Kafulila na Zitto wanaivuruga NCCR - Moses Machali

Kafulila na Zitto wanaivuruga NCCR - Moses Machali

Status
Not open for further replies.
Donyongiape.unamfahamu mmiliki wa tanzania daima na mmiliki wa mwanahalisi.tatizo la wanachadema hawaijui chadema kiundani wanaijua kwa kupitia magazeti ambayo hata wanaandika hizo habari hawamjui na hawajui wanaandika kwa manufaa gani siku wanachadema wakiujua ukweli wengi watakata tamaa.


Tatizo lako ni uwezo mdogo wa kufikiri....
Jadili hoja na uache kurushia vijembe wamiliki wa magazeti.
Tunategemea wewe utoe ushahidi hapa JF ili tujue nani mkweli kati ya ww au magazeti. By the gazeti limemtaja Machali mbunge wa kasulu sasa inakuaje unalituhumu gazeti?
Kwa maoni yangu Machali ndiye wa kutuhumiwa kwani ye ndo mtoa taarifa otherwise athibitishe kwamba hakutamka maneno kama hayo..
 
Watu hawana hata uungwana wa kusema huyu mtu ni mgonjwa, hajatoka hospitali. Huruma ya kibinaadamu hawana.

Kuna uchawi gani zaidi ya huu? Mwelekeo ule ule >Tanzania Daima>MwanaHalisi yote yanamilikiwa na viongozi waandamizi wa chama changu. Nimechukia sana.

Nitawasilisha malalamiko rasmi kwa Katibu Mkuu wa chama ili Wamiliki wa Tanzania Daima (Mhe. Mbowe) na wa MwanaHalisi (Ndugu Komu) waeleze mwenendo wa magazeti wanayomiliki kuhusu mimi. Nimechoka kuzushiwa uwongo na magazeti haya kila kukicha.
 
Tatizo lako ni uwezo mdogo wa kufikiri....
Jadili hoja na uache kurushia vijembe wamiliki wa magazeti.
Tunategemea wewe utoe ushahidi hapa JF ili tujue nani mkweli kati ya ww au magazeti. By the gazeti limemtaja Machali mbunge wa kasulu sasa inakuaje unalituhumu gazeti?
Kwa maoni yangu Machali ndiye wa kutuhumiwa kwani ye ndo mtoa taarifa otherwise athibitishe kwamba hakutamka maneno kama hayo..

Kwa nini magazeti hayo tu yanayomilikiwa na viongozi waandamizi wa chadema ndio yatoe habari hiyo? Kwanini sio RaiaMwema? Kwanini sio Mwananchi? Kwa nini sio Majira?
Wamiliki wa magazeti wanaushawishi mkubwa kwenye sera ya gazeti. Ushahidi gani unaoutaka? Wao wametoa ushahidi gani kwamba nahusika na vurugu za NCCR kama sio kubwabwaja tu kwa mbunge wa Kasulu mjini ambaye kapata huo ubunge kwa mgongo wa Kafulila na anti chadema sentiments za watu wa Kigoma?
Mimi mhusika ninapinga na nimeandika humu, wewe unahitaji ushahidi upi?
 
Zito kama unaona huko sahihi yashitaki hayo magazeti kwenye Baraza la waandishi wa habari au wizara husika na siyo kwa katibu mkuu wa chama chako. Ila uache unafiki na usaliti wako.
 
hii habari itakuwa na ukweli asilimia 95,kwa sababu mwenendo wa zitto cdm siyo ule wa mwanzo,na kwa mtindo huu ccm watatawala milele nchi hii

Siku zote nimekuwa nasimamia yale ninayoamini. Sifanyi kazi zangu ili kufurahisha watu bali kuzingatia maadili yangu na itikadi yangu na maslahi ya nchi yangu. Sifanyi siasa za drama maana naamini katika siasa za hoja. Kamati yangu ya Bunge ndio inaongoza kwa kusimamia vema fedha za Umma. Hutaki kuona kwa kuwa umelishwa sumu ya propaganda za kumchukia Zitto bila sababu yeyote ya msingi. Mimi sijali nafanya kazi zangu.
 
Watu hawana hata uungwana wa kusema huyu mtu ni mgonjwa, hajatoka hospitali. Huruma ya kibinaadamu hawana.

