JK na wabunge wa CCM Dodoma kimenuka

JK na wabunge wa CCM Dodoma kimenuka

Du sasa hivi ndio anajua kuwa TISS wanaweza kumshauri eeh? maana nina imani amekuwa akipuuza sana ushauri wao siku nyingi. Pia JK aache kusikiliza wagaga jamani nao wanampoteza. Tunasubiri mapya kutoka dom leo.
 
Kama una maana JK kawaambia wabunge wampigie kura ya kutokuwa na imani nae, hap namuunga mkono JK, kwani hizo kura hazitatosha na wabunge watajifunza kwa viboko sasa, kwani pamoja na mapungufu aliyonayo Rais, kama alivyo binadamu mwingine, Rais katika hili kasimamia upande sahhihi, na ni upande wa walio wengi nchi hii.
Bila wananchi "kupiga kelele" angefanya hayo unayodhani anayafanya?
 
MkamaP,
Kuhusu swali lako: kinachoendelea ni kwamba - kwa mujibu wa taarifa zinazoenea, wabunge wa CCCM feel offended na kitendo cha Rais Kikwete kukubali mapendekezo ya Chadema kwamba kuna ulazima wa kubadilisha mambo kadhaa ndani ya muswada uliopitishwa na bunge la CCM na CUF mwaka jana, kuhusu mchakato wa katiba mpya. Nasema bunge la CCM na CUF kwasababu wabunge wote wa Chadema (pia nadhani na wachache kutoka NCCR) walisusa na hivyo kutoka nje ya bunge, huku wabunge wa CCM wakiongozwa na kina Anne Kilango na wengine wengi, wakiwazomea. Wabunge wa CCM wanadai kwamba kitendo cha rais kukubali kwa mfano mchakato usimamiwe na wakurugenzi wa halmashari/manispaa kama Chadema wanavyotaka, badala ya wakuu wa wilaya kama wabunge wa CCM wanavyotaka, kitafanya mchakato huo uwe controlled na Chadema kwa madai kwamba wakurugenzi wa halmashauri nchini ni wanachama wa chadema.

Ufa huu baina ya Rais na Wabunge umepanuka zaidi pale alipokataa kuidhinisha ongezeko la posho zao. Kwahiyo hivi sasa ni mkakati wa wewe mwaga ugali, sisi tunamwaga mboga. Na tumeona miswaada miwili ya serikali wiki iliyopita yote ikipigwa chini na wabunge wa CCM. Kwa kifupi hali ndio imekaa hivyo. Tunabaki kushangaa zile kauli za 'ndiyoooooooooo', zikiambatana na makofi kwenye meza kuunga hata hoja zile za kumchekesha matonya, sijui mzuka ule umeenda wapi.

Hivi Rais akiwapiga chini wabunge woooote na akaitisha uchaguzi mpya Rais kama yeye binafisi (Kikwete) atakosa nini? CCM najua wengi hawatarudi mjengoni na wakati huohuo chama chao kitakuwa kimejijenga upya
 
Tuongee KIKATIBA zaidi. Mengi tunayoandika humu hayawezekani kikatiba. Kama hatuifahamu katiba ya sasa, hiyo mpya sijui tutajadili nini!
 
Wana jamvi
Hapa Dodoma kimenuka. JK kafika kutoka MWZ ili kuonana na wabunge. Wabunge wa CCM wakaitwa na kuingizwa ukumbini ili kumsubiri. Awali Katibu wao Jenester Mhagama alitoa tangazo kupitia Naibu Spika kuwa wabunge wote waache simu zao wazi ili kuitwa wakihitajika.
JK aliendelea kupata briefings na kuambiwa hali ni mbaya. Akashauriwa afanye reshuffle upesi ili kupoza moto. Kama kawaida akawa mbishi, lakini pia akasita kuingia ukumbini kuonana na wabunge. Mwishowe wabunge wameambiwa waende kulala kwa sababu JK bado ana kikao na watendaji.
Kuna hatari kesho ya reshufle. Mawaziri wote matumbo moto hususan Afya, Nishati, Fedha na Ujenzi. Vijana wa TISS wamemweleza kuwa baraza zima ni kama haliko kazini isipokuwa wizara moja tu- Ya Pombe Magufuli.
Vijana wa TISS wameingia kazini kwa kasi sana usiku huu kujaribu kubadili upepo miongoni mwa wabunge.

Chanzo: Mimi mwenyewe nikiwa Dodoma mjengoni.
Badili title wewe jukwaa sio la wahuni hili, kimenuka manake nini?
 
Thubutu yake,

Kiwete afanye reshuffle? Hana huo ubavu. Yeye sanasana akishakutana na hao wabunge wake ataendelea ku-SMILE tu kama hamnazo. Mawaziri wote ni washikaji wake na wengi wao ni wale waliomsaidia kuukwaa Urahisi na wengine ni mashemeji.

Ni kweli kabisa kama Kiwete angelikuwa Rais ambaye ni MAKINI na TOUGH ON ISSUES, basi wafuatao walitakiwa kuondolewa haraka sana kwenye Baraza lake la Mawaziri pamoja na Wabunge.
  1. Mizengo Kayanza Peter Pinda- Waziri Mkuu kwa kulidanganya Bunge na kumsingizia Rais uongo kuhusu Posho.
  2. Haji Mponda- Waziri wa Afya- kushindwa kushughulikia mgomo wa Madaktari.
  3. Lucy Nkya-Naibu Waziri wa Afya- kushindwa kushughulikia mgomo wa Madaktari.
  4. Blandina Nyoni- Katibu Wizara ya Afya- kama ilivyo 2 & 3 hapo juu.
  5. Anne Makinda- Spika wa Bunge kwa kulidanganya Bunge na kumsingizia Rais uongo kuhusu Posho.
  6. Beatrice Shelukindo-Mbunge wa Kilindi kwa kumkosea Adabu Rais kwa kutaka Wabunge wa CCM kupiga kura ya kutokuwa na Imani na Rais.
  7. Mustafa Mkullo-Waziri wa Fedha kwa kushindwa kusimamia Uchumi na kusababisha Serikali kuyumba kiuchumi.
  8. Benno Ndullu -Gavana wa Benki Kuu- kwa kushindwa kumshauri Waziri wa Fedha kuhusu hali ya Uchumi wa Nchi.
 
Hata akifanya hiyo reshuffle bado watakuwa ni wale wale. Huyu anahamishwa kutoka A kwenda B, mwingine kutoka C kwenda A, n.k. Kama kweli wabunge wapo pale kwa interests za wananchi wapige kura ya kutokuwa na imani nae. Subutu.

Tatizo ni reshuffle au ni sisi wenyewe pia????? nchi hii bila kufanya reshuffle ya wananchi wenyewe kamwe hatutasonga mbele hata kama tutabadilisha marais 100
 
Hawa wabunge wa CCM wanapoteza muda tu. Wapitishe wasipitishe, there will be a price to pay. Na hii itakuwa fundisho kuwa miswada ikiletwa bungeni wajadili kama wawakilishi wa wananchi na sio wawakilishi wa chama na serikali!
 
mimi bado hii kauli inanichanganya(ukiwashitaki mafisadi ichi itawaka moto)
 
Huyu mama Shelukindo nadhani hajitambui tena. Nilimwona alivyojichanganya na kupanic kwa kuwasilisha barua ya jairo bungeni na kesho yake akawa wa kwanza kuwatetea kina ngeleja. Ni mnafiki wahedi.

Beatrice shelukindo ni kambi ya Lowassa na ameshasema wazi bila kificho kwamba Rais ajaye ni Lowassa. Kila sentensi yake moja nina mashaka nayo.
 
Kama TISS wanaona upuuzi yeye mwenyewe haoni, sasa anafanya nini pale Ikulu?

Actually,..hiyo ndo kazi yao TISS,...waone then waripoti kwa raisi ili a-act.
Raisi hayupo kila mahari hadi aone kila kitu.
 
ili kulinda heshima hata jk anapaswa kukaa pembeni........mtu mbishi sana huyu!!!!

Edson,
hivi unadhani ni rahisi eh?
Ingekua raisi kihivo wasingekua wanatumia nguvu nyingi kuingia ikulu.
Ukiona kiongozi kaachia ngazi ujue yuko katika hali ambayo
political rivals wake wame gundua madudu yake ambayo wakiyatoa
nje basi atakua kwenye hali ngumu kweli.

Na hata hapo,hadi wa mwakikishie immunity sana tu.
Sio rahisi hivo kuachia Ikulu hivi hivi aingie mwingine.
 
Nisiku njema na inayoashiria mswada mpya uliofanyiwa marekebisho makubwa na CDM kurudishwa bungeni na kupitishwa tena na wabunge vilaza na wasio jua wafanyalo wa CCM. wakiwa wamejaa kiburi ujinga, na kukosa uzalendo walikataa katu kusikiliza mawazo ya wenzao CDM mwaka jana. Waliambiwa mswada ule ulikuwa mbovu, haufai, si wakitaifa. Wakiwa na mashati yao ya kijana huku akili wakizeweka miguuni, wakiongozwa na mwanasheria asiyejua kazi yake walipitisha mswada usiofaa hata kwa akili ya mpunguani.

Leo hii wanaliingiza Taifa hasara kwa kutumia fedha za walalahoi kujadili walichokataa na kutokana na taratibu zao kwani wao ndio wengi wamesha ambiwa lazima wakubaliane na mawazo ya CDM kwani ndio yenye mashiko kwa mustakabali wa Taifa.

My Take.
Wabunge wa CCM sio wabunge bali hutimiza tu matakwa ya Ikulu. Wakiambiwa kubali wote wanakubali bila ya kufikiri, kuwaza wala kuchambua. Wakiambiwa kataa yote yatasema hapana bila ya kutumia akili. Ni vizuri kuwatambua hawa watu na kuachana nao kwani hakuna wanalowakilisha wananchi zaidi ya kufilisi nchi na kulilia posho.
 
Kuna tetesi kuwa huenda yale yaliyotokea mwaka 2008 yakajirudia tena. Safari hii mtoto wa Mkulima Mizengo Kayanza Peter Pinda Waziri Mkuu anaachia ngazi ya Uwaziri Mkuu baada ya tuhuma nzito tatu(3)zinazomkabili katika ofisi hiyo nyeti.
  1. Mizengo Pinda anatuhumiwa kuwa kwa kushirikiana na spika wa Bunge Anne Makinda AMELIDANGANYA BUNGE KUHUSU POSHO ZA VIKAO ZA WABUNGE KUWA RAIS KIWETE ALIKUWA AMERIDHIA NYONGEZA HIYO YA POSHO KUTOKA SHS.70,000/= MPAKA SHS.200,000/=kitu ambacho siyo kweli.
  2. Mizengo Pinda akishirikiana na Waziri wa Afya na NAIBU wake anatuhumiwa kushindwa kusimamia ipasavyo ili kuepusha au kuzuia MGOMO WA MADAKTARI MUHIMBILI MGOMO AMBAO HATIMAYE ULIPELEKEA MGOMO WA MADAKTARI NCHI NZIMA.
  3. Mizengo Pinda kama Mkuu wa shughuli za Serikali Bungeni ameonyesha UDHAIFU mkubwa kwa kushindwa kuwasimamia Wabunge wa CCM ambao wametishia kupiga KURA YA KUTOKUWA NA IMANI NA RAIS WAO Kiwete na pia kutishia KUPINGA MSWADA WA KATIBA MPYA YA JMT.
Kwa mwenye habari za undani zaidi kuhusu hizi tetesi naomba aendelee kutupasha zaidi.

Nawasilisha
 
Mkuu, "Preventive Detention Act" ni sheria ambayo constitutionality yake can pass a litmus test internationally. Hata US constitution.
which litmus test?
 
wewe hizo habari ulizoleta si za ndani?........
 
Mkuu Clemmy.

Ni kweli tufike mahali masuala ya kitaifa yapewe kipaumbele mambo ya uchadema na uccm yasipewe nafasi.Tanzania kama taifa kwa muda mrefu pamekuwepo na ombwe la uongozi serekali kuanzia mawaziri makatibu wakuu imekuwa ikiendeshwa kiushaji.


Men,..
am proud of you dude.
Ingawa uko CCM,haubebwi na zimwi la ushabiki.
You air the reality na sio kutoa sifa pasipo sifa.

Natamani Jk angekua na washauri kama wewe (kama ana tabia ya kusikiliza washauri
anyway,yawezekana wapo kweli lakini hafuati ushauri wao).

Tufikie mahali sasa tuangalie uhalisia wa mambo,...
huu ushabiki ushabiki wa kichadema na kiccm ufe na tuwe na
ushabiki wa kitanzania.

Big up bro.
 
Back
Top Bottom