Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Schimids na wenzako huo ni uzushi ambao Rais Kikwete aliouzungumzia kwenye hotuba yake.Hivi nchi zingine uganda nakadhalika ni za kiislaam.Hivi nyie mnalitakia heri taifa hili au ni vipandikizi.Wa wale wanaotaka kuvuruga TZ kama walivyovuruga nchi zingine za kiafrika.Ni watanzania kweli namashaka nanyi
 
mengi tu, yaliyotokea israel yalitokea tena tanzania,vijiji vya ujamaa were modelled on the KIBBUTZ settlements of israel,only diffrence,ujamaa villages were less succesfull
 
Kuna wakati huwa nasoma mambo mengine JF na uchangiaji wake kisha hujiuliza kama kweli ELIMU tuliyopewa ni elimu endelevu ama kudumisha UTUMWA wa akili....Hii ni moja wapo.
Hakika Tanzania ni nchi iliyojaaliwa lakini haina WATU!...
 
Kuna wakati huwa nasoma mambo mengine JF na uchangiaji wake kisha hujiuliza kama kweli ELIMU tuliyopewa ni elimu endelevu ama kudumisha UTUMWA wa akili....Hii ni moja wapo.
Hakika Tanzania ni nchi iliyojaaliwa lakini haina WATU!...

u have every right to say what u have said. akili za watanzania zipo katika kuchallenge bila kureason. watanzania hata akishuka mungu mwenyewe na akiwaambia wakajiunge na ufalme wa mungu mbinguni basi pia wataanza kuchallenge. akili zetu zipo kwenye kubaguana tu basi!! hatufiki maisha.!
 
bora ungeacha hiyo rais ilikuwa imekaa vizuri,. hivi pope si ndio unajinyaka na kufunga kitabu? kwa uelewa wangu mdogo nadhani pope ndio kiongozi wa kanisa katoliki duniani , correct me if i am wrong. sasa hiyo vatican iwe nchi au si nchi utaiona direct inawakilisha ukristo kwasababu kiongozi wa vatikan ndio kiongozi wa katoliki. sasa wakati kiongozi wa vatikan ndio kiongozi wa catholics . je kiongozi wa oic ndio kiongozi wa uislam? au ni muislam tu as muislam! which is worse , vatican (inayoongozwa na kiongozi wa wakristo duniani) or oic (ambayo inaongozwa na muislam lakini sio kiongozi wa uislam)?

Vatican ni absolute Monarchy na si republic ndiyo maana nikamwita mfalme ingawa si wa kurithi. Unachanganya ukatoliki na ukristu. Pope ni kiongozi wa wakatoliki na ni Mfalme wa Vatican lakini haina maana kuwa wakatoliki wote ni raia wa Vatican! You are wrong. Vatican haiwakilishi ukristu. Mbona Malkia wa uingereza ndiye kiongozi wa Church of England ambalo ndilo kanisa mama la Anglicans? Kwa mtazamo wako basi uingereza inawakilisha ukristu! Mbona Ayatollah Ali Khamenei, kiongozi wa mashia ndiye Supreme Leader wa Iran, mwenye mamlaka juu ya Rais. Kwa mantiki yako basi Iran ni mwakilishi wa waislamu! Mbona wasunni wa Iraq na kwengineko hawana imani nae na hawamtambui?

Unarudia makosa ambayo wenzetu mnayofanya kila siku. Kutetea cha kwenu kwa kulinganisha na cha wengine. Tetea OIC kama chombo kinachounganisha waislamu bila kulinganisha na Vatican. Ni vitu viwili tofauti na hauitendei haki OIC.

Mwisho malkia wa Uingereza, kiongozi wa Church of England, ndiye kiongozi wa jumuia ya madola ambamo sisi ni wanachama. Kwa hiyo jumuia ya madola ni shirika la kikristu?


