Don't forget this is tanzania and never Msumbiji or Uganda!
Watanzania tuna madudu ya kuyaogopa kama Nguvu za Kidikteta ambazo kapewa Rais na katiba iliyopo, rushwa iliyokubuhu, ufisadi lakini sio OIC au mahkama ya kadhi.
Kama Msumbiji , Uganda wamejiunga OIC na mpaka leo hawajaona sababu ya kujitoa ni vyema kujifunza au at least kutafuta habari kutoka kwao kwa nini walijiunga na wananufaika vipi kuwa wanachama na athari zipi zimewapata.
La kadhi Court, Kenya zipo, na hapa Tanzania zipo, Ndio Zipo Zanzibar! na tunataka nchi moja serikali moja , kwa hiyo tutawaondolea kadhi court kama hili la nchi moja ,serikali moja litatendeka? Zanzibar pia walijiunga OIC lakini walitakiwa wajitoe kwa kisingizio kuwa TZ itajiunga.
Sasa wakuu tusikurupuke tu kwa hofu bila kudadisi mambo na kujiridhisha kuwa haya mambo yatakuwa na athari kwetu. Ni nini hasa tunachokiogopa? Ni kwa sababu sisi sio katika kundi linalodai au kufurahia kuwa wanachama wa OIC au kuwa na kadhi courts? au ni nini hasa?
Mbona tunakuwa ni watu wa misimamo mikali? wakifaidika wao, tumefaidika na sisi.
Huu ukinzani tunaouonesha kwa kundi hili ndio unaowajengea misimamo mikali na kujenga chuki za kipuuzi na ndio utakaozaa msuguano na malumbano yasiyo na tija.
Tujielimishe, tuone ni athari zipi zitapatikana kama tutakuwa na mambo hayo mawili hapa TZ halafu tuorodheshe hizo athari na tuseme hizi ndizo sababu zetu sisi wa kundi hili tunapinga haya mambo.
Kazi hiyo inaweza hata kufanywa na Kamati ya bunge na kuianika ripoti yake kwa umma.