasiasa nyemelezi.
Hivyo basi, CHADEMA wangembana Zitto wajue msimamo wake kwamba ni nani hasa atamuunga mkono kati ya mgombea wa chama chake na rafiki yake Kafulila.
Ni heri CHADEMA wakamkosa Zitto mapema kuliko kuwachenga saa za mwisho. Huu si wakati wa kucheza pata potea.
Bado Zitto ni mdogo kisiasa na kiumri. Ubunge wa kipindi kimoja hauwezi kumfanya awe yote katika yote hadi kuwa maarufu kuliko chama. Na chama kinapozidiwa umaarufu na mtu mmoja, kama CCM, kijue kinaelekea kuzimu. Nisingetaka CHADEMA wafike huko ingawa dalili zinaonyesha ukomavu wa hali ya juu katika kuyakata mawimbi haya na majaribu makubwa.
Zitto kaamua kumuunga mkono Kafulila wazi wazi, hata kabla ya chama chake kuamua kumsimamisha mgombea Kigoma Kusini. Anajiona si mchezaji bali mwamuzi. Je, alitaka kujenga mtandao ndani ya chama ili baadaye apate madaraka?
Na ikumbukwe. Hii si mara ya kwanza kwa Kabwe kupimana misuli na chama. Nani amesahau mvutano uliotokea hivi karibuni kwenye uchaguzi wa mwenyekiti wa chama? Je, Kabwe anatingisha kiberiti kwa ajili ya kuchukua uamuzi katika chaguzi ujao?
 
[h=1]Mwanangu anatumiwa – Mama Zitto[/h]
maalum.jpg

Na Mwandishi wetu - Imechapwa 18 November 2009

salum_1.jpg

SHIDA Salum, mama mzazi wa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Maendeleo na Demokrasia (CHADEMA), Zitto Kabwe, ameibuka na kusema mwanaye anatumiwa kukivuruga chama chake.
Akizungumzia taarifa zinazoandikwa na baadhi ya magazeti kuhusu kinachoitwa mgogoro wa uongozi katika CHADEMA, kati ya Zitto na viongozi wenzake, Shida alisema, "hakuna mgogoro pale, kuna kikundi cha watu wanaotaka kumtumia mwanangu kufanikisha mambo yao."
Akizungumza na gazeti hili juzi jijini Dar es Salaam, alidai kuna watu walio nje ya CHADEMA wanakula njama za kumgombanisha mwanawe na viongozi wenzake.
Alisisitiza, "kuna baadhi ya wanasiasa ndani ya CHADEMA wanaotumiwa na walio nje kugombanisha viongozi."
Akaongeza, "Mambo ya uchaguzi yalikwisha kitambo na Zitto kwa moyo mmoja alikubali kumaliza tofauti zake na Mbowe (Freeman Mbowe) ndiyo maana akamuacha Mbowe kuwa mgombee pekee wa uenyekiti."
Shida aliwatuhumu watu walio nje ya CHADEMA akisema ndio wanaopandikiza mbegu za chuki kwa lengo la kuwavuruga. Hata hivyo, hakuwataja.
Alisema kila mwenye akili timamu anajua kinachotafutwa, na nani mkweli na yupi anasingiziwa.
"Angalia wanaoandika haya. Kweli Zitto anaweza kutetewa na magazeti ya Habari Corporation yanayomilikiwa na Rostam Aziz halafu ukaamini kile kinachoandikwa?" alihoji.
Aliongeza, "Rostam yupi? Ni huyu tunayemjua au mwingine? Kwa wema upi alionao kwa chama chetu."
Wiki iliyopita magazeti ya Rai na Mtanzania yalinukuu taarifa zikidai kuwa zimetolewa na Shida, kwamba anataka mwanawe aondoke kwenye chama hicho kwa kile ilichoeleza kuwa "kumwepuesha na yaliyomkuta Chacha Wangwe."
Katika kujibu hilo, Shida anasema, "Mimi na Zitto tunajua katiba ya chama chetu. Tunafahamu taratibu za kuendesha chama. Yeye ni naibu katibu mkuu, mimi ni mjumbe wa Kamati Kuu. Tunajua nini maana ya uongozi, hivyo hatuwezi kukurupuka barabarani.
"Kwamba kama kuna malalamiko au tuhuma mathalani juu ya uteuzi wa wabunge wa viti maalum, basi sote ni sehemu ya hicho kinacholalamikiwa. Kutokana na hali hiyo, hatuwezi kujifanya hatuhusiki na tukatuhumu kupitia vyombo vya habari, tena magazeti yanayomilikiwa na mwanachama wa CCM."
Shida alisema anajua kwa mapana chanzo cha yote yanayoandikwa na jitihada za kutaka kumgombanisha Zitto na viongozi wenzake, hasa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa na mwenyekiti wake, Freeman Mbowe.
"Yote haya tunafahamu chazo chake. Si uchaguzi wa ndani ya chama. Uchaguzi ulishakwisha na Zitto kwa moyo mmoja alikubali kumuachia Mbowe uenyekiti ili kulinda maslahi ya chama," alisema.
Alisema kuwa yeye kama mlezi, hawezi kuruhusu hali hiyo, hivyo atatumia nafasi yake ya mjumbe wa CC kuhakikisha kwamba tabia hiyo ya kugombanisha viongozi inakoma.
"Nikiwa mzazi, mlezi na mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA, siwezi kuruhusu Zitto kutumika kuingiza chama katika mgogoro. Nitasimama imara kuhakikisha kwamba CHADEMA inakuwa salama," alisema.
Wiki iliyopita, Dk. Slaa aliwaondoa katika nafasi za utendaji David Kafulila aliyekuwa Afisa Habari na Danda Juju aliyekuwa Afisa anayeshughulika na Halmashauri na Bunge kwa kile kinachoelezwa kuwa utovu wa nidhamu kwa chama na viongozi wake.
Kafulila alinukuliwa na baadhi ya magazeti kuwa alibeza kikao cha viongozi wa juu wa chama hicho kilichofanyika Dodoma ambapo Mbowe na Dk. Slaa walikutana katika kikao cha kawaida na wabunge wa chama hicho na baadhi ya wakurugenzi.
Kafulila alisema mkutano huo wa viongozi haukuwa na maana; na alifika mbali zaidi kwa kuufananisha na vikao vya geto. Ni matamshi hayo na mengine yaliyomfanya Dk. Slaa kutumia mamlaka yake ya kikatiba kumuondoa Kafulila katika wadhifa huo.
Taarifa zinasema hoja ya kumuondoa Kafulila katika kikao ilitolewa na Msafiri Mtemelwa, mmoja wa viongozi wake na ambaye alikuwa meneja wa kampeni za Zitto wakati wa kuwania uenyekiti wa CHADEMA.
 
