JK na wabunge wa CCM Dodoma kimenuka

JK na wabunge wa CCM Dodoma kimenuka

Mtoto wa mkulima amejiharibia sana, tangu aanze kusaini zile posho 250,000 za jairo

Toka uteuzi wake hajadhihirisha na wala sioni dalili za uongozi thabiti toka kwake...viatu alivyopewa vinampwaya sana...
 
Wana jamvi
Hapa Dodoma kimenuka. JK kafika kutoka MWZ ili kuonana na wabunge. Wabunge wa CCM wakaitwa na kuingizwa ukumbini ili kumsubiri. Awali Katibu wao Jenester Mhagama alitoa tangazo kupitia Naibu Spika kuwa wabunge wote waache simu zao wazi ili kuitwa wakihitajika.
JK aliendelea kupata briefings na kuambiwa hali ni mbaya. Akashauriwa afanye reshuffle upesi ili kupoza moto. Kama kawaida akawa mbishi, lakini pia akasita kuingia ukumbini kuonana na wabunge. Mwishowe wabunge wameambiwa waende kulala kwa sababu JK bado ana kikao na watendaji.
Kuna hatari kesho ya reshufle. Mawaziri wote matumbo moto hususan Afya, Nishati, Fedha na Ujenzi. Vijana wa TISS wamemweleza kuwa baraza zima ni kama haliko kazini isipokuwa wizara moja tu- Ya Pombe Magufuli.
Vijana wa TISS wameingia kazini kwa kasi sana usiku huu kujaribu kubadili upepo miongoni mwa wabunge.

Chanzo: Mimi mwenyewe nikiwa Dodoma mjengoni.

Nnajiuliza swali moja,ni kwa nini Jk amekuwa na hofu juu ya Wabunge wake Wa ccm?Ni nini anachokihofu hasa!!?Imekuwa vp akakimbilia Dodoma huku wagonjwa wakifa ktk mahospitali!?.Inamaana Jk anawajibika zaidi kwa Wabunge wake Wa ccm kuliko na anavyowajibika kwa wananchi wake walionchagua?
 
Katika kujadiliana na Waziri Mkuu na Advisors jinsi ya kumaliza Mgomo wa madaktari..JK alimwagiza waziri mkuu arudi tena kuongea na madaktari walogoma kuwaambia kwamba uongozi wote wa wizara ya Afya umewasimamishwa kwa ku-mishandle huu mgomo.

Mh. Pinda akamkumbusha JK kwamba yeye kama waziri mkuu hana uwezo wa kutangaza kusimamishwa kwa waziri au Naibu..akitangaza hivyo madaktari kwa kujua kwamba hana mamlaka hayo wanaweza kumbishia!

Ndipo JK akamjibu kwamba atangaze kusimamishwa kwa Katibu mkuu tu na Mganga Mkuu ila taarifa ya kuondolewa kwa Waziri na Naibu wake ataitangaza yeye mwenyewe pamoja na "Mabadiliko Mengine ya Baraza la Mawaziri"

Hint hii iliacha wajumbe wote wa kikao na mshtuko/mshangao kwamba kumbe kuna mabadiliko ya baraza la mawaziri soon.
 
Hii sio moja ya mastory yetu tuliyoyazoea? Kuna kila sababu ya kubadili safu ya uongozi maana mambo ni kama hayaendi. But who cares? Labda wagonjwa wanaotaabika Muhimbili wanajua usahihi wa kukosa uwezo wa kutatua matatizo yanayotuzunguka kwa sababu ya uongozi. Wengine ni kula kwa upole kwa kwenda mbele
 
abadili tu hata kesho,alete timu mpya sura ya mbuzi ipige mzigo
 
Back
Top Bottom