Kuna uchawi gani zaidi ya huu? Mwelekeo ule ule >Tanzania Daima>MwanaHalisi yote yanamilikiwa na viongozi waandamizi wa chama changu. Nimechukia sana.

Nitawasilisha malalamiko rasmi kwa Katibu Mkuu wa chama ili Wamiliki wa Tanzania Daima (Mhe. Mbowe) na wa MwanaHalisi (Ndugu Komu) waeleze mwenendo wa magazeti wanayomiliki kuhusu mimi. Nimechoka kuzushiwa uwongo na magazeti haya kila kukicha.
Kazi kweli kweli!!! Tafuteni muafaka nyie watu.

Japo wengine hatuujui ukweli wa hizi habari lakini pia haileti afya nzuri kwa magazeti yanayomilikiwa na viongozi wako pekee kukuandama kila mara japo inawezekana kusiwe na influence ya wamiliki. Kwa hiyo unataka kusema ni Komu ambaye hakumaliza hata darasa la saba? Au ni Kubenea?

Ila kwa habari hii kama kweli Rafiki yangu Machali ndio source wa hiyo habari basi lawama zote ziende kwake na ndie anayepaswa kuthibitisha kwanza
 
Good! Ndio maana ninasema Chadema ni chama cha watu makini.Kujitokeza mara moja kujibu hoja hii kunakupa credit kubwa.

Endelea kupigania Chadema na hakika Mungu akipenda baada ya zama za Slaa huenda ukawa wewe.

Kila la kheri.

Angalia ulivyokuwa mnafiki wewe si ndio umeleta umbeya humu JF baada ya Zitto kujitokeza kujibu kwa aibu unaleta unafiki..

Ndio maana hata Zitto kakupotezea kukujibu..

Zitto nadhani wachawi wako umewaona
 
Nadhani unatakiwa kuwa makini sana na kauli zako kama kiongozi;
1.Wewe sio tishio hata kidogo,wananchi walikuamini wakawa wanakupa support hivyo usigeuze nguvu na imani ya wananchi kuwa jitihada zako binafsi.Nakupa angalizo kwa hili kwa kuwa usijidanganye kuwa wewe unaweza kusimama peke yako bila nguvu za wananchi nyuma yako.Ukae utafakari sana kwa nini jukwaa hili ambalo wewe ulikuwa kinara umeanza kujadiliwa negatively.Kwa nini asijadiliwe Dr. Slaa? ama ndio unataka kutudanganya wewe unanguvu,uwezo,mvuto kwa jamii zaidi ya Dr. Slaa! ndio maana unajadiliwa sana kwa mtazamo hasi!?

2.Inawezekana ni kweli kuwa Huyo anayeongoza gazeti la mwanahalisi hajafika darasa la saba ,ila kuuhusisha udhaifu wake na darasa lake bila kuwa na facts ni udhaifu wako kama kiongozi.Unataka kutuambia wananchi wanaokuunga mkono wewe na kukubali kama kiongozi wao hakuna ambao hawajamaliza darasa la saba kama huyo kiongozi wa mwanahalisi!.
Unatuambia kuwa ambao hawajafika darasa la saba hawana mchango wowote kwa maendeleo ya jamii !,Inaelekea wewe huwahitaji wakuunge mkono kama kiongozi wao!?
Kumbuka hawa ni wale ambao wamechoka na manyanyaso ya CCM wakaona walinyiimwa haki yao ya msingi hivyo wakaona wakuunge mkono ili kizazi chao kijacho kisishindwe kufika hata darasa la saba.Leo hii unawadharau.

3.Siku zinavyozidikwenda unapoteza mvuto sana Kamanda,ungeweza kusoma alama za nyakati ungetafuta mbinu mbadala za kujisafisha kama ni kweli wanayosema.Lisemwalo lipo kama halipo laja.
Mimi binafsi sio muumini wa habari za mtaani ila habari inapoletwa na watu wanaanza kukuzungumzia kwa historia jinsi wanavyokufahamu kuanzia TOSAMAGANGA na UDSM ni hatari sana . Binadamu tuna tabia ya kuunganisha matukio kwa hiyo kuwa makini.

Mimi nakwambia wazi "nilianza kupata mashaka na wewe ulipoanza kutembelea magari ya kifahari ambapo unajua wazi kuwa wanaharakati tunapinga matumizi ya magari ya kifahari kwa viongozi wa uma.Hata kama una biashara zako binafsi na hela nyingi jamii yetu sio ya kihivyo ,kuona mtu kama wewe unayefahamika kama mkombozi wa wanyonge kujionyesha kwa ufahari kama wasanii wa marekani."

MTAZAMO

Sina magari ya kifahari. Siamini katika utajiri hata kidogo. Sina biashara yeyote. Kazi yangu ni Ubunge tu. Wenye magari ya kifahari huwaoni?

Mmeaminishwa kwamba mimi nina hela nyingi sana nanyi mkaamini bila hata kuhitaji ushahidi. Ninaishi nyumba ya kupanga Tabata Dar es Salaam. Nina gari moja tu Dar es Salaam aina ya Freelander na moja Kigoma Jimboni GX niliyonunua second hand. Kama una gari yeyote ya kifahari unayoambiwa ni yangu ipige picha uilete hapa JF. Unalishwa sumu na kukubali bila hata kufikiri na unajiita great thinker? Gosh
 
Watu hawana hata uungwana wa kusema huyu mtu ni mgonjwa, hajatoka hospitali. Huruma ya kibinaadamu hawana.

Kuna uchawi gani zaidi ya huu? Mwelekeo ule ule >Tanzania Daima>MwanaHalisi yote yanamilikiwa na viongozi waandamizi wa chama changu. Nimechukia sana.

Nitawasilisha malalamiko rasmi kwa Katibu Mkuu wa chama ili Wamiliki wa Tanzania Daima (Mhe. Mbowe) na wa MwanaHalisi (Ndugu Komu) waeleze mwenendo wa magazeti wanayomiliki kuhusu mimi. Nimechoka kuzushiwa uwongo na magazeti haya kila kukicha.
Duh! Kuna kivumbi hapa! Na Machali kamsemee kwa Mbatia. Ila ww sio CHADEMA nina uhakika 100%! Ingawa mm sio mwanachama wa chama chochote hapa nchini..maana siasa za bongo ni longolongo tu!
 
Watu hawana hata uungwana wa kusema huyu mtu ni mgonjwa, hajatoka hospitali. Huruma ya kibinaadamu hawana.

Kuna uchawi gani zaidi ya huu? Mwelekeo ule ule >Tanzania Daima>MwanaHalisi yote yanamilikiwa na viongozi waandamizi wa chama changu. Nimechukia sana.

Nitawasilisha malalamiko rasmi kwa Katibu Mkuu wa chama ili Wamiliki wa Tanzania Daima (Mhe. Mbowe) na wa MwanaHalisi (Ndugu Komu) waeleze mwenendo wa magazeti wanayomiliki kuhusu mimi. Nimechoka kuzushiwa uwongo na magazeti haya kila kukicha.
pole sana,jipe Moyo usije ukauzidisha ugonjwa bure.NIA YAO si nzuri.

MUNGU AKUPONYE MKUU.
 
Kazi kweli kweli!!! Tafuteni muafaka nyie watu. Japo wengine hatuujui ukweli wa hizi habari lakini pia haileti afya nzuri kwa magazeti yanayomilikiwa na viongozi wako pekee kukuandama kila mara japo inawezekana kusiwe na influence ya wamiliki. Kwa hiyo unataka kusema ni Komu ambaye hakumaliza hata darasa la saba? Au ni Kubenea? Ila kwa habari hii kama kweli Rafiki yangu Machali ndio source wa hiyo habari basi lawama zote ziende kwakena ndie anayepaswa kuthibitisha kwanza

Uandishi wa habari unataka kubalance story. Machali akisema anapaswa kutafutwa Zitto kuthibitisha. How cant you see that logic?

Inawezekana wamiliki hawakusukuma hiyo habari. Inawezekana wamiliki wapo nyuma ya hiyo habari. Yote yanawezekana. Ndio maana nimeamua kupeleka jambo hili kwenye chama. Nitamwandikia rasmi Katibu Mkuu ili wamiliki wa magazeti haya ambao ni viongozi waandamizi wa chama wajieleze juu ya mwenendo wa magazeti yao kuhusu mimi. Hilo lina ubaya?
 
