Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

vatican ni nchi na uislamu ni dini, hao wanakiti mpaka Umoja wa Mataifa , kama iliyo kwa nchi kama Afaganistani na Nchi zote zinazofuta utawala wa kiislamu, na kwa taarifa yako hizo ni nyingi sana
kwa haraka haraka ni
  1. Afganistani
  2. Iran
  3. Mauritanian
  4. Pakistan
hizo zinajulikana kama islamic state
mkuu hata udini na kama unataka kuendekeza udini basi tumia source za kuaminika.
na kama VATICAN ni Tatizo basi hizo nchi NNE za kiislamu ni tatizo tuvunje ubalozi nao pia

source wikipedia hapo chini

An Islamic state is a state that has adopted Islam as its state religion, and more specifically Islamic law as the foundations for political institutions, or laws, exclusively.
The concept is related to the notion of dar al-islam (Arabic دار الإسلام) the "domain of Islam", defined (by the prevailing opinion) as the domain in which:
  1. All the laws governing the area have their roots in islamic jurisprudence.
  2. The security al-amaanah (Arabic الأمانة) is in the hands of Muslims.
Islamic republic is the official name given to several contemporary states in the Muslim world, including the Islamic Republics of Pakistan, Iran, Afghanistan, and Mauritania. Pakistan adopted the title under the constitution of 1956. Mauritania adopted it on 28 November 1958. Iran adopted it after the 1979 Islamic Revolution that overthrew the Pahlavi dynasty. Afghanistan adopted it after the 2001 overthrow of the Taliban. Despite the similar name the countries differ greatly in their governments and laws.
Pan-Islamism is a form of religious nationalism within political Islam which advocates the unification of the Muslim world under a single Islamic state, often described as a caliphate


@VIKWAZO spot-on. Haya majungu ya Alnuur yamefikiwa viwango vya chini mno na niseme ni kama kuwachafulia jina waislam waonekane kama mbumbumbu jambo ambalo si kweli. Haiwezekani mtu achukue kalamu aandake hivi bila kujua kwamba VATICAN is a state! Na kwa kuongeza, nchi kama Saudi Arabia ni Islamic state na Tanzania ina mahusiano mazuri tu ya ki-diplomasia. So why is it ok for Saudia and not for Vatican?

Binafsi nimekuwa nafikiria sana kuhusu hata qualifications za viongozi wa kiislam. Nadhani pamoja na kujua aya za vitabu basi kuwepo na minimum qualifications ya elimu dunia. Mfano kwa sheikh ngazi za wilaya lazima walau afike form VI, Mkoa lazima Advanced diploma. Na kwa mufti mkuu basi walau degree moja. Hii itasaidia sana kung'amua mambo. na pia inampa kiongozi husika 'moral authority' ya kusema waislam wajiendeleze. Jamani tupunguze halua na kashata wenzetu wanaenda mwenzini sisi tunashindwa hata kujua Vatican ni State!
 
hii mahakama ya kadhi ni haki ya waislam kama ulivyo ubalozi wa vatican ni haki wa wakiristo


Malaria Sugu, Wakatoliki wanayo mahama yao ndani ya mfumo wao wa kanisa Kataloki. Imekuwepo kwa muda mrefu na haujasikia malumbano hata siku moja toka kwa wakatoliki wakidai mahakama yao hiyo iingizwe kwenye katiba. Kama nchi tuna sheria moja tu - Tanzanian law inayomlinda mtanzani mcha mungu, mtema mate, mchinja kuku n.k. ONE LAW. So hizi 'domestic arrangement' zinaweza kuwepo kama ambavyo wakatoliki wamefanya ili mradi hazikinzani na sheria za nchi.

