Mchambuzi. Nakubaliana na msimamo wako. Kama kweli hicho kikao kilikuepo,JK awaache hao akina Shelukindo wapige kura,tuone mjaja nani. Hatuwezi endekeza ujinga na upumbavu eti kwa kuogopa kura ya kutokua na imani na Rais.
mkuu katika hii namuunga mkono Kikwete. Na ninatarajia watanzania wote wazalendo tuonataka kuona taifa letu linapata katiba nzuri tujitokeze wazi kumuunga mkono JK. Na tuzipinge kwa nguvu zote hizi posho wanazotaka kulipwa bila ya kutoka jasho.Tanzania imepoteza dira chini ya CCM,yetu macho
Tetesi za reshuffle nimezisikia pia
I hope atasikiliza ushauri wa watanzania. People that he trust are letting him down!Mimi nadhani hii ni nafasi pengine ya mwisho kwa JK kurudisha hadhi yake na ya CCM mbele ya umma. Anahitaji kufanya mabadiliko makubwa na kuondoa mawaziri legelege wote; pia mwanasheria mkuu wa sasa hatoshi, huyu hafai katika mchakato wa kupata katiba mpya. Pia ni muhimu kwa rais kubadili mfumo wa serikali, hasa sekta ya elimu na afya. Pia apunguze ukubwa wa baraza la mawaziri kwa kufuta wizara nyingine au kuziunganisha ili iwe ishara kwa umma ya kuanza kubana matumizi tunapoelekea bajeti mpya mwezi juni. Na katika hotuba yake kuunda baraza jipya, awe mkali na awe tofauti kabisa, na ashike uzi huo huo kwa kipindi chake kilichobakia. Akiachia nafasi hii imponyoke, atakuwa na shughuli nzito sana ya kukipa CCM uhalali mbele ya umma, na pia mawaziri wengi wataendelea kumchukulia kama mshijaki. Hili litakuwa janga kubwa kwake hasa kuelekea uchaguzi mkuu wa ndani wa CCM, Novemba mwaka huu.
Hivi Vicky Kamata naye atapiga kura ya kutokuwa na imani? shombo shombo!
JK directionless government is doomed to fail, no wonder he remained carefree and unconcerned with people's clamour over his cabinet's performance even after repeated calls to substitude his underperforming ministers with competent ones. He, at this point of time, seems to respond to the public sentiment but its too late to rescue this stumbling country from falling. The reshuffle he is contempleting to carry out will not help change deteriorating things but only could diffuse the damage that was otherwise to be spawned by the collapse.
Kama kweli hawamsaidi Rais vya kutosha mabadiliko ni muhimu. Angalia hata suala la posho bungeni mawaziri hawakuisaidia serikali ingawa Rais alionyesha msimamo kwamba sio wakati muafaka.
Hata akifanya hiyo reshuffle bado watakuwa ni wale wale. Huyu anahamishwa kutoka A kwenda B, mwingine kutoka C kwenda A, n.k. Kama kweli wabunge wapo pale kwa interests za wananchi wapige kura ya kutokuwa na imani nae. Subutu.