Kafulila na Zitto wanaivuruga NCCR - Moses Machali

Status
Not open for further replies.
Naona na wewe inakuuma sana, tunafahamu jinsi gani hila zinavyotawala ndani ya mawazo yenu na ubinafsi wa hali ya juu, leo hiii kijana kama wewe una miaka mitano au kumi unapigania kuwa mwenyekiti wa chama ile hali ukiwezeshwa na kundi kubwa la mafisadi, hii haiwezekani.

unasema wenyeviti wa vyama vya upinzani hawapendi challenge, lakini huku ikionekana anayetoa hizo chalenge akitumwa na mafisadi hilo ni jambo ambalo haliwezekani hata kidogo.

Nadhani kwa Zito jinsi anavyokuwa mamluki ndani ya chama hadi kufikia kumsifia JK inadhihirisha hawezi kuwa mwenyekiti wa chama chochote cha upinzani kwani ikitokea hivyo basi hadi vikao vya CCM atakuwa anaalikwa kama Mrema.

Kama zito anafikiri anakubalika basi aanzishe chama chake na awe mwenyekiti na kupigana kufa na kupona ili awe mwenyekiti na hatimaye kugombea urais, na asijidanganye hata kidogo Zito kafikia pale kwa ajili ya CDM na si kitu kingine kama haamini basi ahamie APPT Maendeleo au UPDP kama atakuwa kama alivyo sasa.

Na Zito anatakiwa kuwashukuru kina Mbowa na Slaa kwa kumlea na kumpa opportunity na si kuwa oppose mara kwa mara kama anvyofanya.

NOTE: Vijana wengi wa Kigoma wana uroho wa Madaraka embu subirini mpewa nafasi na si kupigania uongozi kwa staili ya kufa na kupona.

Swali: Dr Walid kabour yuko wapi?

Duh...The haters cartel are hard at work.You have inadequate knowledge of History, reasoning with you might be an up hill task

Miaka mitano au kumi kupigania uenyekiti? Tunaandika kwa hisia tu,hisia sio sehemu ya jukwaa kama hili hata kama unatumia jina la bandia. It is not a coincidence that you are the only one bothered by the my contribution, the whole thing is very self explanatory.Jamani sio lazima watu wengine muandike JF,facebook na twitter kunawatosha.Itendee JF haki kwa kujenga hoja,heshimu inmates wa JF

Tulifanya makosa sana kupokea mfumo wa vyama vingi bila kutoa darasa la elimu ya uraia na itikadi.Kwa hiyo Ed Miliband kiongozi wa chama cha upinzani Uingereza hawezi kusalimiana na David Cameron? Jacob Zuma wa ANC hasalimiani na Hellen Zille wa chama cha upinzani cha DA huko RSA? Arthur Mutambara hasalimiani na Simba makoni kule Zimbabwe kisa wako vyama tofauti?kufanya hivyo kuta-compromise principles za vyma vyao hivyo kuuwa upinzani? We are not living in bubbles buddy!

Refrain from making false statements when you have no proof and be man enough to admit when you are wrong.
 
Mnaomtetea Zitto kutumika mnajisumbua bure, watu wote makini wanajua jinsi Zitto anavyotumika. Hapa hakuna suala la usalama wa taifa kuwagombanisha mwenyekiti Mbowe na Zitto, wala nini. Hapa kuna umalaya wa Zitto.

Zitto amekihujumu sana Chadema, kuliko maelezo. Amesababisha Mizengo Pinda kupita bila kupigwa, baada ya yeye kuandika barua kwa msimamizi (mkurugenzi wa halmashauri ya Mpanda), kwamba Chadema haijapitisha mgombea wa ubunge katika jimbo hilo, wakati viongozi na wanachama wa chama hicho waliweka mgombea. Sasa kama huo siyo usaliti ni nini?

Hapa kuna suala la kugombanishwa na usalama wa taifa, au kuna ujinga na kujipendekeza kwa Zitto? Kama hili, Zitto anaona anasingiziwa, aingie humu ndani akane kuandika hiyo barua.
Nami nitaweka hadharani ushahidi.

Inaonyesha unaongozwa na chuki dhidi ya huyu bwana, unaweza kuniambia mgombea(Mbunge) wa CDM aliyezunguka majimbo mengi kuwanadi wagombea wenzake kwenye uchaguzi uliopita zaidi ya Zitto. Leo bila aibu unasema kua hakufanya chochote wakati mwaka jana alitumia muda mwingi kukinadi chama! Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Hivi unapomshambulia mgonjwa akiwa amelazwa hospitali una tofauti gani na anaekunywa uji wa mgonjwa.
 
Amezunguka katika majimbo yapi? Zitto alikwenda kwenye majimbo machache sana, tena yale ambayo yanawagombea anaona watamtii yeye. Kwa mfano, amekwenda Kahama Mjini, lakini hakufika Maswa kwa Kasulumbay. Hakufika Meatu. Huyu mnafiki. Amemuacha Pinda amepita bila kupingwa.

Na pale Singida Mjini alihongwa na Dewji akataka apite bila kupingwa. Bahati njema, Tundu Lissu akasimama kidete. Ndiyo kisa cha mgogoro kati yake na Josephat Isango aliyegombea kupitia Chadema. Jibuni hoja za undumikuwili wa Zitto, badala ya kujadili watu.
 
hawamtaki Mbowe na Slaa kwa sababu ya misimamo yao makini.mbowe amekuwa kikwazo kikubwa sana kwa mamluki kuimaliza CDM. hawa vijana hawataki democrasia bali wanataka vyeo iwe kupitia CDM au NCCR na hata CCM.

Hivi Mbowe huyu aliyefanya makubaliano na wanamtandao mwaka 2005 ili kuitumia Chadema kuwatishia CCM wabadili taratibu na kumbeba mgombea wao....

