Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

1. sawa kama ipo kwa masilahi ya waislamu na kwa ridhaa yao ..

2. halihitaji seal ya kikatiba in first place....nadhani waislamu waandae kongamano lao na kuamua KUANZISHA HII MAHAKAMA MUDA WOWOTE......

3. ...MUHIMU NA WALA BILA MJADALA NI KUWA GHARAMA ZOTE ZA UENDESHAJI ZIWE JUU YA JUMUIA ZA KIISLAMU....

.SERIKALI HAITANGILIA..UNLESS OTHERWISE...

Serikali must stay away period, serikali yetu itambue ndoa tu zilizofungwa huko ni kuwa ni acceptable kisheria, lakini maneno ya talaka na mirathi ni ya sheria ya jamhuri,

Kwa sababu nia na madhumuni ya kuwa na Juidicial branch, ni pamoja na kulinda haki za minority na wanyonge katika society, now ukichukua Talaka na Mirathi kutoka mikononi mwa Sheria ya Jamhuri, sasa unawaacha wanawake wakiwa hopeless na helpless kisheria, not in 20TH Century.
 
Uinslaam wakati huo ulikuwa ni ndio nguvu ya Uhuru wa nchi za Kiafrika na walikuwa wakipigania haki za binadamu hasa ktk bara hili.

Tafadhali naomba tutajie majina ya hao Wapigania haki za binadamu/Wapigania Uhuru maarufu wa Kiislamu ndani ya Tanzania na Afrika kwa ujumla. Mbona hata Unguja, yenye raia asilimia 90 waliyo Waislamu mapinduzi ya kuikomboa kutoka kwa Wamanga (na mabwana zao waliokuwa Waislamu wenzao) yalipangwa na kuongozwa na Mkristo, John Okello?
 


Serikali must stay away period, serikali yetu itambue ndoa tu zilizofungwa huko ni kuwa ni acceptable kisheria, lakini maneno ya talaka na mirathi ni ya sheria ya jamhuri,

Kwa sababu nia na madhumuni ya kuwa na Juidicial branch, ni pamoja na kulinda haki za minority na wanyonge katika society, now ukichukua Talaka na Mirathi kutoka mikononi mwa Sheria ya Jamhuri, sasa unawaacha wanawake wakiwa hopeless na helpless kisheria, not in 20TH Century.

Mambo ipo hapa......##

Unapolazimisha kile unachoita maneno ya talaka na mirathi iwe chini ya sheria ya jamhuri unadhani ndio njia ya kuhakikisha hizo haki za minority unazodai?

Kaka hivi ina maana wenye kutaka kufuata misingi ya imani ya kislamu wameshakuwa minority na wanyonge hapa Tanzania?

Una maana wanawake wanaofuata imani na misingi ya kislamu ni hopeless?

Na kama suala la kuwa hopeless ina maana wengine wa dini zinginezo hawakumbwi na janga hilo? Hivi ina maana hizo tunazoita secular laws hazitumiki kumkandamiza mwanamke kimaslahi? Hivi unyonge wa wanawake ni katika mirathi na talaka tu na sio mengine tunayowafanyia na kuwalazimu kuyafanya kila siku kila mahali?

Unguided perspectives kama hizi ndio chanzo kimojawapo cha baadhi ya waislam kuamini kuwa kuna umuhimu wa kuanzishwa mahakama za kadhi zinazoendeshwa na wajuvi kweli wa sheria za kiislamu badala ya kuachiwa watu waliojaa prejudices kuhusiana na imani na misingi ya kiislamu kama ilivyo sasa katika mahakama zinazotumika.....

tanzanianjema
 
Unapolazimisha kile unachoita maneno ya talaka na mirathi iwe chini ya sheria ya jamhuri unadhani ndio njia ya kuhakikisha hizo haki za minority unazodai?
Kaka hivi ina maana wenye kutaka kufuata misingi ya imani ya kislamu wameshakuwa minority na wanyonge hapa Tanzania?

