Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu

Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu

haya ni baadhi ya maswali ya sugu bungeni
Supplementary Questions(7)
Contributions(41)

[TD="width: 174"] Questions (5)
[/TD]

[TD="align: center"]
1644.jpg

[/TD]
[TD="align: center"] Matukio mengi ya ajali hutokea katika eneo la Uyole Kati na kona ya Barabara Kuu ya Uyole – Kyela, hivyo kusababisha vifo vya watu wengi:-

Je, ni lini Serikali itasikia kilio cha wakazi wa eneo hilo na kuweka Road Bumps ili kupunguza mwendo kasi wa magari makubwa?
ANSWERS TO PRINCIPAL QUESTION #174 SESSION # 4
Answer From Hon. Mwakyembe, Dr. Harrison George
WORKS
NAIBU WAZIRI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Joseph O. Mbilinyi, Mbunge wa Mbeya Mjini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, eneo la Uyole Kati lipo katika Barabara Kuu ya Uyole – Kasumulu, umbali wa kilometa moja kutoka makutano ya Barabara Kuu ya TANZAM na Barabara Kuu ya Uyole – Kasumulu; ni kweli kuwa, katika eneo hili kuna kona na mahali hapo ajali nyingi hutokea. Hali hiyo ililazimu uchunguzi ufanyike, ambao umebaini kuwa, ajali nyingi katika eneo hilo husababishwa na madereva wasioheshimu au kuzingatia sheria na alama za barabara za kudhibiti mwendo kasi.

Mheshimiwa Spika, kutokana na hali hii isiyoridhisha na upekee wa barabara hii, kwani inaunganisha nchi yetu na nchi jirani za Malawi na Zambia; hivyo kutumiwa na madereva wenye uzoefu na uelewa unaopishana, Serikali kwa ushauri wa wataalamu wake, imejipanga kulitafutia ufumbuzi wa kudumu suala la ajali eneo la Uyole katika Mwaka wa Fedha wa 2011/2012.

swali 2

Mbilinyi, Osmund Joseph [CHADEMA]
Mbeya Mjini Constituency
Session No Question No To the Ministry of Sector Date Asked
3 20 EDUCATION AND VOCATIONAL TRAINING Higher Education 6 April 2011
Principal Question No
Wanafunzi wa Vyuo karibu vyote nchini wamegoma kwa nyakati tofauti kutokana na kutopatiwa fedha za mikopo. Baadhi yao wamepigwa na kujeruhiwa na askari:-

(a) Je, kwanini Serikali inaendelea kukumbatia utendaji mbovu na usiokuwa na tija wa Bodi ya Mikopo?

(b) Je, ni kwa nini kazi ya kutoa mikopo kwa wanafunzi isifanywe na Benki yoyote itakayoteuliwa na Serikali kwani zina uzoefu wa kutoa na kurejesha mikopo tofauti na Bodi?

(c) Je, Serikali haioni kwamba kwa kufanya hivyo itapunguza matumizi?
ANSWERS TO PRINCIPAL QUESTION #20 SESSION # 3
Answer From Hon. Mulugo, Philipo Augustino
EDUCATION AND VOCATIONAL TRAINING
NAIBU WAZIRI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Joseph Osmund Mbilinyi, Mbunge wa Mbeya Mjini, lenye sehemu (a), (b) na (c) kama ifuatavyo:-

(a)Mhehsimiwa Spika, wanafunzi katika Vyuo Vikuu na taasisi za Elimu ya Juu, wamekuwa wakigoma kwa sababu mbalimbali zikiwemo, uhaba wa sehemu za malazi, ubovu na upungufu wa miundombinu, upungufu wa wanataaluma wenye sifa stahiki, baadhi ya Vyuo kudahili wanafunzi kwenye program ambazo haijaidhinishwa na Tume ya Vyuo Vikuu(TCU), utendaji usioridhisha wa baadhi ya viongozi katika Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu na ongezeko la ada lisiloendana na mikopo inayotolewa.

Mheshimiwa Spika, kimsingi malalamiko kutoka kwa wadau kuhusu mfumo wa utoaji wa mikopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu wa Juu unatokana na sababu mbalimbali ikiwemo uhaba wa fedha zitolewazo na Serikali ikilinganishwa na idadi ya mahitaji.

