Julius Mtatiro kushitakiwa kwa uchochezi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Julius Mtatiro kushitakiwa kwa uchochezi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Nov 17, 2008.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Nov 17, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Vyanzo vyangu ndani ya jeshi la Polisi vinaninong'oneza kuwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa TAHLISO Bw. Julius Mtatiro anashikiliwa na Polisi kwa madai ya kuhusika na mgomo wa wanafunzi wa elimu ya juu. Bw. Mtatiro (kwa mujibu wa vyanzo hivyo) amekuwa akihojiwa bila ya kuruhusiwa mwanasheria wake kuwepo na kwa muda wa zaidi ya masaa 24. Tangu jana ambako ka nzi kamekuwa kakifuatilia Bw. Mtatiro amekuwa akihamishwa kutoka kituo kimoja cha POlisi na hatimaye kurundikwa pale Msimbazi ambako Polisi wamekataa mtu yeyote kumuona..

  Licha ya kumhoji inadaiwa mbinu za "kulazimisha" zimekuwa zikitumika dhidi yake..

  Kama kuna Mwanasheria yeyote natoa wito ajaribu kufika Mzimbazi ili kumwakilisha kwani inaonekana kwa mara nyingine tena kijana huyo anajikuta yuko matatani hasa baada ya serikali pia kumnyima nafasi ya kuwa Mwalimu baada ya kukataa kumpatia kazi licha ya qualifications zote alizonazo na baada ya kuambiwa kuwa hatopatiwa kazi mahali popote Tanzania...

  Free Julius Mtatiro NOW!! and Stop the Harrassment!
   
  Last edited by a moderator: Nov 19, 2008
 2. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #2
  Nov 17, 2008
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Ohooooooo! Mauji ya kisirsiri yanataka kuanza tena; nakumbuka miaka ya 1990 wakati wa Mzee Punch na migomo pale UDSM aliyekuwa Rais wa DARUSO somebody Matiku vyombo ya dola vilimfanyia hivyohivyo na baada ya kufukuzwa Chuo haikupita muda mrefu tulisikia kuwa amekufa kwa kujinyonga huko kwao Mara. God forbid yasijirudie hayo.

  Sasa kule DUCE na Mkwawa nao watakamatwa? Kainzi hakajatua huko?
   
 3. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #3
  Nov 17, 2008
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Naomba anayefahamu walipo vijana hawa, Katibu Mkuu wa Umoja wa marais wa Taasisi za Elimu ya Juu nchini (TAHLISO), Mtatiro Julius na Odwang Odong.

  Kuna taarifa kwamba wamekamatwa na wanausalama tokea Jumamosi na hawajulikani wako katika kituo gani ama kama wako salama, yeyote anayejua usalama wao aseme.
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Nov 17, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  hhahaha Halisi naona tumegongana kwenye hii taarifa....
   
 5. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #5
  Nov 17, 2008
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  naona kuingika wewe tu bas

  na thread iliyokuwa inakuhusu umeamaua kuihamisha

  makubwa haya
   
 6. a

  akili Member

  #6
  Nov 17, 2008
  Joined: May 5, 2008
  Messages: 68
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  HATUSHANGAI kwani mlipowapigia debe hawa jamaa, nyie waandishi wa habari ukiwemo wewe mwanakijiji hamkujua wanaolilia sana au kutokwa na udenda sana kwa tamaa ya kitu huwa hawawezi.

  Na wakishindwa hugeuka mbogo na kuanza kuonesha makucha yao ya udikteta na police state? Haya sasa wafichueni. Kugoma kwani dhambi. Kama mambo hayaendi wanataka tufantye nini? Au wanataka tuwaambie kaka zetu waturudishe kulekule mwaka 1964?
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  Nov 17, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Kuna kamanda Mkumbo ndiye ambaye alionekana mara ya mwisho akiwa nayo!
   
 8. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #8
  Nov 17, 2008
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Kwa nini polisi wamkamate huyo kijana peke yake?
   
 9. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #9
  Nov 17, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Ni kweli odong amekamatwa toka juzi na julias ni jana amekamatwa na hao jamaa
   
 10. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #10
  Nov 17, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Waandishi waalimu wanafunzi mapolisi majeshi mahakimu na majaji wacha ya wakute haya au hizi ndizo ahadi za CCM hakuna jingine ,japo wengine hawamo lakini idadi kubwa ni wapigia debe CCM,ndio wapiga kura wa CCM baba yao ni ccm maana huwaga nawasikia wakisema CCM ndio baba.
  Sijui kama watu hubadilika na kama wamisikia kuwa Wamerakani wamempigia na kumpa ushindi wa kishindo Mwafrika Baraka huseini Obama Onyango, hapa watu ukiwambia wabadilishe Chama wao wanabadilisha mtu kwa kuwa tu CCM ndio baba ,mambo badu kwa hali ya uchumi inavyokwenda mambu yatakuwa mengi si hasha Muungwana akaingia mitini uchaguzi ujao.
   
 11. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #11
  Nov 17, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Utawala wa kiimla unaogopa sana mwamko wa wanafunzi wa elimu ya juu! Unajua hawa jamaa kama wangeweza kumkamata kile mtu anayewapinga na isijulikane wangekamata kila mtu; tusipoangalia tutaanza kuokota miili in reminiscent of Idi Amin Dada...
   
 12. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #12
  Nov 17, 2008
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,306
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  Kazi ipo sasa...maana wakimaliza hapo watahamia kwa Mkoba wa Chama cha Walimu...........
   
 13. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #13
  Nov 17, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  nadhani wakati umefika wa kuitisha maandamano makubwa zaidi ya wanafunzi wote na kukomesha mara moja unyanyasaji huu; maana inaonekana punda hendi bila ya fimbo!
   
 14. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #14
  Nov 17, 2008
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Utawala wa kiimla hautakubalika Tanzania, na kwa maoni yangu Serikali ya JK inaanza kuelekea huko. Watanzania naamini wako makini sana katika hilo. Wanafunzi wanadai haki yao, leo hii unawakamata wawakilishi wao. Hii haiwezi kuleta tija katika migomo zaidi ya kuongeza chuki kwa serikali. Kuna thread moja nilichangia kuhusu mgomo wa walimu kuwa Bw. Chiligati anaielekeza serikali kumfikisha Bw. Mukoba (Rais wa CWT). Kisa, mgomo. Hawa watu ni wawakilishi wa victims ambao ni wanafunzi wa vyuo vikuu pamoja na walimu nchini. Sasa kuwakamata au kuwafungulia mashitaka ndiyo ita-solve matatizo hayo!! Serikali pamoja na Rais JK wanatakiwa kuwa serious na matatizo yanayowakabili wananchi. Leo hii wanafunzi wa vyuo vikuu, walimu wana mgomo ili kudai haki zao. Siku zijazo wananchi wengine nao wataleta vuguvungu la kudai haki zao za maendeleo katika maeneo yao kama vile maji, umeme, madawa hospitalini n.k

  Serikali inatakiwa kuacha mambo ya kijanjajanja na kuwa serious na matatizo ya wananchi. Hawa watu wananoshikiliwa na wana usalama wanatakiwa kuachiwa huru mara moja bila ya vikwazo vyovyote. Tanzania haiwezi kuwa salama kwa kutumia vitisho kuwafunga wananchi midomo kudai haki zao. Mwaka huu na kuendelea lazima kuwe na mabadiliko makubwa katika maendeleo ya wananchi na si danganya toto kama ya Msekwa kudai oooh JK kafanya kazi nzuri kwa wananchi. Bull@@<*%t.
   
 15. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #15
  Nov 17, 2008
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Kuna hatari ya hawa vijana kufikishwa mahakamani kesho chini ya ulinzi mkali, huku jamaa wa EPA wakila kuku kwa mrija, wengine wakiwa wamekwenda kujiliwaza nje ya nchi, mmoja akiwa Marekani na mwingine nchi za Ghuba..... Tutaendelea kuzugwa hadi tongo tongo zitutoke tuache kushabikia kila kitu
   
 16. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #16
  Nov 17, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,551
  Likes Received: 1,895
  Trophy Points: 280
  Tusubiri hayo mashtaka kwani hii issue inaelekea ni deeper than this migomo stuff.
  Naona issue hii inaweza kuwa coincedence mbaya kwasababu EPA nayo iko makahamani...Haya mambo ya siasa huwa yanageuka ghafla ghafla mno na si ajabu moshi unafuka kwani moto hauko mbali.

  Sasa wanafunzi wote Tanzania nzima wakigoma nani atanufaika?
  Ama wandhani vijana hao wanataka kupinduwa nchi? Wanausalama kuwanyanyasa wasomi wetu kwa kisingizio cha kuwa wao ni upinzani hakina maana kabisa....Wapewe haki zao na wanafunzi waandamane EPA iwape na ufisadi mwingine ushughulikiwe kwanza ili wanafunzi hao wapate huduma na elimu bora badala ya mafisadi kujiendeleza wao wenyewe.
   
 17. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #17
  Nov 17, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Ndio maana hadi sasa miye sijasema lolote kuhusu watu wa EPA kufikishwa mahakamani.. kwani mazingaombwe siyo lazima kuficha kila kitu wakati mwingine ni kufanya vitu vionekane hadharani!
   
 18. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #18
  Nov 17, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,551
  Likes Received: 1,895
  Trophy Points: 280
  Kwani hiyo pesa ya EPA si ingetosha mara mia kuyashughulikia matatizo sugu ya wanafunzi? Matatizo ya wanafunzi hayajaanza leo..Lakini kwasababu na wao wana upeo...Wanajuwa wazi kuwa viongozi wetu wanakotupeleka siko, Ufisadi uliofanyika hakuna hata jambo moja lilikuwa solved na matatizo ndiyo yanazidi kuongezeka kwasababu wao mafisadi si ndio walianzisha kwa kupeleka siasa badala ya kutatuwa matatizo yao?
  Yamewakuta sasa na mimi naungana na wanafunzi hao kudai haki za msingi na kuupiga vita ufisadi kwa nguvu zote na nawaombea Mungu awalinde na ubaradhuli wa mafisadi hao hatari kabisa kwa jamii na usalama wake.
   
 19. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #19
  Nov 17, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Kubalini tu yaishe.. madaraka ni matamu sana na sasa hivi migomo yanatishia madaraka ya watu... so tuna uamuzi wa kufanya.
   
 20. K

  Kichakoro JF-Expert Member

  #20
  Nov 17, 2008
  Joined: Sep 10, 2008
  Messages: 1,544
  Likes Received: 1,293
  Trophy Points: 280
  kuna habari nimepata hivi punde kwamba wanafunzi wa Primary/Secondary nao wamegoma leo Dar ili kushinikiza serikali kuwaachia Je ni kweli???????
   
Loading...