Salaam

Kuna wakati unaposoma akili za watu humu ndani na hasa wale wanaojitambulisha kama makada wa Chadema unaweza ama kukata tamaa na mabadiliko ya kweli katika nchi yetu ama hata kuamua kujilipua na kujiunga na CCM.

Inashangaza kuona kuna watu wanaojifaragua kama great minds wanakuwa rahisi kuamini sumu za kisiasa ambazo ukweli zinalenga kulinda maslahi ya watu kwa kuwaharibia sifa wengine.

Inakuwaje mtu mwenye akili zake timamu akaamini habari za kutengenezwa za udaku wa kisiasa unaomilikiwa na kufadhiliwa na mahasimu wa Zitto wakiwemo Kubenea na Mweka Hazina wa Kudumu wa Chadema Anthony Komu ambaye kwake yeye Zitto ni tishio kwa maslahi yake na maslahi ya "wenzake" wanaoamini kuwa Chadema ni chama chao?

Inakuwaje wanaojiita great minds kuwa tayari kuamini kuwa Zitto ana mpango wa kugombea urais mwaka 2015 wakati wote tunajuwa kuwa wakati huo atakuwa hajatimiza umri wa miaka 45.

Inasikitisha zaidi kuona kuwa kuna baadhi ya wapenzi wa Chadema wanamshutumu Zitto kwa madai ya kuonyesha dalili za kutaka kugombea Urais eti huku akijua kuwa chama chake tayari kina mgombea. Yaani Chama cha DEMOKRASIA na maendeleo tayari kina mgombea wa Urasi wa mwaka 2015 wakati ndio kwanza tupo mwaka 2011? Halafu mna jeuri ya kuwalaumu wengine kwa ukandamizaji wa haki za kidemokrasia...

Na hili suala la Zitto kuwa na nia ya kuivuruga CHADEMA eti kwa mipango yake ya kuhamia ama kugombea Urais kupitia NCCR linaonyesha dalili kubwa za kutokujiamini ndani ya kundi la wahafidhina wa Chadema. Iweje Zitto huyu mnayemtukana, kumpiga vita na hata kudai kuwa hana nguvu kisiasa suala ama hisia za yeye kuondoka Chadema kuhusishwa na nia ya kuvuruga chama chenu?

Lakini kama wanaDEMOKRASIA inakuwaje mnakuwa na mitazamo hasi ya nia ya mtu (kama ipo) ya kuhama chama kimoja kujiunga na chama kingine atakachoamini kuwa kinaendana na fikira, ndoto ama hata tamaa zake ziwe za kisiasa ama za hatima ya nchi yetu. Hizi si fikira za wanademokrasia, ni fikira za mafashisti wanye nia ya kutumia kauli mbiu za demokrasia kuhalalisha matamanio yao ya kifashisti.

Ninachosoma kutoka katika siasa hizi za kichokoraa zinazoendeshwa na makada na hata viongozi wa Chadema humu ndani ya jukwaa letu na kwengineko dhidi ya Zitto ni ishara za kutojiamini miongoni mwa establishment ya CHADEMA wenye mitazamo na malengo ya kihafidhina. Badala ya kufanya jitihada za kujisafisha na kujipanga upya kuondokana na tuhuma mbalimbali zinazowakabili zinazopelekea chama chao kuvikwa ama kujivika magamba mbalimbali kama ya udini, ukabila, ufisadi nk, wako busy kumsulubu mtu ambaye anaonekana kuwa kama kioo cha Chadema tofauti ambayo watanzania wangependa kuiona inakuwa na sio Chadema waliyoikumbatia wao.

Kwa ujumla na kwa jinsi nijuavyo mimi Zitto bado hajawahi kuwa na nia ya kuondoka CHADEMA ingawa kuna mengi yanayomvunja moyo kila kukicha. Lakini kama atakuja kuhama CHADEMA na kujiunga na NCCR naamini itakuwa ni suala la kiitikadi zaidi kuliko nafasi yake kisiasa.

NCCR tofauti na ilivyo CHADEMA, ni chama pekee cha upinzani chenye mizizi ya itikadi za KIJAMAA zilizojikita katika nia ya kujenga Tanzania yenye kujali na kuthamini utu. Na naamini mpaka sasa Zitto, Mnyika, Baregu, Kitila Mkumbo bado wanaamini katika itikadi ya UJAMAA ingawa wanalazimika kunyamazia sera, nyendo na matamanio ya kibepari ambao ndio mzizi wa CHADEMA.

Na ni wazi kuwa ili NCCR ifufuke na kuteka hisia za watanzania kuwa wanaweza kuwa chama mbadala wanachotamani kukiona na kukiunga mkono kwa dhati, kuna ulazima wa kubadili uongozi uliokuwepo na kusimika uongozi mpya utakaoweza kukipa uhai. Vilevile ni mabadiliko ya uongozi sasa ndiyo yatakayoweza kutoa nafasi kwa WAJAMAA MASALIA wanaolazimika ama kulazimishwa kubaki CHADEMA na CCM kupata uwanda wa kisiasa kujaribu kujenga Tanzania waitakayo na kurudisha siasa za kiitikadi badala kuendelea kutumika kuendeleza siasa za tuhuma, chuki, uzandiki, personalities na ujanjaujanja mwengine.

Napenda kuwaasa wale waliodedicate maisha na akili zao katika kummaliza Zitto iwe kisiasa ama kimaisha watambue kuwa adui wao sio Zitto bali yale anayoamini kuwa yanaopaswa kubadilishwa na kuepukwa na chama chake. Nguvu mnazotumia hapa kujaribu kumbomoa Zitto ni vizuri mkazitumia kujenga chama chenu kiweze kuaminika na watanzania na sio kuendelea kutegemea mtaji wa sumu ya chuki dhidi ya CCM na serikali yake tu.

Naamini historia ipo wazi kuwaamsha kuwa kwa siasa hizi za chuki na uzandiki, kamwe hamtaweza kupambana na nguvu na akili za Zitto kisiasa…..Lakini pia wakati mwengine mjaribu kuonyesha ubinadamu kidogo hata kama uungwana kwenu mwiko!

Mnachokifanya sasa hakina tofauti na aliyokuwa akiyafanya Mchungaji Mtikila wakati Mwalimu alipokuwa amelazwa hospitalini na hata baada ya kufairiki. Huu sio Utanzania!

Comrade Omarilyas,

With today's post, you actually took things to a new level, probably one of the most intelligent item I've seen in Jamii Forums in a long while.My brother ,some folks are merely stating their own personal vengeful desire of what they want to happen because they only know how to transfer hatred and a lack of goodwill to all those who oppose wale wanaowataka.They joined the ranks of "political no-hopers",wengine wamepoteza dira kabisa they are not one of the sharpest knives in the draw katika siasa zetu za kuichinja CCM na sera zake

Some people in Opposition are very wicked . Easily as wicked as the Politicians they malign daily. Add to that the consideration of how some folks are forever condemned to seeing things through an ethnic prism and you will understand the uphill battle the good guys in our politics face . Many who claimed to admire Zitto Kabwe and his brave efforts now speak about him so ungraciously that you begin to realise that those folks never had enduring integrity to start with anyway .

Baadhi ya waandishi wa habari wanatumikia maslahi ya watu binafsi.Media fraternity is loosing credibility.Kuna waandishi makanjanja wapo mjini kwa sababu ya kutumiwa kisiasa,wanaandika habari za ajabu ajabu tu.Bora Global publishers walijipambanua wao wanaandika habari gani.Watanzania wanastahili better than these.Wanalishwa sumu kwa ajili ya kumchafua mtu kisiasa.

Gazeti ambalo lilikuwa limepoteza credibility linataka kuirudisha kupitia mgongo wa watu na mbinu yao ya kuuwa ndege wawili kwa jiwe moja.Sitta pamoja na mapungufu yake lakini alichosema kuhusu mwanahalisi na mtiririko wa majibu ya mwanahalisi desparately unadhihirisha hilo.

Zitto anashambuliwa na watu waoga wa changamoto,ni watu waliodumaa kidemokrasia.Tufuate Misingi ya democracy kama tunataka kuwapeleka watanzania kunakostahili,tuache ukandamizaji.Chuki ambayo watanzania wamejazwa juu ya zitto na wanasiasa wengine wenye mwelekeo wa kweli ni kubwa.Tuendeleze huu mchezo lakini kama ni kuangamiza utatuangamiza sote.Hii ni suicide pact

Niendelee kutoa wito kwa watanzania na hasa hapa Jamii forums,tusikubali kulishwa ovyo na tusikubali kuwa wafuasi na mashabiki vipofu wa mtu .Hoji,chambua,kosoa fikia hitimisho na tuwe flexible katika reasoning

Namshangaa sana mtu anayeita mtu fulani kafanya mawasiliano na mwana CCM au usalama wa Taifa,lakini ukimuuliza atoe ushahidi wa kilichoongelewa hatoi.Tuache siasa za majitaka tujikite kwenye hoja na tusugue fikra kutafuta suluhisho la matatizo yanayowakabili vijana.Tumeshindwa mammbo mazito ambayo ni ajenda za kitaifa tunarukia mambo mepesi ya kuchafua watu na siasa mdebwedo.

Naendelea kuli-encourage gazeti la Raia mwema na akina Jenerali ulimwengu waendelee kulinda heshima yao kwa jamii kwa kuwa ni gazeti lenye weledi wa mambo,waandishi wazuri.Msije mkawa kama wale waandishi wanaoandikiwa habari na kuchapisha kwa mbwembwe kama vile wao ni waandishi wa habari,waendelee kuficha ukanjanja wao na uzandiki lakini ukweli siku moja utasimama
 
Kwa nini magazeti hayo tu yanayomilikiwa na viongozi waandamizi wa chadema ndio yatoe habari hiyo? Kwanini sio RaiaMwema? Kwanini sio Mwananchi? Kwa nini sio Majira?

Wamiliki wa magazeti wanaushawishi mkubwa kwenye sera ya gazeti. Ushahidi gani unaoutaka? Wao wametoa ushahidi gani kwamba nahusika na vurugu za NCCR kama sio kubwabwaja tu kwa mbunge wa Kasulu mjini ambaye kapata huo ubunge kwa mgongo wa Kafulila na anti chadema sentiments za watu wa Kigoma?

Mimi mhusika ninapinga na nimeandika humu, wewe unahitaji ushahidi upi?

Nakubaliana na hoja zako lakini mtu wa kwanza kumnyooshea kidole ni mbunge wa kasulu mh Machali kwa sababu yeye ndo source ya information na kibaya zaidi ametoa taarifa hizo ww ukiwa mgonjwa...

Ugua pole
 
Tatizo lako ni uwezo mdogo wa kufikiri....Jadili hoja na uache kurushia vijembe wamiliki wa magazeti.

Wewe mwenye uwezo mkubwa wa kufikiri unashindwa kutambua nini maana ya hoja na nini propaganda. Yaani tuhumu zilizojengwa na hisia zikasambazwa na siasa za chuki tayari zimekuwa hoja kwako. No wonder kuna maelfu ya watanzania wakiwa tayari kuhalalisha na kushangilia wehu wakimwagia mafuta nyasi kavu zilizo juani wakiamini zitaleta neema kwa viumbe vilivyopo na vijavyo!

Tunategemea wewe utoe ushahidi hapa JF ili tujue nani mkweli kati ya ww au magazeti. By the gazeti limemtaja Machali mbunge wa kasulu sasa inakuaje unalituhumu gazeti?

Hivi kati yako wewe na Zitto ni nani anajua historia, uwezo, uchafu na halihalisi ya sekta yetu ya habari? Hivi unajua asili ya Mwanahalisi na ni nani aliyetoa wazo, mikakati, mtaji na hata kuliwezesha gazeti hilo kusimama na kujitenezea soko kabla ya kujitumbukiza katika ukuwadi wa siasa za majitaka za kulinda na kusafisha maslahi ya maadui wa kweli wa watanzania?


Kwa maoni yangu Machali ndiye wa kutuhumiwa kwani ye ndo mtoa taarifa otherwise athibitishe kwamba hakutamka maneno kama hayo.

Kwa kuwa una uhakika aliyoyasema Machali ndiyo yaliyoandikwa na sio uhandisi wa habari wetu ambao unalenga kuchezea maneno ya watu ili kuhalalisha nia mbaya na maslahi machafu ya waandishi na wamiliki wa magazeti hayo?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom