Kafulila na Zitto wanaivuruga NCCR - Moses Machali

Status
Not open for further replies.
Naanza kuamini hii habari ina ukweli ndani yake.Zito kama sio kweli haya yaliyoandikwa humu angepinga kwa hoja.Nilikua mfuasi mzuri wa zito,lakini niliingiwa na mashaka alipoingia kwenye mgogoro na uongozi wake, lakini pili alipotangaza kwamba 2015 atarudi kwao akigombea nafasi tofauti na aliyooigombea wakati huo.Akimaanisha uraisi.Hili nilijiuliza sana kwa nini afanye hivyo wakati chama bado hakijapendekeza mgombea.Huu niliuona kama mgogoro unaoandaliwa ,maana asipoteuliwa kugombea itakuaje?kwa watu waliosoma na Zito UDSM wanasema ni "opportunist".Bado najaribu kutafakari pia uswahiba wake na JK.Huyu anaweza kuwa ni "KIGEUGEU" napia kuwa Nape wa CDM.
 
hii habari itakuwa na ukweli asilimia 95,kwa sababu mwenendo wa zitto cdm siyo ule wa mwanzo,na kwa mtindo huu ccm watatawala milele nchi hii
 
Salaam

Kuna wakati unaposoma akili za watu humu ndani na hasa wale wanaojitambulisha kama makada wa Chadema unaweza ama kukata tamaa na mabadiliko ya kweli katika nchi yetu ama hata kuamua kujilipua na kujiunga na CCM.

Inashangaza kuona kuna watu wanaojifaragua kama great minds wanakuwa rahisi kuamini sumu za kisiasa ambazo ukweli zinalenga kulinda maslahi ya watu kwa kuwaharibia sifa wengine.

Inakuwaje mtu mwenye akili zake timamu akaamini habari za kutengenezwa za udaku wa kisiasa unaomilikiwa na kufadhiliwa na mahasimu wa Zitto wakiwemo Kubenea na Mweka Hazina wa Kudumu wa Chadema Anthony Komu ambaye kwake yeye Zitto ni tishio kwa maslahi yake na maslahi ya "wenzake" wanaoamini kuwa Chadema ni chama chao?

Inakuwaje wanaojiita great minds kuwa tayari kuamini kuwa Zitto ana mpango wa kugombea urais mwaka 2015 wakati wote tunajuwa kuwa wakati huo atakuwa hajatimiza umri wa miaka 45.

Inasikitisha zaidi kuona kuwa kuna baadhi ya wapenzi wa Chadema wanamshutumu Zitto kwa madai ya kuonyesha dalili za kutaka kugombea Urais eti huku akijua kuwa chama chake tayari kina mgombea. Yaani Chama cha DEMOKRASIA na maendeleo tayari kina mgombea wa Urasi wa mwaka 2015 wakati ndio kwanza tupo mwaka 2011? Halafu mna jeuri ya kuwalaumu wengine kwa ukandamizaji wa haki za kidemokrasia...

Na hili suala la Zitto kuwa na nia ya kuivuruga CHADEMA eti kwa mipango yake ya kuhamia ama kugombea Urais kupitia NCCR linaonyesha dalili kubwa za kutokujiamini ndani ya kundi la wahafidhina wa Chadema. Iweje Zitto huyu mnayemtukana, kumpiga vita na hata kudai kuwa hana nguvu kisiasa suala ama hisia za yeye kuondoka Chadema kuhusishwa na nia ya kuvuruga chama chenu?

Lakini kama wanaDEMOKRASIA inakuwaje mnakuwa na mitazamo hasi ya nia ya mtu (kama ipo) ya kuhama chama kimoja kujiunga na chama kingine atakachoamini kuwa kinaendana na fikira, ndoto ama hata tamaa zake ziwe za kisiasa ama za hatima ya nchi yetu. Hizi si fikira za wanademokrasia, ni fikira za mafashisti wanye nia ya kutumia kauli mbiu za demokrasia kuhalalisha matamanio yao ya kifashisti.

Ninachosoma kutoka katika siasa hizi za kichokoraa zinazoendeshwa na makada na hata viongozi wa Chadema humu ndani ya jukwaa letu na kwengineko dhidi ya Zitto ni ishara za kutojiamini miongoni mwa establishment ya CHADEMA wenye mitazamo na malengo ya kihafidhina. Badala ya kufanya jitihada za kujisafisha na kujipanga upya kuondokana na tuhuma mbalimbali zinazowakabili zinazopelekea chama chao kuvikwa ama kujivika magamba mbalimbali kama ya udini, ukabila, ufisadi nk, wako busy kumsulubu mtu ambaye anaonekana kuwa kama kioo cha Chadema tofauti ambayo watanzania wangependa kuiona inakuwa na sio Chadema waliyoikumbatia wao.

Kwa ujumla na kwa jinsi nijuavyo mimi Zitto bado hajawahi kuwa na nia ya kuondoka CHADEMA ingawa kuna mengi yanayomvunja moyo kila kukicha. Lakini kama atakuja kuhama CHADEMA na kujiunga na NCCR naamini itakuwa ni suala la kiitikadi zaidi kuliko nafasi yake kisiasa.

NCCR tofauti na ilivyo CHADEMA, ni chama pekee cha upinzani chenye mizizi ya itikadi za KIJAMAA zilizojikita katika nia ya kujenga Tanzania yenye kujali na kuthamini utu. Na naamini mpaka sasa Zitto, Mnyika, Baregu, Kitila Mkumbo bado wanaamini katika itikadi ya UJAMAA ingawa wanalazimika kunyamazia sera, nyendo na matamanio ya kibepari ambao ndio mzizi wa CHADEMA.

Na ni wazi kuwa ili NCCR ifufuke na kuteka hisia za watanzania kuwa wanaweza kuwa chama mbadala wanachotamani kukiona na kukiunga mkono kwa dhati, kuna ulazima wa kubadili uongozi uliokuwepo na kusimika uongozi mpya utakaoweza kukipa uhai. Vilevile ni mabadiliko ya uongozi sasa ndiyo yatakayoweza kutoa nafasi kwa WAJAMAA MASALIA wanaolazimika ama kulazimishwa kubaki CHADEMA na CCM kupata uwanda wa kisiasa kujaribu kujenga Tanzania waitakayo na kurudisha siasa za kiitikadi badala kuendelea kutumika kuendeleza siasa za tuhuma, chuki, uzandiki, personalities na ujanjaujanja mwengine.

Napenda kuwaasa wale waliodedicate maisha na akili zao katika kummaliza Zitto iwe kisiasa ama kimaisha watambue kuwa adui wao sio Zitto bali yale anayoamini kuwa yanaopaswa kubadilishwa na kuepukwa na chama chake. Nguvu mnazotumia hapa kujaribu kumbomoa Zitto ni vizuri mkazitumia kujenga chama chenu kiweze kuaminika na watanzania na sio kuendelea kutegemea mtaji wa sumu ya chuki dhidi ya CCM na serikali yake tu.

Naamini historia ipo wazi kuwaamsha kuwa kwa siasa hizi za chuki na uzandiki, kamwe hamtaweza kupambana na nguvu na akili za Zitto kisiasa…..Lakini pia wakati mwengine mjaribu kuonyesha ubinadamu kidogo hata kama uungwana kwenu mwiko!

Mnachokifanya sasa hakina tofauti na aliyokuwa akiyafanya Mchungaji Mtikila wakati Mwalimu alipokuwa amelazwa hospitalini na hata baada ya kufairiki. Huu sio Utanzania!
 
Mwita hii ni propaganda maalumu inafanywa kwa malengo maalumu. Sijawahi kutumika na CCM maisha yangu yote na CCM wanajua hivyo. Lakini ukitaka kuua nyota ya mwanasiasa yeyote wa upinzani ni kusema anatumika. Hata marehemu Chacha Wangwe walisema anatumika na CCM ili kumvunjia heshima wala hapakuwa na ushahidi wowote wa hivyo. Mpaka anakufa alikufa na kinyongo hiki. CCM hawawezi hata siku moja kunitumia. Nimekuwa ninafanya kazi zangu Bungeni kwa umahiri mkubwa sana and yet maadui zangu wa kisiasa wanasema haya mambo ya kipuuzi kabisa.

Umewahi kuandika humuhumu JF ukisema "Wangwe tulimtenda wote". Mwenyewe unajua ulikuwa unam-address nani. Leo huwezi kusema walisema, sema tulisema kwa kuwa ulikuwa sehemu yao.
 
Moja, sina mpango wowote wa kuhama CHADEMA. Kila siku nasema nimekuwa mwanachama wa chama kimoja tu cha siasa maisha yangu yote, nimekuwa mwanachama wa CHADEMA toka nikiwa na umri wa miaka 16 na namwomba Mungu kila siku nife nikiwa ndani ya chama hiki.

Najua kuna watu wanapenda sana nitoke CHADEMA kwa maslahi yao ya kisiasa wakiniona mimi ni tishio kwao. Napenda kuwaambia nimetumia nguvu nyingi sana kujenga chama hiki na sitahama. Waache kabisa kunizushia na kunijengea chuki mbele ya umma.

Pili, sihusikikwa lolote lile na yanayoendelea ndani ya NCCR na wala sina interest ya kuyajua. Mbunge wa Kasulu mjini ambaye alikuwa mwanachadema na kushinda Ubunge kwa sababu ya kutumia jina langu huko kwao Kasulu anaropoka (kama kweli kasema maneno hayo) na nitakapotoka Hospitali nitamtaka anithbitishie anayoyasema. Vijana wanapojiingiza kwenye siasa za uwongo kama wazee wao ni hatari sana kwa nchi. Sihitaji kwenda NCCR ili kugombea Urais kwani chama changu ni kikubwa zaidi na kitanipa Urais kwa urahisi kuliko NCCR ambacho ni chama kisicho na rekodi yeyote ya kupigania maslahi ya nchi hata wakati kilipokuwa chama kikuu cha upinzani nchini.

Katiba hainiruhusu kugombea Urais mwaka 2015 na hata kama ikibadilishwa na kuniruhusu kugombea kwangu kutategemea sana mwafaka ndani ya chama changu. Anayedhani kwamba nia yangu ya kuwa Rais wa Tanzania ni ya kufa na kupona hamjui Zitto. Sifanyi siasa za kufa na kupona. Ninao uwezo wa kuwa Rais bora maana nina ajenda na ninatoka chama bora. Lakini pia nipo tayari kufanya kazi yeyote ile ambayo chama changu kitanipa.

Zittophobics wanaishi kwa siasa za kumwaza Zitto na wamo kwenye vyama vyote vya siasa hapa nchini. Ninafanya kazi zangu za Ubunge kwa ufanisi na mafanikio makubwa sana, ninafanya kazi zangu za Uenyekiti wa Kamati ya Mashirika ya Umma kwa umakini mkubwa na ninafanya kazi zangu za Uwaziri Kivuli wa fedha katika hali ya kuridhisha sana.

Maadui zangu wa kisiasa wanatamani nianguke. Kwa uwezo wa Mungu sitaanguka.

Tatu, Gazeti la Mwanahalisi limekuwa ni gazeti linalonisakama sana kila kukicha lina ajenda yake. Gazeti ambalo limepoteza mvuto wake kwa jamii halinishughulishi. Hata juzi Mzee Samweli Sitta amelishutumu kwa kununuliwa na mafisadi na kutumiwa. Niseme nini zaidi kuhusu gazeti hili linaloongozwa na mtu ambaye hata hajamaliza darasa la saba.

MwanaHalisi wanajua kwamba wakiandika habari yenye jina langu mauzo yao yanakua makubwa. Hili ni gazeti mufilisi ambalo kazi yake ni kutumiwa tu.

Nne, WanaJF mnasema hili ni jukwaa ni Great Thinkers. Great thinkers huwa hawadaki habari na kuziamini na kuanza kutoa maoni bila kwanza kupata uhakika wa habari hizo. Jukwaa hili limegeuzwa kijiwe cha kahawa ambapo kila mtu anaandika atakalo bila hata kufikiria. Jukwaa limeshusha hadhi yake kwa kiasi kikubwa sana. Sisi waasisi wa JF wengi wetu roho inatuuma kuona jukwaa lilikokuwa ni kisima cha mijadala yenye tija linakuwa ni jukwaa 'bashing' tu. Nasikitika kwamba watu wenye ugonjwa wa Zittophobiasis ni wengi sana humu. Ninawashauri kwamba jitahidini muwe objective na muone upande wa pili wa shilingi.

Habari hii ya Mwanahalisi ni habari ya kijinga sana kujaribu tu kunihusisha na vurugu za chama ambacho mimi si mwanachama wake. Kafulila na mimi ni marafiki na ni wabunge wa Kigoma. Lakini Kafulila na mimi hatuongei mambo ya vyama vyetu hata kidogo na yeye anajua kwamba sina interest na NCCR Mageuzi. WanaJF msicheze ngoma isiyo yenu.

Pole bwana Zitto kwa kuugua. Kwa kuwa umejitokeza kujibu tuhuma hizi zilizoelekezwa kwako inaashiria unaendelea vizuri na tunatumai muda si mrefu utakuwa nasi home.

Lakini unajua Zitto wewe ni mwanasiasa mkubwa. Kila kitu unachofanya au kuongea sasa ujue kinaimpact kubwa sana kwa maisha yako ya usoni hasa ya kisiasa. Sasa ilikuwaje wakati wa kampeni mwaka jana ukawaambia watu wa jimboni kwako kwamba utarudi tena 2015 si kuomba ubunge bali urais? Huo mlipuko ulichafua sana hali ya hewa miongoni mwa public na ndio maana hata chechemabaki yake unayaona hata leo wakati Mwanahalisi wanapoandika habari hii. Si tatizo la mwanahalisi. Ni tatizo lako, ulitoa kauli zilizowapa mwanya maadui wako binafsi, maadui wa chama chako na maadui wa maslahi ya nchi kwa ujumla kuzingatia nafasi yako, wakapata nafasi ya kukuchafua.

Whether ni ukweli au ni uongo kwamba unatumika kuivuruga NCCR ni hoja nyinine. Hoja ya msingi ni kwamba you have to be careful boy, please make a calculated move in what you say and what you do. Usiwape nafasi maadui zako kuharibu ndoto zako.
 
Moja, sina mpango wowote wa kuhama CHADEMA. Kila siku nasema nimekuwa mwanachama wa chama kimoja tu cha siasa maisha yangu yote, nimekuwa mwanachama wa CHADEMA toka nikiwa na umri wa miaka 16 na namwomba Mungu kila siku nife nikiwa ndani ya chama hiki.

Najua kuna watu wanapenda sana nitoke CHADEMA kwa maslahi yao ya kisiasa wakiniona mimi ni tishio kwao. Napenda kuwaambia nimetumia nguvu nyingi sana kujenga chama hiki na sitahama. Waache kabisa kunizushia na kunijengea chuki mbele ya umma.

Pili, sihusikikwa lolote lile na yanayoendelea ndani ya NCCR na wala sina interest ya kuyajua. Mbunge wa Kasulu mjini ambaye alikuwa mwanachadema na kushinda Ubunge kwa sababu ya kutumia jina langu huko kwao Kasulu anaropoka (kama kweli kasema maneno hayo) na nitakapotoka Hospitali nitamtaka anithbitishie anayoyasema. Vijana wanapojiingiza kwenye siasa za uwongo kama wazee wao ni hatari sana kwa nchi. Sihitaji kwenda NCCR ili kugombea Urais kwani chama changu ni kikubwa zaidi na kitanipa Urais kwa urahisi kuliko NCCR ambacho ni chama kisicho na rekodi yeyote ya kupigania maslahi ya nchi hata wakati kilipokuwa chama kikuu cha upinzani nchini.

Katiba hainiruhusu kugombea Urais mwaka 2015 na hata kama ikibadilishwa na kuniruhusu kugombea kwangu kutategemea sana mwafaka ndani ya chama changu. Anayedhani kwamba nia yangu ya kuwa Rais wa Tanzania ni ya kufa na kupona hamjui Zitto. Sifanyi siasa za kufa na kupona. Ninao uwezo wa kuwa Rais bora maana nina ajenda na ninatoka chama bora. Lakini pia nipo tayari kufanya kazi yeyote ile ambayo chama changu kitanipa.

Zittophobics wanaishi kwa siasa za kumwaza Zitto na wamo kwenye vyama vyote vya siasa hapa nchini. Ninafanya kazi zangu za Ubunge kwa ufanisi na mafanikio makubwa sana, ninafanya kazi zangu za Uenyekiti wa Kamati ya Mashirika ya Umma kwa umakini mkubwa na ninafanya kazi zangu za Uwaziri Kivuli wa fedha katika hali ya kuridhisha sana.

Maadui zangu wa kisiasa wanatamani nianguke. Kwa uwezo wa Mungu sitaanguka.

Tatu, Gazeti la Mwanahalisi limekuwa ni gazeti linalonisakama sana kila kukicha lina ajenda yake. Gazeti ambalo limepoteza mvuto wake kwa jamii halinishughulishi. Hata juzi Mzee Samweli Sitta amelishutumu kwa kununuliwa na mafisadi na kutumiwa. Niseme nini zaidi kuhusu gazeti hili linaloongozwa na mtu ambaye hata hajamaliza darasa la saba.

MwanaHalisi wanajua kwamba wakiandika habari yenye jina langu mauzo yao yanakua makubwa. Hili ni gazeti mufilisi ambalo kazi yake ni kutumiwa tu.

Nne, WanaJF mnasema hili ni jukwaa ni Great Thinkers. Great thinkers huwa hawadaki habari na kuziamini na kuanza kutoa maoni bila kwanza kupata uhakika wa habari hizo. Jukwaa hili limegeuzwa kijiwe cha kahawa ambapo kila mtu anaandika atakalo bila hata kufikiria. Jukwaa limeshusha hadhi yake kwa kiasi kikubwa sana. Sisi waasisi wa JF wengi wetu roho inatuuma kuona jukwaa lilikokuwa ni kisima cha mijadala yenye tija linakuwa ni jukwaa 'bashing' tu. Nasikitika kwamba watu wenye ugonjwa wa Zittophobiasis ni wengi sana humu. Ninawashauri kwamba jitahidini muwe objective na muone upande wa pili wa shilingi.

Habari hii ya Mwanahalisi ni habari ya kijinga sana kujaribu tu kunihusisha na vurugu za chama ambacho mimi si mwanachama wake. Kafulila na mimi ni marafiki na ni wabunge wa Kigoma. Lakini Kafulila na mimi hatuongei mambo ya vyama vyetu hata kidogo na yeye anajua kwamba sina interest na NCCR Mageuzi. WanaJF msicheze ngoma isiyo yenu.

Nadhani unatakiwa kuwa makini sana na kauli zako kama kiongozi;
1.Wewe sio tishio hata kidogo,wananchi walikuamini wakawa wanakupa support hivyo usigeuze nguvu na imani ya wananchi kuwa jitihada zako binafsi.Nakupa angalizo kwa hili kwa kuwa usijidanganye kuwa wewe unaweza kusimama peke yako bila nguvu za wananchi nyuma yako.Ukae utafakari sana kwa nini jukwaa hili ambalo wewe ulikuwa kinara umeanza kujadiliwa negatively.Kwa nini asijadiliwe Dr. Slaa? ama ndio unataka kutudanganya wewe unanguvu,uwezo,mvuto kwa jamii zaidi ya Dr. Slaa! ndio maana unajadiliwa sana kwa mtazamo hasi!?

2.Inawezekana ni kweli kuwa Huyo anayeongoza gazeti la mwanahalisi hajafika darasa la saba ,ila kuuhusisha udhaifu wake na darasa lake bila kuwa na facts ni udhaifu wako kama kiongozi.Unataka kutuambia wananchi wanaokuunga mkono wewe na kukubali kama kiongozi wao hakuna ambao hawajamaliza darasa la saba kama huyo kiongozi wa mwanahalisi!.
Unatuambia kuwa ambao hawajafika darasa la saba hawana mchango wowote kwa maendeleo ya jamii !,Inaelekea wewe huwahitaji wakuunge mkono kama kiongozi wao!?
Kumbuka hawa ni wale ambao wamechoka na manyanyaso ya CCM wakaona walinyiimwa haki yao ya msingi hivyo wakaona wakuunge mkono ili kizazi chao kijacho kisishindwe kufika hata darasa la saba.Leo hii unawadharau.

3.Siku zinavyozidikwenda unapoteza mvuto sana Kamanda,ungeweza kusoma alama za nyakati ungetafuta mbinu mbadala za kujisafisha kama ni kweli wanayosema.Lisemwalo lipo kama halipo laja.
Mimi binafsi sio muumini wa habari za mtaani ila habari inapoletwa na watu wanaanza kukuzungumzia kwa historia jinsi wanavyokufahamu kuanzia TOSAMAGANGA na UDSM ni hatari sana . Binadamu tuna tabia ya kuunganisha matukio kwa hiyo kuwa makini.

Mimi nakwambia wazi "nilianza kupata mashaka na wewe ulipoanza kutembelea magari ya kifahari ambapo unajua wazi kuwa wanaharakati tunapinga matumizi ya magari ya kifahari kwa viongozi wa uma.Hata kama una biashara zako binafsi na hela nyingi jamii yetu sio ya kihivyo ,kuona mtu kama wewe unayefahamika kama mkombozi wa wanyonge kujionyesha kwa ufahari kama wasanii wa marekani."

MTAZAMO
 
ngoja niongee na PAW aje hapa ...ZITTO amelazwa na amejitolea kuja kujibu hoja zenu ...watakauandika hoja ambazo hazina miguu ...watakula PAW
 
mkuu ulichosema ni ukweli mtupu.Mbatia sio mpinzani wala hajawahi kua mpinzani ni CCM ya JK.
Hata alipogombea ubunge mwaka jana alikua na lengo la kugawa kura za upinzani ili Halima Mdee asipite CCM washinde.

Fabolous,

Kuna watu wamepandikizwa chuki na kuwa wafuasi vipofu.Hii ni aibu sana,pia mimi namuonea huruma mtanzania wa kawaida anavyolishwa visivyolika.Pia ni jambo la ajabu sana mtu akiguswa kwenye mamlaka yake anakuwa furious,ajaribu kukabiliana na changamoto zilizoko ndani ya chama chake badala ya kutumia mbinu mfu za kupata sympathy ya wanachama.Ashughulikie mapungufu yake katika kuongoza chama cha siasa kilichopoteza legacy ya upinzani.NCCR haitasahaulika katika siasa za Tanzania katika kughilibu upinzani

Ben nae yumo kweli hilo group, either kwa kujua au kutokujua. Mungu hatawaacha waja wake.

Unao ushahidi angalao wa madai yako? I wish ungejua kinachoendelea,tusifuate mikumbo ya magazeti na wanasiasa ambao mentally tayari wako frustrated.Kumbuka huu ni muda wa kujenga upinzani imara,tuache kupelekwa pelekwa kama vile tuko kwenye mafuriko
 
kwani zito kesharudi kutoka india?wanasiasa mnatuchanganya,mara darasa la saba mara nini
 
Zitto kaka dnt u worry we got ur back . Ninakuombea urudi na afya njema. Uendelee kuwashamoto bungeni
 
Good news..Kwa mtindo huu kuiondoa serikali ya CCM madarakani itakuwa ni ndoto!
kweli wewe ni punguwani hamnazo kabisa, nani kakwambia lengo ni kuiondoa serikali ya CCM madarakani bila mkakati imara?Waajiri wako wanapaswa waone kuwa unawafedhehesha.
 
Hivi hawa wanasiasa kutoka kigoma huwa wanamatatizo gani?yani umaarufu kidogo tu wanataka wapewe vyeo.misishangai kwa Zitto kuja kukiama Cdm kwenda Nccr hizo huwa ni mbinu chafu za ccm kuzigawanya kura za upinzani ili waendelee kutawala.Ivi mlishawai kujiuliza kwani uchaguzi wa Tanzania kwenye uraisi huwa kuna lundo la wagombea?na je leo ni mgombea gani anaonekana ni tishio kwa magamba?sasa wenzenu wanajua kucheza mchezo wa siasa.najua zitto atagombea urais 2015 lengo sikukamata dola bali ni kupunguza kura za upinzani na support kubwa hataipata kutoka kwa magamba kwa ahadi kedekede.siasa ya tanzania kazi kwelikweli.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom