Kwa Utendaji kazi wa Samia Suluhu Hassan, ni Muda tu kabla Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu hajarudi CCM. Sugu anasema watu wenye ushawishi ni yeye na JK

Robert S Gulenga

JF-Expert Member
Jan 3, 2013
2,151
1,489
Hakuna ubishi kwamba utendaji kazi uliotukuta wa Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan umewafanya Wapinzani wengi kuona kile walichokuwa wanakipigania kwa miaka mingi ndicho kinachofanyika na Serikali ya awamu ya sita.

Wapinzani wamekuwa wakipigania ustawi wa Jamii kwa Watanzania ikiwa ni pamoja na kuboresha utolewaji wa huduma muhimu, kama huduma za Afya- katika hili Mh. Rais Samia Suluhu Hassan amekamilisha na kujenga Vituo vya Afya katika kila Kata, amehakikisha dawa na vifaa tiba vinapatikana katika kila kituo cha kutolea huduma za Afya zilizopo kila kijiji, kata, tarafa, Wilaya na zile Hospital za Mkoa.

Wapinzani kwa miaka yote wamepigania kuhakikisha Miuondo mbinu ya Elimu inaboreshwa, Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Samia Suluhu Hassan ndani ya miaka miwili ya utendaji wake amehakikisha hakuna Mtoto aliyefikisha umri wa kwenda shule yuko nyumbani. Mh Rais amejenga Shule za Sekondari kwa kila kata ambayo haikuwa na Shule ya Sekondari, amejenga kila mkoa Shule Maalum ya Wasichana (Sekondari), amejenga madarasa mapya kwa kila shule iliyokuwa na upungufu, hakuna mtoto wa Kitanzania ambaye kwa sasa anasomea chini ya mti wala kukaa chini. Wakurugenzi wa Halmashauri wanakesha usiku na mchana kuhakikisha miradi hii ya maendeleo inakamilika.

Miradi mingi ya maendeleo ikiwemo ya maji, barabara, Kilimo SGR, JNHPP e.t.c inaendelea kutekelezwa na itakamilika kama ilivyopangwa, Mungu mbariki Mh. Rais Samia Suluhu.

Wpinzani wengi wanaoitakia nia njema Tanzania kwa sasa wameanza kushusha silaha zao na kuamua kuunga mkono juhudi za Mh Rais katika kuwaletea Watanzania Maendeleo. Moja ya wapinzani ambao wamekubaliana na muziki wa Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Mbunge wa zamani wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu au the real Jongwe.

Ukikutana na Sugu atakwambia maisha ni kupigania vitu bora kwa Watanzania, Watanzania wawe na Maisha mazuri, kama Rais anafanya hivyo ya nini kupinga juhudi zake? ni bora kuungana naye. Kifupi ni kwamba Sugu ameona Maendeleo ya Tanzania yatapatikana chini ya CCM tu, na katika kutambua hilo na nukuu "anasema katika Dingi wanaokubalika na Mayanki na itabaki hivyo mpaka siko anadedi..kwa Bongo ni yeye na Mzee Jakaya"'. Sugu anatuma ujumbe kwa Vijana kuwa muwamini Wazee wa CCM ndio maana hajamtaja hata yule ndugu yetu aliyeko Canada kuwa anakubalika.

Sugu, karibu CCM uungane na Mh. Tulia Akson kuijenga Mbeya yetu. Siasa ni Sayansi na Mwanasayansi mahili wa siasa kwa sasa hapa Tanzania ni Samia Suluhu Hassan

Mungu ibariki Tanzania.

Mungu mbariki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.
 
Msimamo ndio unafanya mtu awe upande gani, Sugu na Lady Jay D washatambua upande wanaotakiwa wawe kwa sasa
Vijana wa CCM wa siku hizi hamjiamini kabisa

Yaani hapo unamtamani Sugu zaidi ya Makamba na Mwigullu

Sishangai Katambi, Shonza na Silinde wamewakuta hapo na kujitwalia Uwaziri huku mnawashangilia kama mazuzu vile

Enzi zetu za TYL hatukuwa na huu usimbilisi na umbwiga
 
Alichokiongea huyo form four felia , ndicho kinacho akisi ujinga wake!

Anasema Nyerere afananishwe na Nani?

Upuuzi kabisa!
 
Vijana wa CCM wa siku hizi hamjiamini kabisa

Yaani hapo unamtamani Sugu zaidi ya Makamba na Mwigullu

Sishangai Katambi, Shonza na Silinde wamewakuta hapo na kujitwalia Uwaziri huku mnawashangilia kama mazuzu vile

Enzi zetu za TYL hatukuwa na huu usimbilisi na umbwiga
johnthebaptist mzee CCM ina Vijana wenye uelewa mkubwa, CCM ndio chama kikubwa kilichobaki Afrika
 
Bado maji, umeme na swala la watumishi wa umma.bado hapo hajqmaliza.
 
Bado maji, umeme na swala la watumishi wa umma.bado hapo hajqmaliza.
Mkuu mwaka wa fedha ulioisha zaidi ya Watumishi laki mbili walipandishwa madaraja na vyeo, Watumishi hawa walikuwa na zaidi ya miaka mitano hawajawahi kupandishwa vyeo wala madaraja, mwaka huu wa fedha pia Watumishi wengi watapandishwa madaraja , Mkuu miradi mingi ya maji na umeme inaendelea kutekeleza
 
Back
Top Bottom