Ngd yangu Mwita wa kweli hawa vijana wana mbinu nyingi, ila kumuondoa Mbatia ni mpango wa siku nyingi ila nadhani unakwama. Upinzani unakutana na vikwazo vingi katika kuimalika!!!!!!!!!Kafulila na Zitto iko kazi mbele yao.
Lakini huyo Mbatia tumesikia muda mrefu akitakiwa na wajumbe wa chama chake aachie ngazi, akitajwa Hashim Rungwe kuongoza huo mkakati, sikuwahi kumsikia Kafulila akihusishwa na huo msukumo.
Au kafulila anacheza mpira nje ya uwanja.
Radio Indian Ocean.
Watu hawana hata uungwana wa kusema huyu mtu ni mgonjwa, hajatoka hospitali. Huruma ya kibinaadamu hawana. Kuna uchawi gani zaidi ya huu? Mwelekeo ule ule >Tanzania Daima>MwanaHalisi yote yanamilikiwa na viongozi waandamizi wa chama changu. Nimechukia sana. Nitawasilisha malalamiko rasmi kwa Katibu Mkuu wa chama ili Wamiliki wa Tanzania Daima (Mhe. Mbowe) na wa MwanaHalisi (Ndugu Komu) waeleze mwenendo wa magazeti wanayomiliki kuhusu mimi. Nimechoka kuzushiwa uwongo na magazeti haya kila kukicha.
PRO-MBOWE mi nitasimamia ukweli..kwani chama ni taasisi na c kikundi cha wa2 fulani wanatoka pande fulani na ambao wanaogopa wa2 wengine.
Watu hawana hata uungwana wa kusema huyu mtu ni mgonjwa, hajatoka hospitali. Huruma ya kibinaadamu hawana. Kuna uchawi gani zaidi ya huu? Mwelekeo ule ule >Tanzania Daima>MwanaHalisi yote yanamilikiwa na viongozi waandamizi wa chama changu. Nimechukia sana. Nitawasilisha malalamiko rasmi kwa Katibu Mkuu wa chama ili Wamiliki wa Tanzania Daima (Mhe. Mbowe) na wa MwanaHalisi (Ndugu Komu) waeleze mwenendo wa magazeti wanayomiliki kuhusu mimi. Nimechoka kuzushiwa uwongo na magazeti haya kila kukicha.
kuna tabia imezuka ya kudhalilisha watanzania ambao hatukwenda shule.jamani ina maana saed kubenea (mkuu wa mwanahalisi) hakumaliza darasa la saba! Hii kama ni kweli na anaandika habari ambazo tunazipigia upatu na kuziamini basi ipo shida. Kumbe ndio maana gazeti linakuwa likiyumba halina msimamo; leo linarukia huku kesho kule! Duh tanzania zaidi ya tunavyoijua.
Bora umesema mwenyewe maana kuna watu upeo wa kufikiri upo karibu sana aidha ni wagumu kuelewa na wepesi kusahauMoja, sina mpango wowote wa kuhama CHADEMA. Kila siku nasema nimekuwa mwanachama wa chama kimoja tu cha siasa maisha yangu yote, nimekuwa mwanachama wa CHADEMA toka nikiwa na umri wa miaka 16 na namwomba Mungu kila siku nife nikiwa ndani ya chama hiki. Najua kuna watu wanapenda sana nitoke CHADEMA kwa maslahi yao ya kisiasa wakiniona mimi ni tishio kwao. Napenda kuwaambia nimetumia nguvu nyingi sana kujenga chama hiki na sitahama. Waache kabisa kunizushia na kunijengea chuki mbele ya umma.
Pili, sihusikikwa lolote lile na yanayoendelea ndani ya NCCR na wala sina interest ya kuyajua. Mbunge wa Kasulu mjini ambaye alikuwa mwanachadema na kushinda Ubunge kwa sababu ya kutumia jina langu huko kwao Kasulu anaropoka (kama kweli kasema maneno hayo) na nitakapotoka Hospitali nitamtaka anithbitishie anayoyasema. Vijana wanapojiingiza kwenye siasa za uwongo kama wazee wao ni hatari sana kwa nchi. Sihitaji kwenda NCCR ili kugombea Urais kwani chama changu ni kikubwa zaidi na kitanipa Urais kwa urahisi kuliko NCCR ambacho ni chama kisicho na rekodi yeyote ya kupigania maslahi ya nchi hata wakati kilipokuwa chama kikuu cha upinzani nchini. Katiba hainiruhusu kugombea Urais mwaka 2015 na hata kama ikibadilishwa na kuniruhusu kugombea kwangu kutategemea sana mwafaka ndani ya chama changu. Anayedhani kwamba nia yangu ya kuwa Rais wa Tanzania ni ya kufa na kupona hamjui Zitto. Sifanyi siasa za kufa na kupona. Ninao uwezo wa kuwa Rais bora maana nina ajenda na ninatoka chama bora. Lakini pia nipo tayari kufanya kazi yeyote ile ambayo chama changu kitanipa.
Zittophobics wanaishi kwa siasa za kumwaza Zitto na wamo kwenye vyama vyote vya siasa hapa nchini. Ninafanya kazi zangu za Ubunge kwa ufanisi na mafanikio makubwa sana, ninafanya kazi zangu za Uenyekiti wa Kamati ya Mashirika ya Umma kwa umakini mkubwa na ninafanya kazi zangu za Uwaziri Kivuli wa fedha katika hali ya kuridhisha sana. Maadui zangu wa kisiasa wanatamani nianguke. Kwa uwezo wa Mungu sitaanguka.
Tatu, Gazeti la Mwanahalisi limekuwa ni gazeti linalonisakama sana kila kukicha lina ajenda yake. Gazeti ambalo limepoteza mvuto wake kwa jamii halinishughulishi. Hata juzi Mzee Samweli Sitta amelishutumu kwa kununuliwa na mafisadi na kutumiwa. Niseme nini zaidi kuhusu gazeti hili linaloongozwa na mtu ambaye hata hajamaliza darasa la saba. Mwanahalisi wanajua kwamba wakiandika habari yenye jina langu mauzo yao yanakua makubwa. Hili ni gazeti mufilisi ambalo kazi yake ni kutumiwa tu.
Nne, WanaJF mnasema hili ni jukwaa ni Great Thinkers. Great thinkers huwa hawadaki habari na kuziamini na kuanza kutoa maoni bila kwanza kupata uhakika wa habari hizo.
Nasikitika kwamba watu wenye ugonjwa wa Zittophobiasis ni wengi sana humu. Ninawashauri kwamba jitahidini muwe objective na muone upande wa pili wa shilingi.
Habari hii ya Mwanahalisi ni habari ya kijinga sana kujaribu tu kunihusisha na vurugu za chama ambacho mimi si mwanachama wake. Kafulila na mimi ni marafiki na ni wabunge wa Kigoma. Lakini Kafulila na mimi hatuongei mambo ya vyama vyetu hata kidogo na yeye anajua kwamba sina interest na NCCR Mageuzi.
WanaJF msicheze ngoma isiyo yenu.
Hii ameitoa wakati akijibu hoja/tuhuma za kuhusu yeye na Kafulila na kuivuruga NCCR kwa malengo yao binafsi..
"Gazeti la Mwanahalisi limekuwa ni gazeti linalonisakama sana kila kukicha lina ajenda yake. Gazeti ambalo limepoteza mvuto wake kwa jamii halinishughulishi. Hata juzi Mzee Samweli Sitta amelishutumu kwa kununuliwa na mafisadi na kutumiwa. Niseme nini zaidi kuhusu gazeti hili linaloongozwa na mtu ambaye hata hajamaliza darasa la saba. Mwanahalisi wanajua kwamba wakiandika habari yenye jina langu mauzo yao yanakua makubwa. Hili ni gazeti mufilisi ambalo kazi yake ni kutumiwa tu."
SOURCE;
JF
kuna tabia imezuka ya kudhalilisha watanzania ambao hatukwenda shule.
Tatizo sio kuambiwa, mtoa mada ametamka akiwa na maana kuwa mtu aliyeishia darasa la saba, hana uwezo au hadhi ya kuandika habari kuhusu yeye na watu wakaisoma...sio dharau hizo?Hivi mtu ukiishia darasa la 3 ukiaambiwa ni kudhalilishwa?
well umeandika sanaInakuwaje mtu mwenye akili zake timamu akaamini habari za kutengenezwa za udaku wa kisiasa unaomilikiwa na kufadhiliwa na mahasimu wa Zitto wakiwemo Kubenea na Mweka Hazina wa Kudumu wa Chadema Anthony Komu ambaye kwake yeye Zitto ni tishio kwa maslahi yake na maslahi ya "wenzake" wanaoamini kuwa Chadema ni chama chao?
Na hili suala la Zitto kuwa na nia ya kuivuruga CHADEMA eti kwa mipango yake ya kuhamia ama kugombea Urais kupitia NCCR linaonyesha dalili kubwa za kutokujiamini ndani ya kundi la wahafidhina wa Chadema. Iweje Zitto huyu mnayemtukana, kumpiga vita na hata kudai kuwa hana nguvu kisiasa suala ama hisia za yeye kuondoka Chadema kuhusishwa na nia ya kuvuruga chama chenu?
Lakini kama wanaDEMOKRASIA inakuwaje mnakuwa na mitazamo hasi ya nia ya mtu (kama ipo) ya kuhama chama kimoja kujiunga na chama kingine atakachoamini kuwa kinaendana na fikira, ndoto ama hata tamaa zake ziwe za kisiasa ama za hatima ya nchi yetu. Hizi si fikira za wanademokrasia, ni fikira za mafashisti wanye nia ya kutumia kauli mbiu za demokrasia kuhalalisha matamanio yao ya kifashisti.
Ninachosoma kutoka katika siasa hizi za kichokoraa zinazoendeshwa na makada na hata viongozi wa Chadema humu ndani ya jukwaa letu na kwengineko dhidi ya Zitto ni ishara za kutojiamini miongoni mwa establishment ya CHADEMA wenye mitazamo na malengo ya kihafidhina. Badala ya kufanya jitihada za kujisafisha na kujipanga upya kuondokana na tuhuma mbalimbali zinazowakabili zinazopelekea chama chao kuvikwa ama kujivika magamba mbalimbali kama ya udini, ukabila, ufisadi nk, .
Kwa ujumla na kwa jinsi nijuavyo mimi Zitto bado hajawahi kuwa na nia ya kuondoka CHADEMA ingawa kuna mengi yanayomvunja moyo kila kukicha. Lakini kama atakuja kuhama CHADEMA na kujiunga na NCCR naamini itakuwa ni suala la kiitikadi zaidi kuliko nafasi yake kisiasa.
NCCR tofauti na ilivyo CHADEMA, ni chama pekee cha upinzani chenye mizizi ya itikadi za KIJAMAA zilizojikita katika nia ya kujenga Tanzania yenye kujali na kuthamini utu. Na naamini mpaka sasa Zitto, Mnyika, Baregu, Kitila Mkumbo bado wanaamini katika itikadi ya UJAMAA ingawa wanalazimika kunyamazia sera, nyendo na matamanio ya kibepari ambao ndio mzizi wa CHADEMA.
Naamini historia ipo wazi kuwaamsha kuwa kwa siasa hizi za chuki na uzandiki, kamwe hamtaweza kupambana na nguvu na akili za Zitto kisiasa ..Lakini pia wakati mwengine mjaribu kuonyesha ubinadamu kidogo hata kama uungwana kwenu mwiko!
Mnachokifanya sasa hakina tofauti na aliyokuwa akiyafanya Mchungaji Mtikila wakati Mwalimu alipokuwa amelazwa hospitalini na hata baada ya kufairiki. Huu sio Utanzania!