JK na wabunge wa CCM Dodoma kimenuka

=======
Waliokuwa wanamshauri ni viongozi wa CCM ndani ya bunge (kamati ya CCM) - Mhagama, Ndugai, PM na wajumbe wa Kamati Kuu walio katika serikali. Walikuwapo pia viongozi waandamizi wa TISS. Yeye kang'ang'ania eti Beatrice Shelukindo na wenzake wampigie kura ya kukosa imani naye. Mbishi kweli.
Kama una maana JK kawaambia wabunge wampigie kura ya kutokuwa na imani nae, hap namuunga mkono JK, kwani hizo kura hazitatosha na wabunge watajifunza kwa viboko sasa, kwani pamoja na mapungufu aliyonayo Rais, kama alivyo binadamu mwingine, Rais katika hili kasimamia upande sahhihi, na ni upande wa walio wengi nchi hii.
 
Nina mashaka kama Rais atafanya mabadiliko katika kipindi hiki tete cha msuguano kati ya bunge na serikali tuwe wavumilivu na subira. Rais amewajeruhi wabunge na posho zao na kukubali kukutana na chadema. wanaweza kuasi serikali yao kwa maslahi yao binafsi.
 
mimi nataka kinuke kabisa. yaani kinuke mia kwa mia hadi uchaguzi mkuu ufanyike mwaka huu.
 
asante kwa taarifa. Nathani kitaeleweka tu. Hao wabunge watalegea tu kwa jk. Kwani most of them yy ndio kawapa ubunge kwa nguvu ya dola. So hawana ujanja hao
 
tanzania tanzania nakupenda kwa moyo wote
tanzania tanzania viongozi wako siwapendi popote
nilalapo niamkapo nakuota wewe kwa yote
nchi tangu tanzania jina lako tamu kote
 
Kumpigia Rais kura ya kutokuwa na imani naye maana yake na wao watakaoma kuwa wabunge ambapo kwa katiba ya sasa Rais atalazimika kuvunja bunge na kuitisha uchaguzi mkuu. Chadema mko tayari kwa tukio hili? mnaweza kurudi msiwe chama kikuu cha upinzani bali chama kidogo cha upinzani
 
ni zama zake mabadiliko
ni zamu zao mahangaiko
ni hamu ya kuu anguko
watanganyika watachukua nchi yao.

sokoine wa sasa atarudi
kuchapa makuhadi
ufisadi hata nadi
jasho damu wanaililia nchi yao

nyerere yuko wapi
wanafunzi wake wako wapi
dira watanganyika hawawapi
nchi yao rasilimali zao zatokomezwa.

mandela njoo sasa
mkuruma rudi sasa
naser fufuka sasa
michael satta njoo huku

uchungu wa masikini hawana
machozi ya wajane hayana maana
ujinga mtoto mtanzania si manana
raha zao kero zetu kero zetu raha zao
 
Haya nape ulichoangaikia mda wote wa kushikilia bango la kujivua gamba watu 3 tu linakaribia mpigie basi jk asikusahau kwewnye jopo jipya. Usione haya bwana umeangaikia sana
 
Nina mashaka kama Rais atafanya mabadiliko katika kipindi hiki tete cha msuguano kati ya bunge na serikali tuwe wavumilivu na subira. Rais amewajeruhi wabunge na posho zao na kukubali kukutana na chadema. wanaweza kuasi serikali yao kwa maslahi yao binafsi.

Mkuu,
hakuna mbunge aliye tayari kurudi jimboni kuanza kampeni upya dhidi ya Chadema, CUF, CCK, NCCR, kwa tiketi ya CCM ambayo imelemewa kwa hoja katika kila kitu cha msingi ndani ya nchi hii. Ikitokea uchaguzi mpya, sana sana wengi watagombea kupitia vyama vya upinzani. Vinginevyo, wabunge wengi sana kwa sasa wapo katika harakati za kulipa madeni yao kutokana na mikopo ya kampeni za 2010, ndio maana wanapigania sana posho. Kwa wastani, mbunge ambae hana kipato cha pembeni, huwa anabakia na shillingi zisizozidi laki mbili kwenye account baada ya makato ya madeni haya, pamoja na makato ya madeni ya magari yao (mashangingi), kwahiyo wana survive kwa posho na ndio maana wanakuwa wakali kama mbogo juu ya hilo.

Rais akiweka msimamo na kuwaambia wakitaka wapige kura ya kutokuwa na imani na Rais, wengi watasononeka chini kwa chini lakini hawata piga kura ya namna hiyo kutokana na sababu hizi. Lakini tujiandae kwa wao kufanya utawala wa Kikwete kuwa mgumu sana kuelekea 2015, hasa kuikwamisha serikali kwa makusudi katika mambo mbalimbali, bila ya wao kujua kwamba kufanya hivyo ndio kukimaliza CCM na kuvijenga Chadema, CCK, NCCR....
 
Kikwete usiangalie nyuma, hawa wabunge wa ccm wamezoea kudeka. Kama kweli vidume wapige kura ya kutokuwa na imani.

Beatrice Shellukindo alianza kwa kutoa 'message' toka kwa nabii Joshua, akaja Jairo na sasa naona amekuja na hoja ya kupiga kura ya kutokuwa na imani na rais. Mama haya yote ni mawazo yako au unawakilisha mtu/watu?
 
Nagojea taarifa zaidi wacha niende kusoma kitabu changu wakuu nitarudi baadaye .Kazi bado na JK huwa ana mawazo ya kisaogoni hata akiambiwa nini yeye akisha amua ni kucheka tu .
 
Mchambuzi. Nakubaliana na msimamo wako. Kama kweli hicho kikao kilikuepo,JK awaache hao akina Shelukindo wapige kura,tuone mjaja nani. Hatuwezi endekeza ujinga na upumbavu eti kwa kuogopa kura ya kutokua na imani na Rais.
 
mamaaaaaaaaaaa...
naiwaza tanzania bila jakaya na ccm..
bado tuna safari ndefu
madaktari bingwa nao kinanukia sijui tunakwenda wapi...
neema ya Mungu ishuke tu

hayo ni mambo ya kiutendaji,hayawezi kuwa kama unavojidanganya wewe.
 
Ni heri waendelee kuvunjana viuno ili waonekane na wananchi kwa dhambi zao nyingi walizofanya dhidi ya wanyonge wa Tanzania.
 
Kama una maana JK kawaambia wabunge wampigie kura ya kutokuwa na imani nae, hap namuunga mkono JK, kwani hizo kura hazitatosha na wabunge watajifunza kwa viboko sasa, kwani pamoja na mapungufu aliyonayo Rais, kama alivyo binadamu mwingine, Rais katika hili kasimamia upande sahhihi, na ni upande wa walio wengi nchi hii.

Nakubaliana na wewe kuwa kura hazitatosha za kumwondoa,ila wabunge waelewe kuwa tamko lake moja ambalo haliwezi kuchukua hata dakika moja wao wote si wabunge!!wao wamekaa bungeni kugombania posho badala ya kuangalia sheria kandamizi kama hizi!!wamebaki kupitisha sheria zinazotungwa na serikali badala ya wao kutunga sheria,ajabu ukiwasikia mitaani eti wanajiita watunga sheria!!badala ya kujiita wapitisha sheria.
 
Back
Top Bottom