JK na wabunge wa CCM Dodoma kimenuka

JK na wabunge wa CCM Dodoma kimenuka

HAPANA MKUU MCHAMBUZI.

Rais ndiye kiongozi pekee anayewakilisha watanzania bungeni.
Posho za wabunge ni sheria ya nchi yetu.
Rais hatakiwi ku-caucus na wabunge, bali wananchi kwa faida yetu na vizazi vijavyo.
Kila mswaada wa bunge hauna budi uwe na "bullet-proof" ya rais. Kabla hata haujapigiwa kura.
Je, kabla ya kupitishwa mswaada huu, rais alisema ataupitisha? i.e atapiga signature yake?
Akisema hajaubariki, ina maana atatia saini au hatatia saini?....
Au saini ya rais haihitajiki?

Soby,

Tanzania ilianza na katiba ya mfumo wa mwingireza ambayo serikali inaundwa na waziri mkuu na ambayo inahitaji serikali iwe na kambi na wabunge wa chama chake.

Tulipohamua kuwa jamuhuri hatukutenganisha na majukumu ya bunge na yale ya serikali. Hivyo kusema kuwa Rais hatakiwi ku-caucus na wabunge ni kuwa nje na taratibu za sasa. Hii ni kwa sababu bunge na serikali bado zinaingiliana kishughuli.

Rais anapochaguliwa ni lazima ateuwe Waziri mkuu na mawaziri ambao ni wabunge. Hawa bila kuwa na mahusiano mazuri na wabunge, miswada yao inaweza isipite na kufanya bunge livunjike na uchaguzi kuitwa. Hivyo kwa namna moja au nyingine caucus unayohitaja hipo na huwezi kuiondoa mpaka bunge na serikali vitakapokuwa ni vitu vyenye majukumu yasioingiliana.
 
Wana jamvi
Hapa Dodoma kimenuka. JK kafika kutoka MWZ ili kuonana na wabunge. Wabunge wa CCM wakaitwa na kuingizwa ukumbini ili kumsubiri. Awali Katibu wao Jenester Mhagama alitoa tangazo kupitia Naibu Spika kuwa wabunge wote waache simu zao wazi ili kuitwa wakihitajika.
JK aliendelea kupata briefings na kuambiwa hali ni mbaya. Akashauriwa afanye reshuffle upesi ili kupoza moto. Kama kawaida akawa mbishi, lakini pia akasita kuingia ukumbini kuonana na wabunge. Mwishowe wabunge wameambiwa waende kulala kwa sababu JK bado ana kikao na watendaji.
Kuna hatari kesho ya reshufle. Mawaziri wote matumbo moto hususan Afya, Nishati, Fedha na Ujenzi. Vijana wa TISS wamemweleza kuwa baraza zima ni kama haliko kazini isipokuwa wizara moja tu- Ya Pombe Magufuli.
Vijana wa TISS wameingia kazini kwa kasi sana usiku huu kujaribu kubadili upepo miongoni mwa wabunge.

Chanzo: Mimi mwenyewe nikiwa Dodoma mjengoni.

Kama TISS wanaona upuuzi yeye mwenyewe haoni, sasa anafanya nini pale Ikulu?
 
Soby,

Tanzania ilianza na katiba ya mfumo wa mwingireza ambayo serikali inaundwa na waziri mkuu na ambayo inahitaji serikali iwe na kambi na wabunge wa chama chake.

Tulipohamua kuwa jamuhuri hatukutenganisha na majukumu ya bunge na yale ya serikali. Hivyo kusema kuwa Rais hatakiwi ku-caucus na wabunge ni kuwa nje na taratibu za sasa. Hii ni kwa sababu bunge na serikali bado zinaingiliana kishughuli.

Rais anapochaguliwa ni lazima ateuwe Waziri mkuu na mawaziri ambao ni wabunge. Hawa bila kuwa na mahusiano mazuri na wabunge, miswada yao inaweza isipite na kufanya bunge livunjike na uchaguzi kuitwa. Hivyo kwa namna moja au nyingine caucus unayohitaja hipo na huwezi kuiondoa mpaka bunge na serikali vitakapokuwa ni vitu vyenye majukumu yasioingiliana.
Ni fikra kama hizi ndiyo zinatukwamisha.

Kuwa na mahusiano mazuri? ..... kwa hiyo unataka kuniambia Rais angeupitisha mswaada wa kupunguza kodi ya maji ya chupa?
Kama bunge lingepitisha?

Rais hatakiwi kupitisha miswaada kuwa sheria, just bcoz bunge limepiga kura ya ndiyo. Rais, ili aheshimike, inatakiwa hata ampe barua ya onyo Mkulo for flooring such a bogus bill.

In the same context rais awaambie wabunge wake kuwa mimi sitaki upumbavu wa posho, my government is broke!!!

Kama wataenda kwa Lowassa...... get him, try him, ask him where does he get that dough?.... and if you find a loophole, iuncarcarate him and nationalize his money (use Mnyika's bill).

It's about time we stop this nonsense.
 
=======
Waliokuwa wanamshauri ni viongozi wa CCM ndani ya bunge (kamati ya CCM) - Mhagama, Ndugai, PM na wajumbe wa Kamati Kuu walio katika serikali. Walikuwapo pia viongozi waandamizi wa TISS. Yeye kang'ang'ania eti Beatrice Shelukindo na wenzake wampigie kura ya kukosa imani naye. Mbishi kweli.

Shujaaa halilii bunduki. Wacha wampigie kur ya kutokuwa na imani tuone
 
RAIS Jakaya Kikwete amefanikiwa kuzima uasi uliotaka kufanywa na wabunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM), waliopanga kukwamisha Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Katiba ya mwaka 2011.
Baada ya kushindwa kukutana wabunge wote wa chama hicho, Kamati ya Uongozi ya Bunge imeteua wawakilishi watano kutoka miongoni mwa wabunge wake ambao wameunda kamati maalumu ya kukutana na Rais Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa CCM.
Kilichoibua mawazo ya uasi miongoni mwa wabunge wa CCM kinatokana na hatua ya serikali kuamua kuwasilisha mabadiliko katika sheria hiyo siku chache baada ya Rais Kikwete kukutana kwa nyakati tofauti na viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Chama cha Wananchi (CUF), NCCR-Mageuzi na wadau mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Kikwete aliwasili Dodoma jana akitokea mkoani Mwanza alikokwenda kwa ajili ya kilele cha maadhimisho ya miaka 35 ya kuzaliwa kwa CCM, kisha akaanza kukutana na wawakilishi watano wa wabunge wa chama hicho.
Awali, Rais Kikwete alipanga kukutana na wabunge wote wa CCM, alilazimika kukutana na wawakilishi watano wa chama hicho kutokana na msimamo wa wabunge hao kukataa kuonana naye kwa madai kuwa hawana cha kujadiliana naye.
Mbali ya kukutana na wawakilishi wa wabunge hao mjini Dodoma, Rais Kikwete alibadili upepo wa kisiasa katika viunga vya Bunge kwa hotuba yake aliyoitoa juzi mjini Mwanza kwamba katika marekebisho hayo, CCM nayo ilileta mapendekezo ya marekebisho manane ya sheria hiyo.
Hata hivyo, uchunguzi wa gazeti hili ulibaini kuwa wakati kuna wabunge bado wameshikilia msimamo wa kuukwamisha muswada huo, lakini pia wapo wanaokubaliana na Rais Kikwete.
Habari ambazo gazeti hili imezipata kutoka ndani ya kikao hicho cha rais na wabunge hao zilisema kuwa rais alifafanua kwa kina sababu ya kukubadili marekebisho aliyopokea kutoka kwa ujumbe wa CHADEMA na ule wa vyama vingine kutokana na uzito wa jambo lenyewe.
Habari zinasema kuwa Rais Kikwete mbali ya kuwalainisha wabunge kuhusiana na muswada huo, pia aliweka wazi msimamo wake wa kuwataka wawakilishi hao wa wananchi kuachana na suala la posho kwa sasa kwani linawajengea taswira mbaya.
Ujumbe huo wa wabunge, ulitarajiwa kukutana na wabunge wote jana baada ya kikao chake na rais ili kuwajulisha yaliyojiri katika mazungumzo yao na kama kuna haja ya kukutana nao wote kwa pamoja kabla ya muswada huo kuwasilishwa bungeni.
Awali muswada huo wa marekebisho ya sheria ya Katiba ya mwaka 2011, ulitarajiwa kuwasilishwa bungeni jana, lakini haukuwamo katika orodha ya shughuli za Bunge jana.
Akizungumza wakati wa kuahirisha kikao cha Bunge jana, Naibu Spika, Job Ndugai, aliwataka wabunge wa CCM kuwasha simu zao muda wote kwani Mwenyekiti wao, Jenister Mhagama (Peramiho), angewapigia simu wakati wowote kwa ajili ya kikao.
Wiki iliyopita, upepo wa kisiasa kwa wabunge wa CCM ulibadilika na kusababisha kutoa kauli nzito ndani ya vikao vya ndani, wakimlaumu Rais Kikwete kwa kile walichokiita kuwageuka.
Mambo ambayo yamewakera wabunge wa CCM katika siku za hivi karibuni ni pamoja na hatua ya Rais Kikwete kukana kubariki posho mpya za wabunge wakati Waziri Mkuu Pinda na Spika Makinda, tayari walishautangazia umma kwamba rais amebariki posho hizo.
Jingine ni la marekebisho ya sheria ya Katiba ya mwaka 2011, iliyofanyiwa marekebisho baada ya Rais Kikwete kukutana na viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Wakati serikali iko mbioni kuwasilisha bungeni marekebisho ya sheria ya Katiba ya mwaka 2011, kama ambavyo Rais Kikwete amekubaliana na viongozi wa CHADEMA, wabunge wa CCM, walipitisha azimo la kukataa marekebisho hayo

SOURCE:TANZANIA DAIMA
 
JK ni kigeugeu mkubwa...... Time will tell..... Usitegemee jipya

Namimi nawashangaa watu wanatumia nguvu kubwa kumpa alternatives wakati Rais wetu hataki ugomvi na watu. Ni mtu wa watu, kiongozi asiyependa makuu.
 
Jamani hizi habari sasa amelainisha hao watano au wote, mbona hiyo kamati ya wabunge watano haijakutana na wenzao kuwaambia walichoongea na JK, mwandishi unajuaje kama wakielizwa watalainika.

Hata hivyo wabunge posho na maslahi hawawezi kumbishia mtoa posho.
 
unagoma,sababu,ya,posho?kuwatumikia,wananchi?je,unawapenda,wananchi,wako?
 
Kumekucha!! Mchi mpya imeanza. Nani atajeruhiwa saffari hii. Wabunge watapeleka wapi sura zao!!
 
hao wabunge wa ccm ni wanafiki (ukimtoa january makamba) wangeni waliobaki hawana uwezo wa kupingana na serikali.
 
Siku ingine wajifunze kujadili hoja na si kujadili wajumbe waliotoka nje ya bunge.
 
Jamani hizi habari sasa amelainisha hao watano au wote, mbona hiyo kamati ya wabunge watano haijakutana na wenzao kuwaambia walichoongea na JK, mwandishi unajuaje kama wakielizwa watalainika.

Hata hivyo wabunge posho na maslahi hawawezi kumbishia mtoa posho.

Waliambiwa wabunge wa ccm wasizime simu muda wowote watapigiwa simu kupewa taarifa.
 
Wabunge wa CCM ni POSHO na POSHO ni wabunge wa CCM. Ndio TZ yetu
 
-Wabunge wa CCM waache kuwa mihuri ya kupitisha chochote kinacho letwa mbele yao wangelikuwa makini haya wangeliyaona mapema na kuyafanyia marekebisho makubwa...... tatizo lao wanawaza posho tu

- Sasa hili la huyu Domo kaya ataaibika mno
 
Back
Top Bottom