Mbowe huyuhuyu ambaye kwa makubaliano maalum alikubali gazeti lake la TanzaniaDaima kutumika na kina Lowassa na Rostam kufanyia kampeni za kumjenga mgombea wao na kuwabomoa na kuwatukana wagombea wengine

Mbowe huyuhuyu aliyefikia kuruhusu waajiriwa wake wa TanzaniaDaima kulipwa mishahara na marupurupu mengine ikiwemo kwenda kusomeshwa nje na kina Roastam wa CCM.....

Mbowe huyu ambaye tangia miaka hiyo hadi leo ameingia makubaliano maalum ya kuhakikisha kuwa Magazeti yake yanatumika ama kwa kusifia, kutetea ama kukandamiza habari zinazohusu uchafu wa wanaoitwa MAFISADI wa CCM.....na pia kukubaliana kutoshambuliana nao kupitia majukwaa na vyombo vyao vya habari...

Mbowe huyuhuyu ambaye mwaka 2015 alilazimisha kuchelewesha uteuzi wa mgombea wa Chadema ili kusubiria kuokoteza mabaki ya CCM endapo Samwel Sitta atatimuliwa ama kujitoa CCm ili agombee Chadema...

Mbowe huyuhuyu ambaye amekuwa akipokea misaada ya kuchangia Chadema kutoka kwa vinara wa sura ya UFISADI CCM na kudai kuwa ni fedha zake hivyo akiwakopesha Chadema.....

Mbowe huyuhuyu ambaye siku hizi amekuwa akimtumia Kada wa CCM Mzee Sabodo kupokea michango ya haohao mnaowaita MAFISADI wa CCM na hasa watanzania wenye asili ya Uhindi......

Leo hii ndio mnataka kudanganya watu kuwa Mbowe huyu amekuwa kikwazo kikubwa sana kwa mamluki kuimaliza CDM? Kweli omba Mungu akunyime mali lakini sio akili........

CLARIFICATION: Naamini kuwa uongozi wa Mbowe uliweza kusaidia sana kukuwa kwa Chadema hadi pale wale aliokuwa akiwaamini kuwa wanasaidia ukuaji huo walipoanza kuhoji uadilifu wake na kutishia nafasi yake katika chama na ndoto ya kugombea Urasi ambayo ukweli hadi mwaka 2005 hakuwa nayo lakini makundi yaliyovutiwa na Helikopta yakamdanganya kuwa anaweza....

Naamini kuwa hadi hivi sasa Mbowe amekuwa nguzo ya busara za kisiasa (zenye malengo ya kujijenga kama Kiongozi Mkomavu anayeweza kuwa Rais we nchi kuliko uhalisia wake) ndani ya Chadema ambayo inaelekea kutekwa na wanasiasa waliokosa busara za kiuongozi na kupenda kuamini katika siasa za kichokoraa ambazo ukweli zimeonyesha mafanikio kwa maslahi yao binafsi na chama hasa ukizingatia na hali ya kukosa matumaini ndani ya CCM miongoni mwa watanzania wengi....Ni wazi hata kule Arusha Mbowe alikuwa akijaribu kuinspire busara za kumtoa Lema ili kupre-empty nia halisi ya Lema ambayo ni kuzusha Popular Prostest ambaye ingemjenga yeye binafsi zaidi kuliko chama na kuendeleza jitihada zake na wanasiasa wa aina yake ndani na nje ya Chadema katika kuigawanya na hata kuvunja msingi wa Umoja na Amani wa Taifa.....

Lakini kamwe siwezi kumuamini Mbowe kama ana uwezo, uaminifu na uadilifu wa kuwa Rais wa nchi kwa maslahi ya Watanzania walio wengi...Na wala siamini kuwa yeye ndiyo mzalendo zaidi wa Chadema kuliko Zitto na wengine...Na zaidi yeye ni mabaki ya waumini wa siasa za kidiketa ambao wanapenda kutrumia kauili mbiu za demokrasia pale tu ambapo kuna maslahi yao ya kuyalinda ama kuyatekeleza.

Why namshambulia yeye? Kwa sababu yeye ndiyo sura na kinara wa siasa za chuki na ujanjaujanja dhidi ya wote anaowaona kuwa wanatishia nafasi yake akiwemo Dr Slaa na Zitto kwa pamoja.....kama ambavyo Lowassa alivyo sura ama kinara wa maslahi ya wanasiasa MAFISADI na hovyohovyo pamoja na mabaki ya fikira za kidikteta CCM
 
Zittophobia na siasa za kichokoraa za wakombozi wetu…
Kuna wakati unaposoma akili za watu katika jukwaa la Jamiiforums na hasa wale wanaojitambulisha kama makada wa Chadema unaweza ama kukata tamaa na mabadiliko ya kweli katika nchi yetu ama hata kuamua kujilipua na kujiunga na CCM.

Inashangaza kuona kuna watu wanaojifaragua kama "great minds" wanakuwa rahisi kuamini sumu za kisiasa ambazo ukweli zinalenga kulinda maslahi ya watu kwa kuwaharibia sifa wengine na hata kubomoa misingi mikuu ya utanzania ambayo ni utu, umoja na amani.

Inakuwaje mtu mwenye akili zake timamu akaamini habari za kutengenezwa za udaku wa kisiasa unaomilikiwa na kufadhiliwa na mahasimu wa kisiasa na kibinafsi wa Zitto wakiwemo Kubenea na Mweka Hazina wa Kudumu wa Chadema Anthony Komu ambaye kwake yeye Zitto ni tishio kwa maslahi yake na maslahi ya "wenzake" wanaoamini kuwa Chadema ni chama chao?

