Kafulila na Zitto wanaivuruga NCCR - Moses Machali

Kafulila na Zitto wanaivuruga NCCR - Moses Machali

Status
Not open for further replies.
habari imetoka JF imeenda gazetini inarudi JF. Hata hivyo hawa jamaa ni vema wakaacha plagiarism. Ukiangalia hiyo nukuu ni ya maneno ya zitto kupitia akaunti yake ya jei efu. Sasa mbona sijaona credit kwa JF popote?
 
."Sihitaji kwenda NCCR ili kugombea Urais kwani chama changu ni kikubwa zaidi na kitanipa Urais kwa urahisi kuliko NCCR ambacho ni chama kisicho na rekodi yeyote ya kupigania maslahi ya nchi hata wakati kilipokuwa chama kikuu cha upinzani nchini".alisema Bw. Zitto.

.
Mheshimiwa Zitto Kabwe, kweli ukitoka kwenye matibabu uwawajibishe wanaokuzushia mambo. Lakini hata mimi siku nikitoka salama huku niliko nitakutaka utueleze kwa nini unatudhalilisha namna hii (labda kama haya si maneno yako)
George Kahangwa
 
Zittto Kabwe, tunakuheshimu, na tunatambua mchango wako mkubwa katika taifa hili. wewe ni bado kijana mwenzetu. kauli yako ni ya kiume. tunakuomba uendelee kufanya kazi kwa uadilifu ndani ya Chadema. umri bado mdogo inshallah.siku ikifika, na mungu akipenda, basi tuna uwezo wa kukupatia nafasi ya juu kabisa katika chama chetu na nchi yetu.

tunaomba siku zote uweke moyoni kuwa wenye uwezo tuko wengi, lakini anatakiwa mmoja. mchango sio tu pale mtu akiwa raisi au mweyekiti wa chama. madaraka pia hutoka kwake muumba. umri unavyozidi kwenda utagundua kuwa satisfaction haiko kwenye madaraka peke yake.

hebu imagine ungekuwa mwenyekiti cdm kwa sasa, au mgombea uraisi pale 2010.....where would you be at present?

and after what happened under naive democracy and opressive system, with your young age, what would be in store for you for the future?

all in all, your future is still bright.

Mungu akujalie upone haraka. urudi tena tanzania. Real Madrid (chadema) and the national have been long waiting for you!

best regards.
 
moderetor itakuwa bora kkama utaiondoa hii thread kwani hakuna jipya hapa.kama ni zitto amesha jadiliwa na kugundulika kuwa ni pandikizi la ccm,kigeugeu,mnafki aliye kubuhu.

mnafiki,kigeugeu aliyekubuhu ni wewe!na kwa taarifa yako hakuna mwanasiasa hapa tanzania kijana anayeweza kulinganishwa na zitto.wafitini wote mtakufa!
 
Ability is where looks for it.tunaamini,kwa kauli na vitendo vyako,jana tumeona ulivyouelezea umma nini msimamo wako,tunaamini ni msimamo wa kimwanamapinduzi zaidi kuliko maneno yanayopikwa.Tunaamini umakini wako CDM wanaujua na umakini wa chama chako unaujua.Wakati mwingine watu wanafikiri kuwa ukaribu wako na watu wa magamba ni hujuma fulani.Tunaamini tunapingana bila kupigana,wana wa nchi hii tusiwe wepesi kupinga hata misimamo iliyotolewa na wahusika.Na kama mnafanya kazi ya magamba hapo mtakuwa mnajipalia makaa ya moto.Tunamtaka mwandishi wa gazeti la majira atueleze amepata wapi maelezo hayo ya Zitto yanayopingana na tamko lake alilotoa jana hapa JF?
 
Hivi vyama vya siasa si vina 'whips', maana hizi habari za magazetini na mitandaoni zina ashiria migogoro iliyopo ndani au udaku na uzushi yenye nia na dhamira ya kukipaka chama matope na baadhi ya viongozi.

Wachunguliaji wa siasa tungefaidika zaidi kama wasemaji wa vyama wangekua wanajitokeza mara kwa mara na kutoa kauli zao kichama juu ya tuhuma mbali mbali zinazotolewa magazetini au kwenye mitandao. Si ni jukumu la hawa watu kurekebisha habari zenye lengo la kupotosha na hata kuuzima moto iwapo kweli kuna mgogoro ndani ya chama kutotapakaa, kwani chama si mtu mmoja kikishafika leo level ya utaifa. Kisiasa ninavyofahamu bad publicity akikijengei chama a good reputation to the public na pengine kuwapunguzia potential serious recruits.