Suala la kwamba Zitto ana mazuri mengi haliwezi kutufanya kuamini kuwa ni malaika hapana, ni vema Mh. Zitto akachukulia kwa umakini haya mapungufu yanayoelelkezwa kwake kuliko kuwashambulia, kwani akifanyia kazi hayo itaendelea kumjenga zaidi kuliko kumbomoa
 
Wewe ndo mnafiki mkubwa! aliyejitoa mwingine unalaumu mwingine. Unahitaji elimu gani kujua kua wakati akizunguka kwenye majimbo ya wengine wananchi wa Kigoma Kaskazini walikua wanamuhitaji. Acha unafiki tutajie Mbunge(Mgombea) aliyezunguka majimbo mengi kuliko Zitto. Alijiatahidi kutumia vizuri muda wake kwa kufanya kampeni jimboni kwake na kuzungukia majimbo ya wenzake hilo halipingiki hata kama hutaki kulikubali.
Kwa hiyo ndiyo umejibu nini kwa hoja zilizotolewa, washabiki wake hamji na hoja zaidi ya kulaumu waleta hoja, you are damaging your friend even more.
 
Chama cha Mapinduzi sasa kinaelekea kutimiza lengo lake la kukimaliza Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Mpango huo unaoonekana kusukwa kifundi ulikuwa na lengo la kuwahasimisha Viongozi wawili wenye Mvuto ndani ya Chama hicho yaani Zitto Kabwe na Freeman Mbowe.

Mpango huo ulikuwa na lengo la kumuaminisha ( Kwa Namna yeyote) Mmojawapo kwamba Mwenzir ndiye anaye kikwazo cha Ustawi wa Chama hicho ambacho kutokana na Sera zake kimefanya CCM ichukiwe kila kona ya Nchi. Sasa hivi ni wazi kwamba Sumu waliyolishwa viongozi hao dhidi yao imewaingia kisawasawa kiasi cha kila Mmoja kumuona Mwenzake adui wa Chama na yeye anaweza kukiendesha chama peke yake.

Ugomvi huo uliopandikizwa kwa Ustadi na sasa kuonekana kuota Mizizi umepelekea Mgawanyiko wa Kundi la Vijana kila Mmoja likimtetea Kiongozi wake kwa Nguvu zake, kila kundi liliamini Mentor wao anaonewa na kundi lingine.

Uthibsitisho wa Makundi hayo yanayohasimiana waziwazi yakiamini kwamba yanajenga Chama kumbe yanabomoa ni Mjadala huu unaondelea kuhusu Mgogoro wa NCCR Mageuzi.

Vijana hao wa CDM wameingia kichwakichwa na kufikia hata kutukanana eti kila mmoja akihisi Mbowe/Zitto anahujumiwa na Zitto/Mbowe.

Napenda Kuwaasa Vijana wa CDM hapa jukwaani Mnyika, Ben, Marytyna, Nyakarungu na wengine kwamba URAFIKI WA MBOWE NA ZITTO NI MASIKITIKO kwa CCM ila UADUI WA ZITTO NA MBOWE ni FURAHA kwa CCM. Msifikiri Zitto akifanikiwa kumpindua Mbowe ndio CDM itakuwa Salama ama Mbowe akifanikiwa Kummnaliza Zitto ndio CDM itakuwa Salama.

Mkuu Mkandara Umetoa Wasia Mzuri sana kwa Wapambe wa Mbowe na Zitto ambao mimi naamini kabisa kwamba wao ndio ADUI mkubwa kwa Ustawi wa CDM kuliko Mbowe na Zitto wenyewe

Zitto haters ( Ambao ni Wapambe wa Mbowe) na Mbowe haters( Ambao ni Wapambe wa Ziito) you are killing the party na hamuwatendei haki Watanzania walio Maskini ambao wangependa kuona CDM inakuwa moja.

Kuna waru wanakuja hapa wanajifanya wako Upande wa Mbowe wanamshambulia Zitto na kuna Wengine wanakuja hapa wanajifanya wako Upande wa Zitto wanamshambulia Mbowe. Wote hao wanadhani wanakisaidia chama kumbe wanakipunguzia Momentum.

To you Zitto and Mbowe

You should come open na warn your Wapambes unless otherwise chama kikifa Ninyi ndio mtakuwa Liable na Historia itawahukumu.

To you Mbowe and Zitto haters and Wapambe

Dhambi ya Fitina haiwezi kuishia kwa Mbowe na Zitto mkiwamaliza hao Mtakuja kwa akina Mnyika, Mdee, Dr. Slaa, Tundu Lisu na Mkiwamaliza hao mtageukiana wenyewe kwa wenyewe Ben hafai, Nyakarungu Mkabila, Heche Mdini n.k na Maadam mmeamuwa kuwa Makuwadi wa CCM mkikisaidia Kubomoa Chama Chenu Sitashangazwa. I hate you all
 
Mkuu huwajuii vyema hawa jamaa wawili (Mbowe na Zitto) ndio maana ndio maana unawaongea hivyo, au la upo kazini na mara zote kila kosa linarushiwa UWT na hata pale ambao ipo wazi kuwa wajanja wajanja, wasani, wabinafsi, na waroho wa madaraka wachache wanapobainika kwa kuweka uzembe wao mbale ya maslahi ya Umma na hata wanapo uwa vyama kwa ubinafsi wao bado UWT inarushiwa lawama zote.

Ukweli ni kuwa UWT haina muda, nia wala sababu ya kuuwa chama chochote hapa nchni na mara zote wamekuwa mstari wa mbele kuvijenga hivyo vyama ndio maana hata JF imepata kuwepo hapa nchni yote hii ni bayana ya kuwa UWT na vyombo vyetu vya Usalama vyote havina nia hiyo unayoihubiri hapa, vyama vyote vinakufa na vitakufa kutokana na wanasiasa uchwara tulionao, tokea kuanza kwa siasa ya vyama vingi hii imekuwa bahati mbaya ya Tanzania kuwa vyama vya upinzani vimekuwa bila watu makini na wa kweli bali mmoja mmoja katika vyama. Hawa unaowasema wewe huwajui na hakika watu waongo na wanaotumiwa kama wewe ndio mliotuletea Kikwete 2005, mkome na mjuwe tumewachoka na hakuna nafasi tena ya watu wahuni na wenye ukoma wa ubongo kupewa nafasi katika nchni hii tena maana hatutaki kurudi nyuma na hata kuingia vitani kama. Hao ni wezi na Mafisadi kuliko kama RA, EL na Wengineo wote unawajuwa.

Good counter argument. Hii mambo ya kusingizia maadui wa kufikirika kwa makosa yetu ama yao wenyewe ndio siasa za kudanganyana ambao wote tunajiadai kuwa hatudanganyiki....

But siasa za tuhuma na hisia pembeni just nihakikishie sehemu moja ambayo Zitto ama ameshiriki katika kumsupport Kikwete kuingia madarakani na pia kuwa yeye ameiba sehemu yoyote ile....
 
quote_icon.png
By Mkandara

Wanabodi,

Kwanza kabisa napenda kuwaonya wale wote wanaojaribu kwa nguvu zote kukiua chama cha Chadema kwamba hawatafanikiwa na kama watafanikiwa ni kwa sababu viongozi wa Chadema wenyewe wamepuuzia haya nitakayo andika.

Kutoka reliable sources ambayo ziwezi kuzietaja hapa ni kwamba Chadema kaa chama kinapigwa vita kubwa sana na CCM na vyombo vya usalama vinatumika sana ktk kuendesha zoezi kali na kubwa la kukiua chama. Kuna watu wawili ambao ni tishio kubwa la uongozi wa CCM nao ni Mbowe na Zitto ambao kwa imani yao ndio nguzo ya chama na wanatakiwa kushughulikiwa haraka na mapema..

Kazi hii haikuanza jana imeanza toka mwaka 2003 au 2004 kwa kutengenezwa nyaraka za siri ambazo aidha zinamhusisha Zitto au Mbowe ktk kuleta Upinzani baina yao wenyewe. Hawa wote wawili kama wapo hapa nawaomba wanisome vizuri na kama nasema uongo wanirudi na kupinga maelezo yangu. Kwa nyuakati Tofauti Mbowe au Zitto wamekuwa wakiletewa habari zingine zenye uthibitisho wa kimaandishi jinsi mmoja wao anavyompiga vita mwenzake na kwa bahati mbaya kila mmoja wao amefikia kuamini yale aloyaona na kufikia kweli kuamini na kujenga uhasama baina yao...

Navyoandika hapa Zitto ana ushahidi dhidi ya Mbowe vile vile Mbowe ana ushahidi dhidi ya Zitto na wote hawajawahi kukaa na kuzungumzia maswala haya isipokuwa kila mmoja anamtazama mwenzake kama mchawi bila kufahamu ya kwamba uchawi huu umetengenezwa kisayansi na utakubalika kwa kila hali na kuponza mahusiano ya viongozi hawa. Binafsi naamini kabisa Zitto na washabiki wake waligombea Uenyekiti wa chama kwa sababu walitaka tu kugombea kiti hicho kidemokrasia isipokuwa kwa dhana ya kwamba Chadema inatakiwa kuokolewa toka mikononi mwa Mbowe vile vile Mbowe na washabiki wake walikataa Upinzani wa Zitto kwa imani kwamba Zitto alikuwa analengo la kukiua chama..

Hivi zote ni habari walizolishwa pande zote mbili, namwona OmarIlyas akizungumza kwa machungu na jazba kubwa dhidi ya Mbowe lakini sintomlaumu kwa sababu kawa feeded information ambazo anaamini sawa na kina Mnyika ambao wanayajua mengi ya Zitto kulingana na walicholishwa toka zamani na sasa hivi wanafanya wao wenyewe. Makundi yote haya mawili hawaaminiani kwa sababu Usalama wa Taifa wameisha ifanya kazi yao na kinachosubiriwa tu ni kifo cha Chadema kupitia hawa watu wawili..

Dr.Slaa alikuwa tishio lakini sii tena kwa sababu naye walimjengea Udini na kundi la watu kumpa nafasi kubwa ya kuwa katikati ya mzozo huu mkubwa wa viongozi. Kama mnakumbuka nilipotoa pendekezo la Dr.Slaa kugombea kiti cha Urais ilikuwa na sababu na kusema kweli CCM walikuwa hawakujiandaa kwa hilo..Nilitegemea kabisa Dr.Slaa atashinda uchaguzi huo lakini wakatafuta mbinu ya Udini na ikaweza kufanya kazi japokuwa lengo kubwa la CCM lilikuwa kuleta mgogoro ndani ya Chadema kwa kupitia Mbowe na Zitto..

