John Mrema akanusha taarifa za kifo chake zilizoenea mtandaoni

Kuna siku fahamu zitarudi na utajua maana ya upinzani.
upinzani hawajawai kuwa ni watu wenye akili hapa Tanzania, hawajitambui wanasahau, hawana vision, kwa kifupi hawajielewi. Mara wamponde Kikwete mara tena wamsifie mara wamponde Mwinyi mara tena wamsifie, hivi hawa wanatumia akili sawasawa kweli, unawezaje kumponda mtu alafu wakati huo huo umsifie tena, kama sio ufyatu ni nini.
 
Tatizo kwa sasa taarifa za uvumi na ambazo siyo za kweli zimekuwa zikipewa kipaumbele sana, tumekuwa na kizazi cha ajabu kuliko hata maajabu yenyewe.
Ukisema "tumekuwa na kizazi cha ajabu" unamaanisha namba moja anaivuruga familia!?

Uvumi huja baada ya ukweli kufichwa,

halafu tu ktk kumbukumbu zako kuna jiwe gani kuu lililopita watu walitamani na kulitakia mabaya kama hili la sasa?

Umemjua mchawi sasa?
 
Jamii ikifikia mahali watu wanahasimiana hadi kuombeana vifo na majanga, jee, hiyo jamii ipewe sifa gani? Mimi nitakuwa nimekosea kweli kuiita ni jamii ya watu wenye roho mbaya na unyama unyama?

The Tanzania I used to see and know under Mwalimu (RIP mzee wetu) is totally unrecognizable today!


Mkurugenzi wa mawasiliano chadema John Mrema kupitia mtandao wa Twita amekanusha taarifa zinazoenea katika mitandao mbali mbali zinazodai kuwa amefariki.

Kupitia video fupi John Mrema amesema "Leo nimepata taarifa za kustua zilizozusha kwamba mimi John Mrema nimefariki na nimeanza kupokea salamu za pole, wengine Watanzania wameenda nyumbani kwangu na wengine wakienda kijijini kwetu Moshi.

Nachopenda kuwathibitishia kuwa mimi siumwi, sijasafiri kwenda Afrika Kusini mara ya mwisho kwenda nje ya nchi ilikuwa mwaka jana mwezi wa kumi niko Dar ed Salaam nipo nyumbani kwangu najikinga na Corona."

Aidha, Mrema amesisitiza kuwa "inawezekana taarifa hizo zinazushwa kutokana na kuwepo kwa taarifa zinazozua taharuki ndani ya nchi.

Hivyo, taifa lina haki ya kupewa taarifa sahihi na sio kuweka propaganda na uzushi kuzushiana vifo inaleta taharuki kwa ndugu jamaa na marafiki."
HAKUNA ubaya hata akifa maana HAKUNA wa kuishi milele.
 
Back
Top Bottom