PreGE2025 John Heche akamatwa na Polisi Kariakoo

PreGE2025 John Heche akamatwa na Polisi Kariakoo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Kwahiyo unafurahia Mama Samia kuitwa Dikteta Samia?
Lissu ndio dikteta uchwara, kila anayemuhoji anafukuzwa kwenye chama chenu sio!!? Mama hawezi kuitwa dikteta kwa kulinda amani ya nchi dhidi ya wapumbavu wachache kama nyie.
 
Taarifa rasmi kutoka CHADEMA imesema kwamba Jeshi la Polisi limemkamata Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche, katika eneo la Kariakoo na kumpeleka kituo cha Polisi Msimbazi.

Hata hivyo, baadaye aliondolewa kituoni hapo na kupelekwa kusikojulikana.

Viongozi kadhaa waliokwenda kituo cha Polisi Kati kufuatilia suala hilo wameelezwa kuwa Heche hajawahi kufikishwa hapo.



View attachment 3312400


View attachment 3312401


Polisi wamesema kuwa hawajamkamata mtu
 
Apana wanasombwa tu agano jipya Mnyika mwenyewe njaaa ishamchosha Offisin aya yanayotokea anachekea chooni kimya kimya !!!!!!!!!!@
thubutu mnyika keshakula kona mbaya, hata kutweet hajatweet, kuna mtu aliwahi sema hata ukitupa box la biscuit mnyika mbio
 
Kwa macho ya nyama tu kupitia comparison and contrasting huna tofauti na nyani ambaye anaamini ndizi ni tamu kuliko sega la asali. Pole sana kijana wa hovyo.
Sasa nyie mnaojiita wanyonge mnaweza tambua nini zaidi ya kuona watu ambao siyo wanyonge kuwa ni Nyani. Pole sana Sukuma gang
 
polisi vipi mnamchelewesha mleta fujo kama huyo sokoni?

mnajadiliana nae nini?

OCD msimbazi ukajitathmnini,
hatuwezi kuvuruga shughuli za biashara kariakoo kwa kusumbuana kujibizana na vibaka wa wavuruga biashara wa aina hiyo, mkamatene mkamweke korokoroni mara moja:BASED:
Safi kabisa.Huu ndio ukweli
 
Cheti fake au Cheti halisi mimi cha nini sina ajira sehemu yoyote ila akili yako inawaza kuwa kila mtu ana cheti. Akili hizi kama zako ndizo alikuwa nazo Jiwe. Wanyonge mko wengi sana.
Basi utakuwa shoga! Hahaha...!!
 
Lissu ndio dikteta uchwara, kila anayemuhoji anafukuzwa kwenye chama chenu sio!!? Mama hawezi kuitwa dikteta kwa kulinda amani ya nchi dhidi ya wapumbavu wachache kama nyie.
kabisa, tangu lissu aingie chadema kawafukuza zitto kitilamkumbo kafulila mhonge luhwanya ester matiku ester bulaya halima mdee, john mrema, alimpokonya form dr.slaa, yaani vurugu ka za dadapoa wakimakonde
 
H
Duh hatari! Yale ya Kiza Besigye yamehamia nchini kwetu.

Kumbe alikuwa serious aliposema:
"ukinikuna vizuri mimi nakukuna huku nakupapasa tena nakupuliza ufu ufu, ukinipara nakuparura"

Lakini anachokipanda atakivuna.
😂😂😂😂😂😂
 
Mimi sijawahi kuwa mnyonge. Ni raia mwenye akili timamu tu nayemiliki NIDA na PASSPORT ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hakuna mtu timamu anayejielewa ambaye aliamani kwenye sera za huyo Jiwe wenu. Mtaje hata mmoja kama yupo, au mzee wa Jalalani 😂😂😂😂😂😂
Nida na Passport ni haki yako na siyo mambo ya kujivunia kumiliki. Ukiitwa mnyonge unakataa lakini vitu unavyomiliki hata madada poa wanamiliki pia
 
Ameambiwa akawa anabisha huku gari yake inasababisha msongamano wa magari ulitaka askari wafanyaje?

Tena wamemhurumia kumkamata alitakiwa abondwe hasa aende mahabusu ulimi ukiwa nje

Nimeamini askari polisi wana huruma aisieee
Wana hekima na busara.Askari ni wasomi
 
Dar CHADEMA mwisho ilikuwa kipindi cha Lowassa kaenda CHADEMA

Baada ya Lowasa kurudi CCM

CHADEMA haina Chake Dar es Salaam
Nakumbuka kipindi cha dhalimu Magu kulikuwa na uchaguzi wa marudio. Mtangazaji wa ITV aitwaye Sam Mahela alionyesha jamaa wakiingiza mabox ya kura, vituoni, polisi walikuwepo na msimamizi wa uchaguzi anaangalia! Baadae mtangazaji akaenda kumuuliza msimamizi wa kituo inakuwaje mabox ya kura yanaingizwa yakiwa na kura, msimamizi kwa aibu na hofu akamwambia yeye ana kazi nyingi hapo kituoni, sio kuangalia mabox ya kuta tu! Mtangazaji akamfuata polisi kumuuliza inakuwaje. Polisi akamwambia hiyo ni kazi ya msimamiz wa kituo hilo halimuhusu! Ndani ya dakika 30 matangazo mubashara yakakatwa, na likatoka agizo kuwa hakuna ruhusa kurusha matangazo live. Baadae usiku huo nikasikia ITV wanaomba msamaha kwa kurusha habari ambayo ingeweza kuleta machafuko nchini. Hiyo Dar ya ccm😂😂😂 Na toka siku hiyo ikawa kurusha uchaguzi mubashara ni maeneo tu ccm wanafaidika.
 
Kumbe na wewe ni masikini na bado unafurahia ZULUMA dhidi ya Watanzania wenzako?!
Sijadhulumiwa chochote, kama sina ni uvivu wangu wa kutojituma kwenye biashara zangu na kilimo, baasi! Sina aliyenidhulumu chochote boya we!!
 
Toka jiwe alivyokanyaga katiba na tukanyamaza, basi niwaambie tu hata aje malaika atafanya km alichofanya mtangulizi aliyemuachia kijiti..!! Mitanzania sisi minafki tutulie wote tutafikiwa..!!
 
Basi utakuwa shoga! Hahaha...!!
Ona sasa, umekimbilia kwenye ujinga tena. Wewe ni shoga kwani? Huna unalowaza zaidi ya ushoga. Waza kukuza kupato chako ili uache mambo ya kujiita mnyonge
 
polisi vipi mnamchelewesha mleta fujo kama huyo sokoni?

mnajadiliana nae nini?

OCD msimbazi ukajitathmnini,
hatuwezi kuvuruga shughuli za biashara kariakoo kwa kusumbuana kujibizana na vibaka wa wavuruga biashara wa aina hiyo, mkamatene mkamweke korokoroni mara moja:BASED:
Mimi naona kama wamechelewa kumtia kibindoni, wangefanya hata juzi.
 
Watu wanapenda matatizo!!! Sasa ofisi ya chama ipo wakaenda kuongea na waandishi kariakoo!! Ni kumsika simba sharubu au vp?? Hii nchi haijawahi kuwa na utu !! Kama hujionei huruma wewe mwenyewe kwanza!!
 
Back
Top Bottom