Msemaji wa chama ambae ni 'party whip' (kwenye siasa za wenzetu) ni mtu ambae licha ya kuhakikisha viongozi wapo 'in toe' with party lines, also has the responsibilities of maintaining unit and public relationship. Hili kuhakikisha sera za chama na agenda zao ndio vitu vikuu jamii inavisikia na si mengine zaidi.

Amna chama kisicho na migogoro kokote pale duniani lakini habari ambazo aziwahusu wapiga kura zibakie vilevile, endapo gazeti la mwanachama linahusika kuchafua kiongozi wa chama sasa sijui huyo whip ana kazi gani au ndio kusema kuna watu humo ndani ya vyama ku-control sio sera za kichama bali pia wa control na career steps za wanachama kwa sababu zao binafisi hizi siasa zetu sizielewei kabisa.
 
Hivi si kuna thread humu jf inahusiana na suala hili, ambapo Bw. Kabwe alikanusha tena kwa nguvu zote!!??
Jamani haya mambo ni ya kisiasa tu za kuchafuana!! Najua ni scandel nyingi Zitto anausishwa nazo, lakini wana jf msisahau cdm ni chama ambacho kiko makini sana, sidhani kama mambo haya ambayo Zitto anahusishwa nayo yangekuwa ya kweli alafu aendelee kushika nafasi aliyonayo ndani ya chama. PIGA UA WANGEKUWA WAMEISHAMFANYIA MAAMUZI MAGUMU!!
Pia sidhani kama Bw. Kafulila anaouwezo wa kumshawishi Kabwe hadi aamue kufanya siasa za kitoto!!
Alafu itakuwaje Zitto aame kwa ajili ya kugombea uraisi wakati akijua atakuwa hajatimiza umri wa kugombea?

Mmhhh!! Sidhani!! TUMUACHE APONE KWANZA AKIRUDI TUTAMUOJI VIZURI!!

Tusubiri uchaguzi wa ndani wa CHADEMA hapo 2013 ndipo tutafahamu kama bado atakuwa na hizo nafasi au hapana!!! Ukiniuliza endapo atakuwepo au hapana; jibu langu ni kwamba uwezekano ni mdogo, Lema atachukua nafasi yake labda Mzee Slaa aache Ukatibu na Zitto achukue nafasi yake na Lema awe makamu, otherwise; Zitto will be out...sana sana ili kumpoza watamtengenezea nafasi ya UKURUGENZI!!!

mnafiki,kigeugeu aliyekubuhu ni wewe!na kwa taarifa yako hakuna mwanasiasa hapa tanzania kijana anayeweza kulinganishwa na zitto.wafitini wote mtakufa!

HATA mimi Zitto namkubali but am telling u; don' trust politicians at all....utashangaa huyo huyo kesho na kesho na kesho kutwa; huyoooo ama CCM au hiyo NCCR na kumalizia kile kibwagizo chao "CHADEMA si mama yangu wala baba yangU"
 
HAYA WEWE KIBARAKA WA ROSTAM NA ZOKA, Zitto Kabwe Zuberi, rudi humu ndani umuombe radhi Kubenea, uliyemshambulia jana kwa matusi ya nguoni. Sasa umemsikia Msabaha mwana Kigoma mwenzako anasema wewe ndiye unayevuruga chama chao kwa tamaa yako ya madaraka?

Wanao kufahamu wanajua huna uwezo wa kuwa mwenyekiti wa chama. Huwezi kuongoza hata nyumba yako, utawezaje kuongoza chama? Ndiyo maana umekimbiwa na Jack… Acha kujifanya mwanasiasa makini, wakati unatumiwa na usalama wa taifa na Kikwete.
 
Mwandishi wa hii habari hajaitendea haki JF kwa kunakili maneno ya zitto kutoka humu na bila kuitaja JF.Amekopi post ya zitto bila kuitambua JF...!
 
Wakuu, yawezekana kabisa Kafulila anatumia jina la Zitto ili kutimiza malengo yake ya kuukwaa uenyekiti wa chama chake. Sasa watu kwa kuwa walishakuwa na kinyongo na Kabwe wanaanza kumshutumu yeye badala ya kuangalia udhaifu wa Kafulila na legitimacy ya madai yake kuhusu Kabwe.
 