Hata hivyo ili kujiridhisha na utendaji wa Bodi, Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameunda Tume maalum ambayo pamoja na mambo mengine itapitia kwa kina mfumo wa uombaji na utoaji wa mikopo na kupendekeza jinsi Bodi ya Mikopo inavyoweza kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.

Ni matumaini yangu kwamba mapendekezo ya Tume hii yataboresha utaratibu mzima wa utoaji na urejeshwaji wa mikopo na hivyo kufanya mfumo wa utoaji wa mikopo kuwa endelevu. Tume hii itamaliza kazi yake tarehe 15 Aprili, 2011.

(b)Mheshimiwa Spika, kuhusu uteuzi wa Benki yenye uzoefu wa kutoa na kukusanya mikopo, Sheria iliyoanzisha Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inakinzana na Sheria ya Benki Kuu.

Kwa mfano Sheria ya Benki Kuu inayoongoza biashara za Mabenki hapa nchini hairuhusu benki yeyote kutoa kiasi cha mkopo kinachotolewa kwa wakati mmoja kwa wateja wa aina hiyo hiyo moja kama walivyo wanafunzi wanaosoma kwenye Vyuo vya Elimu ya Juu.

Vilevile Sheria iliyoanzisha Bodi ya Mikopo iliyotungwa na Bunge lako Tukufu inaelekeza kuwa mikopo inayotolewa kwa wanafunzi husika isitozwe riba ya aina yeyote na inarejeshwa kwa kipindi kirefu cha miaka kumi baada ya mwanafunzi kuhitimu masomo yake.

(c)Mhehsimiwa Spika, iwapo utoaji wa mikopo utafanywa na benki gharama za uendeshaji zitakuwa zaidi ya asilimia 10 ya kiasi kilichokopeshwa mbali na riba. Kwa sasa gharama za uendeshaji kwa Bodi ya Mikopo ya wanafunzi wa Elimu ya Juu ni asilimia 3.5 na hakuna riba. Hivyo kutoa mikopo kupitia benki hakutapunguza gharama za uendeshaji.

swali 3

4 310 INDUSTRIES, TRADE AND MARKETING Industry 26 July 2011
Principal Question No
Sababu zilizotolewa wakati Serikali inabinafsisha Kiwanda cha Zana za Kilimo Mbeya ni pamoja na kuongeza ajira kwa wananchi. Lengo la Sera ya Kilimo ya Mwaka 1997 ni kukifanya kilimo kiwe cha kisasa na endelevu hivyo zana za kilimo kuwa muhimu sana:¬

(a) Je, kwa kukibinafsisha kiwanda hicho ajira zimeongezeka kuliko ilivyokuwa kabla ya kubinafsishwa?

(b) Je, kwa nini kiwanda hicho kisirejeshwe Serikalini ili kufanya uzalishaji ukidhi malengo ya uanzishwaji wake kwenda sambamba na mkakakati wa kilimo kwanza pamoja na kuongeza ajira kwa wananchi wa Mbeya?
ANSWERS TO PRINCIPAL QUESTION #310 SESSION # 4
Answer From Hon. Malima, Adam Kighoma Ali
INDUSTRIES, TRADE AND MARKETING
NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI

(K.n.y. WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA) alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Viwanda na Biashara, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Joseph Mbilinyi, Mbunge wa Mbeya Mjini lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:

(a) Mheshimiwa Mwenyekiti, kiwanda cha Zana za Kilimo (ZZK) kilifungwa mwezi Mei, 1998 kutokana na kushindwa kujiendesha na hatimaye kufilisiwa mwaka 2002. Mali za kiwanda ziliuzwa kwa Kampuni ya CMG Investment. Mnunuzi baada ya kumiliki kampuni hiyo na kufanya mchanganuo, amefikia maamuzi kuwa uzalishaji wa zana za kilimo hauna faida kwake na hivyo mnunuzi ameamua kuanza mchakato wa kuanzisha kiwanda cha kuzalisha bia aina ya Serengeti.
Wakati akijiandaa na mpango huo karakana imefufuliwa na kuna uzalishaji mdogo mdogo wa matoroli na vinu vya kukoboa na kusaga nafaka ambao umeanza mwezi Juni, 2011 kulingana na mahitaji ya mteja mmoja mmoja. Ajira iliyoko pale kwa sasa siyo ajira ya kudumu.

(b)Mheshimiwa Mwenyekiti, utaratibu wa ufilisi haumlazimishi mnunuzi kuwasilisha mpango wa uwekezaji wakati wa kununua mali husika.
Aidha kulingana na Sheria ya ufilisi mnunuzi ana haki ya kumiliki mali iliyonunua na kutumia anavyoona itampatia faida. Hivyo endapo Serikali inataka kurejesha kiwanda cha ZZK mikononi mwake ili kiweze kukidhi malengo ya uanzishwaji wake, itabidi ifanye mazungumzo na mnunuzi ya kiwanda hicho ya kununua kiwanda hiki tena na kukifufua ili kiweze kuzalisha zana za kilimo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kumshauri Mheshimiwa Mbunge, endapo atapata wawekezaji wanaoweza kukiendesha kiwanda hicho kwa faida wawasiliane na mmiliki wa sasa au wawasiliane na Wizara ya Viwanda na Biashara ili tuweze kumsaidia kufanya uwekezaji katika maeneo hayo ama kwa kukinunua kiwanda hiki na kuzalisha Zana za Kilimo au kwa kutengeneza utaratibu mbadala. Mbilinyi Joseph Osmund

[/TD]
[TD="align: center"]CHADEMA[/TD]
[TD="align: center"]

[TD="width: 174"][/TD]
[/TD]
 
haya mbona aliyauliza bungeni na majibu yake yapo ukitaka nakuletea yote
swali la 1
Matukio mengi ya ajali hutokea katika eneo la Uyole Kati na kona ya Barabara Kuu ya Uyole – Kyela, hivyo kusababisha vifo vya watu wengi:-

Je, ni lini Serikali itasikia kilio cha wakazi wa eneo hilo na kuweka Road Bumps ili kupunguza mwendo kasi wa magari makubwa?
ANSWERS TO PRINCIPAL QUESTION #174 SESSION # 4
Answer From Hon. Mwakyembe, Dr. Harrison George
WORKS
NAIBU WAZIRI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Joseph O. Mbilinyi, Mbunge wa Mbeya Mjini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, eneo la Uyole Kati lipo katika Barabara Kuu ya Uyole – Kasumulu, umbali wa kilometa moja kutoka makutano ya Barabara Kuu ya TANZAM na Barabara Kuu ya Uyole – Kasumulu; ni kweli kuwa, katika eneo hili kuna kona na mahali hapo ajali nyingi hutokea. Hali hiyo ililazimu uchunguzi ufanyike, ambao umebaini kuwa, ajali nyingi katika eneo hilo husababishwa na madereva wasioheshimu au kuzingatia sheria na alama za barabara za kudhibiti mwendo kasi.

Mheshimiwa Spika, kutokana na hali hii isiyoridhisha na upekee wa barabara hii, kwani inaunganisha nchi yetu na nchi jirani za Malawi na Zambia; hivyo kutumiwa na madereva wenye uzoefu na uelewa unaopishana, Serikali kwa ushauri wa wataalamu wake, imejipanga kulitafutia ufumbuzi wa kudumu suala la ajali eneo la Uyole katika Mwaka wa Fedha wa 2011/2012.

swali 2

Mbilinyi, Osmund Joseph [CHADEMA]
Mbeya Mjini Constituency
Session No Question No To the Ministry of Sector Date Asked
3 20 EDUCATION AND VOCATIONAL TRAINING Higher Education 6 April 2011
Principal Question No
Wanafunzi wa Vyuo karibu vyote nchini wamegoma kwa nyakati tofauti kutokana na kutopatiwa fedha za mikopo. Baadhi yao wamepigwa na kujeruhiwa na askari:-

(a) Je, kwanini Serikali inaendelea kukumbatia utendaji mbovu na usiokuwa na tija wa Bodi ya Mikopo?

