Julius Mtatiro kwenye hili umefeli sana bro

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
6,195
Reaction score
10,709
Katika mazingira ambayo vijana wengi wa Kitanzania wanahangaika kutafuta ajira baada ya kuhitimu vyuo vikuu, mjadala kuhusu elimu ya ufundi na elimu ya juu ni muhimu. Lakini kilichofanywa na mwanasiasa Julius Mtatiro si mjadala wa kujenga taifa — ni propaganda ya kisiasa iliyovuka mipaka ya heshima kwa taasisi za elimu ya juu nchini.
images - 2026-05-17T192155.232.jpeg

Mtatiro alimtumia Maurine, mhitimu wa Shahada ya Usimamizi wa Rasilimali Watu kutoka Chuo Kikuu cha Mipango Dodoma, kama mfano wa kuonyesha kwamba njia ya mafanikio ipo VETA badala ya vyuo vikuu. Kauli hiyo haikuwa tu ya kupotosha, bali pia ya kudhalilisha maelfu ya vijana waliotumia miaka yao kusoma kwa bidii katika vyuo vikuu vya Tanzania.
images - 2026-05-17T190628.034.jpeg

Hakuna anayepinga umuhimu wa VETA. Elimu ya ufundi ni mhimili muhimu wa uchumi wa taifa lolote linalotaka maendeleo ya viwanda. Lakini kuisifia VETA kwa kubeza vyuo vikuu ni ujinga wa kisiasa unaolenga kufurahisha wakubwa badala ya kujenga sera bora za elimu. Ni sawa na kusema daktari hana maana kwa sababu fundi umeme pia anapata kipato.

Mtatiro alionekana kushangazwa na uwepo wa wanafunzi kutoka nchi za Congo DR, Eritrea, Ethiopia na Rwanda katika chuo cha VETA Shinyanga kana kwamba huo ni muujiza wa kipekee. Bro hili ni jambo la kawaida kabisa katika taasisi nyingi za elimu Tanzania, halikuanza kipindi cha Samia kama ambavyo unaropoka.
162A6540-Enhanced-NR_0.jpg

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Muhimbili MUHAS na Chuo Kikuu cha Dodoma, vimekuwa zikipokea wanafunzi wa kimataifa kwa miaka mingi bila maigizo ya kisiasa. Vyuo hivi vinadahili tena kwa idadi kubwa na wala hautokuja kuona wakimsifia sifia Samia hata kidogo.
images - 2026-05-17T192155.232.jpeg

Kinachokera zaidi ni ukimya wa taasisi hizi dhidi ya kauli zinazodhalilisha hadhi ya elimu yao. Kama kweli tunathamini elimu ya juu, basi viongozi wanaotumia propaganda za kisiasa kushusha thamani ya vyuo vikuu wanapaswa kukemewa waziwazi — hata kwa njia za kisheria.
images - 2026-05-17T190628.034.jpeg

Taifa haliwezi kujengwa kwa kuwagawa vijana kati ya “waliosoma sana” na “wenye ujuzi wa mikono.” Tanzania inahitaji vyote, si siasa za kushabikia upande mmoja kwa ajili ya makofi ya kisiasa. Na kingine Mtatiro umesoma Chuo Kikuu cha UDSM sasa kwanini unajizima data kupondea vyuo vikuu wakati wewe mwenyewe umesoma UDSM mzee baba? PUT STOP TO THESE NONSENSE BRO.
 
Attachments

  • images - 2026-05-17T190611.216.jpeg
    images - 2026-05-17T190611.216.jpeg
    24.6 KB · Views: 16
kama wakufunzi wenyewe ni kina kabudi acha avitukane tu

kama wanafunzi ndo wale walivaa juzi never again wakaandamana kwa Wingi wana haki ya kutukanwa

naunganana na mtatiro vijana wa sasa wa elimu ya juu (sugu asha maliza)
 
Kwa level ya Taasisi kazingua kidogo, Yeye angetukana kijana mmoja mmoja hata kwa matusi yote. Graduates wengi jau ila na mfumo umechangua kuwajenga hivyo walivyo.

Point niliyochuku: Tusiwagawe vijana kwa level za kielimu, taifa linawahitaji wote kwa maendeleo.
 
Katika mazingira ambayo vijana wengi wa Kitanzania wanahangaika kutafuta ajira baada ya kuhitimu vyuo vikuu, mjadala kuhusu elimu ya ufundi na elimu ya juu ni muhimu. Lakini kilichofanywa na mwanasiasa Julius Mtatiro si mjadala wa kujenga taifa — ni propaganda ya kisiasa iliyovuka mipaka ya heshima kwa taasisi za elimu ya juu nchini.
View attachment 3590131
Mtatiro alimtumia Maurine, mhitimu wa Shahada ya Usimamizi wa Rasilimali Watu kutoka Chuo Kikuu cha Mipango Dodoma, kama mfano wa kuonyesha kwamba njia ya mafanikio ipo VETA badala ya vyuo vikuu. Kauli hiyo haikuwa tu ya kupotosha, bali pia ya kudhalilisha maelfu ya vijana waliotumia miaka yao kusoma kwa bidii katika vyuo vikuu vya Tanzania.
View attachment 3590126
Hakuna anayepinga umuhimu wa VETA. Elimu ya ufundi ni mhimili muhimu wa uchumi wa taifa lolote linalotaka maendeleo ya viwanda. Lakini kuisifia VETA kwa kubeza vyuo vikuu ni ujinga wa kisiasa unaolenga kufurahisha wakubwa badala ya kujenga sera bora za elimu. Ni sawa na kusema daktari hana maana kwa sababu fundi umeme pia anapata kipato.
View attachment 3590128
Mtatiro alionekana kushangazwa na uwepo wa wanafunzi kutoka nchi za Congo DR, Eritrea, Ethiopia na Rwanda katika chuo cha VETA Shinyanga kana kwamba huo ni muujiza wa kipekee. Bro hili ni jambo la kawaida kabisa katika taasisi nyingi za elimu Tanzania, halikuanza kipindi cha Samia kama ambavyo unaropoka.
View attachment 3590130
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Muhimbili MUHAS na Chuo Kikuu cha Dodoma, vimekuwa zikipokea wanafunzi wa kimataifa kwa miaka mingi bila maigizo ya kisiasa. Vyuo hivi vinadahili tena kwa idadi kubwa na wala hautokuja kuona wakimsifia sifia Samia hata kidogo.
View attachment 3590131
Kinachokera zaidi ni ukimya wa taasisi hizi dhidi ya kauli zinazodhalilisha hadhi ya elimu yao. Kama kweli tunathamini elimu ya juu, basi viongozi wanaotumia propaganda za kisiasa kushusha thamani ya vyuo vikuu wanapaswa kukemewa waziwazi — hata kwa njia za kisheria.
View attachment 3590126
Taifa haliwezi kujengwa kwa kuwagawa vijana kati ya “waliosoma sana” na “wenye ujuzi wa mikono.” Tanzania inahitaji vyote, si siasa za kushabikia upande mmoja kwa ajili ya makofi ya kisiasa. Na kingine Mtatiro umesoma Chuo Kikuu cha UDSM sasa kwanini unajizima data kupondea vyuo vikuu wakati wewe mwenyewe umesoma UDSM mzee baba? PUT STOP TO THESE NONSENSE BRO.
Samahani kuna video ingine? Mtatiro kasema binti kasomea HR ngazi ya shahada akaona haitoshi akaamua kwenda Veta kusomea mitambo na anasukuma mitambo. Kuna kipi kibaya alichosema hapa?

Hayo mengine uliyosema kasema yako wapi?
 
wanatengeneza tatizo lingine tena wakidhani hiyo ndio njia muafaka ya kuondoa tatizo la ajira kwa vijana....
 
Back
Top Bottom