Off course ni minority na ni wanyonge kwa maana ya kuanzishwa kwa Judicial Branch, Wa-Islam wameonewa sana miaka ya mwanzoni ya uhuru wetu hilo sio siri tena, na hilo limewafanya wawe minority ki-sheria kwa sababu hawakuwa na nguvu aambayo ni equal katika kugawana resources za jamii,

Sasa hivi ninaamini kuwa hakuna tena hilo tatizo, lakini hili la Kadhi ni tatizo la misunderstanding ya haki walizonazo kisheria na kisiasa, kwa sababu ni haki yao kuanzisha hizo kadhi things, bila ya kuomba ruhusa ya serikali, na pia sio haki yao kisheria kudai kutambuliwa na serikali, na walitakiwa ku-keeep public out of this debate period!


Una maana wanawake wanaofuata imani na misingi ya kislamu ni hopeless?

Ukishamnyanga'nya mwanamke, haki zinazohusiana na Talaka, na Mirathi kisheria unafikiri anabakiwa na nini kama sio hopeless na helpless?

Hatuwezi ku-afford this katika karne hii ya 21ST Century!


Unguided perspectives kama hizi ndio chanzo kimojawapo cha baadhi ya waislam kuamini kuwa kuna umuhimu wa kuanzishwa mahakama za kadhi zinazoendeshwa na wajuvi kweli wa sheria za kiislamu badala ya kuachiwa watu waliojaa prejudices kuhusiana na imani na misingi ya kiislamu kama ilivyo sasa katika mahakama zinazotumika.....

Sheria za kii-Islam ni haki yao kuzi-practice huko kwenye maeneo yao lakini zisiingiliane na sheria za Jamhuri, kama vile dini zingine zinavyofanya, sijui kama mawazo yako on this ishu kama ni guided,

lakini siwezi kukubali some mis-understanding of one group's right katika society yetu ikatuletea socety nzima a confusion wakati ukweli uko wazi kuwa kuanzishwa kwa hizo mahakama za kadhi ni haki yao bila ya kuuliza serikali wala kutushirikisha society nzima at large!
 
Tofauti ya kufuata udaku na kufanya utafiti hujionyesha kwenye misimamo, hata kama una misimamo ya kuichukia serikali au kwa wazo lako linalozungumza likiwa limenyamaza, kwamba BAKWATA ilianzishwa na wakristo (Nyerere na wenzake) lakini ukweli ulio wazi ni kwamba BAKWATA si mali ya serikali wala haiendeshwi kwa kodi za watanzania

kama unakumbukumbu yoyote ile inayothibitisha kwamba serikali imewahi kuchagua viongozi wa BAKWATA tafadhali sana tukumbushe wenzio!



wakuu wote,
Mimi nimeipenda hii na naomba nipatiwe muda kesho nikirudi ofisini nimuwekee huyu bwana USHAHIDI anao utaka.
 
utimamu huja kwa tafakuri,hivi unadhani vichaa wanatuona sisi tuna akili timamu? lakini swali langu lina mantiki unayotakiwa kuiona na kuijibu. kwenye nchi nyingi zenye mahakama ya kadhi kubadili dini ni dhambi kubwa sana kama uhaini kwenye dola.

watu wanaobadili dini kwa mujibu wa imani za kiislamu wamemuasi mungu na adhabu yao inapaswa kuwa kubwa. sasa kwa kuwa katika nchi yetu imekuwa kawaida mtu kutoka uislamu na kwenda kwenye ukristo au ukristo kwenda uislamu na kuwa hakuna tatizo katika hilo, sawali langu ni kwamba mahakama ya kadhi itavumilia uasi wa waislamu dhidi ya dini yao?




NADHANI UNGEJARIBU KWANZA KUJUA TOFAUTI,TOFAUTI KATI YA MAHAKAMA YA kadhi na MAHAKAMA YA sharia.

Nadhani ndio maana jambo hili lina ugumu wa kueleweka hapa,kwani wanao bisha mahakama hii hawajui tofauti ya mahakama hizi.
 
--------------------------------------------------------------------------------

Tanzania: We Have No Hand in Bakwata Row,Says Govt


The Citizen (Dar es Salaam)

19 July 2008
Posted to the web 21 July 2008

Polycarp Machira

The deputy minister for Home Affairs, ambassador Khamisi Kagasheki, yesterday distanced the Government from the recent leadership row that has rocked the National Muslims Council, Bakwata.

He urged people not to link the government and its officials with the dispute, and advised Muslims to amicably solve their differences. "I would like to make it very clear that the Government was not involved in the recent expulsion of leaders from Bakwata contrary to what is being reported in the media", he said.


The minister, who addressed a press conference in his office in Dar es Salaam, said the Government did not play any role in the row pitting the opposing Bakawata factions against each other. "They should stick to their constitution to solve the wrangles", he advised them.

He said while it was the role of the Government to register all civil societies through the registrar at the ministry, they should govern themselves through their constitutions. He said it is through the constitutions that leaders of civil societies could be replaced in case of any violation of set principles.

Officials of various Muslim trusts have been reported by the media as having blamed the Government for the Bakwata wrangles that saw Chief Sheikh Issa Shaaban Simba expel nine former close confidants at the Bakwata headquarters.

The clarification comes a few days after a special annual general meeting of Bakwata in Dar es Salaam which endorsed the expulsions and swore allegiance to the Chief Sheikh. The meeting also refuted reports that there were serious differences among Bakwata officials.

Those dismissed were branded as "inciters" at the meeting for allegedly spreading documents to divide the faithful. Speaking on behalf of the ailing Chief Sheikh Issa Shaaban Simba, acting Chief Sheikh Suleiman Gorogosi said all representatives had endorsed the recent leadership changes. Leaders dismissed by Sheikh Simba include the deputy Mufti Abubakar Zubeir, who doubled as secretary to the Chief Sheikh.

Others are the chairman of the National executive council, Mr Khamis Mataka, secretary of the ujamaa council of Bakwata, Mr Hasan Chizenga, his deputy, Mr Abdushakur Omar and two other members, Messrs Suleiman Kilemile and Hamid Jongo. Giving a chronology of cases reported to the registrar at the ministry, Mr Florian Mushy, the deputy minister said the row at Bakwata resulted from a letter from seven complainants.

Relevant Links

East Africa
Religion
Tanzania
They had complained about the excessive power of Chief Sheikh Issa Shabaan Simba two years ago and subsequent futile attempts to change their constitution.
 
why say no? unaweza kuwakataza watu wasiabudu? Mahakama ya Kadhi ni sehemu ya ibada ya Waislamu...

kama ulisikiliza hotuba ya Dr. Mwakyembe
Issue hapa ni kwa nini hii mahakama iwe chini/ianzishwe ya serikali? Je waislamu hawawezi kuiendesha? mbona wakristu wanazo mahakama zao (kamati za kusuluhisha matatizo yao) hasa kanisa Katoliki ambalo lina mfumo huo mpaka ngazi ya mwisho pale Vatican?
Mahakama ya Kadhi ina umuhimu kwa waislamu ila ni mzigo mzito kwa Taifa changa ambalo hata bajeti yake ni finyu mno na kuna mambo mengi ya muhimu ya kuyashughulikia.
Mbona kumejengwa misikiti mingi sana humo barabarani, kumbe ingeweza kutumika busara hiyohiyo kutafuta funds kuendeshea hizi mahakama na serikali iombwe kusaidia tu.
Mawazo yangu tu, samahani kama nawakwaza watu
 
Inabidi Watanzania tumuombe sana Mungu ateupeshe na machafuko ambayo yanaweza kulikumba taifa letu kwa sababu ya mahakama hii. Shetani ashindwe na alegee kwa jina la YESU Kwa sie wakristo, sijui kwa wenzetu waislam wanakemea shetani kwa namna gani, nawaomba nao wamkee shetani ashindwe ktk mpango wake wa kutaka kutugawa kwa misingi ya kidini.
 
Waislamu punguzeni pumba

Mkombosi, Nadhani unatakiwa urudi kwanza umwambie MAMA yako akufundishe Lugha vizuri na hasa hii lugha ya kiswahili. Ni wewe ndie unatakiwa kupunguza pumba na uwache mambo yako ya KANISA KANISANI na uje na hoja na si .....................
 
Nyama Hatari,
Mkuu mbona huelewi nachozungumza...jaribu kusoma na kutafakari baina ya maneno...Hakuna aliyesema kwa mifano unayojaribu kuiweka hapa zaidi ya kutafuta kuweka tabaka za dini na yale kila dini iliyoyafanya. Hata hivyo jaribu kutafuta waasisi wa TAA ambao mbali na kuwa waislaam walikuwa wakiongozwa na chama gani?..

Mkuu kuwa muislaam sio hoja wala hii hoja ya mahakama ya Kadhi haihusiani na Uislaam against Ukikristu..HAPO NDIPO WENGI MNAPOKOSEA! ni hoja ya waislaam kwa waislaam! hivyo itazame kama ilivyo.

Mkuu kila mara unapojaribu kutafuta solution ya jambo lolote ni muhimu sana kutazama linawahusu WATU gani na ktk MAZINGIRA gani, lakini kibaya ni kwamba wewe na baadhi wengine mnajitazama nyie wenyewe wakati swala hili haliwahusu hata chembe...ndio maana kila mara nawaomba mtoke ndani ya sanduku mlitazame swala hili kwa fika huru kwa kuzingatia wale wanaohusika na mazingira walikuwepo.

Sasa kwa nini swala hili limefikishwa serikalini ni kwa sababu swala zima linatokana na serikali kushikiria uongozi wa chombo cha kiislaam yaani Bakwata. Ni Bakwata waliotakiwa kujitawala kama vyombo vingine vya dini nyingine hili hamtaki kulielewa..Na nimewapa mfanoo mzuri wa Umoja wa Wanawake - UWT ambao unatambuliwa na serikali na umepata baraka za serikali lakini hakuna mmoja wenu anayehoji hilo. Yapo maswala yaliyokuwa yakiwatatiza wanawake na yameweza kutungiwa sheria kitaifa na yapo ktk mahakama zetu..Ndivyo mimi najaribu kulitazama swala hili..Tofauti na KKK ama vyombo vingine Bakwata ni chombo kinachoendeshwa na serikali kwa ruzuku na kodi zetu sote ndizo zinakiendesha tofauti na KKK ama vyama vingine..WHY?..

Kisha basi Bakwata ni chombo ambacho hakikuwepo toka Uislaam uingie nchini, ni kitu kilichoundwa na Nyerere (mkristu) kuweza kuwa na control tofauti na KKK ama vyombo vinginevyol...Kwa hiyo usiseme kabisa kuwa Bakwata ni chombo cha waislaam kwa sababu hakitambuliki ktk Uislaam ama nje ya mipaka yetu..Lini chombo cha dini kikawa na sijui katibu Mtendaji, secretary na kadhalika mambo ambayo hayahusiani na dini.. Hii ni NGO kama Red cross tu...

Kwa hiyo Waislaam hawawezi kuanzisha korti ya Kadhi bila baraka za serikali kwa sababu kitakacho tumika hapa ni sheria na huwezi kutunga sheria zinazowahusu kundi la watu fulani tu hali kila yanayopiganiwa yapo ktk jamii nyinginezo. Wakristu pia wana wake zaidi ya mmoja, Mapagani vile vile, Wakristu wana tatizo la mirathi kwa watoto ambao wamezaliwa nje ya ndoa na waumini wa dini nyinginzo pia wana tatizo hili...Mume kaoa mke zaidi ya mmoja ni mila yetu hivyo ni muhimu sheria itungwe kuwasitiri watoto ambao wamezaliwa bila hatia kutokana na mfumo wa mila zetu ama U selfish wetu sisi wazazi...

Kwa hiyo tulitazame swala hili nje ya Uislaam pekee isipokuwa kwa ajili yetu sote.. Ndio maana napinga kuwepo kwa korti ya kadhi ambayo hadi sasa hivi haijaweza kusimamisha sheria..Hizo ndoa zenyewe za kiislaam zinafungwa kiholela hakuna anayefuata sheria, Mirathi yetu hao Wajomba bado wana sauti kuliko mke ama watoto iwe kwa waislaam ama wakristu..hakuna swala hata moja linlowahusu waislaam pekee kwa sababu hata Wakristu wa Bongo ni jina tu...Ndoa zetu zinafungwa kwa mseto utakuta Muislaam kaoa mkiristu, na vise versa vile vile utatoa hukumu vipi na utawagawanya vipi hawa watu...

Mwisho wa yote binafsi naamini kabisa kuwa Muislaam ni yule anayesimamisha nguzo tano za kiislaam, hawa ni wachache sana wengi wetu ni waislaam jina, tumezaliwa ktk Uislaam lakini tunafuata zaidi mila na desturi za Kiafrika kuliko Uislaam. Na kwa vile siku ya Kiyama kila mmoja wetu atabeba mzigo wake sioni haja kabisa ya kuwa na korti ya kadhi ambayo itashughulikia maswala ya mirathi na kuacha maswala makubwa zaidi yanayowezakumwondoa mtu ktk Uislaam.

Kifupi hoja ya kadhi haina nafasi kwa waislaam wenyewe..

hapa nimewatazama waislaam na mazingira waliyokuwepo sikuweka mimi ni muumini wa dini gani na napinga kwa sababu ya imani yangu laa hasha!.. tofauti na wengi humu wanachokitazama na kujiuliza ni ktk kusema We (Christians) don't..... THEM (Muslims) badala ya kusema ivi kweli mahakama ya kadhi itawasaidia nini waislaam! hukuna haja ya wewe kuwa Muislaam kuweza kuona athari za mahakama ya kadhi kwa waislaam kwani mahakama hii badala ya kuwahamasisha vijana kuipenda dini yao na kujivunia imani yao chombo hiki kinataka kuwahumu kabla hata sheria haijaweza kujengwa ktk jamii ya kiislaam.

Wakati huo huo kuna kila sababu ya Bakwata kuvunjwa kwa sababu haiwakilishi waislaam isipokuwa ni chombo cha serikali kinacho control waislaam. Bakwata ibakie kama Wold vision ama chombo kingene cha NGO chenye malengo ya kusaidia jumuiya ya Waislaam na sio baraza la waislaam.

Nina hakika kama waislaam watapewa uwezo wa kuchagua viongozi wao wenyewe kwa taratibu zao kama zamani tusinge fika huku... serikali ni lazima ijivue kabisa nje ya Bakwata na mimi hapa nitaendelea kumuunga mkono Marehemu Sheikh Kassim bin Jumaa katika jitihada zake za kuivunja Bakwata ambayo inaendeshwa na watu ambao kwanza hawaifahamu dini zaidi ya kuwa wanasiasa na wapiga ramri (bao)...
 
Waislamu punguzeni pumba

Hukufunzwa na mamayo jinsi ya kuishi kistaarabu, kuna haja gani ya kuwatukana wengine kwa ajili tu ya misingi ya kidini? nani mwengine ulioona kakutukana kwakuwa unadini tofauti? Ninawasiwasi hata na kiwango chako cha elimu au ufaulu wako kuwa ndio ule wa kutumia madesa. Walimwengu sasa tunakufundisha kuwa hoja hujibiwa kwa hoja na sio tusi. Yakupasa uwatake radhi watanganyika na wazanzibari kwa kauli yako hiyo mbovu. La sivyo tunamuomba webmaster akufungie maana wewe ni mtu hatali kwa ustawi wa jamii yetu hii tulivu.
Watch out!!!!!!!!
 
Kitu chs msingi ni kuzitenga mahakama za kadhi na serikali. Hakuna sababu ya kupeleka dini kwa kaisari maana imeandikwa ya Mungu mpe Mungu, na ya Kaisari mpe Kaisari.

Je, uislamu ni Kaisari?
 
Mzee mwanakijiji, naona kama umeruka hatua moja!!!!

Ingependeza ungeanza na jinsi ya mahakama ya kadhi itakavyofanya kazi TZ. Si vibaya ungetupa na mifano michache kwa jirani zetu kama Kenya, Mozambique, Uganda n.K. Yawezekana Wanaotetea Mahakama ya Kadhi, wanatoa hoja ya kuwepo mahakama ya kadhi ktk nnji hizo kama jibu kwa wanaopinga kwa hoja kuwa Mahakama ya kadhi itagawa wanannji na kuleta vurugu!! Pengine wao wanauliza mbona huko hamna vurugu???

Mzee mwanakijiji pengine pia ktk makala yako inayoendelea yafaa utafiti kipi kilichofanya mahakama ya kadhi ifutwe TZ baada ya ukoloni. Pengine ktk hili wanaotetea kuwepo mahakama ya kadhi pia wanahoji vipi ukoloni uliruhusu waTZ wenyewe wafute?? Mbona Ubote, Kenyata, Samora hawakufanya kama alivyofanya Nyerere kufutilia mbali mahakama hiyo?? pengine kwa kuonyesha hasara/matatizo waliyopata hao jirani zetu kwa kuendeleza mahakama za kadhi inaweza kuonyesha sasa tunapata hoja zenye nguvu! Vinginevyo itakuwa tunapoteza muda, kwani hatutakuwa na tofauti na waliotoa hoja za kutetea mahakama hiyo.

Kuhusu ahadi ktk ilani ya uchaguzi ya CCM, mzee umeliweka sawa!!
Kama waislamu wanafikiri wamepigwa changa la macho basi kazi kwao 2010.

Mzee mwanakijiji, nimekuwa mfuatiliaji mzuri sana wa hoja zako. Nyingi kama si zote ziko ktk msitari. Naamini hii pia iko katika usawa. Umeianza vizuri! Naomba uiweke vizuri zaidi kwa kuimalizia kwa Kuelezea hoja za wanaopinga kama zina nguvu au la!! Kwa hili ni vizuri hata kama utahitimisha kwa kuonesha madhara yatakayotupata kwa kurejeshwa mahakama ya kadhi. Wanaotoa hoja kuwa zitaleta uhasama kati ya waislamu na wakristo, kuwa ni kosa kutumia pesa za walipa kodi kunufaisha kundi la jamii fulani nk hawajanishawishi kuona kuwa hoja zao zina nguvu. Bado naona kama ni ushabiki wa kidini tu!!!

Mwisho, nami nihitimishe kama mzee ulivyoanza kuwa ni vizuri tulijadili suala hili tukijua kuwa ni kwa faida yetu kama matokeo ya mjadala yatakuwa mazuri kama itakavyokuwa hasara kwetu tukiboronga!! Tukizingatia hilo ndio tutaishia kuwa wamoja mwisho wa mjadala badala ya kugawanyika kati ya wanaotaka na wasiotaka Mahakama ya kadhi.


uhuru wa kweli, amani ya kweli na haki ya kweli tutajiletea waTZ wenyewe.

Mzee mzima katika wachangiaji walionigusa nathani ww ni mmoja wao.... keep it up
 
Huenda Nyerere alikuwa na sababu binafsi ambazo wenzetu kila siku wanazipigia kelele... UKATOLIKI WAKE!!!
 
i like you signature,surely result may vary..!
Hv unaishi Tanzania au uko nnje?
Ni nacho ona mimi hapa kwenye hili swala la miadhara unakosea au unatoka nnje ya HOJA au labda ndio unavyo jenga HOJA yako ya kukataa Hii mahakama.
For you information hata wakristo wanavyo vikundi vyao vya miadhara na hii imekua hivyo kwa muda sasa hapa Bongo,sasa sijui nani anamtukana mwenzie na wote wanatumia hivyo vipaza sauti na kutukana (kama hivyo ndivyo what you see) na maisha yanaendelea na sijasikia kwamba muhadhara wa waisilamu wametoka wakaenda kwa wakristo wakashikana mashati.

Kwa kusema ukweli, wakristo wanaotumia mihadhara kukashifu uislamu mara nyingi ni wale wanao'react' kwa kashfa zilizotolewa kwao. Wengine wanaamua tu kukaa kimya kwa vile wanaona upuuzi wa namna hiyo hauwapeleki kokote.

Mimi nilifiwa na mke wangu hapa Dar, lakini watu walipoenda kwa baadhi ya waislamu jirani kuazima mikeka waliambiwa mikeka yao haiazimishwi kwa makafiri. Lakini watu walewale wakija kuomba mchango kwa ajili ya sherehe za watoto wanaosoma madrasa nawachangia.

Ni tofauti kama hizi hizi na hasa kuwaita wengine makafiri ndiyo kunakoleta mafarakano. Wayahudi na Wakristo, Mtume Mohamad hakuwaita makafiri. Iweje, leo wafuasi wa Mohamed wawaite hawa kama makafiri?

Ila mimi najua wale wanaokashifu dini za wenzao bado imani yao ni haba - ni wachanga kiimani na hawajui watendalo.
 
Leo najitumbukiza kwenye mjadala wa mahakama ya Kadhi kwa lengo la kuwawekea wazi nini Mahakama ya Kadhi na Hoja ya kuwepokwake nchini Tanzania.

Sijambo la kushangaza kwa watu kupinga Mahakama hiyo iwapo mtazamo tulionao ni kuwa hii itakuwa ni mahakama ya kuhukumu kesi Kiislamu na hivyo kukatana mikono na vichwa. La hasha, maana ya mahakama ya kazi hapa ni kufatilia maamuzi yahusuyo Ndowa na Urithi.

Si kweli kuwa kinachotakiwa hapa kuweko mahakama kama mahakama nyengine zinazoongozwa na sheria zilizotungwa na Bunge.
Hoja ya kuwepo mahakama hiyo inakuja kutokana na kuwajibika kwa Waislamu kufuata walioamrishwa kufanya kuhusiana na Ndoa na Urathi. Waislamu hawana choice kwa hili kwani msingi wa dini yao unasema hivyo. Kuwanyima kile ambacho kitawapa nafuu kwa safari ya baadae ambayo sote mbali na tofauti zetu tunakiamini haitokuwa sahihi.
Ndani ya mahakama zetu tunaamini baadhi ya sheria za Kiislamu lakini mahakimu huwa hawaelewi sheria hizo na misingi yake. Kuondowa tatizo hilo ni kuundwa mahakama za kadhi zitakazoendeshwa na wajuzi wa sheria hizo.
Msururu wa hoja uliotolew kama ni hoja dhaifu za kuundwa kwa Mahakama hiyo sio hoja halisi za kuwepo kwa mahakama hiyo bali nionavyo mimi hoja hizo zinaletwa na Waislamu ili kuonyesha kuwa kuwepo kwa mahakama hiyo hakuna madhara kama Watanzania wengi wanavyofikiri.
Watanzania ni watu wanaoamini Mungu na ni watekelezaji wa maamrisho ya dini zao, hivyo tuwape Waislamu nafasi ya kutekeleza maamrisho ya dini yao.
 
Back
Top Bottom