Yote sawa, lakini lazima amuombe radhi Kubenea. Kama yeye alimnukuu Machali, kosa lake ni nini, mpaka Zitto akamparamia kamanda wetu. Aacha unafiki Zitto unaharibu mageuzi kwa faida ya Kikwete na Zoka...
 
zito atatumia muda mwingi sana kujitetea badala ya kujijenga, tatizo yeye anshauku sana ya madaraka ya juu na ndiyo maana ansyumba kutafuta madaraka ya haraka haraka. kumbuka kauli yake na Jk kuwa anataka Rais mwenye umri siyo kama yeye, na harakati za kugombea uenyekiti ndani ya CDM. ukimtazama kwa haya utajua nini shauku yake na hata haya yanawezekana yakawa ya kweli unless otherwise proved. Naomba nimshauri Zito mambo mazuri hayahitaji haraka kama alishaandikiwa kuwa Rais wa nchi hii atakuwa wakati ukifika. kauli zake nje ya CDM zinaonyesha namna alivyo na shauku ya madaraka makubwa. Nakushauri utulie
 
[h=1]Usalama wa Taifa wavamia CHADEMA[/h]
Imechapwa 08 December 2010
zoka_218.jpg



VIGOGO kadhaa wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) wametajwa “kuingilia” Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), MwanaHALISI limegundua.
Taarifa zilizopatikana kutoka ndani ya idara hiyo zinaeleza kuwa vigogo hao wana mahusiano ya karibu na Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Zitto Kabwe.
Anayetajwa rasmi kuwa na mahusiano na Zitto ni Naibu Mkurugenzi wa TISS, Jack Zoka.
Kufichuka kwa taarifa za kuwapo “uswahiba” kati ya Zoka na Zitto kumekuja katika kipindi ambacho CHADEMA kimekuwa kikituhumu maofisa wa juu wa usalama wa taifa kuvuruga uchaguzi mkuu uliopita.
Aidha, kuibuka kwa tuhuma hizi kumekuja wiki moja baada ya gazeti hili kuchapisha taarifa mbalimbali za mawasiliano kati ya Zitto na Rais Jakaya Kikwete.
Baadhi ya mawasiliano hayo, ambayo Zitto ameyapeleka kwa rais, aliyapeleka pia kwa baadhi ya watuhumiwa ufisadi nchini.
Kwa mujibu wa mgombea urais wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa ambaye alitangazwa kushika nafasi ya pili nyuma ya Rais Kikwete; viongozi wa TISS walihusika, kwa kiasi kikubwa, katika kile alichoita, “Kuchakachua matokeo ya uchaguzi.”
MwanaHALISI limefanikiwa kupata rekodi ya mshororo wa mawasiliano kati ya Zitto na Zoka.
Kuna mwingiliano wa simu za mdomo na maandishi (sms) kutoka kwa Zitto kwenda kwa baadhi ya vigogo wa ngazi ya juu serikalini na TISS, hasa Zoka.

Nyaraka za mawasiliano zinaonyesha kuwa Zitto amekuwa akiwasiliana na naibu mtendaji mkuu wa TISS huyo zaidi ya mara tatu kwa siku.
Kwa mfano, Zitto na Zoka walifanya mawasiliano ya simu mara tisa hapo tarehe 8 Agosti. Simu iliyotumika katika mawasilino hayo, ni Na. +255756809535 ambayo hutumiwa na Zitto na +255754787550 ambayo hutumiwa na Zoka.
Wakati mawasiliano hayo yanafanyika, Zitto alikuwa katika maeneo tofauti.
Mawasiliano ya kwanza kati ya Zitto na Zoka yalipokuwa yanafanyika, simu ya Zitto ilisomeka kuwa alikuwa katika maeneo mbalimbali.
Mathalani, wakati mwingine simu ilikuwa ikisomeka kuwa yuko Mtambani, Kinondoni Dar es Salaam, Kigoma Urban (Mjini), Kigoma Rural (Vijijini), Mtwara, Uwanja wa ndege-Ilala, Oyster Bay, Ukonga, Upanga na katikati ya mji.
Gazeti hili halikuweza kugundua mara moja undani wa mawasiliano ya Zitto na Zoka.
Kinachofanya baadhi ya wachunguzi wa mambo kujenga shaka ni kwamba mmoja ni mwanasiasa, tena kutoka chama kilichopo nje ya utawala; na mwingine ni mtumishi wa idara ya usalama inayolalamikiwa kukandamiza upinzani nchini.
Hata hivyo, taarifa zinaonyesha kuwa mawasiliano kati ya Zitto na Zoka yalianza kupamba moto kuanzia tarehe 6 Agosti 2010, siku moja baada ya CHADEMA kuzindua kampeni zake za urais.
Kulingana na uchunguzi, siku hiyo, tarehe 6 Agosti, simu ya Zitto ilisomeka kuwa yuko Kigoma Urban.
Katika mkutano wa ufunguzi wa kampeni, CHADEMA kupitia kada wake mashuhuri, Mabere Marando, iliibuka na lundo la tuhuma dhidi ya vigogo kadhaa wa serikali, CCM na idara ya usalama wa taifa.
Akizungumza na maelfu ya wananchi katika viwanja vya Jangwani, Dar es Salaam, Marando alisema wizi wa fedha katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), ndani ya Benki Kuu ya taifa (BoT), ulifanywa na serikali na washirika wake.
Miongoni mwa vigogo aliodai kuwa walihusika kufanikisha wizi huo, ni rais wa sasa, Jakaya Kikwete, rais mstaafu Benjamin Mkapa, mbunge wa Igunga, Rostam Aziz na Edward Lowassa.
Akiongea kwa kujiamini, Marando alisema, “fedha za EPA ni wizi uliotiwa baraka na serikali ya CCM na ndio uliomsaidia rais Kikwete kuingia madarakani mwaka 2005.”
Kuanzia hapo hadi sasa, Zitto na Zoka wamekuwa na mawasilino ya mara kwa mara, na karibu kila siku huzungumza kwa simu.
Mawasiliano mengine ya mara kwa mara yalifanyika tarehe 7 Agosti 2010, siku mbili tangu hotuba kali ya Jangwani. Yalianza saa 10:17 na kuendelea tena saa 10:50, saa 10:51:31, saa 11:46:13, saa 12: 14:46, saa 12:26:48 na saa 13:50: 21.
Lakini Zitto alipoulizwa kuhusu sababu ya yeye kufanya mawasiliano ya mara kwa mara na vigogo wa TISS, alisema hajui na hakumbuki lolote kuhusu kuwapo mawasiliano hayo na Zoka au mkuu yeyote wa idara hiyo.

Zitto amesema yeye, akiwa mwanasiasa na kiongozi, anazungumza na watu wengi kutoka katika taasisi na mashirika mbalimbali ndani na nje ya nchi, lakini hajui kitu kuhusu usalama wa taifa.

Alipobanwa kuhusu mazungumzo yake na Zoka, hasa yale ya 3 Novemba 2010, saa nne na dakika 56 asubuhi, siku mbili baada ya uchaguzi kumalizika, Zitto alisema, “Siku hiyo nilizungumza na watu wengi sana. Siwakumbuki ni akina nani hasa.”
Alisema, “Hicho ndicho kipindi ambacho matokeo ya uchaguzi nchini kote yalikuwa yakizuiwa ikiwamo kwetu Kigoma. Na ukumbuke mimi nilipigwa mabomu na polisi na usalama wa taifa. Nakumbuka viongozi wengi wa vyombo vya ulinzi na usalama walinipigia simu kunijulia hali na kupata taarifa ya kilichotokea,” anaeleza.

“Sasa kama Zoka naye alinipigia siku hiyo sikumbuki; lakini nilipigiwa na wengi…Naomba uniambie kitu, hivi mnachokitafuta hasa ni nini?” aliuliza.
Katika njia ya kujitetea, Zitto aliuliza, “Mwanasiasa kuongea na wakuu wa vyombo vya usalama ni kosa? Maana, hata kama ningekuwa nimezungumza naye, kosa langu liko wapi?” alieleza mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini.

Alipoelezwa kuwa haoni hiyo ni hujuma dhidi ya chama chake kwa kuzungumza na viongozi wa TISS na kile ambacho amekuwa akikizungumza kikiwa hakifahamiki kwa viongozi wake, Zitto alisema, “Sijawahi kukihujumu chama changu mahali popote, siku yoyote.”

Jitihada za gazeti hili kuzungumza na Zoka hazikufanikiwa katika kipindi chote
cha mwishoni mwa wiki, kwa vile kila alipopigiwa, simu yake ya mkononi ilikuwa haipokelewi.