The Organization of the Islamic Conference (OIC) is the second largest inter-governmental organization after the United Nations which has membership of 57 states spread over four continents. The Organization is the collective voice of the Muslim world and ensuring to safeguard and project the interests of the Muslim world in the spirit of promoting international peace and harmony among various people of the world. The Organization was established upon a decision of the historical summit which took place in Rabat, Kingdom of Morocco on 12th Rajab 1398 Hijra (25 September 1969) as a result of criminal arson of Al-Aqsa Mosque in occupied Jerusalem.

ref:http://www.oic-oci.org/oicnew/page_detail.asp?p_id=52

OIC imeundwa kama wanavyosema wenyewe kwenye tovuti yao, kulinda maslahi ya waislamu na ni sauti ya jumla ya dunia ya kiislamu. Ina lengo la kuendeleza amani na ushirikiano baina ya watu tofauti wa dunia. Hili ni shirikisho la kiislamu, kwa ajili ya waislamu. Hakuna ubaya kwenye hili. Ubaya ni kujaribu kukana na kujaribu kukigeuza kuwa secular. Tukijiunga, kitaangalia maslahi ya waislamu walio Tanzania kwanza na si wengineyo. Hivyo hivyo kwa Uganda. Tetea hoja yako kwa misingi hii.


The Commonwealth of Nations, usually known as the Commonwealth, is a voluntary association of 53 independent sovereign states, most of which are former British colonies, or dependencies of these colonies (the exceptions being the United Kingdom itself and Mozambique).

No one government in the Commonwealth, British or otherwise, exercises power over the others, as in a political union. Rather, the relationship is one of an international organisation through which countries with diverse social, political, and economic backgrounds are regarded as equal in status, and co-operate within a framework of common values and goals, as outlined in the Singapore Declaration.[1] These include the promotion of democracy, human rights, good governance, the rule of law, individual liberty, egalitarianism, free trade, multilateralism, and world peace,[2] and are carried out through multilateral projects and meetings, as well as the quadrennial Commonwealth Games. The symbol of this free association is Queen Elizabeth II, known for this purpose as Head of the Commonwealth. This position, however, does not imbue her with any political or executive power over any Commonwealth member states; the position is purely symbolic, and it is the Commonwealth Secretary-General who is the chief executive of the organization.

Ref:http://en.wikipedia.org/wiki/Commonwealth_of_Nations

Linganisha malengo ya jumuia ya Madola na OIC na utaelewa kwa nini moja ni la kidini na lengine sio.
 
bora ungeacha hiyo rais ilikuwa imekaa vizuri,. hivi pope si ndio unajinyaka na kufunga kitabu? kwa uelewa wangu mdogo nadhani pope ndio kiongozi wa kanisa katoliki duniani , correct me if i am wrong. sasa hiyo vatican iwe nchi au si nchi utaiona direct inawakilisha ukristo kwasababu kiongozi wa vatikan ndio kiongozi wa katoliki. sasa wakati kiongozi wa vatikan ndio kiongozi wa catholics . je kiongozi wa oic ndio kiongozi wa uislam? au ni muislam tu as muislam! which is worse , vatican (inayoongozwa na kiongozi wa wakristo duniani) or oic (ambayo inaongozwa na muislam lakini sio kiongozi wa uislam)?

wewe usiangalie upande mmoja.
kwani yule mfalme sijui wa saudia sio SHEIKH? viongozi wa nchi za kiaarabu wengi ni masheikh sasa wanapokuja hua wanawakirisha ushehe wao ama kama wakuu wa nchi zao?
 
Kuna wakati huwa nasoma mambo mengine JF na uchangiaji wake kisha hujiuliza kama kweli ELIMU tuliyopewa ni elimu endelevu ama kudumisha UTUMWA wa akili....Hii ni moja wapo.
Hakika Tanzania ni nchi iliyojaaliwa lakini haina WATU!...

Acha matusi kaka.
Huo ndio uhuru na demokrasia ,kuna watu humu ndani walishasema hata yule kichaa huwaona watu wenye akili timamu kua wao ndio vichaa ila yeye ndio aliye timamu.
 
u have every right to say what u have said. akili za watanzania zipo katika kuchallenge bila kureason. watanzania hata akishuka mungu mwenyewe na akiwaambia wakajiunge na ufalme wa mungu mbinguni basi pia wataanza kuchallenge. akili zetu zipo kwenye kubaguana tu basi!! hatufiki maisha.!


