Jokate: Rais Samia kamaliza yote, deni lipo kwetu sisi kuhakikisha tunamtendea haki

Hamduni

Senior Member
Apr 25, 2020
155
108
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) Ndugu. Jokate Mwegelo amesema kuwa Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kipindi cha miaka 3 ya Uongozi wake kwakuwa amefanya makubwa katika sekta mbalimbali za Afya, Elimu, Miundombinu, Maji na Kuimarisha Demokrasia.

Ndugu. Jokate amesema kulingana na kazi kubwa iliyoifanya Rais Samia hakika amepitiliza kiwango na kuwataka Wanawake wote kumshukuru na kuhakikisha wanamtendea haki kwa kumpa kura nyingi za kishindo ifikapo muda rasmi wa uchaguzi.

IMG-20240326-WA0017.jpg
IMG-20240326-WA0012.jpg

🗓️ 26 Machi, 2024
 
Kamaliza yote kwake kumpa ulaji, huku mtaani bado ana madeni makubwa ambayo hana uwezo wa kuyalipa asiwasemee ambao hajamalizana nao
 
WANAWAKE HATUTACHOKA NA TUTAENDELEA KUMTII, KUMSEMEA, KUMTETEA NA KUMSHUKURU RAIS DKT. SAMIA KATIBU MKUU UWT JOKATE

"Wanawake wa Tanzania hatujaja kumpongeza tuu bali tumekuja kumshukuru Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi njema na nzuri anayoendelea kuifanya katika kuliongoza Taifa letu."

"Tunamshukuru Rais Dkt. Samia katika kukiongoza vema Chama Cha Mapinduzi nasi UWT tunatambua kazi yake kubwa anayoifanya ndio jeuri yetu na kupelekea Wanawake kuendelea kuwa wamoja yote kwasababu amekuwa Mama mwenye kutulea katika misingi ya Umoja na Mshikamano"

"Wanawake tunaendelea kumtii Rais Dkt. Samia na hatutachoka kumsemea, kumtetea na kumshukuru kwa kuwa amekuwa akifanya kazi bila kuchoka kwa vitendo na yenye kuonekana"

"Watanzania wanaamini vitendo vina sauti na kishindo kikubwa nasi tuendelee kumuunga mkono kwa kuwa mabalozi wazuri wa kumsemea na kumlinda kwakuwa kazi anayoifanya ni kubwa na inaoekana"

Ndugu. Jokate Mwegelo
Katibu Mkuu wa UWT

🗓️ 26 Machi, 2024

#KongamanoLaKumshukuruRaisSAMIA
#Miaka3YaRaisSamia
#UWTImaraJeshiLaMamaSamia
#MwanamkeNipo
#KaziIendelee
 
Attachments

  • IMG-20240326-WA0390(3).jpg
    IMG-20240326-WA0390(3).jpg
    533.7 KB · Views: 1
SAMIA KAMALIZA YOTE, DENI LIPO KWETU SISI KUHAKIKISHA TUNAMTENDEA HAKI - CDE. JOKATE

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) Ndugu. Jokate Mwegelo amesema kuwa Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kipindi cha miaka 3 ya Uongozi wake kwakuwa amefanya makubwa katika sekta mbalimbali za Afya, Elimu, Miundombinu, Maji na Kuimarisha Demokrasia.

Ndugu. Jokate amesema kulingana na kazi kubwa iliyoifanya Rais Samia hakika amepitiliza kiwango na kuwataka Wanawake wote kumshukuru na kuhakikisha wanamtendea haki kwa kumpa kura nyingi za kishindo ifikapo muda rasmi wa uchaguzi.

🗓️ 26 Machi, 2024

#KongamanoLaKumshukuruRaisSAMIA
#Miaka3YaRaisSamia
#UWTImaraJeshiLaMamaSamia
#MwanamkeNipo
#KaziIendelee
 
Attachments

  • IMG-20240326-WA0388(2).jpg
    IMG-20240326-WA0388(2).jpg
    543.9 KB · Views: 1
Mnamtetea dhidi ya nani nakwakosa gani? Badala yeye awatetee nyie ndio mumtetee. Majeshi ndio yanatetea maiki hazitetei.
Mbona kama watu wamechanganyikiwa
 
Sasa huyo Mwegelo sihataki wanawake wakipigia kura wanaume? Anayokazi kushawishi wanaume wenye akili timamu wapigie wanawake
Ametangaza ubaguzi huyo atulie upepo upite
 
Mfumo wetu wa elimu ubadilishwe ili utengeneze viongozi wenye faida tofauti na Hawa wa sasa ambao Kila kitu wanasifi rais wakati kiuhalisia hakuna Cha maana alichofanya.ikiwezekana tuige mfumo wa elimu wa Kenya au uganda.huko hakuna upuuzi wa kusifu hata pasiposifika
 
Kawaulize watu wa kata ya Kasingirima kule Kigoma/Ujiji kama demokrasia imeimarika.

Halafu mwenezi amewapiga marufuku uchawa na kujipendekeza.
 
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) Ndugu. Jokate Mwegelo amesema kuwa Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kipindi cha miaka 3 ya Uongozi wake kwakuwa amefanya makubwa katika sekta mbalimbali za Afya, Elimu, Miundombinu, Maji na Kuimarisha Demokrasia.

Ndugu. Jokate amesema kulingana na kazi kubwa iliyoifanya Rais Samia hakika amepitiliza kiwango na kuwataka Wanawake wote kumshukuru na kuhakikisha wanamtendea haki kwa kumpa kura nyingi za kishindo ifikapo muda rasmi wa uchaguzi.

View attachment 2945029View attachment 2945030
🗓️ 26 Machi, 2024
Uyo mwanaume nae ni umoja wa kina mama?
 
Mhh ni hiihii Tanzania ameimaliza .... ambayo bado watoto wanakaa chini ya mti, Maji hakuna, Barabara na umeme kizungumkuti au ni apo Daslamu tu.
 
Back
Top Bottom