Kwenye red - Vatican ni State kama ilivyo Saudi Arabia, Pakistan, Iran, Yemen n.k. Makahama ya kadhi ni mfumo wa kusimamia sheria/kutoa haki kupitia imani ya ki-islam . Narudia, Vatican ni State, Makahakama ya kadhi ni mfumo wa usimamizi wa sheria kwa misingi ya imani.
Tanzania haingozwi na sheria za Vatican au Saudia au Iran. Tunayo katiba yenye cover rangi ya purple na imeandikwa 'Katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania'

Kama tunaongelea usawa basi VATICAN iko Tanzania kama ambavyo Saudia, Iran, Yemeni wapo. Niliwahi kusema huko nyuma kwamba hili jukwaa mara nyingine tunajidhalilisha sana kama nchi. Inakuwaje mtu analingalisha Mahakama na State? aibu!
 
Vatican si nchi ni Taasisi na ndio maana haitambuliki hata kwenye international laws na UN kama maaskofu hawaitaki mahakama ya kadhi na waislamu hawaitaki vatican.

umeitoa wapi hiyo au unatunga kwa kujifulaisha soma hapa kuhusu VATICAN kutambuliwa katika international Laws na UN vatican wana balozi wa kudumu

source wikipedia
Vatican the central governing body of the Catholic Church and sovereign entity recognized by international law, consisting of the Pope and the Roman Curia. The Vatican can also be referred to as "The Holy City".

Vatican City State, in Italian officially Stato della Città del Vaticano , which translates as State of the Vatican City, is a landlocked sovereign city-state whose territory consists of a walled enclave within the city of Rome, Italy. It has an area of approximately 44 hectares (110 acres), and a population of just over 800.
Vatican City was established in 1929 by the Lateran Treaty, signed by Cardinal Secretary of State Pietro Gasparri, on behalf of the Holy See and by Prime Minister Benito Mussolini on behalf of the Kingdom of Italy. Vatican City State is distinct from the Holy See, which dates back to early Christianity and is the main episcopal see of 1.2 billion Latin and Eastern Catholic adherents around the globe. Ordinances of Vatican City are published in Italian; official documents of the Holy See are issued mainly in Latin. The two entities even have distinct passports: the Holy See, not being a country, issues only diplomatic and service passports; Vatican City State issues normal passports. Very few passports are issued by either authority.
 
hapa ndipo wapinga ufisadi wanapowaunga mkono ccm

Hawa c ndio wanaompinga Msekwa na Ccm yake? Leo wana msaport kwa sababu kazungumzia udini kama walivyo wao? Sasa nimewafaham hawa watu kwa uelewa mpana! Nilidhani wangeendelea kumpinga kwa kuwa mada imetoka kwa ccm!
Kwa hiyo kama Vatican kuna muislam kwa mfano, anawakilishwa na rais papa pia? Ama Lutheran etc......
 
Vatican si nchi ni Taasisi na ndio maana haitambuliki hata kwenye international laws na UN kama maaskofu hawaitaki mahakama ya kadhi na waislamu hawaitaki vatican.


National embarassment nyingine tena. Mdondoaji angalia list ya nchi zenye viti Umoja wa Mataifa ndio utajua hii point yako kwa kiasi kikubwa inatulidhilisha watanzania wote.

Kuondoka kwa ubalozi wa Vatican wala isikupe shida. Lakini kumbuka usirushe mawe kama uko ndani ya nyuma ya glass! Ubalozi wa Vatican ukifutwa Tanzania tafsiri ni kwamba umefutwa kwa sababu unawakilisha nchi inayoongozwa kwa kanuni/sheria za imani fulani in this case - Catholism. Now, the very same prescription itatolewa kwa balozi zote hapa nchini zinawakilisha nchi zenye kuongozwa na kanunu/sheria za imani. Let's start; Iran, Pakistan, Saudi Arabia, Yewen, Kuwait, Sultan on oman, etc etc.

On practicle level, halua na zile annual deliveries za nyama zitapotea! and worse, masjid lukuki zitaguaka kuwa something you never thought of. I dare you make to make good on your threat!
 
Duh umealisha kama bata, umeweka nini humo kichwani?
Kwanza wewe dini hahahahahaahahahaha

Hawa c ndio wanaompinga Msekwa na Ccm yake? Leo wana msaport kwa sababu kazungumzia udini kama walivyo wao? Sasa nimewafaham hawa watu kwa uelewa mpana! Nilidhani wangeendelea kumpinga kwa kuwa mada imetoka kwa ccm!
Kwa hiyo kama Vatican kuna muislam kwa mfano, anawakilishwa na rais papa pia? Ama Lutheran etc......
 
Katika majibu yake kwa malalamiko hayo Rais alisema kuhusiana na Tanzania kujiunga na OIC, serikali yake inazingatia kwanza maoni ya Wakristo kabla ya kuamua ijiunge au isijiunge na jumuiya hiyo.

Swali langu moja tu: Je waislam sio rai halali wa nchi hii? Mbona wao maoni yao haya zingatiwi?
 
the-borgias-showtime-poster-550x739.jpg
 
Haya ndio manufaa ya demokrasia kwamba kila Mtanzania ananafasi ya kuchukua mic na kuongea mawazo yake hata kama mengine ni pointless. Kikwete na kundi lake sasa wanaona ni wakati wa kwamba wanaonewa na yeye kuiba kura pia sio human right violations sio? Hizi discussions za kujiunga na OIC tumezisikia tangu tulipokuwa wadogo na hasa hizi za mahakama za kadhi kwani hizi mahakama za serikali ya ccm kumbe hazifanyi kazi. Kama hizi mahakama za ccm na serikali yake hazifanyi kazi kwanini kikwete awabadilishie ili justice system ibadilike? Kama wakristo wakitaka mahakama zao si itakuwa moja zaidi. Nina maswali kwa huyu mwandika thread, hizi mahakama za kadhi kwa kuwaadhibu waislamu kwa makosa gani ambayo mahakama za serikali zinashindwa? Mkristo au asie na dini yeyote akimfanyia kosa mwislamu, ataadhibiwa na mahakama ipi? Sijui hawa jamaa wataelimika na kuheshimu lini maana ya kuwa Watanzania kwanza badala ya kuwa wazalendo na nchi za kiarabu? Wazi kinachowasumbua sio solutions za uchumi, elimu wala umaskini kwa Watanzania wote, ni sera za ubaguzi na udini? Watanzania wengi wameshawaona hawa ni wasanii kama jk na wananchi wanajua nia yao ni kuleta mihadhara na kuchafua Utanzania thats it. Waislamu wengi wameshawagundua trick zenu...Siwasikii mashehe na hawa maradicals wakizungumzia wizi wa mafisadi na Umuhimu wa Constitution na watabaki hivyo hivyo na umaskini wao...

The study of the United States Bureau of Democracy, Human Rights, and Labor for 2009 suggests that 62% of the population of Tanzania is Christian, 35% is Muslim, and 3% are members of other religious groups.[2]
Ninety-seven percent of the population on the Zanzibar archipelago is Muslim. On the mainland, Muslim communities are concentrated in coastal areas, with some large Muslim minorities also in inland urban areas.[1] Between 80 and 90 percent of the country's Muslim population is Sunni; the remainder consists of several Shi'a subgroups, mostly of Asian descent.[1]
The Christian population is composed of Roman Catholics, Protestants, Pentecostals, New Apostolic Christians, Seventh-day Adventists, members of the Church of Jesus Christ of Latter-day Saints (Mormons), and members of Jehovah's Witnesses.
Religion in Tanzania - Wikipedia, the free encyclopedia
 
Wakuu zangu, nadhani tunapozungumzia maswala yanayoihusu nchi yetu sii vizuri kufanya dhihaka na imani za watu. Hoja hujibiwa kwa hoja na sii kutafuta sababu nje ya hoja iliyopo ili mradi kutukana au kukejeri imani ya watu. Fanyeni heshima na kumbukeni tu kwamba sababu zote ulizokuwanazo wewe kutokuwa dini nyingine, mwenzako pia ana sababu zake kutokluwa dini yako...
Na hasa kwa ndugu zangu Waislaam nitawakumbusha kwamba Kuran inatufundisha kwamba mtume alifuatwa na MAKAFIR, sii wakristu wala Wayahudi - ila Makafir wakimtaka awafuate, hakufanya hasira wala kejeri na hawa ni makafir bali aliwaambia nini? -

Surah 109 - Al-Kafirun..
Say: Oh you nonbelievers..I do not worship what you worship, nor do you worship what I worship.
And I will not worship what you worship, Nor will you worship what I worship.
Your way is yours, and my way is mine..