Kwa hiyo tuwe makini sana na jitihada za CCM ktk kukibomoa chama. Zitto kayafanya makosa aloyafanya ni kutokana na jinsi alivyolishwa na Mbowe pia amekuwa akilishwa habari mbaya dhidi ya Zitto lakini nawahakikishia hakuna lolote kubwa la ukweli isipokuwa chuki imeundwa. Zipo Nyaraka za Udini na zina mihuri ya Chadema, zipo nyaraka, sms, e-mails za Chadema, Zitto na Mbowe ambazo zimetengenezwa kwa utaalam mkubwa kuonyesha aidha chuki baina yao au agenda za chama na Udini ili mradi CCM na wana IT wake wanaifanya kazi kubwa ya kukibomoa chama kutoka ndani... kazi hii haikuanza jana na sasa hivi tunaona matunda ya kazi kubwa ilitangulia. Mbowe ataendelea kuwa kiongozi bora wa chama kisiasa na Zitto ataendelea kuwa kiongozi bora wa kisera na utekelezaji.

Jihadharini sana na nguvu ya kiza!.. Masalaam

Good propaganda kaka. I always respect kazi za kutumia akili na hasa kama zina lengo jema ingawa ni kazi chafu..

Just one thing, mention one incidence ambayo mimi nimemuatack Mbowe bila ya yeye ama watu wake kuanzisha na kuendeleza mashambulizi yao kwa Zitto...so kama unahitaji kutumia busara zako kumuokoa mtu ama chama ni bora ukazitumia kuwashauri na kuwalazimu hao maadui wa Zitto kuacha siasa chafu. 2005 ilinifundisha one thing...Adui anayeaamini katika siasa chafu akishambulia hakuna ujinga kama kakaa pembeni na kutegemea busara kufanya kazi yake...U hit back harder!!
 
Kama Mbowe angekuwa anaunga mkono Kikwete mwaka 2005, kwa nini alikubali kugombea urais? Acheni unafiki na majungu ya kufikirika. Ushahidi wa Zitto kutumika umewekwa wazi kwenye matendo na kauli zake.
 
Mkuu ya CCM yanawashindeni ya nini kuwaingilia CDM? Tatueni Matatizo YENU CCM kwanza la sivyo 2015 bye bye
 
Inaonyesha unaongozwa na chuki dhidi ya huyu bwana, unaweza kuniambia mgombea(Mbunge) wa CDM aliyezunguka majimbo mengi kuwanadi wagombea wenzake kwenye uchaguzi uliopita zaidi ya Zitto. Leo bila aibu unasema kua hakufanya chochote wakati mwaka jana alitumia muda mwingi kukinadi chama! Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Hivi unapomshambulia mgonjwa akiwa amelazwa hospitali una tofauti gani na anaekunywa uji wa mgonjwa.
Ni mgombea gani wa CDM alisaidiwa na Zito kwa kupewa magari ya kampeni kama alivyomsaidia Kafulila? Au alikuwa na uchungu na Mgombea wa NCCR kuliko wagombea wenzake ndani ya chama?
 
Hizi personal issues hazina logic wala hazijabeba ujumbe wenye maslahi kwa taifa.Frustration za aina hii ndiyo zinazowafanya muwe na Rais wa aina hii tuliye naye leo,tunaishi kufanya chaguo lisilo sahihi.Voting for beauty,not for duty.Tukishakuwa na twisted minds tunaishia kutumia vigezo vya hovyo kumchagua au kumkataa mtu,ndipo tunapojikuta tunampa mtu aliyestahili pengine kuwa tourism minister Urais.

Mie nina wasiwasi sana na zito na ninapokumbuka mambo ya Kafulila, Walid Kaburou na Nsanzugwako naanza kuwatilia shaka watu wa kigoma kuwa wanapopewa uongozi wanahitaji uangalizi wa karibu. Nilikuwa namtegemea Zito lakini ukaribu wake na mwenyekiti wa magamba na jinsi anavyojaribu kujenga mtandao ndani ya CDM inadhihirisha hafai kupewa dhamana ya kuiongoza CDM. Na akiondoka mbowe atafutwe mtu makini ambaye atatufikisha tunakotaka, mtu huyu asiwe mfuasi wa zito wala mbowe. Binafsi nikifuatilia utendaji wa Mtei, Makani na Mbowe naona mbowe amefanya mambo makubwa. Najua vijana kama zito wanakuwa aidha wamejiamini kupita kiasi au wamekosa washauri makini au wamemenunulika kwa hiyo hata nyota zao zinazong'aa huathiriwa na tamaa za kupata ukuu mapema.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom