WALIOPITIA Charter ya OIC kiudini wameangalia vipengee vilivyogusa tu maslahi ya Waislamu na kuikosoa Charter kwa kile walichokielewa wao kutokana na hili. Lakini kuna mengi yamo katika 'charter' ambayo yamelenga pamoja na mengine:
. Kumpunguzia umasikini Mtanzania wa kawaida.
. Kuwaondolea wanawake ugumu wa maisha,
. Kuwalea watoto na vijana wetu ili waapukane na madawa ya kulevya, ngono na ukimwi,
. kusaidia biashara ndogondogo na kubwakubwa,
. kuisaidia Tanzania kupata masoko nchi za nje bila kujali mfanyabiashara ni mkiristo au Muislamu kama walivyo wafanyabiashara wengi wa Tanzania (asilimia 76%) ya wanaokwenda Dubai na UAE.
. kutusaidia kujenga miundo mbinu ikiwemo daraja la Kifgamboni ambalo NSSF imejiondoa baada ya kuona Viiongozi wa Kikiristo hawataki Maendeleo ila dini,
. kuhakikisha kuwa hatuingiliwi kimabavu na nchi za nje, uhuru na mipaka yetu vinaheshimika daima dawamu.
Kwa hiyo ninachokiona mimi hapa ni kuwa kwa kila zuri OIC inalotaka kulifanya Wakatoliki, Mapentakoste na Waludherani hawayataki na hawataki wananchi wa nchi hii wafaidike nayo:
1.
In the name of Allah, the most Compassionate, the most Merciful
Wakiristo wanachosema hapa ni kuwa haifai kutaja jina la Mungu katika nia njema, na wala Mungu sio mwenye Rehema wala Huruma!
2.
to be guided by the noble Islamic values of unity and fraternity, and affirming
Wanachosema wenzetu ni kwamba hawataki maadili, umoja wala udugu na Waislamu.
3.
the essentiality of promoting and consolidating the unity and solidarity among
the Member States in securing their common interests at the international
arena;
Hawataki pia kujiunga na taasisi yoyote ile itakayowapa nguvu na uwezo wa kupambana na mataifa makubwa.... Yaani, wakiristo, wabnaamini kuwa sisi kama nchi tuna uwezo wa kutoshirikiana na mashirika yoyote ya kimataifa na tukafanikiwa mambo yetu.....
4.
to adhere our commitment to the principles of the United Nations Charter, the
present Charter and International Law;
Na pia hawatambui kwamba IOC ina baraka za Umoja wa Mataifa.
5.
to preserve and promote the lofty Islamic values of peace, compassion,
tolerance, equality, justice and human dignity;
Na zaidi ya hayo nia njema ya OIC kuchangia katika maadili mema. amani, huruma, uvumilivu, usawa, haki na utu wa mwanadamu vyote hivi havina maana kwa wenzetu.
6.
to endeavour to work for revitalizing Islams pioneering role in the world
while ensuring sustainable development, progress and prosperity for the
peoples of Member States;
Misaada na kujitolea kwa OIC kuhakikisha nchi wanachama wanafanikiwa katika masuala ya kiuchumi na kijamii pia ni nongwa kwao. Kote huku wanaona harufu mbaya ya maneno mawili tu: UISLAMU NA WAISLAMU!
7.
to enhance and strengthen the bond of unity and solidarity among the Muslim
peoples and Member States;
to respect, safeguard and defend the national sovereignty, independence and
territorial integrity of all Member States;
Hawataki IOC kusaidia kujenga daraja kati ya nchi za Kiislamu na nchi kama Tanzania kwa sababu za hofu ya Wakiristo kumezwa na Waislamu?
8.
to contribute to international peace and security, understanding and dialogue
among civilizations, cultures and religions and promote and encourage
friendly relations and good neighbourliness, mutual respect and cooperation;
Je, kuna nchi yoyote au mtu yeyote anayepata hasara kwa kuzungumza, kujadili au kuingia katika midahalo na watu wengine. Hivi hatujui kuwa mazungumzo ndio mwanzo wa maendeleo yote?
9.
to promote human rights and fundamental freedoms, good governance, rule of
law, democracy and accountability in Member States in accordance with their
constitutional and legal systems;
Wakiristo hawataki hili pia, yaani, haki za binadamu (kama wao wanavyotaka kuwanyima Waislamu haki zao), uhuru wa kila mtu,utawala bora,utawala wa kisheria,demokrasia na uwajibikaji.....halafu hapo hapo wanaicharura serikali kwa kushinda eti majukumu yake ya msingi. Kuna majukumu makubwa zaidi ya haya.
10.
to promote confidence and encourage friendly relations, mutual respect and
cooperation between Member States and other States;
Hawataki pia kupromoti kuaminiana na urafiki kati yetu. Hivi wakiristo hawa wa miaka hii wana nia njema na sisi kweli?
11.
to foster noble Islamic values concerning moderation, tolerance, respect for
diversity, preservation of Islamic symbols and common heritage and to defend
the universality of Islamic religion;
Kinachosemwa hapa kina ubaya gani. Huku waislamu wanalumiwa kwa Ugaidi na sheria ya ugaidi imeptishwa kwa shinikizo la manasara na Marekani. Hapa IOC inatuambia kuunga mkono Waislamu wasio na siasa kali; wavumilivu; kuheshimu tofauti baina yetu; na kulinda mali na urithi wa Waislamu nini hapa Tatizo? Au wao hawataki kulinda mali na urithi wao?
12.
to advance the acquisition and popularization of knowledge in consonance
with the lofty ideals of Islam to achieve intellectual excellence;
Elimu na maarifa nayo imekuwa nongwa kwa Wakiristo pia siku hizi? Angelifuka Mtakatifu Mtarajiwa wenu Mwalimu Nyerere angeliwaelewa kweli katika hili?
13.
to promote cooperation among Member States to achieve sustained socioeconomic
development for effective integration in the global economy, in
conformity with the principles of partnership and equality;
Hapa tunapewa pia silaha ya kupambana na utandawazi, ajira kwa machinga wetu na kunyanyuliwa biashara ndogo ndogo kwa masoko ya uhakika kwenye nchi za Kiislamu tunakaataa au Wakiristo wanatulazimisha kukataa na sisi tunakubali. Ni viziwi? Ni vipofu? Kwanini?
14.
to preserve and promote all aspects related to environment for present and
future generations;
Wakiristo hawana shida pia ya IOC kutusaidia kulinda mazingira yetu ya bahari yanayoharibiwa (labda kwa sababu waathirika wakubwa ni waislamu?)
15.
to respect the right of self-determination and non-interference in the domestic
affairs and to respect sovereignty, independence and territorial integrity of
each Member State;
Wakiristo wanasema hapana kuhusu suala la kutoingiliwa na mataifa makubwa. Kwa hiyo Marekani ikipenda kwa mujibu wa wenzetu au Waingereza au Wafaransa au wachina basi ruksa kwao wao kutuvamia tu. Mlipinga tusipewe uhuru sasa mnaomba tuvamiwe na mataifa ya nej?
16.
to support the struggle of the Palestinian people, who are presently under
foreign occupation, and to empower them to attain their inalienable rights,
including the right to self-determination, and to establish their sovereign state
with Al-Quds Al-Sharif as its capital, while safeguarding its historic and
Islamic character, and the holy places therein;
Bila shaka kwa kuwa jamaa zetu hapa wanakula sahani moja na Vatican na Mayahudi hili linawaumwa wanaona miji hiyo ni yao na sio yetu. Lakini Haqq itafichika hadi lini?
17.
to safeguard and promote the rights of women and their participation in all
spheres of life, in accordance with the laws and legislation of Member States;
Tunalaumiwa tunakandamiza wanawake wetu. OIC inakuja kutushikisha adabu wakiristo wanakataa sasa mnalaumu nini na mnamlaumu nani ndugu zetu katika Kitabu?
18.
to create conducive conditions for sound upbringing of Muslim children and
youth, and to inculcate in them Islamic values through education for
strengthening their cultural, social, moral and ethical ideals;
Mnadai vijana wetu ndio wezi wakubwa, wavuta bangi, ndio walevi wakubwa, ndio malaya wakubwa, watumiaji madawa ya kulevya, wamejaza magereza yote nchini. Halafu hamuitaki IOC inayokuja kusaidia serikali kupunguza baa hili hivi tuwaelewaje jamaa hawa?