John Mrema akanusha taarifa za kifo chake zilizoenea mtandaoni

Hivi ukizushiwa kifo..., alafu ukatokea ni mpaka useme kwamba nipo hai ? (Si kutokea kwako tu, by default ni kwamba ni mzima)?

Au unaweza ukawa mzimu?, Ila hii Awamu imeharibu kabisa taifa hili..., kuendekeza USISI na UWAO umeleteleza watu kuwa na tabia za kichawi na kufurahia vifo vya wengine. Hivi kweli mababu zetu walipigania Uhuru na kumuondoa Mkoloni ili tuje tuishi kama wakoloni weusi na mafukara ?
 
Tatizo kwa sasa taarifa za uvumi na ambazo siyo za kweli zimekuwa zikipewa kipaumbele sana, tumekuwa na kizazi cha ajabu kuliko hata maajabu yenyewe.
 
Sijui hiki kizazi cha Watanzania waliokosa utu kiasi cha kushabikia wenzao kufa ni wa aina gani😥😥

Wewe unayeombea na kufurahia umauti kwa wengine kwanza ujue tuu kwamba wakifa wao wewe hufutiwi kifo chako na pia hujui wewe utaondoka lini

Pole sana kwa John Mrema na familia
 
Kwahiyo wanaufipa wanataka wamuone Rais ambaye hawakumpigia kura au nia yao nini hasa???? rais wenu yupo kwa amsterdam beberu sugu... Rais wa wanyonge anachapa kazi mpaka sasa Tz
 
Imekanushwa Rasmi haumwi

======

Leo nimepata taarifa za kustua zilizozushwa kwamba Mimi John Mrema nimefariki, na nimeanza kupokea salamu za pole. Wengine Watanzania wakienda nyumbani kwangu, wakienda kijijini kwetu Moshi.

Ninachopenda tu ni kuwathibitishia tu kuwa mimi siumwi, sijasafiri kwenda Afrika ya Kusini. Mara ya mwisho kwenda nje ya nchi ilikuwa mwaka jana mwezi wa 10. Nipo Dar es Salaam, nipo nyumbani kwangu najikinga na Corona.

Kwahiyo, taarifa hizo ni za uzushi na ninaomba kila mtu azipuuze.

Lakini nawashukuru wale wote walionitumia salamu za pole. Nimejua Watanzania mnanithamini. Nashukuru sana.

Lakini, naamini taarifa hizo zimezushwa na watu ambao hawataki kinga ndiyo maana wanahusisha kwamba nimeenda kupata chanjo ya kinga dhidi ya Corona nchini AFrika Kusini. Waliozusha ni watu wanaopinga chanjo dhidi ya Corona.

Mimi naamini chanjo ni muhimu kwasababu italinda maisha yetu. Na tatu, Inawezekana pia taarifa hizo zinazushwa kwasababu kuna taarifa nyingine zenye kuzua taharuki kwenye nchi.

Kwahiyo taifa lina haki ya kupewa taarifa sahihi na siyo propaganda na uzushi, kuzushiana vifo. Inasababisha maumivu kwa familia, kwa ndugu jamaa na marafiki.

Nawashukuru sana, ahsanteni sana!



 
Back
Top Bottom