Inakuwaje wanaojiita "great minds" kuwa tayari kuamini kuwa Zitto ana mpango wa kugombea urais mwaka 2015 wakati wote tunajuwa kuwa wakati huo atakuwa hajatimiza umri wa miaka 45.

Inasikitisha zaidi kuona kuwa kuna baadhi ya wapenzi wa Chadema wanamshutumu Zitto kwa madai ya kuonyesha dalili za kutaka kugombea Urais eti huku akijua kuwa chama chake tayari kina mgombea. Yaani Chama cha DEMOKRASIA na maendeleo tayari kina mgombea wa Urasi wa mwaka 2015 wakati ndio kwanza tupo mwaka 2011? Halafu wana jeuri ya kuwalaumu wengine kwa ukandamizaji wa haki za kidemokrasia.

Na hili suala la Zitto kuwa na nia ya kuivuruga CHADEMA eti kwa mipango yake ya kuhamia ama kugombea Urais kupitia NCCR linaonyesha dalili kubwa za kutokujiamini ndani ya kundi la wahafidhina wa Chadema. Iweje Zitto huyu mnayemtukana, kumpiga vita na hata kudai kuwa hana nguvu kisiasa ama hisia za yeye kuondoka Chadema kuhusishwa na nia ya kuvuruga chama hicho? Kama kweli yeye ni kama wanavyotaka watu waamini na kuwa hana umaarufu tena kama hapo awali kuondoka kwake si ndio kulitakiwa kuonekana kama baraka kwa Chadema?

Lakini kama wanaDEMOKRASIA inakuwaje mnakuwa na mitazamo hasi ya nia ya mtu (kama ipo) ya kuhama chama kimoja kujiunga na chama kingine atakachoamini kuwa kinaendana na fikira, ndoto ama hata tamaa zake ziwe za kisiasa ama za hatima ya nchi yetu. Hizi si fikira za wanademokrasia, ni fikira za mafashisti wanye nia ya kutumia kauli mbiu za demokrasia kuhalalisha matamanio yao ya kifashisti.

Ninachosoma kutoka katika siasa hizi za kichokoraa zinazoendeshwa na makada na hata viongozi wa Chadema humu ndani ya jukwaa letu na kwengineko dhidi ya Zitto ni ishara za kutojiamini miongoni mwa establishment ya CHADEMA wenye mitazamo na malengo ya kihafidhina. Badala ya kufanya jitihada za kujisafisha na kujipanga upya kuondokana na tuhuma mbalimbali zinazowakabili zinazopelekea chama chao kuvikwa ama kujivika magamba mbalimbali kama ya udini, ukabila, ufisadi nk, wako busy kumsulubu mtu ambaye anaonekana kuwa kama kioo cha Chadema tofauti ambayo watanzania wangependa kuiona inakuwa na sio Chadema waliyoikumbatia wao. Chadema yenye kufikiri na kutenda kidemokrasia. Chadema yenye kuongoza katika kuleta suluhu ya matatizo ya watanzania na nchi kwa ujumla na sio kuongeza, kupalilia na hata kufurahia kuongezeka kwa matatizo hayo.

Kwa ujumla na kwa jinsi nijuavyo mimi Zitto bado hajawahi kuwa na nia ya kuondoka CHADEMA ingawa kuna mengi yanayomvunja moyo kila kukicha. Lakini kama atakuja kuhama CHADEMA na kujiunga na NCCR naamini itakuwa ni suala la kiitikadi zaidi kuliko nafasi yake kisiasa.

NCCR tofauti na ilivyo CHADEMA, ni chama pekee cha upinzani chenye mizizi ya itikadi za KIJAMAA zilizojikita katika nia ya kujenga Tanzania yenye kujali na kuthamini utu. Na naamini mpaka sasa Zitto, Mnyika, Baregu, Kitila Mkumbo bado wanaamini katika itikadi ya UJAMAA ingawa wanalazimika kunyamazia sera, nyendo na matamanio ya kibepari ambao ndio mzizi wa CHADEMA na unaolindwa na kuendelezwa na mahafidhina wa chama hicho ambao hawaishi kufanya kila wawezalo kutumia frustrations za watanzania waliowengi kwa ajili ya maslahi yao binafsi na chama chao nay a watanzania wote kama wanavyolaghai.

Na ni wazi kuwa ili NCCR ifufuke na kuteka hisia za watanzania kuwa wanaweza kuwa chama mbadala wanachotamani kukiona na kukiunga mkono kwa dhati, kuna ulazima wa kubadili uongozi uliokuwepo na kusimika uongozi mpya utakaoweza kukipa uhai. Vilevile ni mabadiliko ya uongozi sasa ndiyo yatakayoweza kutoa nafasi kwa WAJAMAA MASALIA wanaolazimika ama kulazimishwa kubaki CHADEMA na CCM kupata uwanda wa kisiasa kujaribu kujenga Tanzania waitakayo na kurudisha siasa za kiitikadi badala kuendelea kutumika kuendeleza siasa za tuhuma, chuki, uzandiki, personalities na ujanjaujanja mwengine.

Napenda kuwaasa wale waliodedicate maisha na akili zao katika kummaliza Zitto iwe kisiasa ama kimaisha watambue kuwa adui wao sio Zitto bali yale anayoamini kuwa yanaopaswa kubadilishwa na kuepukwa na chama chake. Nguvu mnazotumia hapa kujaribu kumbomoa Zitto ni vizuri mkazitumia kujenga chama chenu kiweze kuaminika na watanzania na sio kuendelea kutegemea mtaji wa sumu ya chuki dhidi ya CCM na serikali yake tu.

Naamini historia ipo wazi kuwaamsha kuwa kwa siasa hizi za chuki na uzandiki, kamwe hamtaweza kupambana na nguvu na akili za Zitto kisiasa. Lakini pia wakati mwengine mjaribu kuonyesha ubinadamu kidogo hata kama uungwana kwenu mwiko.

Mnachokifanya sasa hakina tofauti na aliyokuwa akiyafanya Mchungaji Mtikila wakati Mwalimu alipokuwa amelazwa hospitalini na hata baada ya kufairiki. Huu sio Utanzania!

Kuna wale wanaojidanganya kuwa udikteta wa Mbowe ni sawa kwani una nia ya kuzuia Chadema isitekwe na CCM.

Hivi Mbowe huyu aliyefanya makubaliano na wanamtandao mwaka 2005 ili kuitumia Chadema kuwatishia CCM wabadili taratibu na kumbeba mgombea wao.

Mbowe huyuhuyu ambaye kwa makubaliano maalum alikubali gazeti lake la TanzaniaDaima kutumika na kina Lowassa na Rostam kufanyia kampeni za kumjenga mgombea wao na kuwabomoa na kuwatukana wagombea wengine.

Mbowe huyuhuyu aliyefikia kuruhusu waajiriwa wake wa TanzaniaDaima kulipwa mishahara na marupurupu mengine ikiwemo kwenda kusomeshwa nje na kina Roastam wa CCM.

Mbowe huyu ambaye tangia miaka hiyo hadi leo ameingia makubaliano maalum ya kuhakikisha kuwa Magazeti yake yanatumika ama kwa kusifia, kutetea ama kukandamiza habari zinazohusu uchafu wa wanaoitwa MAFISADI wa CCM na pia kukubaliana kutoshambuliana nao kupitia majukwaa na vyombo vyao vya habari.

Mbowe huyuhuyu ambaye mwaka 2015 alilazimisha kuchelewesha uteuzi wa mgombea wa Chadema ili kusubiria kuokoteza mabaki ya CCM endapo Samwel Sitta atatimuliwa ama kujitoa CCm ili agombee Chadema.

Mbowe huyuhuyu ambaye amekuwa akipokea misaada ya kuchangia Chadema kutoka kwa vinara wa sura ya UFISADI CCM na kudai kuwa ni fedha zake hivyo akiwakopesha Chadema.

Mbowe huyuhuyu ambaye siku hizi amekuwa akimtumia Kada wa CCM Mzee Sabodo kupokea michango ya haohao mnaowaita MAFISADI wa CCM na hasa watanzania wenye asili ya Uhindi.

Leo hii ndio mnataka kudanganya watu kuwa Mbowe huyu amekuwa kikwazo kikubwa sana kwa mamluki kuimaliza CDM? Kweli omba Mungu akunyime mali lakini sio akili.

CLARIFICATION: Nakubali kuwa uongozi wa Mbowe uliweza kusaidia sana kukuwa kwa Chadema hadi pale wale aliokuwa akiwaamini kuwa wanasaidia ukuaji huo walipoanza kuhoji uadilifu wake na kutishia nafasi yake katika chama na ndoto ya kugombea Urasi ambayo ukweli hadi mwaka 2005 hakuwa nayo lakini makundi yaliyovutiwa na Helikopta yakamdanganya kuwa anaweza.

Naamini kuwa hadi hivi sasa Mbowe amekuwa nguzo ya busara za kisiasa (zenye malengo ya kujijenga kama Kiongozi Mkomavu anayeweza kuwa Rais we nchi kuliko uhalisia wake) ndani ya Chadema ambayo inaelekea kutekwa na wanasiasa waliokosa busara za kiuongozi na kupenda kuamini katika siasa za kichokoraa ambazo ukweli zimeonyesha mafanikio kwa maslahi yao binafsi na chama hasa ukizingatia na hali ya kukosa matumaini ndani ya CCM miongoni mwa watanzania wengi. Ni wazi hata kule Arusha Mbowe alikuwa akijaribu kuinspire busara za kumtoa Lema ili kupre-empty nia halisi ya Lema ambayo ni kuzusha Popular Protest ambaye ingemjenga yeye (LEMA) binafsi zaidi kuliko chama na kuendeleza jitihada zake na wanasiasa wa aina yake ndani na nje ya Chadema katika kuigawanya na hata kuvunja msingi wa Umoja na Amani wa Taifa.

Lakini kamwe siwezi kumuamini Mbowe kama ana uwezo, uaminifu na uadilifu wa kuwa Rais wa nchi kwa maslahi ya Watanzania walio wengi...Na wala siamini kuwa yeye ndiyo mzalendo zaidi wa Chadema kuliko Zitto na wengine...Na zaidi yeye ni mabaki ya waumini wa siasa za kidikteta ambao wanapenda kutrumia kauli mbiu za demokrasia pale tu ambapo kuna maslahi yao ya kuyalinda ama kuyatekeleza lakini sio kama muumini wa kweli wa UANADEMOKRASIA.

Why namshambulia Mbowe? Kwa sababu naamini kuwa yeye ndiyo sura na kinara wa siasa za chuki na ujanjaujanja ndani ya Chadema ambayo huelekezwa dhidi ya wote anaowaona kuwa wanatishia nafasi yake kama ilivyokuwa kwa Walid Kaborou na Marehemu Chacha wangwe na sasa wakiwemo Dr Slaa na Zitto kwa pamoja.....kama ambavyo Lowassa alivyo sura ama kinara wa maslahi ya wanasiasa MAFISADI na hovyohovyo pamoja na mabaki ya fikira za kidikteta CCM.
 
Amezunguka katika majimbo yapi? Zitto alikwenda kwenye majimbo machache sana, tena yale ambayo yanawagombea anaona watamtii yeye. Kwa mfano, amekwenda Kahama Mjini, lakini hakufika Maswa kwa Kasulumbay. Hakufika Meatu. Huyu mnafiki. Amemuacha Pinda amepita bila kupingwa.

Na pale Singida Mjini alihongwa na Dewji akataka apite bila kupingwa. Bahati njema, Tundu Lissu akasimama kidete. Ndiyo kisa cha mgogoro kati yake na Josephat Isango aliyegombea kupitia Chadema. Jibuni hoja za undumikuwili wa Zitto, badala ya kujadili watu.

Nlitegemea unginieleza mbunge(mgombea) aliyezunguka majimbo mengi kuliko Zitto ukaishia kuendeleza chuki, hivi ulikuwa wapi wakati wa kampeni mwaka jana mpaka usijue majimbo aliyoenda. Kwa CDM mbar na Dr Slaa hakuna aliyetoa msaada kwenye majimbo ya watu wengine kama huyu bwana(huo ndo ukweli hata kama unauma). Kanusheni mazuri aliyoyafanya Zitto kwa chama chake msiishie kuongea maneno ya kinafiki.
 
Haya tuambia majimbo mengi, mangapi? Je, huko alikozunguuka alikwenda kunadi wagombea, au alikwenda kuhujumu chama? Katika hayo mengi, ni pamoja na Muhambwe amabako A. Ntagazwa alishindwa? Usitetee kwa akili za Masabuli.i
 
ZITTO alikuwa na kazi ya kuhujumu chama tu. Ndivyo alivyofanya kule kwa Pinda, Singida Mjini, Musoma Vijijini na kwingineko. Pale Musoma Vijijini, Zitto kwa urafiki wake na Nimrod Nkono alikubali kumuondoa mgombea wa chama chake baada ya kuhongwa Sh. 60 milioni na yule kijana kumpa paundi 1000 kwa ahadi kwamba nyingine atazikuta Dar es Salaam.

Yule kijana alikamatwa na vijana wa Chadema pale makao makuu na kueleza kila kitu juu ya jambo hili. Je, hapa nani atakuwa anamchimba bwana mdogo huyu? ZITOOOOO adui yako ni tamaa yako ya kutaka kuishi maisha ya anasa na kupenda mabibi.

Tunamjua vema Zitto, hana maadili. Kama anabisha katika hili, ajitokeze hapa tuweke ushahidi.
 
Sema SPANNER... Mwaga unyagu hapa ili umuanike huyu kibaraka wa Rostam, Zoka na Kikwete, ZITTO, ZUBERI KABWE.
 
HUYU ZITTO kaba kuja humu na kujifanya mjuaji aeleze kwanza aliko JACK, yule mwanadada wa UDSM. Tatizo la ZITTO anaongozwa na mama yake, Shida.
 
Zittophobia na siasa za kichokoraa za wakombozi wetu…
Kuna wakati unaposoma akili za watu katika jukwaa la Jamiiforums na hasa wale wanaojitambulisha kama makada wa Chadema unaweza ama kukata tamaa na mabadiliko ya kweli katika nchi yetu ama hata kuamua kujilipua na kujiunga na CCM.

Inashangaza kuona kuna watu wanaojifaragua kama "great minds" wanakuwa rahisi kuamini sumu za kisiasa ambazo ukweli zinalenga kulinda maslahi ya watu kwa kuwaharibia sifa wengine na hata kubomoa misingi mikuu ya utanzania ambayo ni utu, umoja na amani.

Inakuwaje mtu mwenye akili zake timamu akaamini habari za kutengenezwa za udaku wa kisiasa unaomilikiwa na kufadhiliwa na mahasimu wa kisiasa na kibinafsi wa Zitto wakiwemo Kubenea na Mweka Hazina wa Kudumu wa Chadema Anthony Komu ambaye kwake yeye Zitto ni tishio kwa maslahi yake na maslahi ya "wenzake" wanaoamini kuwa Chadema ni chama chao?

Inakuwaje wanaojiita "great minds" kuwa tayari kuamini kuwa Zitto ana mpango wa kugombea urais mwaka 2015 wakati wote tunajuwa kuwa wakati huo atakuwa hajatimiza umri wa miaka 45.

Inasikitisha zaidi kuona kuwa kuna baadhi ya wapenzi wa Chadema wanamshutumu Zitto kwa madai ya kuonyesha dalili za kutaka kugombea Urais eti huku akijua kuwa chama chake tayari kina mgombea. Yaani Chama cha DEMOKRASIA na maendeleo tayari kina mgombea wa Urasi wa mwaka 2015 wakati ndio kwanza tupo mwaka 2011? Halafu wana jeuri ya kuwalaumu wengine kwa ukandamizaji wa haki za kidemokrasia.

Na hili suala la Zitto kuwa na nia ya kuivuruga CHADEMA eti kwa mipango yake ya kuhamia ama kugombea Urais kupitia NCCR linaonyesha dalili kubwa za kutokujiamini ndani ya kundi la wahafidhina wa Chadema. Iweje Zitto huyu mnayemtukana, kumpiga vita na hata kudai kuwa hana nguvu kisiasa ama hisia za yeye kuondoka Chadema kuhusishwa na nia ya kuvuruga chama hicho? Kama kweli yeye ni kama wanavyotaka watu waamini na kuwa hana umaarufu tena kama hapo awali kuondoka kwake si ndio kulitakiwa kuonekana kama baraka kwa Chadema?

Lakini kama wanaDEMOKRASIA inakuwaje mnakuwa na mitazamo hasi ya nia ya mtu (kama ipo) ya kuhama chama kimoja kujiunga na chama kingine atakachoamini kuwa kinaendana na fikira, ndoto ama hata tamaa zake ziwe za kisiasa ama za hatima ya nchi yetu. Hizi si fikira za wanademokrasia, ni fikira za mafashisti wanye nia ya kutumia kauli mbiu za demokrasia kuhalalisha matamanio yao ya kifashisti.

Ninachosoma kutoka katika siasa hizi za kichokoraa zinazoendeshwa na makada na hata viongozi wa Chadema humu ndani ya jukwaa letu na kwengineko dhidi ya Zitto ni ishara za kutojiamini miongoni mwa establishment ya CHADEMA wenye mitazamo na malengo ya kihafidhina. Badala ya kufanya jitihada za kujisafisha na kujipanga upya kuondokana na tuhuma mbalimbali zinazowakabili zinazopelekea chama chao kuvikwa ama kujivika magamba mbalimbali kama ya udini, ukabila, ufisadi nk, wako busy kumsulubu mtu ambaye anaonekana kuwa kama kioo cha Chadema tofauti ambayo watanzania wangependa kuiona inakuwa na sio Chadema waliyoikumbatia wao. Chadema yenye kufikiri na kutenda kidemokrasia. Chadema yenye kuongoza katika kuleta suluhu ya matatizo ya watanzania na nchi kwa ujumla na sio kuongeza, kupalilia na hata kufurahia kuongezeka kwa matatizo hayo.

Kwa ujumla na kwa jinsi nijuavyo mimi Zitto bado hajawahi kuwa na nia ya kuondoka CHADEMA ingawa kuna mengi yanayomvunja moyo kila kukicha. Lakini kama atakuja kuhama CHADEMA na kujiunga na NCCR naamini itakuwa ni suala la kiitikadi zaidi kuliko nafasi yake kisiasa.

NCCR tofauti na ilivyo CHADEMA, ni chama pekee cha upinzani chenye mizizi ya itikadi za KIJAMAA zilizojikita katika nia ya kujenga Tanzania yenye kujali na kuthamini utu. Na naamini mpaka sasa Zitto, Mnyika, Baregu, Kitila Mkumbo bado wanaamini katika itikadi ya UJAMAA ingawa wanalazimika kunyamazia sera, nyendo na matamanio ya kibepari ambao ndio mzizi wa CHADEMA na unaolindwa na kuendelezwa na mahafidhina wa chama hicho ambao hawaishi kufanya kila wawezalo kutumia frustrations za watanzania waliowengi kwa ajili ya maslahi yao binafsi na chama chao nay a watanzania wote kama wanavyolaghai.

Na ni wazi kuwa ili NCCR ifufuke na kuteka hisia za watanzania kuwa wanaweza kuwa chama mbadala wanachotamani kukiona na kukiunga mkono kwa dhati, kuna ulazima wa kubadili uongozi uliokuwepo na kusimika uongozi mpya utakaoweza kukipa uhai. Vilevile ni mabadiliko ya uongozi sasa ndiyo yatakayoweza kutoa nafasi kwa WAJAMAA MASALIA wanaolazimika ama kulazimishwa kubaki CHADEMA na CCM kupata uwanda wa kisiasa kujaribu kujenga Tanzania waitakayo na kurudisha siasa za kiitikadi badala kuendelea kutumika kuendeleza siasa za tuhuma, chuki, uzandiki, personalities na ujanjaujanja mwengine.

Napenda kuwaasa wale waliodedicate maisha na akili zao katika kummaliza Zitto iwe kisiasa ama kimaisha watambue kuwa adui wao sio Zitto bali yale anayoamini kuwa yanaopaswa kubadilishwa na kuepukwa na chama chake. Nguvu mnazotumia hapa kujaribu kumbomoa Zitto ni vizuri mkazitumia kujenga chama chenu kiweze kuaminika na watanzania na sio kuendelea kutegemea mtaji wa sumu ya chuki dhidi ya CCM na serikali yake tu.

Naamini historia ipo wazi kuwaamsha kuwa kwa siasa hizi za chuki na uzandiki, kamwe hamtaweza kupambana na nguvu na akili za Zitto kisiasa. Lakini pia wakati mwengine mjaribu kuonyesha ubinadamu kidogo hata kama uungwana kwenu mwiko.

Mnachokifanya sasa hakina tofauti na aliyokuwa akiyafanya Mchungaji Mtikila wakati Mwalimu alipokuwa amelazwa hospitalini na hata baada ya kufairiki. Huu sio Utanzania!

Kuna wale wanaojidanganya kuwa udikteta wa Mbowe ni sawa kwani una nia ya kuzuia Chadema isitekwe na CCM.

Hivi Mbowe huyu aliyefanya makubaliano na wanamtandao mwaka 2005 ili kuitumia Chadema kuwatishia CCM wabadili taratibu na kumbeba mgombea wao.

Mbowe huyuhuyu ambaye kwa makubaliano maalum alikubali gazeti lake la TanzaniaDaima kutumika na kina Lowassa na Rostam kufanyia kampeni za kumjenga mgombea wao na kuwabomoa na kuwatukana wagombea wengine.

Mbowe huyuhuyu aliyefikia kuruhusu waajiriwa wake wa TanzaniaDaima kulipwa mishahara na marupurupu mengine ikiwemo kwenda kusomeshwa nje na kina Roastam wa CCM.

Mbowe huyu ambaye tangia miaka hiyo hadi leo ameingia makubaliano maalum ya kuhakikisha kuwa Magazeti yake yanatumika ama kwa kusifia, kutetea ama kukandamiza habari zinazohusu uchafu wa wanaoitwa MAFISADI wa CCM na pia kukubaliana kutoshambuliana nao kupitia majukwaa na vyombo vyao vya habari.

Mbowe huyuhuyu ambaye mwaka 2015 alilazimisha kuchelewesha uteuzi wa mgombea wa Chadema ili kusubiria kuokoteza mabaki ya CCM endapo Samwel Sitta atatimuliwa ama kujitoa CCm ili agombee Chadema.

Mbowe huyuhuyu ambaye amekuwa akipokea misaada ya kuchangia Chadema kutoka kwa vinara wa sura ya UFISADI CCM na kudai kuwa ni fedha zake hivyo akiwakopesha Chadema.

Mbowe huyuhuyu ambaye siku hizi amekuwa akimtumia Kada wa CCM Mzee Sabodo kupokea michango ya haohao mnaowaita MAFISADI wa CCM na hasa watanzania wenye asili ya Uhindi.

Leo hii ndio mnataka kudanganya watu kuwa Mbowe huyu amekuwa kikwazo kikubwa sana kwa mamluki kuimaliza CDM? Kweli omba Mungu akunyime mali lakini sio akili.

CLARIFICATION: Nakubali kuwa uongozi wa Mbowe uliweza kusaidia sana kukuwa kwa Chadema hadi pale wale aliokuwa akiwaamini kuwa wanasaidia ukuaji huo walipoanza kuhoji uadilifu wake na kutishia nafasi yake katika chama na ndoto ya kugombea Urasi ambayo ukweli hadi mwaka 2005 hakuwa nayo lakini makundi yaliyovutiwa na Helikopta yakamdanganya kuwa anaweza.

Naamini kuwa hadi hivi sasa Mbowe amekuwa nguzo ya busara za kisiasa (zenye malengo ya kujijenga kama Kiongozi Mkomavu anayeweza kuwa Rais we nchi kuliko uhalisia wake) ndani ya Chadema ambayo inaelekea kutekwa na wanasiasa waliokosa busara za kiuongozi na kupenda kuamini katika siasa za kichokoraa ambazo ukweli zimeonyesha mafanikio kwa maslahi yao binafsi na chama hasa ukizingatia na hali ya kukosa matumaini ndani ya CCM miongoni mwa watanzania wengi. Ni wazi hata kule Arusha Mbowe alikuwa akijaribu kuinspire busara za kumtoa Lema ili kupre-empty nia halisi ya Lema ambayo ni kuzusha Popular Protest ambaye ingemjenga yeye (LEMA) binafsi zaidi kuliko chama na kuendeleza jitihada zake na wanasiasa wa aina yake ndani na nje ya Chadema katika kuigawanya na hata kuvunja msingi wa Umoja na Amani wa Taifa.

Lakini kamwe siwezi kumuamini Mbowe kama ana uwezo, uaminifu na uadilifu wa kuwa Rais wa nchi kwa maslahi ya Watanzania walio wengi...Na wala siamini kuwa yeye ndiyo mzalendo zaidi wa Chadema kuliko Zitto na wengine...Na zaidi yeye ni mabaki ya waumini wa siasa za kidikteta ambao wanapenda kutrumia kauli mbiu za demokrasia pale tu ambapo kuna maslahi yao ya kuyalinda ama kuyatekeleza lakini sio kama muumini wa kweli wa UANADEMOKRASIA.

Why namshambulia Mbowe? Kwa sababu naamini kuwa yeye ndiyo sura na kinara wa siasa za chuki na ujanjaujanja ndani ya Chadema ambayo huelekezwa dhidi ya wote anaowaona kuwa wanatishia nafasi yake kama ilivyokuwa kwa Walid Kaborou na Marehemu Chacha wangwe na sasa wakiwemo Dr Slaa na Zitto kwa pamoja.....kama ambavyo Lowassa alivyo sura ama kinara wa maslahi ya wanasiasa MAFISADI na hovyohovyo pamoja na mabaki ya fikira za kidikteta CCM.
Omar Ilyas, angalia hoja zako kuhusu Chadema, kuna points zako zinaonyesha unayajua mambo ya ndani kabisa yale ya chumbani kwa Chadema.
Sasa unapoandika na kuyataja waziwazi kwa lengo la kusimama na rafiki yako kwa kumtetea kwa nguvu zako zote, unaweza kujikuta, badala ya kumtetea, ndio kwanza unamuangamiza.

Badhi ya mashabiki na manazi wa Chadema humu jukwaani, wanamtindo sio tuu wa kumshabikia mtu, bali wengine wanafikia hadi kuwaabudu viongozi wao kama miungu watu, sasa yote uliyoyasema kuhusu kamanda mkuu wa Chadema, utaonekana sio msimamo wako tuu, bali hivyo ndivyo wewe na rafiki yako mnavyomuona kamanda huyo. Hata kama mtazamo huo ni wako binafsi, unaweza kutafsiriwa kuwa ndio wenu, hivyo kuishia kumponza rafiki badala ya kumtetea!.

Pasco.
 
Inaonyesha unaongozwa na chuki dhidi ya huyu bwana, unaweza kuniambia mgombea(Mbunge) wa CDM aliyezunguka majimbo mengi kuwanadi wagombea wenzake kwenye uchaguzi uliopita zaidi ya Zitto. Leo bila aibu unasema kua hakufanya chochote wakati mwaka jana alitumia muda mwingi kukinadi chama! Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Hivi unapomshambulia mgonjwa akiwa amelazwa hospitali una tofauti gani na anaekunywa uji wa mgonjwa.
...........ugonjwa haufuti kilichofanyika kabla!
 
OmarIlyas,
Wow! nimekusoma na hakika unatisha lakini pale tu ulipoandika haya sasa ndio naipata picha halisi..Umeandika:-

"Kwa ujumla na kwa jinsi nijuavyo mimi Zitto bado hajawahi kuwa na nia ya kuondoka CHADEMA ingawa kuna mengi yanayomvunja moyo kila kukicha. Lakini kama atakuja kuhama CHADEMA na kujiunga na NCCR naamini itakuwa ni suala la kiitikadi zaidi kuliko nafasi yake kisiasa.

NCCR tofauti na ilivyo CHADEMA, ni chama pekee cha upinzani chenye mizizi ya itikadi za KIJAMAA zilizojikita katika nia ya kujenga Tanzania yenye kujali na kuthamini utu. Na naamini mpaka sasa Zitto, Mnyika, Baregu, Kitila Mkumbo bado wanaamini katika itikadi ya UJAMAA ingawa wanalazimika kunyamazia sera, nyendo na matamanio ya kibepari ambao ndio mzizi wa CHADEMA na unaolindwa na kuendelezwa na mahafidhina wa chama hicho ambao hawaishi kufanya kila wawezalo kutumia frustrations za watanzania waliowengi kwa ajili ya maslahi yao binafsi na chama chao nay a watanzania wote kama wanavyolaghai.

Na ni wazi kuwa ili NCCR ifufuke na kuteka hisia za watanzania kuwa wanaweza kuwa chama mbadala wanachotamani kukiona na kukiunga mkono kwa dhati, kuna ulazima wa kubadili uongozi uliokuwepo na kusimika uongozi mpya utakaoweza kukipa uhai. Vilevile ni mabadiliko ya uongozi sasa ndiyo yatakayoweza kutoa nafasi kwa WAJAMAA MASALIA wanaolazimika ama kulazimishwa kubaki CHADEMA na CCM kupata uwanda wa kisiasa kujaribu kujenga Tanzania waitakayo na kurudisha siasa za kiitikadi badala kuendelea kutumika kuendeleza siasa za tuhuma, chuki, uzandiki, personalities na ujanjaujanja mwengine."

Kumbuka hapa ni uwanja wa great thinkers.. tunaweza kujumlisha mawazo ya mtu na tukapata jibu..
 
ZITTO alikuwa na kazi ya kuhujumu chama tu. Ndivyo alivyofanya kule kwa Pinda, Singida Mjini, Musoma Vijijini na kwingineko. Pale Musoma Vijijini, Zitto kwa urafiki wake na Nimrod Nkono alikubali kumuondoa mgombea wa chama chake baada ya kuhongwa Sh. 60 milioni na yule kijana kumpa paundi 1000 kwa ahadi kwamba nyingine atazikuta Dar es Salaam.

Yule kijana alikamatwa na vijana wa Chadema pale makao makuu na kueleza kila kitu juu ya jambo hili. Je, hapa nani atakuwa anamchimba bwana mdogo huyu? ZITOOOOO adui yako ni tamaa yako ya kutaka kuishi maisha ya anasa na kupenda mabibi.

Tunamjua vema Zitto, hana maadili. Kama anabisha katika hili, ajitokeze hapa tuweke ushahidi.
Hawa Chadema mbona wanamuogopa sana huyu Zitto? anafanya yote haya unayomtuhumu dhidi ya chama chake, kinayajua na bado wanamuangalia tu. Ana nini?
 
OmaryIlyas,
Nimeyasoma pia maelezo na madai yako kuhusu Mbowe na aloyafanya. Kama kweli ameyafanya hayo basi makosa ni ya chama kizima kumpa mamlaka makubwa kiasi hiki mwenyekiti wa chama. Nachoamini mimi Mkapa, JK wote wameyafanya waloyafanya kwa sababu Katiba imewaruhusu na kuwapa madaraka makubwa ya Kiungu...Kwa nini wafuasi wake wasiwaabudu?..

Hivyo makosa yote yanaanza na katiba, hivyo kama Mbowe amefikia kutumia vibaya madaraka yake na asishtakiwe kwa sababu ni mwenyekiti basi bila shaka katiba ya Chadema ina mapungufu mengi ambayo yanatakiwa kushughulikiwa haraka iwezekanavyo... hii ndio dawa na sii kumwondoa Mbowe ukamweka mwingine anayetaka uenyekiti kwa sababu kunakupa Uungu. Na ndio maana kumbe watu wanagombani Uenyekiti badala ya kutazama jinsi ya kukiboresha chama isipokuwa kugombea nafasi za uongozi wa kiti hiki ili wafanye nini?.. utajaza!
 
Moses Machali anataka kuhamia CHADEMA, hivyo anajipendekeza kwa chama hicho kwa kujenga njia itakayo mrahisishia safari hiyo akidhani kuwa Zitto akifukuzwa yeye atapewa vyeo vinavyoshikiriwa na Zitto
 
OmaryIlyas

Unaogopa ugonjwa wa Zitophobia na huku unapatwa ugonjwa wa Zittomaniac. Sasa sijui tukutibu na nini, maana ulianza kwa kutetea kuwa Zitto hahami Chadema kwenda NCCR, sasa umeibuka na kuwa anahama kwa sababu za kiitikadi. Tuletee mengine.
 
HUYU ZITTO kaba kuja humu na kujifanya mjuaji aeleze kwanza aliko JACK, yule mwanadada wa UDSM. Tatizo la ZITTO anaongozwa na mama yake, Shida.

Hizi personal issues hazina logic wala hazijabeba ujumbe wenye maslahi kwa taifa.Frustration za aina hii ndiyo zinazowafanya muwe na Rais wa aina hii tuliye naye leo,tunaishi kufanya chaguo lisilo sahihi.Voting for beauty,not for duty.Tukishakuwa na twisted minds tunaishia kutumia vigezo vya hovyo kumchagua au kumkataa mtu,ndipo tunapojikuta tunampa mtu aliyestahili pengine kuwa tourism minister Urais.

Moses Machali anataka kuhamia CHADEMA, hivyo anajipendekeza kwa chama hicho kwa kujenga njia itakayo mrahisishia safari hiyo akidhani kuwa Zitto akifukuzwa yeye atapewa vyeo vinavyoshikiriwa na Zitto

vinavyoshikiriwa = vinavyoshikiliwa
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom