Jamani jana usiku kwa bahati usingizi uliinishia nikaamua kuwasha Tv, bahati nzuri sijui mbaya nikakuta documentary Iliyokuwa inahusu suala la nyuklia la Iran.Amabalo liliongelewa kwa takribani 1hr.
Mmoja wa waliohusika katika mahojiano hayo ni aliyekuwa anapokea pesa za Mr Khan,Khan mwenyewe na wawili toka Iran kati ya waliotumwa na Yatola kutafuta hiyo technojia.Mtu wa Khan alikuwa ni Mwindonesia.Madili yote yalifanyikia Dubai,baada ya vita kati ya Iraq na Iran ambayo inasemekana raia na askari wengi wa Iran waliuawa na hivyo Yatola akamua Iran itafute ultimate weapon(Nyuklia bom).Baada ya kuhangaika kutafuta ndipo Dr. Khan akajitokeza na kuwaelekeza kwenda Dubai ambako alikuwa tayari amefungua ofisi iliyokuwa inaendeashwa na huyo kijna wa Indonesia.Yeye hakwenda kwa kuwa CIA walikuwa wanamfuatia.Walipewa dili kwa kulipa Dola 8 milion.wakapewa tech hiyo ila wakapigwa mzinga kwenye vifaa,vilikuwa vimechoka.Hivyo dili lilibidi lifungwe kwa mara ingine baada ya Khan kuwatengenezea vifaa vipya na wakatoa Dola 32mil.Baada ya pesa kuwa tam Khan akauza tech hiyo North Korea na Libya.Ila mtu wa kwanza kuuziwa alikuwa Sadam kabla ya Iran.