(b) Je, ni kwa nini kazi ya kutoa mikopo kwa wanafunzi isifanywe na Benki yoyote itakayoteuliwa na Serikali kwani zina uzoefu wa kutoa na kurejesha mikopo tofauti na Bodi?

(c) Je, Serikali haioni kwamba kwa kufanya hivyo itapunguza matumizi?
ANSWERS TO PRINCIPAL QUESTION #20 SESSION # 3
Answer From Hon. Mulugo, Philipo Augustino
EDUCATION AND VOCATIONAL TRAINING
NAIBU WAZIRI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Joseph Osmund Mbilinyi, Mbunge wa Mbeya Mjini, lenye sehemu (a), (b) na (c) kama ifuatavyo:-

(a)Mhehsimiwa Spika, wanafunzi katika Vyuo Vikuu na taasisi za Elimu ya Juu, wamekuwa wakigoma kwa sababu mbalimbali zikiwemo, uhaba wa sehemu za malazi, ubovu na upungufu wa miundombinu, upungufu wa wanataaluma wenye sifa stahiki, baadhi ya Vyuo kudahili wanafunzi kwenye program ambazo haijaidhinishwa na Tume ya Vyuo Vikuu(TCU), utendaji usioridhisha wa baadhi ya viongozi katika Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu na ongezeko la ada lisiloendana na mikopo inayotolewa.

Mheshimiwa Spika, kimsingi malalamiko kutoka kwa wadau kuhusu mfumo wa utoaji wa mikopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu wa Juu unatokana na sababu mbalimbali ikiwemo uhaba wa fedha zitolewazo na Serikali ikilinganishwa na idadi ya mahitaji.

Hata hivyo ili kujiridhisha na utendaji wa Bodi, Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameunda Tume maalum ambayo pamoja na mambo mengine itapitia kwa kina mfumo wa uombaji na utoaji wa mikopo na kupendekeza jinsi Bodi ya Mikopo inavyoweza kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.

Ni matumaini yangu kwamba mapendekezo ya Tume hii yataboresha utaratibu mzima wa utoaji na urejeshwaji wa mikopo na hivyo kufanya mfumo wa utoaji wa mikopo kuwa endelevu. Tume hii itamaliza kazi yake tarehe 15 Aprili, 2011.

(b)Mheshimiwa Spika, kuhusu uteuzi wa Benki yenye uzoefu wa kutoa na kukusanya mikopo, Sheria iliyoanzisha Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inakinzana na Sheria ya Benki Kuu.

Kwa mfano Sheria ya Benki Kuu inayoongoza biashara za Mabenki hapa nchini hairuhusu benki yeyote kutoa kiasi cha mkopo kinachotolewa kwa wakati mmoja kwa wateja wa aina hiyo hiyo moja kama walivyo wanafunzi wanaosoma kwenye Vyuo vya Elimu ya Juu.

Vilevile Sheria iliyoanzisha Bodi ya Mikopo iliyotungwa na Bunge lako Tukufu inaelekeza kuwa mikopo inayotolewa kwa wanafunzi husika isitozwe riba ya aina yeyote na inarejeshwa kwa kipindi kirefu cha miaka kumi baada ya mwanafunzi kuhitimu masomo yake.

(c)Mhehsimiwa Spika, iwapo utoaji wa mikopo utafanywa na benki gharama za uendeshaji zitakuwa zaidi ya asilimia 10 ya kiasi kilichokopeshwa mbali na riba. Kwa sasa gharama za uendeshaji kwa Bodi ya Mikopo ya wanafunzi wa Elimu ya Juu ni asilimia 3.5 na hakuna riba. Hivyo kutoa mikopo kupitia benki hakutapunguza gharama za uendeshaji.

swali 3
Mbilinyi, Osmund Joseph [CHADEMA]
Mbeya Mjini Constituency
Session No Question No To the Ministry of Sector Date Asked
4 310 INDUSTRIES, TRADE AND MARKETING Industry 26 July 2011
Principal Question No
Sababu zilizotolewa wakati Serikali inabinafsisha Kiwanda cha Zana za Kilimo Mbeya ni pamoja na kuongeza ajira kwa wananchi. Lengo la Sera ya Kilimo ya Mwaka 1997 ni kukifanya kilimo kiwe cha kisasa na endelevu hivyo zana za kilimo kuwa muhimu sana:¬

(a) Je, kwa kukibinafsisha kiwanda hicho ajira zimeongezeka kuliko ilivyokuwa kabla ya kubinafsishwa?

(b) Je, kwa nini kiwanda hicho kisirejeshwe Serikalini ili kufanya uzalishaji ukidhi malengo ya uanzishwaji wake kwenda sambamba na mkakakati wa kilimo kwanza pamoja na kuongeza ajira kwa wananchi wa Mbeya?
ANSWERS TO PRINCIPAL QUESTION #310 SESSION # 4
Answer From Hon. Malima, Adam Kighoma Ali
INDUSTRIES, TRADE AND MARKETING
NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI

(K.n.y. WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA) alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Viwanda na Biashara, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Joseph Mbilinyi, Mbunge wa Mbeya Mjini lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:

(a) Mheshimiwa Mwenyekiti, kiwanda cha Zana za Kilimo (ZZK) kilifungwa mwezi Mei, 1998 kutokana na kushindwa kujiendesha na hatimaye kufilisiwa mwaka 2002. Mali za kiwanda ziliuzwa kwa Kampuni ya CMG Investment. Mnunuzi baada ya kumiliki kampuni hiyo na kufanya mchanganuo, amefikia maamuzi kuwa uzalishaji wa zana za kilimo hauna faida kwake na hivyo mnunuzi ameamua kuanza mchakato wa kuanzisha kiwanda cha kuzalisha bia aina ya Serengeti.
Wakati akijiandaa na mpango huo karakana imefufuliwa na kuna uzalishaji mdogo mdogo wa matoroli na vinu vya kukoboa na kusaga nafaka ambao umeanza mwezi Juni, 2011 kulingana na mahitaji ya mteja mmoja mmoja. Ajira iliyoko pale kwa sasa siyo ajira ya kudumu.

(b)Mheshimiwa Mwenyekiti, utaratibu wa ufilisi haumlazimishi mnunuzi kuwasilisha mpango wa uwekezaji wakati wa kununua mali husika.
Aidha kulingana na Sheria ya ufilisi mnunuzi ana haki ya kumiliki mali iliyonunua na kutumia anavyoona itampatia faida. Hivyo endapo Serikali inataka kurejesha kiwanda cha ZZK mikononi mwake ili kiweze kukidhi malengo ya uanzishwaji wake, itabidi ifanye mazungumzo na mnunuzi ya kiwanda hicho ya kununua kiwanda hiki tena na kukifufua ili kiweze kuzalisha zana za kilimo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kumshauri Mheshimiwa Mbunge, endapo atapata wawekezaji wanaoweza kukiendesha kiwanda hicho kwa faida wawasiliane na mmiliki wa sasa au wawasiliane na Wizara ya Viwanda na Biashara ili tuweze kumsaidia kufanya uwekezaji katika maeneo hayo ama kwa kukinunua kiwanda hiki na kuzalisha Zana za Kilimo au kwa kutengeneza utaratibu mbadala.
 
You can't expect more from him. He's Form 4 leaver.

Huyo naibu waziri wako aliyesemaga Tanzania ni Muungano wa visiwa vya Zimbabwe na Tanganyika tena with brocken english yeye ana elimu ya Phd za vyuo vikuu vya kata au umeshasahau. Elimu yenyewe unayoizungumzia ni hii isiyo na mataala. Kwa hiyo wakiitwa wenye digree na wewe utepeleka makanyagio yako. Ulishawahi kumwonaga Dewji ata siku moja akichangiaga hoja ata siku moja? Shame on you.
 
Kwanza nadeclare interest me ni CHADEMA.
Huyu mkuu huwa hachangii chochote akiwa bungeni, labda ishu ihusu bongo fleva au Ruge.
Ameshindwa hata na Maji marefu ambaye huuliza maswali ya nyongeza na ya msingi kuhusu wapiga kura wake.
Ivi Mbeya mjini hamna matatizo ya maji, barabara , shule na clinic kweli?

Anadhani alichaguliwa kwa ajili ya kuongelea hati miliki za wasanii?

SIJUI HII YOUTUBE inaongelea BONGO FLEVA na RUGE??? BE REAL YOUNG MAN acha CHUKI

[video=youtube_share;JAajYxzjvPA]http://youtu.be/JAajYxzjvPA[/video]​
 
KakaJambazi ( mara nyingi hutumia mtutu kuiba vihela vidogo ) kwani shida za Mbeya unazozijua wewe ni zipi ? Kumbuka Mbeya siyo Kama Iramba , wanakotegemea Mahindi ya Misaada.
 
Yaani huwa najiuliza waliomchagua walitarajia nini kutoka kwake, ila anachofanya ndio kilicho ndani ya uwezo wake.

Huo uwaziri kivuli wenyewe sijui kama anajua majukumu yake zaidi ya kuendesha mapambano na clouds kwa kutumia wasanii.

Kwenye filamu sioni mapambano yoyote, Wasanii wana vilio mpaka makoo yamekauka, matatizo ya usambazaji, Mikoani hakuna cha maana kinaendelea kuhusu filamu kila msanii analazimika kukimbilia Dar ndio aonekane anafanya kitu.

Ni mikoa mingapi ameshatembelea na kukutana na wasanii wa filamu kusikiliza matatizo yao ?

Hiyo bongo fleva anaonekana kuishupalia ili tu atekeleze mapambano yake na clouds kama mlivyoona kwenye msiba wa Ngwair.

Kesho na keshokutwa chadomo wanatarajia huyu ndio awe waziri wa utamaduni vijana na michezo.....ee Mungu tunusuru waja wako.

KUNA WABUNGE WAKISIMAMA BUNGENI UTAWASIKIA TU...KUDADADEKI......Deus Kibamba

Mbona hujamuuliza dr J M Kikwete yako wapi maisha bora kwa watanzania? Aliahidi kwa mbwembwe 2005 and now it's almost 8 years and no sign of it!!
 
Kwanza nadeclare interest me ni CHADEMA.
Huyu mkuu huwa hachangii chochote akiwa bungeni, labda ishu ihusu bongo fleva au Ruge.
Ameshindwa hata na Maji marefu ambaye huuliza maswali ya nyongeza na ya msingi kuhusu wapiga kura wake.
Ivi Mbeya mjini hamna matatizo ya maji, barabara , shule na clinic kweli?

Anadhani alichaguliwa kwa ajili ya kuongelea hati miliki za wasanii?
Hakuna matatizo hayo Mbea.ila wasanii wananyoywa na kufa maskini. Mf marijani rajabu.sugu anawakilisha jamii Fulani itambulike haki zake. Masaburi hayana ubongo usiyatumie kueneza ujinga
 
wewe uliesoma una nini cha maana??kumzidi asiyesoma..mfano;umesoma unakufa na vumbi la chaki,asiyesoma anakula ful kipupwe..nan mwenye akili ?

hahahahahh! uzuri naweza kuwa mwl kokote kule duniani lkn huyo Sugu wako anawe akuwa mbunge wa tz tu!
akienda hata hapo kenya ubunge hana
 
unalako jambo au na wewe ni redio ya wafu, siyo mpenzi wa kufatilia bunge lakini niliwahi kumsikia sugu akishupalia swala la hospital ya mbeya kwa rushwa na jenereta kuwashwa wanapoenda wakubwa kutibiwa..ukumbuke bongo flava inamhusu yeye kwasababu kuu 2, yeye ni waziri kivuri,yeye ni mwana bongo flava

Siyo kila jambo lazima upinge!! mshauri kamanda kuwa Mbeya kwanza siasa baadaye!!!
 
hahahahahh! uzuri naweza kuwa mwl kokote kule duniani lkn huyo Sugu wako anawe akuwa mbunge wa tz tu!
akienda hata hapo kenya ubunge hana

nakumbuka mwl wangu wa grammar alinifundisha moja ya matumizi ya conditional sentences ni kujifariji..ok yaishe tusije wafaidisha watu
 
Back
Top Bottom