Kwisha ubishi, lakini nashangaa leo nyie mnakiuka hata mafundisho ya kuran na kuanza kumtumikia sheitwan kwa malumbano ambayo hayakusaidii lolote wala kuusaidia Umma.

Nanyi ndugu zangu Wakristu, jaribuni kuwa wasikivu kidogo tu, hoja iliyopo ubaoni haihusiani na Vatican kama nchi kwa sababu tunajua Vatican ni nchi lakini balozi wenu anatumikia falme mbili..mbali na nchi ya Vatican pia ni mwakilishi wa The Holy see, hii ndio inawapa taabu waislaam...Leo hii mimi na wewe hatufahamu kama Kardinal Pengo analitumikia taifa letu Tanzania, Vatican au Holy see na bila shaka akiulizwa nadhani jibu lake ni rahisi sana - Holy see comes first..

Sasa kama yeye ni balozi wa Holly see na tunayaona matunda ya uwakilishi wake iweje shida na taabu kwenu kuwakubalia OIC ili kuwawezesha Waislaam kama kanisa linavyowawezesha Wakristu? Na hatuhitaji kubishana juu ya hili kwani sisi sote tumeona mafanikio makubwa ya kanisa na mara kibao mnajisifia sana kwa kuwezeshwa na kanisa inapokuwa swala la kulinganisha Waislaam na Wakristu.. halafu ajabu tena mnakuja kataa Waislaam kuwezeshwa ili mradi tu wasipate huduma kama zenu, Wasiwe sawa nanyi, Hii kweli imekaa sawa jamani au tunazungumza kwa ushabiki na chuki ya kiroho!
 
Hivi mahakama ya kadhi na ubalozi wa vatkani vinauhusiano wowote? ni vitu viwili tofauti kabisa. Mahakama ya kadhi ni mahakama ya kiislamu ambayo inasikiliza kesi kwa kutumia sheria za kiislamu na kuhukumu, na inataka kutumia fedha za serikali ambayo haina dini kujiendesha. Ubalozi wa Vatcan ni ubalozi kama ubalozi wowote wa nchi za nje zilizopo nchini, unajiendesha wenyewe kwa kutumia fedha za vatkani sio za serikali ya tanzania. Vatcan kimuundo wa Rome ni nchi, sasa kama wao wameamua kuweka ubalozi wao tz siye kama tz tunahasara gani? wanatumia fedha zetu? hapana, sasa shida ipo wapi? ule ni ubalozi tu kama ubalozi wa Iran, Libya, Morocco, Algeria nk za nchi za kiislamu zilizopo nchini. Kwa hiyo kama shida ni dini basi na balozi hizo za kiislam nazo ziondoke, kama hoja ni dini. Mahakama ya kadhi imesharuhusiwa Tanzania ila waislam wenyewe ndio hawataki kuianzisha, mmeshaambiwa kwa kuwa hiyo mahakama ni moja ya imani zenu muhimu za kiislam IANZISHENI NA KUIENDESHA KWA GHARAMA ZENU nyie hamtaki. Serikali haina dini, na fedha za serikali ni za watz wote, ambao ni waislam, wakristu na wapagani, sasa iweje serikali hiyo ya mseto ianze kutumia fedha za mseto kwa ajili ya sehemu ndogo ya mseto huo? Nyie anzisheni na kuigharamia mahakama ya kadhi, nyie wenyewe wala hakuna anayewazuia, tatizo lipo kwenu wenyewe gharama ya imani yenu kutaka kututwisha watz wote, kila muumini na abebe gharama za imani yake. Nje ya hapo nyie wenyewe ndio mjilaumu sio kulalamikia serikali wala vatican, vatican hawatumii bajeti ya serikali ya tz, wangekuwa wanatumia fedha zetu hiyo ingekuwa hoja. Commonwealth ni international organization, na wala hatuna hasara nayo kwa kuwa haitumii fedha zetu kujiendesha na mkuu wake kwamba anadini yake nayo siyo hoja kwa kuwa commonwealth siyo umoja wa kidini, ungekuwa ni umoja wa kidini ingeweza kuwa hoja.Leteni hoja za maana zijadiliwe siyo hizi hoja za kipuuzi za kidini, hoja za kidini ni za kipuuzi tu kwa kuwa imani ni suala binafsi, na unapaswa ulipie mwenywewe gharama za imani yako, kama hauwezi chagua kuwa mpagani hata hivyo nako kuna gharama yake.
 
Tatizo ni ufinyu wa mang'amuzi na elimu duni ikichangiwa na udini. Ubalozi wa Vatican kuwepo nchini ni kinyume cha katiba ipi? Kifungu gani? Waislamu wamedhulumiwa kwa muda mrefu na nani? Ni nani aliyetaifisha mashule yote ya kanisa na kuruhusu wananchi wote wasome bila ubaguzi kama sio Nyerere?

Inasikitisha! Hoja hii kama si ya mtu mshirikina iliyojaa harufu ya damu za watu, basi ni ya mtu mwendawezazimu aliyepagawa na pepo!
 
Vatican city is a country jaribuni hata ku-google kabla ya kupinga kila kitu hapa
Google wewe, bila Holy see hakuna nchi inayoitwa Vatican City, kifupi huwezi kuzitenganisha kwani hata rais wake yuko chini ya Papa. vatican kuna aina mbili ya mabalozi wapo wanaowakilisha nchi pekee na wapo wanaowakilisha nchi na Holy see, balozi wao Tanzania anawakilisha vyote.

Na tunabisha kitu gani haswa? ikiwa sisi wote tumeona jinsi Vatican ilivyoweza kuwasaidia Wakristu na hata mnajisifia kwa elimu, iweje iwe taabu sana kusikia kuna chombo cha Waislaam kinachotaka kuwasaidia kama nyie mnavyojivunia? au nchi yetu ina dini moja..Na kwa jinsi mnavyopinga yaonyesha wazi kuna jambo hapa hatulijui sisi tunaotazama sarufi kwa pande zote mbili..Yapo mabenki ya kikiristu lakini mkisikia ya Kiislaam haiwezekani hii sio nchi ya kiislaam..

Na hulka ya kibinadamu inatuumbua sote.. Jaribu kufikiria wewe mwenyewe ama fanya utafiti wako binafsi. Ni watoto wangapi wa Kikristu hujisikia huru studing at Muslim schools or Muslims at Catholic schools?.. ukweli ni kwamba kati ya 10 only few and could be none lakini kwa sababu hawana jinsi watasoma shule zinazoongozwa na dini nyingine.

Kama kweli nchi yetu haina dini basi shule, Hospital na huduma zote za kijamii zisiwe za kidini bali liwe ni jukumu la serikali iliyopo madarakani hapa tutaondoa matatizo mengi ya kidini ndani ya serikali, lakini kama dini zitaingilia kazi na huduma za serikali tutasemaje kwamba nchi yetu haina dini wakati dini ndizo zinatoa huduma?
 
SINDBAD, naomba unisaidie katika suala hili la kadhi.
1. Kwani hamuwezi kuweka hao makadhi bila ya bunge kuidhinisha?????
2.Hiyo mahakama ya kadhi itatoa adhabu gani?? na je kuna magereza ya Kadhi yatakayoanzishwa????

Wasiwasi wetu ni kuwa mahakama hizo ndio mwanzo wa kuwa na taifa la kiislamu ambalo sharia za kukata watu mikono zitakuwa ninatawala.
Usichokijua ni sawa na usiku wa kiza.. mkuu ni bora uliza ufahamishwe kuliko kutunga maneno ambayo hayahusiani kabisa na mahakama ya kadhi..

Labda nirudie tena kusema kwamba mimi napinga Mahakama ya kadhi na naipinga kama Muislaam..Kwa nini naipinga mahakama ya kadhi.. nilikwisha sema sana wala sii mara moja wala mbili..
Waislaam hawatakiwi kuchukua sheria moja na kuacha sheria nyinginezo kwa sababu ya mapenzi yao. Kesi nyingi zimetolewa maamuzi kinyume cha dini kwa sababu waislaam wenyewe wamefunga ndoa kinyume au wamezaa nje ya ndoa kinyume jambo ambalo kisheria hizi ndoa zisingetambulika na pengine hata wahusika kuawa kwa sheria za jinai.

Hivyo hatuwezi kuacha sheria za jinai ili mradi kurukia sheria za kijamii kuondoa makali ya sheria za dini.. Uislaam haupo kumfurahisha Kadhi wala Sheikh mkuu bali kama tunafuata sheria basi sheria zote zifuatwe na kama haiwezekani basi tutahukumiwa huko mbele ya safari kwani kila mtu atabeba msalaba wake..Na kama yupo Muislaam yeyote anataka malumbano ktk hili anijulishe na tujadili kwa kufuata dini na maamrisho yake.
 
Umenipa RAHA sana! we now see your true colors! hapa hampumui wala hamchomoi, tunakaba mpaka PENALT!!

kuna ukwl kwy madai yako bt u'v gone so far,dn insult dini dat much,kila k2 kilikuwa poor enzi izo ulitaka wa2mie toilet paper?thk logical,it shows u dn believ even presence of God
 
Waislamu wanajua kuwa hata leo wakitaka wenyewe wanaweza kuanzisha mahakama ya kadhi bila kibali cha serikali. Lakini hawataki kufanya hivyo! Baadala yake wanaishinikiza serikali ifanye hivyo kwa niaba yao kwa kuwa wanataka gharama za uendeshaji wa mahakama hiyo utokane na kodi za wananchi.

Hii si halali hata kidogo kwa sababu tatu: Kwanza si haki kutumia kodi za wananchi wengine wasio waislamu kwa ajili ya kuendesha mahakama ya kiislamu. Pili Kikatiba tulikwishakubaliana kwamba kila mtu ashike dini yake, lakini serikali yetu isiwe na dini. Tatu, serikali tayari inazo mahakama zake za kiraia na wakati wowote waziri wa sheria na katiba hajasikika akisema kuwa mahakama hizo zina mapungufu ya kisheria.

Suala la mahakama ya kadhi liko wazi kimaamuzi lakini linaendekezwa tu kwa masilahi ya kisiasa, ambapo ni hatari kwa mustakabali wa taifa. Hivi basi, kwa sababu hizo za wazi, waziri wa Sheria na katiba achague uamuzi mmoja kati ya maamuzi haya matatu. Aidha ajitokeze hadharani na majibu kuwa suala la mahakama ya kadhi haliko chini ya maamuzi ya bunge; au ajiuzuru; au awaeleze wananchi kigugumizi chake katika kutoa maamuzi yaliyo wazi kinatokana na nini.
 
Katika majibu yake kwa malalamiko hayo Rais alisema kuhusiana na Tanzania kujiunga na OIC, serikali yake inazingatia kwanza maoni ya Wakristo kabla ya kuamua ijiunge au isijiunge na jumuiya hiyo.

Swali langu moja tu: Je waislam sio rai halali wa nchi hii? Mbona wao maoni yao haya zingatiwi?

Kuondoa mzizi wa fitina BAKWATA wajiunge na OIC ili wapate zile "fedha za shetani!" Alternatively, kama OIC wana nia ya dhati ya kuisaidia Tanzania waisaidie kwa kuipatia hizo "fedha za shetani" bila kujiunga nayo!
 
Siyo mahakama ya kadhi tu mimi nataka hata SHARIAH ije bongo ila itumike kwa waislam tu.
Tutaona lundo la vijana wakiikana dini yao, kuikimbia hii mahakama.
 
Back
Top Bottom