MkamaP,
Kuhusu swali lako: kinachoendelea ni kwamba - kwa mujibu wa taarifa zinazoenea, wabunge wa CCCM feel offended na kitendo cha Rais Kikwete kukubali mapendekezo ya Chadema kwamba kuna ulazima wa kubadilisha mambo kadhaa ndani ya muswada uliopitishwa na bunge la CCM na CUF mwaka jana, kuhusu mchakato wa katiba mpya. Nasema bunge la CCM na CUF kwasababu wabunge wote wa Chadema (pia nadhani na wachache kutoka NCCR) walisusa na hivyo kutoka nje ya bunge, huku wabunge wa CCM wakiongozwa na kina Anne Kilango na wengine wengi, wakiwazomea. Wabunge wa CCM wanadai kwamba kitendo cha rais kukubali kwa mfano mchakato usimamiwe na wakurugenzi wa halmashari/manispaa kama Chadema wanavyotaka, badala ya wakuu wa wilaya kama wabunge wa CCM wanavyotaka, kitafanya mchakato huo uwe controlled na Chadema kwa madai kwamba wakurugenzi wa halmashauri nchini ni wanachama wa chadema.
Ufa huu baina ya Rais na Wabunge umepanuka zaidi pale alipokataa kuidhinisha ongezeko la posho zao. Kwahiyo hivi sasa ni mkakati wa wewe mwaga ugali, sisi tunamwaga mboga. Na tumeona miswaada miwili ya serikali wiki iliyopita yote ikipigwa chini na wabunge wa CCM. Kwa kifupi hali ndio imekaa hivyo. Tunabaki kushangaa zile kauli za 'ndiyoooooooooo', zikiambatana na makofi kwenye meza kuunga hata hoja zile za kumchekesha matonya, sijui mzuka ule umeenda wapi.