John Mrema akanusha taarifa za kifo chake zilizoenea mtandaoni

Huyo bwashee anajulikana na nani hadi azushiwe kifo?
Nimekutana na michango yako ya kizandikizi na ya kihila hii ni mara ya pili kwenye thread mbili tofauti ndani ya muda huu mchache, kwanini huishi mtaja mtu kwa kabila lake, inakusaidia nini au unafaidika na nini ukifanya hivyo? Pia wewe ni kabila gani ili tuende sawa?
 
Chadema wataalam wa kuvumishia wenzao vifo sasa naona wameanza kuvumishiana wenyewe kwa wenyewe: chickens have come home to roost!
 
Sio kuwa ccm ndo wamelileta hili ili lile la faru john wa kule nairobi lipungue kufuatiliwa??
Ah jiwe kweli kweli korona inamuonyesha adabu na kumtaka ahache dharau
Chadema wataalam wa kuvumishia wenzao vifo sasa naona wameanza kuvumishiana wenyewe kwa wenyewe: chickens have come home to roost!
 
Nimekutana na michango yako ya kizandikizi na ya kihila hii ni mara ya pili kwenye thread mbili tofauti ndani ya muda huu mchache, kwanini huishi mtaja mtu kwa kabila lake, inakusaidia nini au unafaidika na nini ukifanya hivyo? Pia wewe ni kabila gani ili tuende sawa?
Mi sijui kabila lake, ila najua aliwahi kusema humu kuwa nyumbani kwao ni Useri (Rombo), sasa sijui atakuwa kabila gani?!
 
Imekanushwa Rasmi haumwi

======

Leo nimepata taarifa za kustua zilizozushwa kwamba Mimi John Mrema nimefariki, na nimeanza kupokea salamu za pole. Wengine Watanzania wakienda nyumbani kwangu, wakienda kijijini kwetu Moshi.

Ninachopenda tu ni kuwathibitishia tu kuwa mimi siumwi, sijasafiri kwenda Afrika ya Kusini. Mara ya mwisho kwenda nje ya nchi ilikuwa mwaka jana mwezi wa 10. Nipo Dar es Salaam, nipo nyumbani kwangu najikinga na Corona.

Kwahiyo, taarifa hizo ni za uzushi na ninaomba kila mtu azipuuze.

Lakini nawashukuru wale wote walionitumia salamu za pole. Nimejua Watanzania mnanithamini. Nashukuru sana.

Lakini, naamini taarifa hizo zimezushwa na watu ambao hawataki kinga ndiyo maana wanahusisha kwamba nimeenda kupata chanjo ya kinga dhidi ya Corona nchini AFrika Kusini. Waliozusha ni watu wanaopinga chanjo dhidi ya Corona.

Mimi naamini chanjo ni muhimu kwasababu italinda maisha yetu. Na tatu, Inawezekana pia taarifa hizo zinazushwa kwasababu kuna taarifa nyingine zenye kuzua taharuki kwenye nchi.

Kwahiyo taifa lina haki ya kupewa taarifa sahihi na siyo propaganda na uzushi, kuzushiana vifo. Inasababisha maumivu kwa familia, kwa ndugu jamaa na marafiki.

Nawashukuru sana, ahsanteni sana!




Inawezekana wanaccm wamekuweka wewe kuwa mbadala.
 
"wakienda nyumbani kwangu ... nipo nyumbani kwangu". Sasa vipi uoneshe haukuwepo nyumbani halafu upo nyumbani na wale walioenda nyumbani kwako hawakukuona. Una nyumbani ngapi?

Sasa hiyo ya taifa linastahili kupata taarifa inaingiaje hapa?
 
Back
Top Bottom