Julius Mtatiro kushitakiwa kwa uchochezi

Naona Mtatiro fasta fasta, upekuzi na mashtaka kuandaliwa chap chap. Chenge, Mramba wao kimyaaa, mafile bado yanapekuliwa.

Ahsante sana mama. Mambo kama haya ndiyo yanayoudhi sana ndani ya nchi yetu. Mafisadi wa EPA, Richmond, Kiwira, TRL, Ununuzi wa ndege ya Rais, Rada, magari na helicopters za jeshi, nyumba za serikali, mikataba ya madini (Tanzanite, Almasi na Dhahabu) wakati bado wanapeta na mkuu wa TAKUKURU anathubutu kutamka hadharani tena bila hata woga kwamba mafisadi ni matajiri wakubwa sana wakikamatwa uchumi wa nchi utaanguka!!! lakini wameenda kumdaka kijana wa watu asiye na hatia yoyote na kumfungulia mashtaka haraka haraka ili kuwaweka wanafunzi wa vyuo mbali mbali nchi roho juu kuhusu migomo yao.

Ni dalili za serikali ambayo haina mwelekeo na sasa imeanza kutawala kwa vitisho dhidi ya Raia wake. Naona kuna kila dalili ya kuwa na Mugabe wetu bongo, usitofautiane naye katika lolote lile vinginevyo cha moto utakiona.

mwanafunzikiz.jpg

Katibu Mkuu mstaafu vyuo vikuu Tanzania Bara
na Visiwani Julius Mtatiro akisalimiana na Askari magereza katika
mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jana,baada ya kutuhumiwa
kwa kosa la kuwahamasisha wanafunzi wa vyuo vikuu kugoma
kuingia madarasani.
 
So,he didn't ask for a lawyer.
Wasn't mistreated...well,expect for the ''kipanda uso thing''.
What now?Change of stories?

Suki, na mimi nasubiri maelezo.

Ile kujijengea kuaminika ingekuwa vizuri kama mleta habari angekuja kurekebisha hadithi aliyoambiwa na "inzi" kwamba wanasheria hawakuruhusiwa kumwona detainee.

Leo mleta habari mwenyewe amesikia kutoka kwa mtuhumiwa mwenyewe kwamba ni yeye ndie hakutaka wakili. Kijana anamwambia mleta habari kwamba alivyoona yeye alikuwa anaweza ku handle maswali ya polisi.

mtatilo.jpg

Mleta habari, madam umeshapata ukweli, rekebisha hadithi yako ambayo ulikuwa mkali sana ilipokuwa challenged mara ya kwanza ulipoileta.
 
Original story still stands kama ushahidi wa kilichosemwa, habari mpya ndiyo hiyo. Pia ni lazima ujue kuwa kuna vitu vingine tunavyoletewa kama vilivyo na sisi tunavirusha jinsi vilivyo na vinaweza kuwa tofauti kubwa sana katika hatima ya mtu.

Yeye hajabadili story, vyanzo ndiyo vilikuwa vinaleta stori hiyo na tumeshasikia mwenyewe alichosema.
 
Mwenzenu naomba mnieleweshe huyu Mtatiro bado ni mwanachuo au alishamaliza lakini wakahisi anachochea migomo akiwa uraiani?
 
Huyu jamaa tayari yuko nje kwa dhamana.Hivi na taarifa kwamba Odong Odwali amesimamishwa masomo UDSM na kurudishwa Uganda chini ya ulinzi mkali wa polisi kuna ukweli hapa?
Maana sasa naona serikali imeamua kuwakatili hawa wadai haki za wenzao!
 
Ni taarifa zimezagaa mtaani kwamba Odong amekamatwa na tayari amerudishwa kwao Uganda!Huyu ni mmoja wa wanamapinduzi wa pale mlimani.Yumkini kuna mtu ana info zake za kutosha please atuwekee hapa
 
Ni taarifa zimezagaa mtaani kwamba Odong amekamatwa na tayari amerudishwa kwao Uganda!Huyu ni mmoja wa wanamapinduzi wa pale mlimani.Yumkini kuna mtu ana info zake za kutosha please atuwekee hapa

Hakuna ukweli wowote juu ya hili swala, Odong bado anashikiliwa na polisi na si kweli kama amesharudishwa kwao Uganda, ila once polisi watakapomaliza uchunguzi wao basi itawekwa wazi na kama kutaonekana kuna uonevu wowote juu yake hapo ndo tutakuwa na haki ya kulipigia kelele lakini sasa hivi halitatusaidia kitu tutabakia kupayuka mambo meeengi lakini hatutaweza kulitatua till polisi watakapotoa statement yao
 
..then 2010 sitashangaa majority ya UD student watavote CCM kama kawaida yao,maana hata diwani sehemu yao ni wa CCM,wanaume wa shoka wako tarime na ndio wana deserve support yetu sio hawa matapeli wanaobeba gari la kikwete na makamba huku wakicheza mdundiko then wakinyimwa pesa wana act kama watoto kwa kuvunja viti na milango,hata kuendesha migomo hawajui sijui ni wasomi gani hawa? ndio maana tunaishia kuwa na mikataba ya Richmond na EPA kwa wasomi wa namna hii....akili zao ni sawa na CCM!

Wale waleee......wavivu wakufikiri!
 
Hakuna ukweli wowote juu ya hili swala, Odong bado anashikiliwa na polisi na si kweli kama amesharudishwa kwao Uganda, ila once polisi watakapomaliza uchunguzi wao basi itawekwa wazi na kama kutaonekana kuna uonevu wowote juu yake hapo ndo tutakuwa na haki ya kulipigia kelele lakini sasa hivi halitatusaidia kitu tutabakia kupayuka mambo meeengi lakini hatutaweza kulitatua till polisi watakapotoa statement yao

Habari rasmi zilitotangazwa kwenye local news ni kwamba bwana Odong aliondolewa nchini jana usiku kwa ndege ya KQ mpaka kwao Uganda. Na alipofika huko alikamatwa na maafisa uhamiaji wa nchi hiyo. Hii ni taarifa rasmi kutoka jeshi la polisi hapa nchini na idara ya uhamiaji.
 
Hakuna ukweli wowote juu ya hili swala, Odong bado anashikiliwa na polisi na si kweli kama amesharudishwa kwao Uganda, ila once polisi watakapomaliza uchunguzi wao basi itawekwa wazi na kama kutaonekana kuna uonevu wowote juu yake hapo ndo tutakuwa na haki ya kulipigia kelele lakini sasa hivi halitatusaidia kitu tutabakia kupayuka mambo meeengi lakini hatutaweza kulitatua till polisi watakapotoa statement yao

Kama unafuatilia news utakuwa tayari unafahamu kama hapa ulikosea.Amesharudishwa kwao!
 
Kama unafuatilia news utakuwa tayari unafahamu kama hapa ulikosea.Amesharudishwa kwao!

Kama upo makini kusoma kila post inayokuwa published humu basi utagundua umekurupuka,, angalia hiyo post yangu nimeiweka alhamisi na wewe umesubiria magazeti ya jana yakwambie kuwa odong amerudishwa ndo unakuja kukosoa.... Hehehehe hiyo nilipost hata kabla polisi hawajatoa tamko lao, Odong amerejeshwa kwao ijumaa asubuhi na ndege ya Kenya airways KQ.
Kuwa makini unapotaka kutoa boriti kwenye jicho la mwenzako
 
[/COLOR]

Nasikitika sana kuona serikali yetu inajikanyagakanyaga. Kwani megomo yote ilianzishwa na huyo Odongo na sasa hakutakuwa na migomo tena? Nasikia huyo bwana ni 'critical thinker' - ana 'backbone' na kwa hili ni adui mkubwa wa serikali yetu.

Serikali inataka wanafunzi ambao ni wanafiki na wanaweza kusema uongo. Ukweli unachukiwa. Kama muda huo wote alikuwa akisoma na mpaka akachukua kadi ya umoja wa vijana wa sisiemu na eti leo kwa vile kuna mgomo chuo kikuu ndio waone kuwa anaishi nchini kinyume cha sheria?

Mbona wanaohujumu uchumi wetu hawatendewi hivyo? Serkali yetu inakosa viongozi kama Nyerere - nilimpenda Nyerere kwa vile alikuwa 'bright' na aliongea mambo ambayo unaona yana maana. Sijui kwa kweli nchi yetu inaelekea wapi!

Na sijui kwa mgomo wa walimu na makundi mengine watampata nani!
 
[/COLOR]

Kama upo makini kusoma kila post inayokuwa published humu basi utagundua umekurupuka,, angalia hiyo post yangu nimeiweka alhamisi na wewe umesubiria magazeti ya jana yakwambie kuwa odong amerudishwa ndo unakuja kukosoa.... Hehehehe hiyo nilipost hata kabla polisi hawajatoa tamko lao, Odong amerejeshwa kwao ijumaa asubuhi na ndege ya Kenya airways KQ.
Kuwa makini unapotaka kutoa boriti kwenye jicho la mwenzako

Rudia tena kusoma hii thread,halafu utafahamu mimi na wewe nani anapost bila kusoma whole thread! Na hatakama nasubiri magazeti tatizo lako nini.Post yangu ilitaka kukueleza kuwa ulichosema kuwa bado anashikiliwa si kweli maana tayari nilipata habari kuwa amerudishwa kwao uganda,na nikapost kuwa habari hizo zimezagaa,then vyombo vya habari vilipo confirm nikakuhabarisha! Wawapi wewe, huelimishwi!!? Yaelekea unapenda kujibizana!
 
Whaaaaaaaat?? Hebu fuatilia post zangu then utagundua kuwa ni mmoja kati ya watu wasiopenda watu walumbane humu na kupotosha maana na uhalisia wa thread husika, na kwa wewe hapa naona unataka kunipeleka kule kule, wawa what am going to say SITOJIBU KITU CHOCHOTE KUTOKA KWAKO sababu unaonyesha ni mvivu wa kufikiri thats y unafikiri unaweza kunielimisha mimi... watch out u'r steps Jamii forum si ya vilaza as u think, naona unakurupuka kuandika ili mradi tu uongeze number ya post......

Inv ameweka kitu sahihi kabisa

FICHA UPUMBAVU WAKO USIFICHE HEKIMA YAKO
 
Utawala wa kiimla unaogopa sana mwamko wa wanafunzi wa elimu ya juu! Unajua hawa jamaa kama wangeweza kumkamata kile mtu anayewapinga na isijulikane wangekamata kila mtu; tusipoangalia tutaanza kuokota miili in reminiscent of Idi Amin Dada...
Kumbe na jakaya alikuwa na utawala wa kiimla?
 
Back
Top Bottom