Tatizo letu ni wale wasomi wetu waliosoma ili kulinda KATIBA na MUSTAKBALI wa nchi yao.Badala yake wana i BYPASS kwa masilahi yao.

Hawa watu wanaopindisha KATIBA wakati wakielewa wanapindisha KATIBA ya nchi hao ndio kikwazo kikubwa.

Msomi muelewa anapoaamua kutofuata KATIBA ama KANUNI za jamii husika kwa makusudi huyo ndiyo hatari kwa jamii husika.

Msomi aliye elimika ili aondoe contradictions ktk jamii lazima aanze na misingi ya katiba kuzibadili na baadae kuanzisha kitu akipendacho ili jamii ama kizazi kisije kuja jichanganya kwa WAHUNI wachache kuamua Ku BYPASS katiba.

Kama nchi Inaongozwa kwa misingi ya katiba lazima tuzifuate misingi hiyo hiyo ya katiba.
Mfano nchi yetu inasema sio nchi ya kidini sasa kutuingiza ktk chama cha dini ya uislamu ni KITUKO kwa anayejiita msomi,Labda mtuambie UISLAMU sio DINI bali ni dola ama falme fulani.

Mtu msomi mzima anakuja na hoja nyepesi ama mfu kabisa kusema Mbona msumbiji na uganda zimo OIC.

Huyu huyu anayejita msomi anashindwa kujiuliza je KATIBA ya UGANDA na MSUMBIJI ina sema nini ktk suala la DINI.
Je katiba yao imesema bayana kua haina dini? je imesema ni dini ya kiislamu? je imesema ni dini ya kikristu? je? imesema itafuata dini yoyote yenye masilahi?je imekaa kimya ktk suala la dini? hivyo kuipa nafasi serikali kuamua kufuata ama kuchagua kujiunga na dini yoyote?

HAYA mambo yakotofuata KATIBA na SHERIA inasema nini ndipo uhuni unapoanzia.
Ndio inafikia wezi wakubwa wa fedha zetu kupewa mda eti wa kuripa deni.Badala ya kufuata na kuangalia sheria inasema nini ktk suala la wizi?.
 
Fundi Mchundo,

tatizo lako wewe mwepesi sana wa kusahau hata baada ya kurasa tatu tu unashindwa kuelewa mfulululizo wa hoja zinazoendelea hapa.
Kumbuka huko nyuma nimekwambia kuhusiana na habari hizi za waandishi ambao kwanza huwa hazina ukweli na kama utasoma kwa makini beteen lines utaona makosa makubwa na pengine uongo wa habari yenyewe..

Kwa hiyo nilipokuuliza umepata wapi habari hii najua kabisa hukusoma between line kuelewa uongo uliopo ktk taarifa nzima ya mwandishi...
Si kweli kwamba Islamilia hawatambuliwi kama waislaam na kama haya maneno ni ya kweli basi msingesema huko Iraq wanapigana waislaam kwa waislaam. Tofauti za madhehebu ndani ya dini moja hakuwezi kuondoa uhalali wa dhehebu jingine ni sawa kabisa na ukimuuliza Anglican kuhusiana na Mkatoliki.. Wewe unatakiwa kujua tofauti hizi kabla hujaandika kitu kuhusiana na dini unayojaribu kuipaka tope. Ismailia ni dhehebu ndani ya Shia Muslims na wamejitenga kutokana na sababu sawa na zile za makanisa mengine yalivyoitenga toka Ukatoliki..lakini pamoja na tofauti zao zote wote wanasoma Biblia.. Hakuna tofauti yoyote na madhehebu ndani ya Uislaam ni tofauti za kawaida na hazina maana dhehebu moja linatambulika zaidi ya jingine hali sisi sote hatufahamu kilichoko huko juu... Hilo moja..

Pili ni wewe uliyezungumzia kwamba EAMWS founder wake ni AghaKhan kutokana na habari uliyoisoma na kuiamini ndio maana umeitoa hapa. Sasa ikiwa founder ni AghaKhan imekuwaje tena chombo hiki hiki alichokianzisha kiwe ni chombo cha Shia Muslims lakini kabla hakijaanza kazi huyo huyo founder wake ajipinge na kusema ni chombo cha Waislaam wote hali yeye mwenyewe ndiye founder!....
Hapa ulichokosa kuangalia ni between the lines kuwa EAMWS kilikuwa chombo cha waislaam kilichoanzishwa (registered) na waislaam wahindi kwa kupata support ya mfuko toka kwa sponsor ya mfuko wa AghaKhan na chombo chake (Network) AKDN..huu ni utaratibu wa kawaida kabisa lakini kwa sababu gazeti haliwezi kuandika kila hatua ya vitu hivi kwa sababu zao wenyewe huwa kuna mapungufu ambayo untakiwa kusoma kwa makini kuweza kuyachambua... siku zote hapa lugha yetu ni kutoa pumba ktk mchele, haina maana waandishi wengine nje ni exceptional.

Sasa kama wewe ni msomi mzuri utaelewa jinsi misaada inavyotolewa na pengine makosa madogo mdogo ya ya makusudi ktk uandishi ili kuweka hizo tofauti za rangi na kugawa watu kwa makundi ya rangi zao.

Mathlan, nitakupa mfano mmoja kisha uweke ktk kuanzishwa kwa EAMWS. Tuseme World Vison ni chombo kilichoanzishwa na wazungu kuwasaidia wakristu Africa kwa kupitia kanisa la katoliki (vatican) haina maana chombo hicho ni cha wazungu na mwanzilishi wake ni papa Paul..Na yawezekana kabisa mwandishi mkatoliki, mzungu mkazi wa vatican akasema founder wa World Vision ni Papa Paul akiwa na maana ya support yake na pengine hata kuhudhulia kukata utepe wa ufunguzi rasmi wa chombo hicho lakini ukweli sii yeye mwanzilishi..
Kwa hiyo kaa mimi Muislaam nitasoma bila kuangalia between the lines naweza kusema kanisa katoliki limetuingilia nchini na pengine kutoa tafsiri kama zako kuhusiana na tofauti zilizopo kati ya Wakatoliki weusi na wazungu na kuzitumia kisiasa kuuhabarisha umma.

Nne, Sii kweli kwamba EAMWS kilikuwa hakipendwi na waislaam wa TANU wakati ukweli ni kwamba waislaam wote waliokuwa TANU wakati huo walikuwa wanachama wa EAMWS nadio walioanzisha chama cha TA iweje tena hao waislaam waliokuwa TANU wajipinge wenyewe...
Kisha kwa taarifa kamili na yenye ukweli nakuomba kamtafuta mzee Ally Skyes ambaye ni mmoja wa waasisi wa TANU pamoja na kwamba kajitoa ktk siasa muulize vizuri nafasi ya EAMWS ndani ya TANU kabla ya mwaka 1968...
Maelezo yaliyotangulia na mwandishi haya make sense at all!... isipokuwa kama msomi mzuri inabidi uzame ndani zaidi kuelewa kilichotokea.
Huko nyuma nimekueleza vizuri nini ilitokea na kitu gani kichosababisha mwalimu kukiua chombo hiki ambacho kusema kweli Waislaam kutokana na mchango wao ktk kutafuta Uhuru walianza kutamani fadhila fulani za madaraka au fehda kama binadamu.. kama haya yanayompata Kikwete leo hii toka kwa wafadhila wake wa uchaguzi uliopita.
Kisha kwa sababu hawa jamaa hawakupata kile walichokitaka walijaribu kufanya mapinduzi ambayo hayakufanikiwa. mwalimu alikuwa Arusha ktk mkutano akabonyezwa na Sheikh Kassim Bin Jumaa kuhusiana na jaribio la kumwondoa madarakani na wahusika kwa bahati mbaya wengi wake walikuwa waislaam na kama nilviyosema viongozi wote wa kiislaam ndani ya TANU wakati huo walikuwa members of EAMWS..
Hapa mwandishi alijaribu kuweka tabaka kuingiza siasa ktk maswala ya dini kwamba ikiwa mwenyekiti wa EAWMS ni toka chama cha Upinzani basi waislaam wa chama kingine watakikataa chombo chao cha dini kwa sababu za kisiasa hali wapinzani wakubwa wa mwalimu miaka ya 1968 walikuwa ndani ya chama chake mwenyewe yaani TANU pamoja na kwamba wengi wao walikuwa waislaam na ndio maana nikawataja kina Kambona..
hapa nikiwa na maana hata wewe mwenyewe umetaka kuchanganya dini na siasa ukitumia vigezo vya rangi za watu kufikia maamuzi. hakuna kabisa uhusiana wa karibu kati ya maswala haya ya siasa na mahakama ya kadhi ikiwa huna imani kuwa swala la mahakama ya kadhi linahusiana na siasa.. na sijui kama unataka kusema hata hiyo mahakama ya kadhi aliyeianzisha ni Agha Khan..
Ni wewe uliyesema ama kuamini mwanzilishi wa EAMWS ni Aghan Khan na kuwa kilikuwa cha wahindi Ismailia, kikapigwa marufuku wakati wa Nyerere ukauliza kwa nini wasiifungue tena wakati wa Mwinyi bila kujiuliza why Muslims weusi ambao hawana asili ya kihindi ndio wanaopiga kelele leo kuhusiana na chombo hicho?..Yote ni katika kukuonyesha kwamba EAMWS kilikuwa ni chombo cha waislaam kwa waislaam sawa na BAKWATA ambacho ni chombo cha waislaam kwa ajili ya maslahi ya watawala na hujiulizi kuhusiana na mwanzilishi wake ambaye alikuwa Nyerere, asili yake ama dini yake, sasa sijui hapa utakuwa na story gani mpya kuhusiana na chombo hiki Bakwata kuwa nacho ni chombo cha watu gani!...wakatoliki na Wazanaki au?... hii ndio shida ya kuangalia rangi na ukashindwa kutazama upande wa pili kwa kipimo kile kile. Muda wote nimekuwa nikijaribu kukufahamisha ukweli huu...

Nadhani sasa unaipata picha vizuri..Toka kushindwa kwa jaribio hilo Nyerere ndipo alipochukua mkondo mpya, mkondo ambao uli affect sii tu waislaam ama wahindi waislaam bali kila mmoja wetu kwa dini, kabila ama jinsia....Nyerere aliamua kuchukua mkondo wa UJAMAA kuondoa kabisa hizi nguvu za tabaka na kujaribu kujenga taifa lisilo tazama rangi, kabila ama jinsia..

Hayo mawali mengine ya Wapi umesema mkuu nadhani jaribu kurudi nyuma utayaona mwenyewe ulipoandika.. Kama nilivyosema unapo copy na Kupaste maelezo fulani ukayaunga mkono ina maana maelezo hayo yanawakilisha mtazamo ama imani yako..Hakuna haja ya kurudia vitu!..
 
mmmmmmmmmmmm iko siku wakristo na waislamu wa nchi hii watazichapa!!!! maana mmevutana kweli na YNIM anaonekana kajaza jaziba kweli kwa mwanawasu MKAMP? shauri yenu!
 
bwahahahahaha unajua lakini maana halisi ya neno "sheikh" au unakurupuka tu!!?? sawa viongozi wengi wa nchi za kiarabu ni masheikh lakini sio kweli kwamba ni viongozi wa kidini!! LOL...tafuta maana 'halisi' ya "sheikh" halafu ujione ulivyo mtu wa oovyo......acha udini kaka, aibu mpaka unaongea vitu ambavyo huvielewi!!

kwa kifupi naweza kukuita wewe mkamap sheikh wangu kama heshima aidha kwa busara zako, umri au uongozi ulionao ambao si lazima uwe wa dini ya kiislamu!! Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Kikwete wote ni masheikh ktk masuala ya uongozi wa serikali ya Tanzania.....bisha!

tulia na acha udini, unajidhalilisha!! shame.

wewe acha kupindisha na maneno ya mtaani.
wewe pia ninaweza kukiita baharia wangu lakini wewe si baharia na neno shehe unalotaka tuliamini sio hilo linalotumika kwa watu hao.

Maneno hayana maana ila yanategemea mazingira yaliyopotumika. Jina kuanza na utangulizi lina maana kubwa kama MR ,PROF,DR,MWL,SHEHE SIMBA.

Harafu matusi hayasaidii wewe gonganisha hoja hapa.Gadhabu za nini sasa unataka kutuambia huyo mfalme sio pia kiongozi wa dini?
 
The King of Saudi Arabia is Saudi Arabia's head of state and absolute monarch. He serves as the head of the Saudi Monarchy and House of Saud.

Within Saudi Arabia the king is known by the title of The Custodian of the Two Holy Mosques (خادم الحرمين الشريفي&#1606😉, which refers to Saudi Arabia's jurisdiction over the mosques of Masjid al Haram in Mecca and Masjid al-Nabawi in Medina.
 
mkamap,
Kweli mkuu lakini huo uhuru wa kusema na demokrasia haukuwekwa kwa vichaa au sio?...
Kichekesho ni kwamba sijui kati yetu nani kichaa..sijatukana bado.
 
Utaelewa taratibu tu.

Unadhani kama katiba Ni BIBLIA ni viongozi gani watakaokua wanaielewa BIBLIA.

The politics of Saudi Arabia takes place in a framework of an absolute monarchy whereby the King of Saudi Arabia is not only head of state, but also the head of government. The central institution of Saudi Arabian Government is the monarchy. The Basic Law adopted in 1992 declared that Saudi Arabia is a monarchy ruled by the sons and grandsons of King Abd Al Aziz Al Saud, and that the Qur'an is the constitution of the country, which is governed on the basis of Islamic law
 
Saudi Arabia does not permit religious freedom and bans all visible forms of non-Muslim worship. Non-Muslims, as well as Muslims who do not adhere to the Sunni Islam, are advised by Mutawwa'in (the religious police) for acts considered offensive to state ideology. Citizenship is restricted to Muslims, but non-Muslims are allowed in many jobs across the country. However, Jewish people or persons with evidence of travel to Israel in their passport are not permitted to enter the kingdom.

The government maintains 50 Call and Guidance centers to encourage foreigners to convert to Islam. [3] Religious police enforce a modest code of dress and many institutions, from schools to ministries, are not co-educational.
 
mjadala sasa ni Saudia na sio tena Bongo ya Darisalame kujiunga na OIC!?? yayayayiiiiiiii kaazi kweli....au ndio mwisho wa mwezi nini? bwahahahaha!

Tatizo unafikiri matusi yatasaidia.

Mimi hapa nataka kukuonyesha uongozi wa VATICAN hauna toauti na wa SAUDIA.

Ila kwa vile matusi na ghadhabu ni moja ya huruka -------- sishangai sana mimi nayakubali hayo matusi yote.

Tukirudi kwenye hoja.

Ni mpumbafu tu ama hakimu mpumbafu atakaye hukumu kesi kwa huruka ama hisia zaidi ya kusoma hukumu kwa kufuata SHERIA zinasema nini.

Na kiongozi wa nchi atakua mpumbafu vilevile kama ataongoza nchi kwa matakwa yake bila kufuata KATIBA ya nchi inasema nini.

Hili suala wala halikuhitaji mjadala sisi kama kweli tu waelewa turudi ktk mstaafu wetu yani KATIBA tuone inasema nini kuhusu mambo ya DINI.

Tutakua wapuuzi kujadili kitu kwa sisi tupendavyo bila kuwa na mwongozo wetu ambao utatuongoza yani KATIBA.

Maana humu watu wanajadili kwa visingizio eti oo VATICAN oo msumbiji oo Uganda huu ni ulemavu huwezi jadili mambo yetu kwa vigezo vya nchi nyingine ,kwani tunatumia katiba moja.
 


There is no harm in Tanzania joining the Organisation of Islamic Countries (OIC), the government said yesterday. Comment on this article

Nafikiri huko tuendako. Katika Wizara za Mambo ya Nje. Ulinzi. Mambo ya Ndani, Na Hata Mawasiliano( kwa maana ya miundo mbinu mikuu)- Tanzania (SMTna SMZ)zinabidi ziwe na formula inayoeleweka ya kuratibu maslahi yao na jinsi yanavyoingiliana na utekelezaji wa kila siku.
 
...nani kati yetu hapa ni kichaa? yaani unakwenda hovyo tu, kila unachopata kwenye google wewe unabandika bila hata kuona kama kitasaidia kujenga hoja yako.........

tafuta maana ya sheikh kwanza, ukishaipata utakuwa umejitendea haki...LOL.

Usiwe mgumu wa kuelewa.
Nimekwambia neno halina maana ,sitochoka kukupa mfano.

maana ya neno FATHER ni nini?

Lakini Padre pia wanaitwa ma FATHER ,using'ang'anie neno na maana moja. Mfano KIAZI ni zao.Lakini nikisema karimanzira ni KIAZI halima maana hapo ya zao.
Ndivyo hivyo kwa neno SHEHE likitangulizwa neno likawa PREFIX sio kama wewe unachotaka tuamini hapo linakua limetumika kama wadhifa ama hadhi ya mtu husika.
Lakini nikisema unasema je shehe wangu hapo ni tofauti kabisa.
 
Na kiongozi wa nchi atakua mpumbafu vilevile kama ataongoza nchi kwa matakwa yake bila kufuata KATIBA ya nchi inasema nini.

Hili suala wala halikuhitaji mjadala sisi kama kweli tu waelewa turudi ktk mstaafu wetu yani KATIBA tuone inasema nini kuhusu mambo ya DINI.

Tutakua wapuuzi kujadili kitu kwa sisi tupendavyo bila kuwa na mwongozo wetu ambao utatuongoza yani KATIBA.

Maana humu watu wanajadili kwa visingizio eti oo VATICAN oo msumbiji oo Uganda huu ni ulemavu huwezi jadili mambo yetu kwa vigezo vya nchi nyingine ,kwani tunatumia katiba moja.

Ndugu yangu Mkamap,

Jana kwenye post yangu nilidiriki kunukuu kwa urefu kabisa Katiba yetu inasemaje kuhusu swala hili la dini. Kulingana na Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, serikali haina dini, wala haijihusishi na masuala yoyote kuhusu dini, kwani Katiba inasema, mambo yote yanayohusu dini ni masuala ya mtu binafsi na hivyo serikali haitaingilia masuala hayo, hivyo basi suala la Serikali kujaribu kujiunga OIC au kujiingiza kwenye mchakato wa uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi ni kinyume na ukiukwaji wa Katiba. Kwa kifupi nanukuu tena Ibara (kifungu) ya 19 cha Katiba ya Jamhuri wa Mungano wa Tanzania:

19(1)- Kila mtu anastahili kuwa uhuru wa mawazo, imani na uchaguzi katika mambo ya dini, pamoja na uhuru wa mtu kubadilisha dini au imani yake.

19(2)- Kazi ya kutangaza dini, kufanya Ibada na kueneza dini itakua ni huru na jambo la hiari la mtu binafsi, na shughuli na uendeshaji wa jumuia za dini zitakuwa nje ya shughuli za mamlaka ya Nchi.

19(3)- Hifadhi ya haki zilizotajwa katika ibara hii itakua chini ya taratibu zilizowekwa na sheria ambazo ni muhimu katika jamii ya kidemokrasia kwa ajili ya usalama wa jamii, amani katika jamii maadili ya jamii na umoja wa kitaifa.

19(4)- Kila palipotajwa neno "dini" katika ibara hii ifahamike kwamba maana yake ni pamoja na madhehebu ya dini, na maneno mengineyo yanayofanana ua kuambatana na neno hilo nayo yatatafsiriwa kwa maana hiyo.


Hivyo basi, naomba kusisitiza kauli yangu kwamba, Katiba yetu ipo wazi kabisa kwamba serikali haina dini wala haijihusihi kwa namna yoyote na masuala ya dini, Kama ni kujiunga na OIC basi BAKWATA inaweza ikajiunga kama institution na sio Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kujiunga kama Nchi.
 
Back
Top Bottom