John Mrema akanusha taarifa za kifo chake zilizoenea mtandaoni

M-mbabe

JF-Expert Member
Oct 29, 2009
13,203
23,019
Jamii ikifikia mahali watu wanahasimiana hadi kuombeana vifo na majanga, jee, hiyo jamii ipewe sifa gani? Mimi nitakuwa nimekosea kweli kuiita ni jamii ya watu wenye roho mbaya na unyama unyama?

The Tanzania I used to see and know under Mwalimu (RIP mzee wetu) is totally unrecognizable today!


Mkurugenzi wa mawasiliano chadema John Mrema kupitia mtandao wa Twita amekanusha taarifa zinazoenea katika mitandao mbali mbali zinazodai kuwa amefariki.

Kupitia video fupi John Mrema amesema "Leo nimepata taarifa za kustua zilizozusha kwamba mimi John Mrema nimefariki na nimeanza kupokea salamu za pole, wengine Watanzania wameenda nyumbani kwangu na wengine wakienda kijijini kwetu Moshi.

Nachopenda kuwathibitishia kuwa mimi siumwi, sijasafiri kwenda Afrika Kusini mara ya mwisho kwenda nje ya nchi ilikuwa mwaka jana mwezi wa kumi niko Dar ed Salaam nipo nyumbani kwangu najikinga na Corona."

Aidha, Mrema amesisitiza kuwa "inawezekana taarifa hizo zinazushwa kutokana na kuwepo kwa taarifa zinazozua taharuki ndani ya nchi.

Hivyo, taifa lina haki ya kupewa taarifa sahihi na sio kuweka propaganda na uzushi kuzushiana vifo inaleta taharuki kwa ndugu jamaa na marafiki."
 
Kwani kwazinduka mara ngapi ? Maana reporter wetu anasema ana tabia ya kuzinduka

Mwenyewe natamani niskie kuwa............ tena
 
Tutamzika shetani na kazi zake zote siku si nyingi, kila kitu kitakua sawa, Tanganyika yetu aliotuachia Nyerere itakua salama.
 
R.I. P Azory!

R.I.P kamanda Mawazo!

R.I. P Akwelina!

R.I.P Saanane!

R.I.P wapigania haki wote !
 
Baada ya watu duni wanaolipwa kusambaza taarifa za uongo za kifo cha Mkurugenzi wa Itifaki wa Chadema Mh John Mrema , Yeye Mwenyewe amejitokeza hadharani na kuthibitisha kwamba yuko hai na wala hana hata kikohozi wala mafua ya vumbi .

IMG_20210310_141952.jpg
 
uvccm wanazushia watu misala ili kupunguza kasi ya taharuki yao.. hakuna kinachodumu milele..mitano tena
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom