Zitto tatizo ni wewe mwenyewe na tatizo lenyewe haliko kwenye siasa bali liko kwenye mitazamo yako kuhusu maisha. Mimi mwenyewe umeniudhi, Umenikera na kunihuzunisha sana pale ulipochanganya "kutokumaliza darasa la saba" kwa mmiliki wa Gazeti la Mwanahalisi na Hoja ya Machali. Inaonyesha huwa ukifika kijijini kwako unawaona wapiga kura wako hawastahili kuwa na mbunge "Msomi" kama wewe kwani najua wengi wao hawajamaliza darasa la saba!!
Usihusishe demokrasia na CDM, kwanini alikataliwa kugombea uenyekiti?.... kwanini Dr. Slaa alimfukuza kiongozi wa CDM kwenye mkutano wa hadhara?... Hiyo ndiyo demokrasia kweli?Ushauri wa bure kwa Zitto!, abadilike aache kuwa dictator!, aanze kuamini katika ''wengi wape'' na sio ''akili yangu ndio mwongozo'' hiyo ndio democracy. Bila kubadilika kwa vitendo, utazirai kisiasa kama alivyokua mrema!
Narudia tena, wanaomponda zitto, kama wanayosema ni ya kweli waje hapa na majina yao real. Sio tunajificha nyuma ya hizi IDs fake kumshambulia mtu...
Mwita hii ni propaganda maalumu inafanywa kwa malengo maalumu. Sijawahi kutumika na CCM maisha yangu yote na CCM wanajua hivyo. Lakini ukitaka kuua nyota ya mwanasiasa yeyote wa upinzani ni kusema anatumika. Hata marehemu Chacha Wangwe walisema anatumika na CCM ili kumvunjia heshima wala hapakuwa na ushahidi wowote wa hivyo. Mpaka anakufa alikufa na kinyongo hiki. CCM hawawezi hata siku moja kunitumia. Nimekuwa ninafanya kazi zangu Bungeni kwa umahiri mkubwa sana and yet maadui zangu wa kisiasa wanasema haya mambo ya kipuuzi kabisa.
Ni juu yako unaamini hizi propaganda au unazipuuza. Lengo ni kunivunjia heshima mbele ya jamii. Kwa muda mrefu Mwanahalisi wamekosa cha kuandika juu yangu na wameamua kutumia mgogoro wa NCCR kunihusisha ili tu kuendeleza propaganza zao chafu dhidi yangu.
Nimeisoma hii thread yote nikataka nisichangie kabisa lakini nimeona niwaambie vijana wenzangu tunafanya makosa yale yale! Hii thread imeibua wapinzani wa Mbowe na wengine wazi wazi na wengine kwa kipropaganda wamemnanga Mbowe humu utafikiri wengine hatuelewi mlengo wao! Mbowe ana mapungufu kama binadamu lakini kama mwenyekiti ktk siasa za Tz anafanya kazi kubwa sana! Chama hakiwezi kuendelea kama kina mwenyekiti dhaifu,hali ya sasa ya CDM tunaiona na haijatokea kwa bahati mbaya bali uongozi bora chini ya Mbowe!Mungu wangu, utaacha taifa hili lichanganyikiwe na kukosa msimamo hata lini? Tunahitaji uongozi imara kwa maslahi ya nchi hii, ee Bwana utuhurumie.
'Salvation shall come from the hills, the man shall rise and save the people at their hour of need'.
Hawa vijana wenzetu wanatuhumu kwa namna ile ile wasiyoipenda wakituhumiwa, mbaya zaidi wanamuita Mbowe mzee na asiyetaka challenge! Inashangaza sana, Mbowe ana mapungufu yake lakini amekuwa imara sana, hiyo "demokrasia" mnayoisema kwa uchanga wa siasa zetu leo CDM ingekuwa na mwenyekiti kama Mbatia!!mkuu sasa wanaosema unatumika ni kina nani? Na ni kweli unawashutumu mbowe na komu? Inawezekana hao ndio wanaotengeneza mazingira ya wewe kuonekana unatumika?
Sasa kusema ukweli kuwa Kubenea kaishia darasa la 4 ndio amekuudhi? Ndio ukweli hakuna neno jingine la kusema..
Ulitaka aseme Kubenea ana Masters wakati hana?
Kwa nini SITA na Zitto hawataki waguswe na vyombo vya habari???Wewe ni mjinga kuliko hata Kubenea unabwabwaja ujinga hapa bila hata aibu!..hivi kweli unaweza ukamlinganisha zitto na mbowe katika nyanja ya uongozi hapa tanzania?
...hivi haujui kama Mbowe amekuwa akihakikisha hakuna mtu anayechipua kumpiku ktk chadema? ...kwanini huko kutumiwa kwa zitto kuanzie pale tu alipoamua kugombea uenyekiti na si pengine popote?...hivi kweli unatumia akili kufikiri au ndo yale yale masaburi yenu watoto wa mbowe?
...hebu waulize mapacha watatu=mbowe, slaa na komu ni nini hasa kinawasumbua kwa zitto zaidi ya dhamira?...zitto amafaa sio tu kuwa raisi wa tanzania hata wa afrika kwa ujumla au umesahau kuwa kiongozi bora hapatikani kwa kabila lake wala pesa zake kama mbowe bali ni uwezo wake?
una ushahidi gani kuwa hawakwenda kumuona?unaweza usiende kumuona mgonjwa lakini msaada unaoutoa kwa ajili yake ukawa mkubwa zaidi,tatizo la sisi huwa tunaona kumsalimia mgonjwa hospitali ni la maana zaidi kuliko kuchangia matibabu yakeKomu na mbowe ni wezi wa ruzuku na wanampiga vita Zito...hv wakati Zito kalazwa Muhimbili,Komu na Mbowe walikwenda kumuona?
Kusema mtu ni std. 7 ni uwezo wa kipuuzi wa kufikiri. That is character assasination. A very poor strategy of debating. Jifunze debate parameters, ZITTO
manchali nchama halal wa NCCR,anaijua NCCR nje ndani,anayoyaongea yanaukwel 100%,coz manchali sio mlopokaji,na anataswira nzuri mbele ya wanajamii,Afu kwanin kila siku awe ZITO tu,