Hata ujumbe mfupi wa maneno uliotumwa kwenye simu yake saa 2:53 asubuhi ya Jumapili; ukieleza sababu za gazeti kuzungumza naye, haukujibiwa.

Aidha, tarehe 2 Novemba, siku moja baada ya kuzungumza na Zitto, Zoka alinukuliwa akikana madai ya Dk. Slaa, kuwa TISS imesaidia kuvuruga uchaguzi.
Katika taarifa yake aliyoitoa mbele ya waandishi wa habari, ofisini kwake jijini Dar es Salaam, Zoka alisema, “Dk. Slaa amekuwa akidanganywa na watu wanaojiita maofisa wa usalama wa taifa.”
Hata hivyo, kuna meseji mbalimbali kuhusu udini na uamuzi wa CHADEMA kususia hotuba ya rais Kikwete ambazo zilitumwa na Zitto kwa baadhi ya wabunge wa CHADEMA ambazo zinadaiwa kuandaliwa na idara ya usalama wataifa.
Ujumbe huo unadaiwa kuandaliwa kwa ustadi mkubwa katika kukuza suala la udini na kuleta mtafaruki katika chama.
 
Sio siri nimevunjwa moyo na zitto,naomba chadema wamwangalie kwa makin ikiwezekana piga chini kabisa kwan yeye ni nani kwnza sahz tusamdharau .Lakini na amin kabisa chadema nichama thabiti kwahiyo wasikubali kurudishwa nyuma kwaajili ya mtu mmoja corrupted.Waendeleze mapapambono na sisi tupo nyuma yao,sisi sahivi hatudanganywi na propaganda oh sijui udini sijui ukabila hatudanganyiki.Endelezeni mapambano chadema mana nyie ndio wakombozi wetu.
 
Anachofanya zito ni usaliti kwa demokrasia. Kama anahisi kutoridhishwa na jinsi CHADEMA inavyoendeshwa ajiunge na hao anofikiri ni marafiki zake. Hatuhitaji watu wa namna hii ndani ya CHADEMA.
 
Sihitaji kwenda NCCR ili kugombea Urais kwani chama changu ni kikubwa zaidi na kitanipa Urais kwa urahisi (FINE) kuliko NCCR ambacho ni chama kisicho na rekodi yeyote ya kupigania maslahi ya nchi (WHAT?) hata wakati kilipokuwa chama kikuu cha upinzani nchini. .
Brother Zitto, you are also called to ‘think great’. Nothing grants you any right to tarnish the image and/or obliterate the history of NCCR-Mageuzi.
 
Sio siri nimevunjwa moyo na zitto,naomba chadema wamwangalie kwa makin ikiwezekana piga chini kabisa kwan yeye ni nani kwnza sahz tusamdharau .Lakini na amin kabisa chadema nichama thabiti kwahiyo wasikubali kurudishwa nyuma kwaajili ya mtu mmoja corrupted.Waendeleze mapapambono na sisi tupo nyuma yao,sisi sahivi hatudanganywi na propaganda oh sijui udini sijui ukabila hatudanganyiki.Endelezeni mapambano chadema mana nyie ndio wakombozi wetu.

Kaazi kweli kweli ndugu yangu...ukiona mtu anasemwa sana kwa mabaya mengi yake ni ya kupikwa ujue mbele yake kuna neema kubwa sana...historia inasema nyerere pia alisemwa amenunuliwa na wazungu mwaka 1958 pale tabora aliposimamia hoja ya TANU kushiriki uchaguzi ulioitwa wa kibaguzi wa kupiga kura tatu lakini hakurudi nyuma...leo hii kila mmoja anamwona nyerere kama shujaa hata sie wapinzani tunamtumia kama reference majukwaani...naiona hali hii kujitokeza kwa zitto, yawezekana presence yake inasababisha kihoro kwa watu wengi sana..lakini sisi tunaisoma siasa na kuipractice tunaamini kuwa kiongozi ni yule mtu ambaye yupo tayari kuachia madaraka( platonic ideas says only philosophers can govrn the country because of two things, first they have the qualifications and second they don't want to do so) hapo ndio ninapomwona zitto kama kiongozi anayeweza kupita humo tofauti na viongozi wengi wao ni ma mangi meza hawataki kuachia madaraka hata kwa nguvu na ndio maana leo hii baadhi ya watu wanakubali kutumika..
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom